papa-francesco_esortazione-ap_20160319_amoris-laetitia-sw


papa-francesco_esortazione-ap_20160319_amoris-laetitia-sw

1 Pages 1-10

▲back to top

1.1 Page 1

▲back to top
The Holy See
WOSIA WA KITUME
BAADA YA SINODI
AMORIS LAETITIA
WA BABA MTAKATIFU
FRANSISKO
KWA MAASKOFU,
MAPADRE NA MASHEMASI
KWA WATU WENYE NADHIRI
KWA WANANDOA WAKRISTO
NA KWA WAAMINI WOTE WALEI
JUU YA UPENDO KATIKA FAMILIA
Faharasa
SURA YA KWANZA
KATIKA MWANGA WA NENO LA MUNGU
Wewe na mkeo.
Wanao kama miche ya mizeituni
Njia ya mateso na kumwaga damu.
Taabu ya mikono yako.
Upole wa kukumbatia.
SURA YA PILI
HALI HALISI NA CHANGAMOTO ZA FAMILIA
Hali halisi ya familia wakati huu.
Changamoto nyingine.

1.2 Page 2

▲back to top
2
SURA YA TATU
KUMTAZAMA YESU: WITO WA FAMILIA.
Yesu anahuisha na kuukamilisha mpango wa Mungu.
Familia katika hati za Kanisa.
Sakramenti ya ndoa.
Mbegu za Neno na hali zenye mapungufu.
Uzazi na malezi ya watoto.
Familia na Kanisa.
SURA YA NNE.
UPENDO KATIKA NDOA.
Upendo wetu wa kila siku.
Uvumilivu.
Moyo wa ufadhili
Kuponya husuda.
Bila kutakabari wala kujivuna.
Adabu.
Kujibandua na ubinafsi kwa ukarimu.
Bila ukatili wa ndani
Msamaha.
Kufurahi pamoja na wengine.
Huvumilia yote.
Unaamini
Hutumaini
Hustahimili yote.
Kukua katika mapendo ya kindoa.
Kwa maisha yote, mambo yote katika umoja.
Furaha na uzuri
Kufunga ndoa kwa upendo.
Upendo unaojidhihirisha na kukua.
Mazungumzano.
Upendo wa tamaa.
Ulimwengu wa mihemuko.
Mungu anapenda furaha ya watoto wake.
Upendo kama mapenzi
Ukatili na ulaghai

1.3 Page 3

▲back to top
3
Ndoa na ubikira.
Mabadiliko ya upendo.
SURA YA TANO.
UPENDO UZAAO MATUNDA.
Kuukaribisha uhai mpya.
Upendo wakati wa kusubiri ujauzito.
Upendo wa mama na wa baba.
Kupanuka kwa uzaaji
Kuutambua mwili
Maisha katika familia pana.
Kuwa wana.
Wazee.
Kuwa ndugu.
Moyo mkuu.
SURA YA SITA.
BAADHI YA MITIZAMO YA KICHUNGAJI.
Kuitangaza Injili ya familia leo.
Kuwaandaa wachumba kwa ajili ya ndoa.
Maandalizi ya adhimisho.
Kusindikiza mwanzoni mwa maisha ya ndoa.
Baadhi ya mbinu za kufanya.
Kutia mwanga kwenye migogoro, fadhaa na magumu.
Changamoto ya migogoro.
Vidonda vya zamani
Kusindikiza baada ya kuvunjika uhusiano wa ndoa na baada ya talaka.
Baadhi ya mazingira magumu.
Maumivu makali ya kifo.
SURA YA SABA.
KUIMARISHA MALEZI KWA WATOTO.

1.4 Page 4

▲back to top
4
Watoto wako wapi?
Mafundisho ya kimaadili kwa watoto.
Umuhimu wa adhabu kama kichocheo.
Kukubali hali halisi kwa uvumilivu.
Maisha ya familia kama mazingira ya malezi
Hitaji la elimu ya jinsia.
Kurithisha imani
SURA YA NANE.
KUSINDIKIZA, KUPAMBANUA NA KUTEGEMEZA UDHAIFU.
Kazi ya kichungaji hatua kwa hatua.
Upambanuzi wa hali zinazoitwa “zisizo kadiri ya kanuni”
Mambo tetezi katika upambanuzi wa kichungaji
Kanuni na upambanuzi
Mantiki ya huruma ya kichungaji.
SURA YA TISA.
TASAUFI (MAISHA YA KIROHO) KATIKA NDOA NA FAMILIA.
Tasaufi ya ushirika wenye kupita maumbile.
Kuungana katika sala kwa mwanga wa Pasaka.
Tasaufi ya upendo unaojitoa kwa mwenzake tu kwa uhuru.
Tasaufi ya kujali, kufariji na kuhamasisha.
Sala kwa Familia Takatifu.
1. Furaha ya upendo (Amoris Laetitia) ambayo watu wanaiishi katika familia ni furaha ya Kanisa
pia. Kama walivyosisitiza Mababa wa Sinodi, licha ya dalili nyingi za migogoro ya taasisi ya ndoa,
“hamu ya kuwa na familia inadumu kuwa hai, hasa kati ya vijana, na hamu hiyo inalihimiza
Kanisa”[1]. Kama jibu la matamanio haya “tangazo la Kikristo kuhusu familia ni kwa hakika habari
njema”[2].
2. Mwendo wa sinodi uliruhusu kuchanganua hali ya familia katika ulimwengu wa leo, kuupanua
mtazamo wetu na kuihuisha dhamiri yetu juu ya umuhimu wa ndoa na familia. Wakati huohuo,
mchangamano wa mada zilizopendekezwa umetuonyesha hitaji la kuendelea kuchambua kwa
uhuru masuala kadhaa ya kimafundisho, kimaadili, kiroho na kiuchungaji. Tafakari ya wachungaji
na wanateolojia, ikiwa ni aminifu kwa Kanisa, nyofu, ikizingatia hali halisi kwa ubunifu, itatusaidia
kuufikia utambuzi wa kina zaidi kuhusu masuala haya. Mijadala inayofanyika katika vyombo vya

1.5 Page 5

▲back to top
5
mawasiliano au katika machapisho au hata kati ya wahudumu wa Kanisa, inahusu mambo mengi
mbalimbali, kuanzia hamu isiyo na lijamu ya kupindua kila utaratibu bila kutafakari au kuwa na
msingi tosha, hadi ule msimamo unaodai kutatua kila suala kwa kukazia kanuni za jumla au kwa
kuchukua uamuzi mkali kutokana na matafakari fulani ya kiteolojia.
3. Kwa kukumbuka kuwa wakati ni muhimu kuliko mahali, ninapenda kusisitiza kwamba si lazima
mijadala yote ya kimafundisho, ya kimaadili au ya kiuchungaji itatuliwe kwa njia ya matamko ya
majisterio. Bila shaka katika Kanisa inatakiwa kuwa na umoja wa mafundisho na wa utendaji,
lakini hilo halizuii kuwepo kwa namna mbalimbali za kufasiri masuala kadha wa kadha ya
mafundisho au mambo mengine yatokanayo nayo. Na hali hiyo itaendelea hadi hapo Roho
atakapotuongoza atutie kwenye kweli yote (rej. Yn 16:13), yaani atakapotuingiza kikamilifu katika
fumbo la Kristo na tutaweza kuona yote kwa mtazamo wake. Aidha, katika kila nchi au ukanda
inawezekana kutafuta masululisho yaliyotamadunisha zaidi, yanayozingatia desturi na
changamoto za mahali husika. Kwani, “tamaduni zinatofautiana sana, na kila kanuni msingi […]
inahitaji kutamadunishwa, ikipaswa kushikwa na kutekelezwa”[3].
4. Kwa vyovyote, lazima niseme kwamba mwendo wa sinodi ulikuwa una uzuri mkubwa na kutoa
mwanga kwa wingi. Ninatoa shukrani kwa michango mingi iliyonisaidia kutazama matatizo ya
familia za sehemu zote za dunia katika upana wake wote. Ujumla wa hoja walizotoa Mababa,
ambazo nilizisikiliza daima kwa makini, umeonekana kwangu kama poliedri yenye thamani,
iliyojaa kero zilizo halali na maswali manyofu na ya kweli. Ndiyo maana niliona vema kuandika
Wosia wa Kitume wa baada ya sinodi unaokusanya michango ya sinodi hizi mbili za hivi karibuni
kuhusu familia, kwa kuunganisha pia mawazo mengine yanayoweza kutoa dira kwa matafakari,
mazungumzano na matendo ya kiuchungaji, na wakati huohuo yatie moyo, yawe kichocheo na
yalete msaada kwa familia zote katika juhudi wanazofanya na magumu wanayokutana nayo.
5. Wosia huu unapata maana maalumu katika muktadha wa Mwaka huu wa Jubilei ya Huruma.
Kwanza kabisa, kwa sababu nimenuia uwe kama mwaliko kwa familia za kikristo, wa kuwahimiza
kuthamini tunu za ndoa na familia, na kudumisha upendo thabiti uliojaa tunu za ukarimu, juhudi,
uaminifu na ustahimilivu. Pili, kwa sababu unaazimia kuwatia wote moyo ili kuwa ishara za
huruma na ukaribu popote pale maisha ya kifamilia hayatimizwi kikamilifu au yanakosa amani na
furaha.
6. Kuhusu mpangilio wa sura za Wosia huu, nitaanzia kwa utangulizi uliovuviwa na Maandiko
Matakatifu, utakaoutia Wosia wenyewe kwenye kiwango kifaacho. Kutokana na hayo, nitaangalia
hali ya kisasa ya familia, kwa lengo la kutokwepa hali halisi ya dunia ya leo. Halafu nitakumbushia
vipengele vichache vya msingi vya mafundisho ya Kanisa kuhusu ndoa na familia, ili kuandaa
nafasi kwa sura mbili za kati, zinazohusu upendo. Baadaye nitasisitiza njia kadhaa za kiuchungaji
zinazoweza kutuelekeza katika uundaji wa familia imara na zenye kuzaa matunda kadiri ya
mpango wa Mungu, na nitatumia sura moja kwa kuzingatia malezi ya watoto. Baada ya hayo,
nitabakia katika mwaliko wa kuwa na huruma na kufanya upambanuzi wa kichungaji mbele ya hali

1.6 Page 6

▲back to top
6
za maisha ambazo haziendani kikamilifu na mashauri ya Bwana, na mwisho nitachora mistari
michache juu ya tasaufi ya kifamilia, yaani maisha ya kiroho katika familia.
7. Kutokana na utajiri wa miaka miwili ya kutafakari ulioletwa na mwendo wa sinodi, Wosia huu
unachambua, kwa mitindo mbalimbali, mada nyingi na za aina tofauti. Jambo hilo linaelezea kwa
nini hati hii haikuweza kuwa mfupi. Na ndiyo sababu mimi nishauri isisomwe yote katika ujumla
wake kwa haraka. Itapokelewa vizuri zaidi na katika thamani yake yote, kwa upande wa familia na
vilevile wa wahudumu wa uchungaji wa familia, ikiwa wataitafakari polepole sehemu kwa sehemu,
au wakiwa watatafuta humu yale ambayo wanahitaji katika kila mazingira mahsusi. Inawezekana,
kwa mfano, kwamba wenzi wa ndoa watatambua kwa urahisi zaidi kuwa sura ya nne na ya tano
zinawaongelea wao, au kwamba wahudumu wa uchungaji wataona ni muhimu zaidi sura ya sita,
na kwamba wote wanajadiliwa na sura ya nane. Ninatumai kwamba kila mmoja, kwa njia ya
kuusoma, ajisikie kuwa ameitwa kuwajibika kwa upendo juu ya maisha ya familia mbalimbali, kwa
sababu zenyewe “wala si tatizo, bali hasa ni fursa”.[4]
SURA YA KWANZA
KATIKA MWANGA WA NENO LA MUNGU
8. Katika Biblia zinapatikana habari nyingi za familia mbalimbali, vizazi, mapenzi, shida
zilizokumba mazingira ya kifamilia; kuanzia ukurasa wa kwanza, ambao unaonyesha familia ya
Adamu na Eva, pamoja na mambo ya ujeuri yaliyoilemea, lakini pia na nguvu ya uhai
unaoendelea katika vizazi (taz. Mwa 4), hadi ukurasa wa mwisho unaoonyesha ndoa ya Bibi arusi
na Mwanakondoo (taz. Ufu 21:2,9) Mfano uliotolewa na Yesu wa nyumba mbili zilizojengwa moja
juu ya mwamba na moja juu ya mchanga, unadokeza hali nyingi za kifamilia zinazotokana na
uhuru wa wana familia, kwa maana, kama alivyoandika mshairi, “kila nyumba ni kama
kinara”.[5] Na tuingie sasa katika moja ya nyumba hizo, kwa kuongozwa na Mzaburi kwa njia ya
utenzi ulioimbwa hadi leo katika liturujia ya ndoa ya kiyahudi, na ya kikristo pia.
“Heri kila mtu amchaye Bwana,
aendaye katika njia yake.
Taabu ya mikono yako hakika utaila,
utakuwa heri, na kwako kwema.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
vyumbani mwa nyumba yako;
Wanao kama miche ya mizeituni
wakizunguka meza yako.
Tazama, atabarikiwa hivyo,
yule amchaye Bwana.
Bwana akubariki toka Sayuni;
uone uheri wa Yerusalemu

1.7 Page 7

▲back to top
7
siku zote za maisha yako.
Naam, ukawaone wana wa wanao.
Amani ikae Israeli!” (Zab 128)
Wewe na mkeo
9. Tuvuke mlango na kuingia katika nyumba hii ya amani, ambayo familia yake wamekaa
wakizunguka meza yake siku ya sherehe. Kiini chake ni jozi: mama na baba, pamoja na maisha
yao ya kupendana. Katika hao unatimizwa mpango ule wa asili ambao Kristo mwenyewe
anakumbuka wazi, “Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba Mtu mume
na mtu mke?” (Mt 19:4) Naye anataja ile amri ya kitabu cha Mwanzo, “Kwa sababu hiyo, mtu
atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”
(Mt 19:5; taz. Mwa 2:24)
10. Sura mbili nzuri sana za kwanza za kitabu che Mwanzo zinatuonyesha jozi la mume na mke
katika kweli yake ya msingi Katika matini hizi za mwanzo za Biblia, kauli kadhaa muhimu sana
zinang’aa. Kauli ya kwanza, ambayo Yesu ametaja kwa kifupi, ni, “Mungu akaumba mtu kwa
mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwa
1:27) Inashangaza kuwa “mfano wa Mungu” ni sambamba na jozi “mnanamume na mwanamke”
kama maelezo yake. Je, maana yake ni kwamba Mungu mwenyewe ana jinsia yake, au ana
mwenzi wake wa kike, kama zilivyodhani dini fulani za zamani? La, sivyo! Maana, twajua jinsi
Biblia inavyokataa kwa wazi dini hizi zilizoenea kati ya Wakananayo wa Nchi Takatifu kwa kuona
kuwa ni kuabudu miungu. Dhana ya upekee usiofikika wa Mungu inahifadhika; lakini, kwa kuwa
yeye ni Muumba pia, uzaaji wa jozi la kibinadamu ni “mfano”, hai na wa maana, na alama
inayoonekana ya kazi ya kuumba.
11. Jozi lililo na upendo, na kuzalisha uhai, ni kwa kweli “ikona” hai, yenye uwezo wa
kumdhihirisha Mungu muumbaji na mwokozi, kinyume na sanamu za jiwe au dhahabu ambazo
Amri kumi zinakataza. Kwa hiyo upendo wenye kuzaa unakuwa ni ishara ya mtima wa Mungu
(taz. Mwa 1:28; 9:7; 17:2-5,16; 28:3; 35:11; 48:3-4) Ndiyo sababu simulizi la kitabu cha Mwanzo,
kwa kufuata mapokeo yaliyoitwa “ya kikuhani”, lina ndani yake orodha nyingi za vizazi (taz. Mwa
4:17-22,25-26; 5:10; 11:10-32; 25:1-4,12-17,19-26;36): maana, uwezo wa jozi la kibinadamu wa
kuzaa ni njia ambayo kwa hiyo historia ya wokovu yaendelea. Kutokana na hayo, uhusiano wenye
kuzaa wa jozi ni mfano kwa ajili ya kugundua na kuonyesha fumbo lile la Mungu, la msingi katika
mtazamo wa kikristo wa Utatu Mtakatifu, ambalo humdhihirisha Mungu kama Baba, Mwana, na
Roho wa upendo. Mungu Utatu Mtakatifu ni ushirika wa upendo; na familia ni kioo hai
kinachomwakisi. Maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II yanatuangaza: “Mungu wetu, katika fumbo
lake la undani zaidi, si upweke, bali ni familia, kwa sababu ana ndani yake ubaba, umwana, na
uhai wa familia, yaani upendo. Upendo huo, katika familia ya kimungu, ndiye Roho
Mtakatifu”.[6] Familia, basi, si jambo geni kwa uhai wenyewe wa Mungu.[7] Hali hii ya jozi
inayohusiana na Utatu Mtakatifu, inaonyeshwa kwa namna mpya katika teolojia ya Paulo, pale

1.8 Page 8

▲back to top
8
ambapo Mtume analihusisha na “fumbo” la muungano wa Kristo na Kanisa (taz. Efe 5:21-33).
12. Lakini Yesu, anapotafakari juu ya ndoa, anatukumbusha pia sehemu nyingine ya kitabu cha
Mwanzo, yaani sura ya pili, pale ambapo inapatikana picha nzuri sana ya jozi la mume na mke, na
yenye sifa zinazolieleza wazi. Tuzichague mbili tu. Ya kwanza ni hamu isiyotulizika ya mtu ya
kutafuta “msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18,20), anayeweza kushinda upweke wake
unaomlemea, ambao hata wanyama na viumbe vyote vinavyomzunguka haviwezi kuutuliza.
Msemo wa Kiebrania wa asili unatudokezea fikra ya uhusiano wa moja kwa moja, kama wa mtu
mmoja mbele ya mwingine, uso kwa uso, macho kwa macho; katika mazungumzano ambayo ni
ya unyamavu pia, kwa kuwa katika kupendana, mara nyingi kubaki kimya kunaeleza kwa namna
bora kuliko kunena. Ni kukutana na uso wa mtu mwingine, na“mtu-wewe” anayeakisi upendo wa
Mungu, na ambaye ni “mali iliyo bora, msaidizi wa kumfaa, na nguzo ya kumtegemeza”, (YbS
36:24), kama anavyosema mwenye hekima wa Biblia. Au, kama anavyosema bibi arusi wa Wimbo
Ulio Bora, kwa kukiri kwa namna nzuri sana hisia ya kupendana na ya kutoleana mmoja kwa
mwingine, “Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake è [...] Mimi ni wake mpendwa wangu,
naye ni wangu” (Wim 2:16; 6:3).
13. Kufuatana na kukutana huko, kunakoponya upweke, uzazi na familia vinaanza. Nalo ni jambo
la pili tunaloweza kusisitiza: Adamu, aliye pia mfano wa mtu wa kila wakati na kila mahali pa dunia
yetu hii, anaanzisha familia mpya pamoja na mke wake, kama anavyorudia kusema Yesu kwa
kunukuu kitabu cha Mwanzo: “Ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja” (Mt
19:5; taz. Mwa 2:24) Kitenzi “kuambatana” kwa lugha ya asili ya Kiebrania, kinaonyesha ulinganifu
mkubwa, muambatano wa kimwili na wa undani; kiasi kwamba kinatumika ili kueleza muungano
na Mungu: “Nafsi yangu inaambatana na Wewe” (taz. Zab 63:8), kama alivyoimba mzaburi. Kwa
hiyo muungano wa ndoa unaonyeshwa si tu katika ujinsia na umwili, bali pia katika matoleo yake
ya upendo kwa hiari. Tunda la muungano huo ni “kuwa mwili mmoja”, nalo ni kweli kimwili, na
katika muungano wa mioyo na ya maisha pia, na, kama itatokea, katika mtoto atakayezaliwa na
hao wawili, ambaye atapokea ndani yake na kuunganisha “miili” yote miwili, si kijenetiki tu bali
kiroho pia.
Wanao kama miche ya mizeituni
14. Tuangalie tena utenzi wa Mzaburi: ndani ya nyumba ambapo mume na mke wake wamekaa
mezani, wapo pia pamoja nao wanao, walio “kama miche ya mizeituni”, yaani wamejaa nguvu na
ari motomoto. Wazazi ni kama misingi ya nyumba; na wanao ni kama “mawe hai” ya familia (taz.
1Pet 2:5). Ni jambo la maana kwamba neno linalopatikana mara nyingi zaidi katika Agano la Kale,
usipofikiria jina la Mungu (YHWH, Bwana), ni “mwana” (Kiebrania: ben), neno linalohusiana na
kitenzi cha Kiebrania “banah”, ambacho maana yake ni “kujenga”. Ndiyo sababu katika Zaburi
127, zawadi ya wana inafananishwa na picha zinazohusu ujenzi wa nyumba, na pia shughuli za
kijamii na za biashara zilizofanywa kwenye lango la mji: “Bwana asipoijenga nyumba waijengao
wafanya kazi bure [...] Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, uzao wa tumbo ni thawabu. Kama

1.9 Page 9

▲back to top
9
mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani. Heri mtu yule aliyelijaza podo lake
hivyo. Naam, hawataona aibu wanaposema na adui langoni” (Zab 127:1,3-5). Ni kweli kwamba
picha hizo zinahusiana na utamaduni wa jamii ya kale, lakini uwepo wa wana ni kwa vyovyote
alama ya utimilifu wa familia katika mfululizo wa historia ya wokovu, kizazi baada ya kizazi.
15. Kutokana na hayo, tunaweza kusisitiza sifa nyingine ya familia. Twajua kuwa katika Agano
Jipya inasemwa kuhusu “Kanisa linalokusanyika nyumbani” (Taz. 1Kor 16:19; Rum 16:5; Kol 4:15;
Flm 2). Mahali pa kuishi kwa familia palikuwa pakigeuka kuwa kanisa la nyumbani, mahali pa
kuadhimisha Ekaristi Takatifu, pa kuwepo kwa Kristo amekaa kwenye meza ileile. Haiwezekani
kusahau yaliyoandikwa katika Kitabu cha Ufunuo, “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; Mtu
akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye
pamoja nami” Ufu 3:20). Basi, hapa tunapata picha ya nyumba yenye ndani yake uwepo wa
Mungu, sala ya pamoja, na, kwa hiyo, baraka ya Mungu. Hayo ndiyo yanayosemwa katika Zaburi
128, iliyo msingi wa kauli yetu, “Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. Bwana
akubariki toka Sayuni” (Zab 128:4-5).
16. Biblia inafikiria familia pia kama mahali pa katekesi kwa wana. Hiyo inaonekana wazi katika
maelezo ya adhimisho la Pasaka (taz. Kut 12:26-27; Kum 6:20-25); na halafu ilikuwa dhahiri katika
haggadah ya kiyahudi, yaani katika mazungumzo simulizi yaliyopo katika ibada ya karamu ya
kipasaka. Zaidi, Zaburi moja inakutilia mkazo kutangaza imani katika familia; “Mambo tuliyoyasikia
na kuyafahamu, ambayo baba zetu walituambia, hayo hatutawaficha wana wao; huku
tukiwaambia kizazi kingine, sifa za Bwana na nguvu zake, na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.
Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, na sheria aliiweka katika Israeli, aliyowaamuru baba zetu
wawajulishe wana wao; ili kizazi kingine wawe na habari, ndio hao wana watakaozaliwa.
Wasimame na kuwaambia wana wao” (Zab 78:3-6). Kwa hiyo, familia ni mahali ambapo wazazi
wanakuwa ni walimu wa kwanza wa imani kwa wana wao. Si huduma ya hadhara, bali ya mtu kwa
mtu: “Itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni [...] utamwambia ...”(taz. Kut 13:14). Hivyo,
vizazi tofauti vitamwimbia Bwana wimbo wao, “vijana waume, na wanawali, wazee, na watoto”
(Zab 148:12).
17. Ni wajibu wa wazazi kutimiza kwa makini utume wa kulea, kama wanavyofundisha mara nyingi
wenye hekima wa Biblia (Mit 3:11-12; 6:20-22; 13:1; 22:15; 23:13-14; 29:17). Wana wanaitwa
kushika na kutimiza amri: “Waheshimu baba yako na mama yako” (Kut 20:12); pale ambapo
kitenzi “kuheshimu”, maana yake ni kutekeleza kwa utimilifu wajibu wao wa kifamilia na wa kijamii,
bila kuuacha kwa visingizio vya kidini (taz. Mk 7:11-13). Maana, “Amheshimuye baba yake
atafanya upatanisho wa dhambi, naye amtukuzaye mama yake huweka akiba iliyo azizi” (YbS 3:3-
4)
18. Injili inatukumbusha pia kwamba wana si mali ya familia, bali wao wana mwendo ulio wa
pekee kwa ajili ya maisha yao ya mbeleni. Ni kweli kuwa Yesu amejionyesha kama mfano wa utii
kwa wazazi wao wa kidunia, maana “alikuwa akiwatii” (taz. Lk 2:51); lakini kwa hakika

1.10 Page 10

▲back to top
10
ameonyesha pia kwamba mwana kuchagua njia yake ya kuishi, na wito wake wa kikristo pia,
kunaweza kudai ajitenge ili kutimiliza kujitoa kwake kwa ajili ya Ufalme wa Mungu (taz. Mt 10:34-
37; Lk 9:59-62). Yesu mwenyewe, alipokuwa na umri ya miaka kumi na miwili, aliwajibu Maria na
Yosefu kuwa yeye ana utume wa juu zaidi wa kutimiza, licha ya kuheshimu familia yake ya kidunia
(taz. Lk 2:48-50). Ndiyo sababu anasisitiza kwamba inabidi kuwa na vifungo vingine, vya kina
zaidi, hata katika mahusiano ya kifamilia: “Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno
la Mungu na kulifanya” (Lk 8:21). Zaidi, ingawa katika jamii ya kale ya Mashariki ya Kati watoto
walikuwa wakifikiriwa kama wasio na haki maalumu na kama sehemu ya mali za ukoo, ni kweli
kwamba Yesu anawaangalia sana, kiasi cha kuwatambulisha mbele ya watu wazima kama walimu
wao, kutokana na watoto kuwategemea wengine kwa moyo safi na kwa hiari: “Amin, nawaambia:
Msipoongoka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Basi, yeyote
ajinyenyekeshaye mwenyewe kama Mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa
mbinguni” (Mt 18:3-4)
Njia ya mateso na kumwaga damu
19. Hali ya kupendana sana inayodhihirishwa katika Zaburi 128, haifuti hali nyingine
inayoonyeshwa katika Maandiko Matakatifu yote, yaani uwepo wa huzuni, maovu, ujeuri, vitu
vinavyorarua maisha ya familia na ushirika wake wa uhai na upendo. Ndiyo sababu, hata
mazungumzo ya Yesu juu ya ndoa (taz. Mt 19:3-9) yamo ndani ya majadiliano juu ya talaka. Neno
la Mungu ni shahidi daima juu ya kweli hii ya giza ambayo asili yake inapatikana mwanzoni, pale
ambapo kwa sababu ya dhambi, uhusiano wa upendo na usafi wa moyo kati ya mwanaume na
mwanamke umegeuka kuwa utawala: “Tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala” (Mwa
3:16).
20. Ni njia ya mateso na kumwaga damu inayopatikana katika kurasa nyingi za Biblia, kuanzia
ukatili wa Kaini juu ya ndugu yake Abeli, na mabishano mengi kati ya wana na kati ya wake wa
mababu Ibrahimu na Isaka na Yakobo, hadi kufikia misiba ya umwagaji damu iliyokumbana sana
na familia ya Daudi, na shida za kifamilia zinazopatikana katika simulizi la kitabu cha Tobiti, au
ungamo la Ayubu alipoachwa na wengine: “Ndugu zangu wamejiepusha nami, na wanijuao
wametengwa nami kabisa. [...] Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu, nami ni
machukizo kwa watoto wangu” (taz. Ayu 19:13,17)
21. Yesu mwenyewe amezaliwa katika familia ya hali ya chini; na mapema walipaswa kukimbia
kwenda katika nchi ya kigeni. Yeye anaingia nyumbani kwa Petro, ambapo mkwewe amelala,
hawezi homa (taz. Mk 1:30-31); na kukubali kushirikishwa katika msiba wa kifo nyumbani kwa
Jairo na nyumbani kwa Lazaro (taz. Mk 5:22-24,35-43; Yn 11:1-44). Anasikiliza kilio cha mjane wa
Naini mbele ya maiti ya mwanae (taz. Lk 7:11-15), na kupokea ombi la baba wa kijana mwenye
kifafa kwenye kijiji kidogo cha mashambani. (taz. Mk 9:17-27; Lk 17:14-20). Anakutana na watoza
ushuru kama Matayo na Zakayo nyumbani kwao (taz. Mt 9:9-13; Lk 19:1-10), na wenye dhambi,
kama yule mwanamke aliyeingia katika nyumba ya Farisayo (taz. Lk 7:36-50). Anajua mahangaiko

2 Pages 11-20

▲back to top

2.1 Page 11

▲back to top
11
na mivutano vilivyopo katika mazingira ya familia, na anavitumia anapotunga mifano: kama vile
wana wanaoacha nyumba yao ili kuishi maisha ya vituko (taz. Lk 15:11-32), au wana wagumu
wenye mienendo isiyoelezeka (taz. Mt 21:28-31), au wanaodhulumiwa kwa ukatili (Mk 12:1-9). Au,
tena, anajali mafanikio ya arusi, inapojitokeza shida ya divai kuwatindikia (taz. Yn 2:1-10), au ya
walioalikwa kukataa kuishiriki (taz. Mt 22:1-10); naye anafahamu jinsi familia iliyo maskini
inavyopata wasiwasi inapopoteza sarafu moja (taz. Lk 15:8-10).
22. Hata kwa muhtasari mafupi hayo, tunaweza kuona kuwa Neno la Mungu si mlolongo wa
dhana za kinadharia, bali ni mwenzi katika safari hata kwa familia zenye migogoro au huzuni, na
kuonyesha kwao kikomo cha safari, Mungu “atakapofuta kila chozi katika macho yao, wala mauti
haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena” (Ufu 21:4).
Taabu ya mikono yako
23. Mwanzoni mwa Zaburi 128, baba anaonekana kuwa mfanyakazi ambaye kwa kazi ya mikono
yake anaweza kutegemeza ustawi na usalama wa familia yake, “Taabu ya mikono yako utaila,
utakuwa heri, na kwako kwema” (Zab 128:2). Kwamba kazi ni sehemu muhimu sana ya hadhi ya
maisha ya wanadamu, ni fikra tunayoipata katika kurasa za kwanza za Biblia, pale ambapo
imeandikwa, “Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na
kuitunza” (Mwa 2:15). Ni picha ya mfanyakazi ambaye, kwa kulima ardhi na kwa kutumia nguvu za
vilivyoumbwa, anazalisha “chakula cha taabu” (Zab 127:2), pamoja na kustawisha karama zake
mwenyewe.
24. Wakati huohuo, kazi inawezesha kupata maendeleo ya jamii, riziki kwa ajili ya familia, pamoja
na uthabiti wake na uzaaji wake: “Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; Naam,
ukawaone wana wa wanao.” (Zab 128:5-6). Tena, kitabu cha Mithali kinatuonyesha wajibu wa
mama wa familia, ambaye kazi yake ya kila siku inaelezwa kinaganaga; nayo ni sababu ya mume
na wana wake kumsifu (taz. Mit 31:10-31). Mtume Paulo mwenyewe alijisifu kwa sababu ya
kutowalemea wengine, kwa kujipatia riziki kwa njia ya kazi ya mikono yake (taz. Mdo 18:3; 1Kor
4:12; 9:12). Alikuwa na uhakika kwamba kufanya kazi ni kitu cha lazima, kiasi cha kuweka sheria
kali hii kwa jumuiya zake: “Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula” (2The 3:10; taz.
1The 4:11).
25. Kutokana na hayo, inaeleweka kuwa kukosa ajira au kutokuwa na uhakika wa kazi
kunasababisha taabu, kama kinavyoonyesha kijitabu cha Ruthu na kama anavyokumbusha Yesu
katika mfano wa vibarua waliosimama sokoni bila kazi (taz. Mt 20:1-16), au kama alivyoonja Yeye
mwenyewe mara nyingi alipokutana na watu maskini na wenye njaa. Hiyo ndiyo balaa
inayojitokeza kwenye jamii katika nchi nyingi; na huko kukosa kazi kunaathiri amani ya familia kwa
namna mbalimbali.
26. Wala hatuwezi kusahau upotovu ambao dhambi huingiza katika jamii, wanadamu

2.2 Page 12

▲back to top
12
wanapokandamiza viumbe vya dunia, kwa kuharibu mazingira, na kuvitumia viumbe kwa faida
yake binafsi na kwa ukatili pia. Athari ya hayo ni hali ya ujangwa wa ardhi (taz. Mwa 3:17-19) na
wakati huohuo tofauti zisizo za haki za kiuchumi na kijamii, ambazo dhidi ya hizo sauti ya manabii
imevuma wazi, kuanzia Eliya (taz. 1Fal 21), hadi maneno aliyosema Yesu mwenyewe dhidi ya
udhalimu (taz. Lk 12:13-21; 16:1-31).
Upole wa kukumbatia
27. Kristo ameweka kama sifa bainishi ya wanafunzi wake hasa sheria ya upendo na ya kujitoa
nafsi kwa ajili ya wengine (taz. Mt 22:39; Yn 13:34); naye amefanya hilo kwa msimamo ambao
baba au mama hushuhudia kwa kawaida katika maisha yao: “Hakuna aliye na upendo mwingi
kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yn 15:13). Huruma na msamaha pia
ni matunda ya upendo. Ishara dhahiri ya hayo ni sura ya yule mama mzinifu penye mahali pa
hekalu la Yerusalemu, ambaye, washtaki wake wakiisha kumzunguka, akabaki peke yake tu
pamoja na Yesu ambaye hakumhukumu, akamhamasisha kuishi maisha maadilifu zaidi (taz. Yn
8:1-11).
28. Katika upeo wa upendo, ulio kiini cha mang’amuzi ya kikristo katika ndoa na familia, ina
umuhimu fadhila nyingine inayosahauliwa mara nyingi katika nyakati hizi za mahusiano ya haraka
haraka na ya juujuu: moyo mpole. Tuangalie Zaburi ya 131, ambayo ni mwanana na imejaa
maana. Kama inavyopatikana pia katika matini nyinginezo, (taz. Kut 4:22; Isa 49:15; Zab 27:10),
muungano wa mwamini na Bwana wake unadhihirishwa kwa sifa za upendo wa kibaba na wa
kimama. Katika hiyo Zaburi ya 131, unaonekana uhusiano wa undani, wa upendo mwanana na
mpole, unaounganisha mama na mtoto wake mchanga aliyelala mikononi mwake alipokwisha
kunyonyeshwa. Ni mtoto aliyekwisha kuachishwa, kulingana na maana ya neno la kiebrania
gamul, ambaye kwa utambuzi anamshika mama yake anayemwinua kifuani pake. Ni uhusiano wa
undani wenye utambuzi, wala si tu wa kimaumbile. Kwa hiyo mzaburi anaimba, “Hakika
nimeituliza nafsi yangu na kuinyamazisha; kama mtoto aliyeachishwa kifuani mwa mama yake”
(taz. Zab 131:2). Sambamba na hayo, tunaweza kufikiria sura nyingine, ambapo nabii Isaya
anaweka maneno haya yenye kugusa moyo midomoni mwa Mungu, kama baba, “Israeli
alipokuwa mtoto, nalikuwa nakipenda [...] Nalimfundisha Efraimu kwenda kwa miguu;
naliwachukua mikononi mwangu [...] Naliwavuta kwa kamba za kibinadamu, kwa mafungo ya
upendo; nami nalikuwa kwao kama baba amwinuaye mtoto mchanga mpaka shavuni mwake,
nikaandika chakula mbele yao” (taz. Hos 11:1-4).
29. Kwa mtazamo huu, wenye imani na upendo, neema na bidii, unaounganisha familia ya
kibinadamu na Utatu wa kimungu, tunatazama fumbo la familia ambalo Neno la Mungu
anawakabidhi baba na mama na watoto ili waunde ushirika wa watu ulio mfano wa umoja wa
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Tena, kazi ya kuzaa na ya kulea, inaakisi kazi ya Mungu ya
kuumba. Wanafamilia wanaitwa kushirikishana sala ya kila siku, somo la Neno la Mungu na
komunyo ya Ekaristi ili kukuza upendo na kugeuka kuwa zaidi na zaidi kwa pamoja hekalu

2.3 Page 13

▲back to top
13
anamokaa Roho.
30. Kila familia ina mbele ya macho yake mfano wa familia ya Nazareti, pamoja na maisha yake
ya kila siku yenye taabu na hata majinamizi, kwa mfano walipoteswa kwa ukatili usioeleweka wa
Herode; nalo ni msiba unaoendelea kutokea hadi leo kwa familia nyingi za wakimbizi
wanaokataliwa na wasio na msaada. Sawa na mamajusi, familia zinaitwa kumtazama Mtoto
pamoja na Mamaye, kusujudu na kumwabudu (taz. Mt 2:11) Sawa na Maria, zinahimizwa
kukabiliana kwa ujasiri na amani na changamoto za kifamilia, na kutunza na kutafakari moyoni
mambo ya ajabu ya Mungu (taz. Lk 2:19,51). Katika hazina ya moyo ya Maria, pana matukio yote
ya kila moja ya familia zetu, ambayo yeye anatunza kwa upendo angalifu. Ndiyo sababu anaweza
kusaidia kutoa fasili ya hayo matukio, ili kutambua ujumbe wa Mungu katika maisha ya familia.
SURA YA PILI
HALI HALISI NA CHANGAMOTO ZA FAMILIA
31. Ustawi wa familia ni jambo la msingi kwa mustakabali wa ulimwengu na Kanisa Chambuzi
nyingi sana zimefanyika kuhusu ndoa na familia, matatizo yao na changamoto za nyakati zetu. Ni
vizuri kuangalia kwa makini hali halisi, kwa sababu “wito na maagizo ya Roho yapatikana pia
katika matukio ya historia”. Kupitia matukio hayo “Kanisa linaweza kuongozwa kulielewa kwa kina
zaidi fumbo lisilo na mwisho la ndoa na familia”.[8] Sina nia ya kuainisha na kufafanua hapa yale
yote yahusuyo familia katika mazingira ya sasa. Lakini, kwa vile Mababa wa Sinodi walichangia
uchambuzi wa hali halisi ya familia toka pande zote za dunia, naona vema kati ya michango yao
ya kichungaji niipokee mingine, na kuongeza mawazo mengine yanayotokana na mtazamo wangu
mimi.
Hali halisi ya familia wakati huu
32. “Huku tukiwa waaminifu kwa mafundisho ya Kristo tunaangalia hali halisi ya familia wakati huu,
katika mchangamano wa miali yake ya mwanga na vivuli vya giza. […] Mabadiliko ya
kianthropolojia na kitamaduni yanaathiri leo hali zote za maisha na kudai yatazamwe kwa kutumia
mbinu mbalimbali za kiuchambuzi”.[9] Katika mazingira ya karibu miaka arobaini iliyopita
Maaskofu wa Hispania tayari walikuwa wakitambua kwamba katika maisha ya nyumbani kulikuwa
na uhuru zaidi, na "majukumu, uwajibikaji na kazi ziligawiwa kwa usawa zaidi [...] Kwa kuthamini
zaidi mawasiliano ya ndani na ya kiutu kati ya wanandoa, maisha ya kifamilia yanakuwa na utu
zaidi [...]. Wala jamii tunamoishi wala tunapoelekea inaruhusu tuendeleze mitindo na mifumo ya
zamani bila kuichambua”.[10] Lakini “tunafahamu mwelekeo mkuu wa mabadiliko ya
kianthropolojia na kitamaduni, ambayo yanasababisha watu binafsi wasiweze kuutegemea kama
zamani msaada wa jamii kwa maisha yao ya kifamilia”.[11]
33. Kwa upande mwingine, ni lazima kuzingatia pia hatari inayozidi kuongezeka kutokana na

2.4 Page 14

▲back to top
14
ubinafsi wa kupita kiasi, unaopotosha mahusiano ya kifamilia hadi kusababisha kumtazama kila
mwanafamilia kuwa sawa na kisiwa, ukishabikia, mara nyingine, picha ya mtu anayejijenga kadiri
ya mapenzi yake yanayochukuliwa kama pekee yenye maana”.[12] “Migogoro inayosababishwa
na utamadumi unaotukuza ubinafsi wa kumiliki mali na wa kula raha inazaa ndani ya familia hali
ya kutovumiliana na kushambuliana”.[13] Ningependa kuongeza mchakamchaka wa maisha ya
sasa, uchovu unaotokana na kubanwa na kudaiwa kila wakati, mfumo wa jamii na wa utendaji
kazi, kwa sababu ni tamaduni zinazohatarisha uwezo wa kuwa na chaguo la kudumu. Wakati
huohuo tunaona kwamba kuna mambo yanayoweza kuchukua sura mbili. Kwa mfano,
yanathaminiwa zaidi malezi yanayomwezesha mtu kuwa na msimamo wake halisi kuliko kuiga
tabia iliyokwisha pangwa. Ni tunu iwezayo kuviendeleza vipaji tofauti na uhuru wa kutenda, lakini
ikielekezwa vibaya, inaweza kuzaa tabia ya kutoaminiana, kukwepa majukumu, kujifungia katika
starehe, ubabe. Uhuru wa kuchagua unamwezesha mtu kuweka malengo katika maisha yake na
kukuza kilicho bora ndani yake, lakini, bila malengo safi na nidhamu, huharibika na kupoteza
uwezo wa kujitoa kwa ukarimu. Tukiangalia hali halisi, katika nchi nyingi ambapo idadi ya ndoa
inapungua, inaongezeka idadi ya watu wanaoamua kuishi peke yao, au wanaoshirikiana bila
kukaa pamoja. Tunatambua pia kwamba watu huitafuta zaidi haki, Lakini kama jambo hilo
halieleweki vizuri, raia wanageuzwa kuwa wateja wanaodai tu kupewa huduma.
34. Hatari hizi zikiathiri namna ya kuielewa familia, familia yenyewe inaweza kugeuzwa kuwa
mahali pa kupitia tu, mahali pa kukimbilia inapoonekana kuna manufaa binafsi, au ambapo mtu
anakwenda kwa kudai haki zake, na wakati huo vifungo vinavyounganisha wanafamilia
vinasahauliwa kwa kutegemea tamaa geugeu na mazingira tu. Kimsingi, leo ni rahisi kuchanganya
uhuru halisi na itikadi ya kuwa kila mmoja huweza kuamua kadiri anavyopenda, kana kwamba
kilicho na maana ni mtu binafsi tu, hakuna tena ukweli, tunu, na misingi inayotuelekeza, kana
kwamba mambo yote ni sawa na kila kitu kinaruhusiwa. Katika mazingira hayo, tarajio la ndoa,
likiwa na jukumu la chaguo pekee na la kudumu, linafutwa kwa kuzingatia marupurupu ya papo
kwa hapo au matamanio ya kipuuzi. Watu huogopa upweke, hutamani mahali penye usalama na
uaminifu, lakini wakati huohuo hofu ya kufungwa katika uhusiano unaoweza kuchelewesha
mafanikio ya matamanio binafsi hukua.
35. Kama wakristo hatuwezi kuacha kupendekeza maisha ya ndoa kwa lengo ya kutopingana na
mawazo ya kisasa, kwa kufuata mitindo, au kwa sababu tunaona hatuna nguvu za kupambana na
mmomonyoko wa maadili na wa utu. Tungefanya hivyo tungeinyima dunia tunu ambazo tunaweza
na tunapaswa kuitolea. Kwa kweli, haina maana kubaki kuyalaumu tu maovu yanayotendeka kana
kwamba kwa kufanya hivyo tungeweza kubadili kitu. Wala haisaidii kutaka kuzilazimisha sheria
kwa nguvu ya mamlaka. Tunadaiwa kuwa na juhudi yenye uwajibikaji na yenye ukarimu zaidi,
yaani kueleza mantiki na sababu za kuchagua ndoa na familia, hivyo watu wawe tayari zaidi
kuitikia kwa neema wanazopewa na Mungu.
36. Wakati huohuo inatupasa kuwa wanyenyekevu na wenye kuzingatia uhalisia ili tuweze kukiri
kwamba namna yetu ya kueleza mafundisho ya kikristo na namna yetu ya kuwatendea watu

2.5 Page 15

▲back to top
15
imesaidia kuyasababisha yale ambayo leo tunayalaumu, hivyo inabidi na inafaa tujichunguze sisi
wenyewe. Mara nyingi tulipokuwa tunalijadili suala la ndoa tulikuwa kama tunaliweka pembeni
lengo lake la kuwa kitu kimoja, wito wa kukua katika upendo na shabaha ya kusaidiana, na
kuweka msisitizo, kama si msisitizo pekee, kwa jukumu la kuzaa. Wala hatukuwasindikiza vizuri
wanandoa wapya katika miaka yao ya mwanzo wanapoanza maisha ya ndoa, hatukujali taratibu
zao, msamiati wao na mahangaiko yao halisi na ya kawaida. Mara nyingine tumeeleza
mafundisho ya kidini yanayohusu ndoa kinadharia mno, kama mchezo wa kiakili tu, mbali na
mazingira halisi na uwezo halisi wa familia jinsi zilivyo. Namna hii ya kiitikadi mno, hasa kama
hatujachochea roho ya kuitegemea neema ya Mungu, haijasaidia watu wavutiwe na watamani
maisha ya ndoa, bali kinyume chake.
37. Kwa muda mrefu tuliamini kwamba kwa kusisitiza tu masuala ya kiitikadi na ya kimaadili bila
kuelekeza kujikabidhi kwa neema ya Mungu, tumeshazisaidia ya kutosha familia, kuimarisha
muungano wa wanaarusi, na kuyajazia na maana kubwa maisha yao ya pamoja. Tuna ugumu
zaidi kueleza ndoa kama mchakato, kama safari ya kuelekea ukomavu na utimilifu, kuliko kama
mzigo wa kuubeba kwa uvumilivu kwa maisha yote. Hatujawa wepesi pia kuziachia nafasi dhamiri
za waamini, ambao mara nyingi wanaitikia vizuri jinsi wanavyoweza wito wa Injili katika mipaka ya
udhaifu wao na wanaweza kuendeleza upambanuzi wao katika nafsi yao mbele ya mazingira
ambapo mifumo yote imefumuka. Tunaitwa kuzilea dhamiri, wala si kuzichukua nafasi zao.
38. Lazima tushukuru kwa sababu watu walio wengi wanayaheshimu mahusiano ya kifamilia
yanayolenga kudumu na yanayohakikisha heshima kwa kila mmoja. Hivyo inapendezwa Kanisa
linapokuwa na nafasi ya kusindikiza na kusaidia katika masuala yahusuyo kukua katika upendo,
kufikia mwafaka katika migogoro na malezi ya watoto. Wengi hutambua nguvu wanayopewa na
neema inayopatikana katika sakramenti ya Upatanisho na ya Ekaristi, nguvu hii huwezesha
kupambana na changamoto za ndoa na familia. Katika nchi nyingine, hasa katika sehemu nyingi
za Afrika, mfumo wa kumweka Mungu pembeni haujafaulu kudhohofisha tunu za jadi na katika kila
ndoa koo mbili zinaungana kwa nguvu, na hivyo huwa na mfumo unaoeleweka wa kutatua
migogoro na shida. Katika dunia ya leo inathaminiwa pia ushuhuda wa watu wa ndoa ambao si
kwamba walidumu katika ndoa yao kwa muda mrefu tu, lakini pia huendelea na mpango wao wa
pamoja na hudumu katika kupendana. Hali hiyo inafungua mlango kwa kazi ya kichungaji yenye
lengo la kujenga, yenye tabia ya kupokea kwa ukarimu, na hivyo kuwezesha kupiga hatua katika
kuyaelewa kwa kina zaidi majukumu yatokanayo na Injili. Hata hivyo, mara nyingi tumetenda
kama kwa kujihami na tunapoteza nguvu za kiuchungaji kwa kuishambulia dunia inayopotea,
tukiwa na uwezo mdogo tu wa kuwaelekeza watu katika njia ziendazo kwenye furaha. Wengi
hawatambui kwamba mafundisho ya Kanisa kuhusu ndoa na familia yametokana wazi na mahubiri
na mwenendo wa Yesu, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa akipendekeza lengo linalowajibisha
bila kuacha kamwe kuwa karibu na watu wadhaifu kama mwanamke Msamaria au mwanamke
aliyefumaniwa katika uzinzi.
39. Hilo halina maana ya kutotambua mmomonyoko wa kiutamaduni unaofifisha upendo na moyo

2.6 Page 16

▲back to top
16
wa kujitolea. Maoni yaliyotolewa kabla ya Sinodi mbili za mwisho yameibua dalili mbalimbali za
"utamaduni wa yaliyo ya muda tu”. Kwa mfano, tunaona jinsi watu wanavyobadilisha wapenzi wao
haraka. Wanaamini kwamba upendo, kama inavyotokea katika mitandao ya kijamii, anaweza
kuufunga au kuufungua anavyotaka mlaji na hata kuusimamisha ghafla. Ninawazia pia hofu
inayowaingia watu wanapofikiria juu ya majukumu ya kudumu, hali ya kutingwa na wazo la kuwa
na muda wa kutumia binafsi tu, mahusiano yaliyo kama ya kibiashara kwa kupima mapato na
matumizi na ambayo yanadumu yakiwa tu kama njia ya kuukwepa upweke, kuwa na usalama au
kupata huduma fulani. Mahusiano ya kimapenzi kati ya watu yanakuwa kama mahusiano kati ya
watu na vitu, kati ya watu na mazingira: yote yaweza kutupwa, kila mmoja hutumia na kutupa,
hutumia bila kiasi na kuharibu, hunyonya na kukamua mpaka kushiba. Na baadaye basi, nenda
zako! Tabia ya kinarchizo hufanya watu washindwe kuangalia zaidi ya mipaka yao, matamanio
yao na haja zao. Lakini atumiaye wengine hatimaye naye pia atatumiwa, atarubuniwa na kuachwa
kwa mtindo huohuo. Ni jambo la kutafakari kwamba mahusiano yanavunjika mara nyingi kati ya
watu wazima ambao wanatafuta namna fulani ya "kujitegemea (uhuru)” na wanakataa wazo la
kuzeeka pamoja kwa kutunzana na kutegemezana.
40. "Ingawa kuna hatari ya kuongea kijuujuu, tunaweza kusema kwamba tunaishi katika
utamaduni unaowasukuma vijana wasijenge familia, kwa sababu wanakosa uwezo kwa siku zao
za mbele. Lakini utamaduni huohuo kwa wengine unawapatia machaguo mengi kiasi kwamba wao
pia hushawishiwa kutojenga familia”.[14] Katika nchi nyingine vijana wengi wanasukumwa
kuahirisha ndoa yao kwa sababu ya shida za kiuchumi, za kikazi, au za kimasomo. Mara nyingine
kwa sababu zingine pia, kama vile ushawishi wa itikadi zinazoishusha hadhi ya ndoa na familia,
kuogopa kushindwa kwa kuona walivyoshindwa wengine katika ndoa yao, hofu mbele ya jambo
ambalo wanaliona zito mno na takatifu, fursa za kijamii na unafuu wa kiuchumi zinazotokana na
kuishi pamoja bila kufunga ndoa, kuelewa upendo kama jambo la kihisia tu, hofu ya kupoteza
uhuru na uwezo wa kujitegemea, kukataa jambo linaloonekana kama la kitaasisi na lenye
urasimu”.[15] Tunahitaji kupata maneno, sababu na ushuhuda zitakazotusaidia kuwagusa mpaka
ndani kabisa vijana pale ambapo wana uwezo zaidi wa kuwa na ukarimu, na ari, na upendo, na
hata kuwa na ushujaa, ili kuwaalika wakubali kwa moyo wa furaha na kwa ushupavu changamoto
ya ndoa.
41. Mababa wa Sinodi wamejadili kuhusu hali ya sasa ambapo “mielekeo ya kitamaduni ni kama
inataka kulazimisha mapenzi bila mipaka [...], mapenzi ya kutafuta faida binafsi, yasiyo ya kudumu
na yenye kubadilika, ambayo hayawasaidii watu kufikia ukomavu mkubwa zaidi”. Wamesema
kwamba wanahangaika na “hali ya kuenea kwa ponografia (picha za ngono) na biashara ya mwili,
kunakochangiwa hata na matumizi mabaya ya mtandao wa intaneti, na “hali ya watu kulazimishwa
kufanya ukahaba”. Katika mazingira haya, “majozi mara nyingine yanayumba, yanasita na
yanapata shida kuona njia ya kukua. Wengi wanaelekea kubaki katika hatua za chini kabisa
kimihemuko na kimapenzi. Mgogoro katika jozi unayumbisha familia, na kutokana na matengano
na talaka, athari kubwa zinawapata watu wazima, watoto na jamii, na hivyo hudhoofisha mtu na
mahusiano ya kijamii”.[16] Migogoro ya wanandoa mara nyingi inakabiliwa “juujuu na bila ushujaa

2.7 Page 17

▲back to top
17
wa subira, wa uchambuzi wa kina, wa kusameheana, wa upatanisho na wa sadaka pia. Basi,
kuvunjika kwa ndoa kunaanzisha mahusiano mengine, majozi mwngine, miungano mingine na
ndoa nyingine, na hivyo kunasababisha hali ya kifamilia kuwa ngumu na yenye utata kwa chaguo
la kikristo”.[17]
42. “Hata kushuka kwa idadi ya vizazi kunakotokana na fikra na mitazamo ya kupunguza uzazi
iliyoenezwa na sera za kiulimwengu juu ya afya ya uzazi, si tu kwamba kunatengeneza mazingira
ambamo kubadilishana kwa vizazi hakuna uhakika, bali kuna hatari ya kutufikisha kwenye zama
za umaskini mkubwa wa kiuchumi na kupoteza matumaini ya wakati ujao. Maendeleo ya
kibioteknolojia nayo yameathiri sana uzazi.[18] Tunaweza kuorodhesha mambo mengine kama
"maendeleo ya viwanda, mapinduzi ya kijinsia, hofu ya ongezeko la idadi ya watu, matatizo ya
kiuchumi, [...]. Jamii ya kiulaji inaweza pia kuwashawishi watu wasizae watoto ili wabaki na uhuru
wao na mtindo wao wa maisha”.[19] Ni kweli kwamba dhamiri sahihi ya wanandoa, baada ya
kupata watoto wengi, inaweza kuwaelekeza kuchukua uamuzi wa kuweka mipaka katika idadi ya
watoto kwa sababu zilizo za msingi, lakini “Kanisa daima kwa kuipenda heshima hii ya dhamiri
linakataa kwa nguvu zake zote hatua za serikali zinazowalazimisha watu kuzuia mimba, kufunga
njia ya uzazi au hata kuiharibu mimba”.[20] Hatua hizi hazikubaliki kamwe hata pale ambapo watu
wanazaa sana, lakini tunaona kwamba wanasiasa wanazishinikiza hatua hizo hata pale ambapo
kuna janga la ongezeko kidogo mno la watu. Kama walivyosema maaskofu wa Korea, “namna hii
ya kutenda inajipinga yenyewe na inakwepa majukumu”.[21]
43. Katika jamii nyingine kudhoofika kwa imani na kwa ushiriki katika ibada kunaathiri familia na
kuziacha pweke wanapokabiliana na matatizo yao. Mababa wanasema kwamba “katika
utamaduni wa leo upweke ndio sura kuu mmojawapo wa umaskini, nao unasababishwa na
kumweka Mungu mbali na maisha ya watu, pia na udhaifu wa mahusiano. Kuna pia hisi ya jumla
ya kutoweza kitu mbele ya hali halisi ya kijamii na kiuchumi, ambayo, mara nyingi, inafikia hatua
ya kuzigandamiza familia. […] Mara nyingi familia zinajihisi kuwa zimeachwa kwa sababu ya
kutojali na mapungufu ya uangalifu kwa upande wa taasisi. Matokeo hasi, kwa mtazamo wa
mpangilio wa kijamii, ni wazi: kuanzia mpunguo wa kupita kiasi wa uzazi na shida katika kulea,
ugumu wa kupokea kuzaliwa kwa mtoto, kuwaona wazee kama mzigo, hadi kuenea kwa fadhaa
za kimapendo zinayoweza kumfikisha mtu hata katika kutenda ukatili. Ni wajibu wa Serikali ya
Nchi kutunga sheria na kuongeza nafasi za ajira ili kuhakikisha mustakabali mzuri kwa vijana, na
kuwasaidia kutekeleza mpango wa kuunda familia yao”.[22]
44. Kukosa makazi yenye hadhi au yanayofaa mara nyingi kunasababisha kuahirisha kuweka
uhusiano katika mfumo ulio rasmi. Lazima tukumbuke kwamba “familia ina haki ya kuwa na
makazi yenye hadhi, yanayofaa kwa maisha ya familia na yanayolingana na idadi ya wanafamilia,
katika mazingira yenye huduma za msingi kwa ajili ya familia na jumuiya”.[23] Familia na nyumba
ni mambo yanayoendana. Mfano huo unatuonyesha kwamba inatupasa kusisitiza haki za familia,
na si haki za mtu binafsi tu. Familia ni tunu ambayo haiwezi kukosekana katika jamii, lakini
inahitaji kulindwa.[24] Utetezi wa haki hizo “ni wito la kinabii kwa ajili ya familia kama taasisi,

2.8 Page 18

▲back to top
18
ambayo lazima iheshimiwe na ilindwe na kila aina ya unyanyasaji,[25] hasa katika mazingira ya
sasa ambapo kawaida ina nafasi ndogo katika sera ma mipango ya kisiasa. Kati ya haki zingine
familia zina haki “ya kutegemea mamlaka ya kiraia iandae na kusimamia sera ya familia inayofaa
katika nyanja ya sheria, uchumi, jamii na kodi”.[26] Mara nyingine familia inapata mahangaiko ya
kutatanisha wakati mpenzi wao unaugua, lakini hawawezi kupata huduma ya kiafya inayofaa, au
wanapobaki muda mrefu bila kupata ajira yenye hadhi. “Masharti ya kiuchumi yanazinyima familia
uwezekano wa kupata elimu na kushiriki vizuri maisha ya kiutamaduni na ya kijamii. Mfumo wa
uchumi wa sasa unasababisha familia zikataliwe na jamii kwa namna nyingi. Kwa namna ya
pekee familia zinaumia kwa sababu ya shida zinazohusiana na kazi. Nafasi wanazopewa vijana ni
chache na nafasi za ajira zina masharti mengi na ni za wasiwasi. Saa za kazi kwa siku ni nyingi na
mara nyingi mtu hutumia muda mrefu kwa kusafiri kufika kazini. Hali hii haisaidii wanafamilia
wakutane wao kwa wao na pamoja na watoto wao ili kuustawisha kila siku mahusiano kati
yao”.[27]
45. Katika baadhi ya nchi, watoto wanaozaliwa nje ya ndoa ni wengi, na wale ambao baadaye
wanalelewa na mzazi mmoja au katika mazingira ya familia pana au yaliyoundwa upya, nao ni
wengi. […] Moja ya kashfa kubwa na jambo linalodhihirisha kupotoka kwa jamii ya sasa ni
udhalilishaji wa kingono wa watoto. Hata jamii zilizojeruhiwa kwa vita, ugaidi au kuwepo kwa
mfumo wa uhalifu, zinajikuta zikiwa katika hali ya kifamilia iliyodhoofika, na hasa katika miji
mikubwa na pembezoni mwake idadi ya watoto wanaoitwa ‘wa mitaaani’ inazidi
kuongezeka”.[28] Ubakaji wa watoto unakuwa kashfa kubwa zaidi ikitokea pale ambapo watoto
waliwekwa ili walindwe: familia, shule, jumuiya na taasisi za kikristo.[29]
46. Uhamiaji “ni alama nyingine ya nyakati inayotakiwa kuangaliwa na kueleweka pamoja na
matokeo yake mazito kwa maisha ya familia”.[30] Sinodi ya mwisho imelipa suala hilo umuhimu
mkubwa, ikisema kwamba: “linayagusa, kwa namna tofauti, mataifa mengi, katika sehemu
mbalimbali duniani. Kanisa limekuwa mstari wa mbele katika kukabiliana nalo. Ulazima wa
kudumisha na kustawisha ushuhuda huu wa kiinjili (taz. Mt 25:35) leo inaonekana kama jukumu
nyeti kabisa. […] Kuhama kwa watu, ambalo ni jambo la kawaida katika historia ya mataifa,
kunaweza kuwa nafasi ya kujitajirisha kwa familia za wahamiaji na kwa wale wanaozipokea.
Jambo lingine, tofauti, ni uhamisho wa familia kwa kulazimishwa, kutokana na mazingira ya vita,
madhulumu, umaskini, udhalimu, uhamisho ulio na hatari nyingi safarini ambapo mara nyingi watu
wahatarisha maisha yao, wanachanganyikiwa, na familia zinavurugwa. Kuwasindikiza wahamiaji
kunadai kazi ya uchungaji ya pekee inayozielekea familia zinazohama, lakini pia wanafamilia
waliobaki nyumbani. Kazi hii lazima ifanyike kwa kuziheshimu tamaduni zao, malezi ya kidini na ya
kiutu ya mahali wanapotoka, utajiri wa kiroho wa ibada zao na mapokeo yao, pia kwa
kuwahudumia kwa matunzo ya kichungaji ya pekee. […] Uhamiaji unakuwa wa kusikitisha na
wenye maumivu makali kwa namna ya pekee unapokuwa haramu na wenye kutegemea mitandao
ya kimataifa ya wafanyabiashara ya watu. Vilevile kwa akinamama na watoto wasio na msaada,
wanaolazimishwa kukaa kwa muda mrefu kwenye makampi ya mapito, kwenye makampi ya
wakimbizi ambapo haiwezekani kabisa kujenga mtangamano wa maana. Umaskini wa kupindukia

2.9 Page 19

▲back to top
19
na mazingira mengine magumu kabisa mara nyingine yanawasukuma familia hata kuwauza
watoto wao kama malaya au kwa ajili ya biashara ya viungo”.[31] “Madhulumu ya wakristo na pia
ya makabila madogo au makundi mengine ya kidini, sehemu mbalimbali duniani, hasa Mashariki
ya Kati, huwa majaribu makubwa: si kwa Kanisa tu, bali pia kwa jumuiya nzima ya kimataifa.
Inapaswa kutegemeza kila juhudi inayolenga kuzisaidia familia na jumuiya za kikristo zibaki katika
maeneo yao ya asili”.[32]
47. Mababa waliangalia kwa umakini wa pekee pia “familia walio na walemavu, ambapo ulemavu
unaoibuka katika maisha yao unaleta changamoto kali na isiyotarajiwa, na huvuruga utulivu,
matamanio na matarajio. [...] Familia zinazopokea kwa upendo jaribio zito la kuwa na mtoto
mlemavu zinastahili pongezi kubwa. Zinatoa kwa Kanisa na kwa jamii ushuhuda wenye thamani
wa uaminifu kwa zawadi ya uhai. Familia itaweza kugundua, pamoja na jumuiya ya kikristo,
matendo mapya, msamiati mpya, namna ya kujielewa na kujitambua, katika safari ya kulipokea na
kulitunza fumbo la udhaifu. Walemavu kwa ajili ya familia wanakuwa kama zawadi na nafasi ya
kukua katika upendo, katika kusaidiana na katika umoja. [...] Familia inayopokea kwa jicho la
imani uwepo wa walemavu itaweza kuutambua na kuutetea ubora na tunu ya kila uhai, pamoja na
mahitaji yake, haki zake na fursa zake. Familia hiyo itahamasisha huduma na matunzo, na
itaendeleza ukaribu na mapendo, wakati wote wa maisha”.[33] Napenda kusisitiza kwamba
uangalifu unaotumika kwa ajili ya wahamiaji na walemavu ni dalili ya Roho. Hali hiyo ni kama ya
mfano: inaonyesha hasa jinsi leo tunavyojali mapokezi yenye huruma na mtangamano na watu
wadhaifu.
48. “Familia zilizo nyingi zinawaheshimu wazee, zinawapenda na kuwapokea kama baraka.
Pongezi wa pekee kwa mashirika na makundi ya kifamilia zinazofanya kazi kwa ajili ya wazee,
kwa upande wa kiroho na wa kijamii [...]. Katika jamii zenye viwanda vingi, ambapo idadi ya wazee
inazidi kuongezeka wakati idadi ya watoto inapungua, kuna hatari ya kuwachukua wazee kama
mzigo. Kwa upande mwengine matunzo wanayohitaji mara nyingi ni majaribu makubwa kwa
jamaa zao”.[34] “Kukithaminisha kipindi cha mwisho wa maisha, leo ni ya lazima zaidi kutokana na
kujaribu zaidi kuweka kando hatua ya kuaga dunia, kwa kutumia kila njia. Udhaifu na utegemezi
wa wazee mara nyingine hutumika kikatili kama nafasi ya kupata faida ya kiuchumi. Familia nyingi
zinatufundisha kwamba inawezekana kuzikabili hatua za mwisho wa maisha kwa kuthamini
maana ya utimilifu wa maisha katika fumbo la kipasaka. Idadi kubwa ya wazee wamepokelewa
katika taasisi za Kanisa ambapo huweza kuishi katika mazingira ya utulivu na ya kifamilia
wakipata huduma ya kiroho na ya kimwili. Kifo laini na kujiua kwa msaada ni vitisho vikali kwa
familia duniani kote. Katika nchi nyingi matendo hayo yamepata uhalali wa kisheria. Kanisa,
wakati linaposhupaa kuyapinga matendo hayo, linapokea jukumu la kuzisaidia familia zinazotunza
wazee na wagonjwa”.[35]
49. Nataka niweke wazi zaidi hali ya familia zinazogubikwa na unyonge, zinazobanwa kwa namna
nyingi, ambapo magumu ya maisha yanawasababishia majeraha makali. Wote tunayapata
matatizo, lakini katika nyumba iliyo maskini sana yanakuwa makali zaidi.[36] Kwa mfano, kama

2.10 Page 20

▲back to top
20
mama hulazimika kumlea mtoto peke yake, kwa sababu ya kutengana na mumewe au kwa
sababu nyingine, na anapofanya kazi hawezi kumwachia mtu mwengine, mtoto huyo atakua
katika upweke wa mazingira hatarishi, na kukomaa kwake kutaathirika. Katika hali ngumu ya
maisha inayowakabili watu wenye shida, Kanisa linapaswa kuwatunza kwa namna ya pekee kwa
kuwaelewa, kuwafariji, kuwashirikisha, bila kuwabana na sheria nyingi zinazoonekana kama
mzigo unawalemea, jambo ambalo lingewafanya watu kujisikia wamehukumiwa na kuachwa na
Mama yule ambaye kiukweli hutumwa kuwapelekea huruma ya Mungu. Kwa namna hiyo, badala
ya kuwapatia watu nguvu ya kuponya ya neema na mwanga unaotokana na Injili, wengine
wanataka kushinikiza “ufundishaji” wa Injili, na kuibadilisha kuwa “mawe yasiyo na uhai ya
kuwatupia wengine”.[37]
Changamoto nyingine
50. Majibu yaliyopatikana katika mashauriano mawili yaliyofanyika wakati wa maandalizi ya
Sinodi, yameonyesha mazingira na hali mbalimbali na tofauti sana zinazoleta changamoto mpya.
Zaidi ya zile zilizotajwa hapo juu, wengi waligusia kazi ya malezi, kazi ambayo ina shida kutokana
na kwamba, pamoja na sababu nyingine, wazazi wanarudi nyumbani hali wamechoka na hawana
hamu ya kuongea, katika familia nyingi hata desturi ya kula pamoja imepotea, na, zaidi ya kuwa
tegemezi wa televisheni, namna za kupoteza mawazo kwa kujiburudisha zinazidi kuongezeka.
Hali hii inasababisha kazi ya wazazi ya kuwarithisha imani watoto kuwa ngumu. Wengine
wameona kwamba mara nyingi familia ni kama zinaugua mfadhaiko mkubwa sana. Inaonekana
kama wanahangaika sana kuwaganga matatizo yajayo kuliko kushirikiana katika maisha ya leo.
Hali hii, ambayo ni suala la kiutamaduni, huwa mbaya zaidi kutokana na wasiwasi kuhusu ajira
kwa siku za mbele, kuyumba kwa uchumi, au hofu kwa maisha ya watoto siku za mbele.
51. Yameongelewa pia utegemezi unaotokana na dawa ya kulevya kama moja kati ya majeraha
ya wakati wetu, ambalo linazitesa familia nyingi, na si mara chache linazimaliza kabisa. Jambo
linalofanana linatokana na ulevi, michezo ya kamari, na utegemezi wa namna nyingine. Familia
ingeweza kuwa mahali pa kinga na pa kujifunza kanuni nzuri, lakini jamii na siasa zinashindwa
kuelewa kwamba familia iliyo katika mazingira hatarishi “hupoteza uwezo wa kutenda kwa
kuwasaidia wanafamilia [...]. Tunaona matokeo mazito ya hali hiyo katika familia zilizovunjika
kabisa, watoto wasio na msingi, wazee waliotelekezwa, watoto yatima ingawa wazazi wao wako
hai, vijana wasio na mwelekeo wala nidhamu”.[38] Kama walivyoeleza maaskofu wa Meksiko,
kuna mazingira ya kusikitisha ya ukatili katika familia ambayo yanakuwa chanzo cha ukatili mpya
katika jamii kwa sababu “mahusiano ya kifamilia pia yanamwelekeza mtu kutenda kwa ukatili.
Familia zenye mwelekeo huo ni zile ambapo zinakosekana mawasiliano; zile ambapo kila mmoja
anajihami na wanafamilia hawategemeani; Ambapo zinakosekana shughuli zinazosaidia
kuonyesha ushirikiano; Ambapo mahusiano kati ya wazazi mara nyingi ni migongano na ya kikatili,
na kati ya wazazi na watoto ni migogoro. Ukatili ndani ya familia ni shule ya kinyongo na chuki
kwenye uhusiano wa msingi wa kibinadamu”.[39]

3 Pages 21-30

▲back to top

3.1 Page 21

▲back to top
21
52. Hakuna mtu anayeweza kufikiri kwamba kwa kuidhoofisha familia kama jamii asilia iliyo na
msingi katika ndoa ni jambo linaloisaidia jamii. Ni kinyume chake: ni kikwazo kwa ukomavu wa
mtu, kwa utunzaji wa tunu za jumuiya na kwa maendeleo ya maadili ya miji na vijiji. Haieleweki
tena kwa dhahiri kwamba muungano tu wa pekee na usiofunguliwa kati ya mwanamume na
mwanamke una nafasi timilifu katika jamii, kwa sababu ni jukumu thabiti na kwa vile
unavyowezesha uzaaji. Inatupasa kuzitambua aina nyingi za hali ya kifamilia zinazowezesha
kuongozwa na kanuni fulani za maisha, lakini watu kuishi pamoja tu bila kufunga ndoa, au ndoa ya
jinsia moja, kwa mfano, haziwezi kuhesabiwa sawa kama ndoa. Hakuna muungano usio wa
kudumu na usiowezesha uzazi ambao huweza kutuhakikishia maendeleo ya jamii kwa siku za
mbele. Lakini ni nani leo aliye na bidii ya kutegemeza wanandoa, anayewasaidia kuzishinda hatari
zinazowatisha, kuwasindikiza katika jukumu lao la kulea, anayewasaidia kuimarisha muungano
wao wa kindoa?
53. “Katika jamii nyingine bado kuna desturi ya mitara; katika mazingira mengine bado unaendela
utaratibu wa ndoa zinazopangwa na wakubwa tu. Katika sehemu nyingi, na wala si katika nchi za
Magharibi tu, unaenea sana mfumo wa kuishi unyumba kabla ya ndoa, au kuishi unyumba bila
kuwa na lengo la kufunga ndoa rasmi”.[40] Katika nchi mbalimbali sheria zinarahisisha uwepo wa
aina nyingi za kuishi pamoja, kwa namna hiyo ndoa ya mume mmoja na mke mmoja, isiyovunjika
na inayotarajia kupata watoto, hatimaye inaonekana kama jambo lililopitwa na wakati kati ya aina
nyingi za kuishi pamoja. Katika nchi nyingi wengine wanaendelea kudhoofisha sheria zinazolinda
familia wakielekea kuutetea mfumo unaojali tu uhuru wa kijiamulia. Ingawa ni haki kuukataa
mfumo wa zamani wa familia ya "kimapokeo” yenye tabia ya udikteta na pia yenye ukatili, lakini
haitakiwi jambo hilo lielekee kuidharau na kuichukia ndoa, bali liwe nafasi ya kuielewa upya
maana yake ya kweli na kuifanya upya. Nguvu ya familia tunaiona hasa katika uwezo wake wa
kupenda na wa kufundisha kupenda. Familia hata iwe na jeraha kubwa namna gani, ikitegemea
upendo itakuwa daima na nafasi ya kukua”.[41]
54. Katika kuiangalia kwa kifupi hali halisi, napenda niseme kwamba, ingawa leo haki za
mwanamke na ushiriki wake katika jamii zinatambulika zaidi, katika nchi nyingine safari bado ni
ndefu. Bado tamaduni zisizokubalika hazijang’olewa. Kabla ya yote ukatili wa aibu wanaofanyiwa
mara kwa mara wanawake, kutendewa vibaya nyumbani na namna mbalimbali ya utumwa
ambazo hazionyeshi nguvu za wanaume bali fedheha. Ukatili wa maneno, dhidi ya mwili na wa
kijinsia wanaofanyiwa wanawake katika ndoa ni kinyume kabisa na asili ya muungano wa kindoa.
Nafikiria kuhusu ukeketaji wa wanawake unaofanyika kwa kuzingatia tamaduni za sehemu fulani,
lakini pia ubaguzi unaofanyika katika kutoa ajira yenye heshima na katika kupata nafasi
zinazowawezesha kutoa maamuzi mazito. Historia inafuata nyayo za ukali wa tamaduni za mfumo
dume, ambapo mwanamke alihesabiwa kama mtu wa daraja la pili, lakini tunakumbuka pia mtindo
wa “tumbo la kupanga”au “jinsi mwili wa mwanamke katika utamaduni wa mawasiliano wa siku
hizi unavyodhalilishwa na kutumiwa kibiashara”.[42] Wengine wanafikiri kwamba matatizo mengi
tuliyo nayo sasa yameanza kujitokeza wanawake walipoanza kupata nafasi zaidi. Lakini hoja hii
aina nguvu, “ni uongo, na haina ukweli. Ni mtazamo unaotokana na mfumo dume”.[43] Heshima

3.2 Page 22

▲back to top
22
sawa kwa mwanamke na mwanamume inatufurahisha kwa sababu mifumo ya ubaguzi ya zamani
inakoma na katika familia inaendelezwa mfumo wa kutegemeana. Hata kama zinaweza kuwepo
namna za kutetea haki za wanawake ambazo zina kasoro, tunastaajabia kazi ya Roho kwa kuona
jinsi heshima ya mwanamke na haki zake zinavyotambulika kwa namna iliyo wazi zaidi.
55. Mwanamume “ni muhimu katika maisha ya familia, mintarafu ulinzi na huduma kwa mke na
watoto. […] Wanaume wengi wanaelewa umuhimu wa nafasi yao katika familia na huwajibika kwa
namna inayoendana na tabia ya wanaume. Kutokuwepo kwa baba kunaathiri sana maisha ya
kifamilia, malezi ya watoto na ushiriki wao katika jamii. Kutokuwepo kwa baba kunaweza
kuchukua sura nyingi: kutokuwepo kimwili, kimapendo, kiakili na kiroho. Upungufu huo unafanya
watoto wokose mfano unaofaa wa tabia ya kibaba”.[44]
56. Changamoto nyingine inaibuka kutokana na aina mbalimbali za itikadi zinazoitwa kwa jumla
gender. Itikadi hiyo “inakataa kwamba kiasili katika mwanamume na mwanamke kuna tofauti na
kuna kukamilishana. Mtazamo wa itikadi hiyo ni kuwa na jamii ambapo utofauti wa jinsia haupo,
na kwa namna hiyo kuuondoa msingi asilia ya familia. Itikadi hiyo inakuwa msingi na nguvu kwa
mipango ya malezi na mielekeo ya kisheria inayohamasisha tabia binafsi na moyo wa kimapenzi
ambavyo havijali kabisa utofauti wa kimwili kati ya mwanamume na mwanamke. Hivyo
utambulisho wa mtu unakuja kutegemea chaguo lake binafsi, linaloweza pia kubadilika baada ya
muda”.[45] Inatisha kuona kwamba itikadi nyingine za namna hii, ambazo zinadai kuwa jibu kwa
matamanio ambayo mara nyingine ni ya maana, zinajaribu kulazimisha itikadi hiyo kama wazo
pekee linalotawala pia malezi ya watoto. Haipaswi kutojua kwamba “jinsia asilia (sex) na nafasi ya
jinsia kijamii na kiutamaduni (gender) zinaweza kutofautishwa, lakini bila kutenganishwa”.[46] Kwa
upande mwingine mapinduzi ya bioteknolojia katika medani ya uzazi wa binadamu yamewezesha
kuingilia tendo la kuzaa, na kulifanya lisitegemee tena mahusiano ya kijinsia kati ya mwanamume
na mwanamke. Kwa namna hiyo, uhai wa binadamu na uzazi yamekuwa mambo yanayoweza
kuunganishwa au kutenganishwa, yakitegemea zaidi matamanio ya mtu binafsi au ya
jozi”.[47] Kitu kimoja ni kuuelewa udhaifu wa kibinadamu au ugumu wa maisha, kitu kingine
kuzikubali itikadi zinazodai kuzitenganisha mambo ambayo kiasilia hazitenganishwi. Tusianguke
katika dhambi ya kudai kuchukua nafasi ya Muumba. Sisi ni viumbe, hatuwi na enzi isiyo na
mipaka. Ulimwengu umetutangulia na lazima tuupokee kama zawadi. Wakati huohuo tunaitwa
kuulinda utu wetu, na kwa mantiki hiyo kabla ya yote tuukubali na kuuheshimu kama
ulivyoumbwa.
57. Namshukuru Mungu kwa sababu familia nyingi, ingawa ni mbali na kujisikia kamilifu, huishi
katika upendo, hutekeleza wito wao na zinasonga mbele ingawa zinaanguka mara nyingi njiani.
Tukizingatia tafakari za Sinodi hatubaki na picha moja ya familia kamili, bali mifano mbalimbali
zinazotokana na mazingira tofauti, iliyojaa furaha, machungu na ndoto. Mambo
yanayotuhangaisha yanakuwa changamoto Tusianguke katika mtego wa kuishia kuwa na
malalamiko ya kujitetea badala ya kuuibua ubunifu wa kimisionari. Katika kila aina ya mazingira
“Kanisa linaelewa haja ya kutamka neno la ukweli na la tumaini. […] Tunu kubwa za ndoa na

3.3 Page 23

▲back to top
23
familia ya kikristo zinaendana na kile binadamu anachokitafuta katika maisha.”[48] Tukikabiliana
na shida nyingi - kama walivyosema Maaskofu wa Kolombia - shida hizo ni mwaliko wa “kuzipa
nafasi nguvu za tumaini zilizo ndani yetu zizae ndoto za kinabii, matendo yaletayo mabadiliko na
mapendo yenye ubunifu”.[49]
SURA YA TATU
KUMTAZAMA YESU: WITO WA FAMILIA
58. Mbele na ndani ya familia inatakiwa isikike mbiu msingi, iliyo “nzuri zaidi, iliyo kubwa zaidi,
inayovutia zaidi na wakati huohuo iliyo muhimu”[50], na “inatakiwa iwe kiini cha shughuli ya
uinjilishaji”.[51] Ni mbiu msingi, “ile ambayo hatuna budi daima kurudi kuisikiliza kwa namna tofauti
na tunayotakiwa kurudi kuitangaza katika katekesi kwa namna moja au nyingine”.[52] Kwani
“hakuna kilicho thabiti zaidi, kilicho cha ndani zaidi, cha uhakika zaidi, kilicho imara zaidi na kilicho
cha hekima zaidi ya mbiu hiyo" na “malezi yote ya kikristo kabla ya yote ni uelewa wa kina wa
kerigma”.[53]
59. Mafundisho yetu kuhusu ndoa na familia hayawezi kutovuviwa na kung’arishwa na mbiu hii ya
upendo na upole, ili yasiwe ni kulinda tu mafundisho baridi na yasiyo na uhai. Kwa kweli,
haiwezekani kulielewa kikamilifu fumbo la familia ya kikristo bila mwangaza wa upendo usio na
mwisho wa Baba, uliofunuliwa katika Kristo, ambaye amejitoa mpaka mwisho na yupo hai kati
yetu. Kwa hiyo ninapenda kumtazama Kristo aliye hai na aliyemo ndani ya historia nyingi za
upendo, na kuomba moto wa Roho uzishukie familia zote duniani.
60. Katika picha hii, sura hii fupi inakusanya ufupisho wa mafundisho ya Kanisa juu ya ndoa na
familia. Pia nitanukuu michango mbalimbali ya Mababa wa sinodi katika fikra zao kuhusu
mwangaza tunaopewa na imani. Mababa walianza na mtazamo wa Yesu na wakaonyesha
kwamba Yeye “aliwatazama wanawake na wanaume aliokutana nao kwa upendo na upole,
akiwasindikiza katika hatua zao kwa ukweli, uvumilivu na huruma, katika kutangaza masharti ya
Ufalme wa Mungu”.[54] Na kwa mtindo huohuo, leo Bwana anatusindikiza katika bidii ya kuishi na
kutangaza Injili ya familia.
Yesu anahuisha na kuukamilisha mpango wa Mungu.
61. Mbele ya wale waliokuwa wanazuia ndoa, Agano Jipya linafundisha kuwa “kila uumbaji wa
Mungu ni mzuri, Wala hakuna cha kukataliwa” (1Tim 4:4). Ndoa ni “zawadi” ya Bwana (1Kor 7:7).
Wakati huohuo, kutokana na tathmini chanya, unawekwa mkazo mkubwa wa kuitunza zawadi hii
ya Mungu: “Ndoa iheshimiwe na wote na kitanda cha ndoa kisiwe na doa” (Ebr 13:4). Ujinsia na
tendo la ndoa ni sehemu ya zawadi hii ya Mungu: “Msinyimane” (1Kor 7:5).
62. Mababa wa sinodi wamekumbusha kuwa Yesu, “akirejea mpango asili wa Mungu juu ya jozi la

3.4 Page 24

▲back to top
24
wanadamu, anathibitisha tena muungano usiovunjika kati ya mwanaume na mwanamke, pamoja
na kusema kwamba “kwa ugumu wa mioyo yenu Musa aliwaruhusu kuwapa talaka wake zenu,
lakini toka mwanzo haikuwa hivi” (Mt 19:8). Kutovunjika kwa ndoa (“Aliowaunganisha Mungu,
mwanadamu asiwatenganishe”: Mt 19:6), hili kwanza kabisa halitakiwi lichukuliwe kama “nira”
waliyotwishwa watu, badala yake lichukuliwe kma “zawadi” wanayopewa watu walioungana katika
ndoa. [...] Uhisani wa Mungu unasindikiza daima watu katika safari yao, huponya na hugeuza
moyo mgumu kwa neema, ukiwaongoza kuelekea asili yao, kwa njia ya msalaba. Katika Injili
tunauona waziwazi mfano wa Yesu, ambaye [...] alitangaza ujumbe unaohusu maana ya ndoa
kama ukamilifu wa ufunuo unaorudisha mpango asili wa Mungu (taz. Mt 19:8)”.[55]
63. “Yesu, aliyepatanisha yote katika nafsi yake, amerudisha ndoa na familia kwenye hali yake ya
asili (taz. Mk 10:1-12). Familia na ndoa zimekombolewa na Kristo (taz. Efe 5:21-32),
zimekarabatiwa kwa mfano wa Utatu Mtakatifu, fumbo ambalo kwalo upendo wote wa kweli
unatoka. Agano la kindoa, lililoanzishwa katika uumbaji na likafunuliwa katika historia ya wokovu,
linapata ufunuo kamili wa maana yake katika Kristo na katika Kanisa. Familia na ndoa zinapokea
toka kwa Kristo kwa njia ya Kanisa neema inayohitajika ili kushuhudia upendo wa Mungu na kuishi
kwa kushirikiana. Injili ya familia inaipitia historia yote ya ulimwengu tangu kuumbwa kwa
mwanadamu kwa sura na mfano wa Mungu (taz. Mwa 1:26-27) hadi utimilifu wa fumbo la Agano
katika Kristo mwisho wa nyakati kwa njia ya arusi ya Mwanakondoo (taz. Ufu 19:9)”.[56]
64. "Mfano wa Yesu ni msingi kwa Kanisa. [...] Yeye aliyazindua maisha yake ya hadhara kwa
ishara ya Kana, aliyoifanya kwenye muktadha wa arusi (taz. Yn 2:1-11). [...] Alishiriki maisha ya
kila siku ya familia ya Lazaro na dada zake (taz. Lk 10:38) na familia ya Petro (taz. Mt 8:14).
Alisikiliza kilio cha wazazi kwa ajili ya watoto wao, akawafufua (taz. Mk 5:41; Lk 7:14-15),
akaonyesha hivyo maana halisi ya huruma, inayomaanisha kuweka Agano upya (taz. Yohane
Paulo II, Dives in misericordia, 4). Hili linaonekana wazi anapokutana na mwanamke Msamaria
(taz. Yn 4:1-30) na yule mzinifu (taz. Yn 8:1-11), ambapo utambuzi wa dhambi unaamshwa mbele
ya upendo wa bure wa Yesu”.[57]
65. Umwilisho wa Neno katika familia ya kibinadamu, Nazareth kwa upya wake unagusa historia
ya ulimwengu. Tunahitaji kuzama kwenye fumbo la kuzaliwa kwa Yesu, katika ndiyo ya Maria
wakati wa kupashwa habari na malaika, Neno alipotungwa mimba tumboni mwake; hata katika
ndiyo ya Yosefu, aliyempa jina Yesu na akamtunza Maria; katika sherehe ya wachungaji pangoni;
katika maabudu ya Mamajusi; katika kutorokea Misri, ambapo Yesu alishiriki mateso ya Taifa lake
lililopelekwa uhamishoni, likateswa na kudhalilishwa; katika subira ya Zakaria na katika furaha
inayosindikiza kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji; katika ahadi iliyotimizwa kwa Simeoni na Anna
hekaluni; katika mshangao wa walimu wa sheria wanaposikiliza hekima ya Yesu kijana mdogo. Na
hivi yatupasa kuingia ndani ya miaka thelathini wakati Yesu alipojipatia mkate kwa kufanya kazi
kwa mikono yake, akisali na kufuata mapokeo ya imani ya watu wake na kuzidi kujifunza imani ya
wazee wake, hata kuifanya izae katika fumbo la Ufalme. Hili ni fumbo la Noeli na siri ya Nazarethi,
iliyojaa manukato ya familia! Ni fumbo lililowavutia sana watakatifu: Fransisko wa Asizi, Teresia

3.5 Page 25

▲back to top
25
wa Mtoto Yesu na Charles de Foucauld, na linalotazamwa na familia za kikristo ili kuhuisha
matumaini na furaha zake.
66. “Agano la upendo na uaminifu, ambalo kwalo Familia Takatifu ya Nazareth inaishi,
linauangaza mwanzo unaotengeneza msingi wa familia zote na linaziwezesha vema zaidi
kukabiliana na changamoto za maisha na historia. Juu ya msingi huu, kila familia, pamoja na
udhaifu wake, inaweza kuwa mwanga katika giza la ulimwengu. “Hapa tunaelewa namna ya kuishi
katika familia. Nazareth itukumbushe nini maana ya familia, nini ushirika wa upendo, uzuri wake
usio na anasa na wa kawaida, utakatifu wake na kutoharibika kwake; itufanye tuonje utamu wa
malezi ya familia, ambayo hayawezi kukasimishwa kwa yeyote, ituonyeshe nafasi yake ya asili
katika jamii” (Paulo VI, Hotuba huko Nazarethi, 5 Januari 1964)”.[58]
Familia katika hati za Kanisa
67. Mtaguso wa kiekumene wa pili wa Vatikano, katika kostitusio ya kichungaji Gaudium et spes,
umeshughulikia ukuzaji wa hadhi ya ndoa na familia. 47-52). “Umeileza ndoa kama jumuiya ya
uhai na upendo (taz. na. 48), ukiweka upendo kama kiini cha familia [...]. ‘Upendo wa kweli kati ya
mume na mke’ (na. 49) unamaanisha mmoja kujitoa kwa mwingine, ikiwemo mahusiano katika
tendo la ndoa na mapenzi, kadiri ya mpango wa Mungu (taz. na. 48-49). Zaidi ya hayo Mtaguso
unakazia juu ya Kristo kuwa msingi wa wanandoa: Kristo Bwana ‘anakutana na wanandoa
wakristo katika sakramenti ya ndoa’ (na. 48) na anabaki pamoja nao. Katika umwilisho, Yeye
anauchukua upendo wa kibinadamu, anausafisha, anautimiliza, na kwa Roho wake anawapa
wanandoa uwezo wa kuuishi, ukiyapenya maisha yao yote ya imani, matumaini na mapendo. Kwa
mtindo huu wanandoa wanakuwa kama wamewekwa wakfu na, kwa neema ya pekee, wanajenga
Mwili wa Kristo na wanakuwa Kanisa la nyumbani (taz. Lumen Gentium, 11), kiasi kwamba
Kanisa, ili lijitambue kikamilifu katika fumbo lake, linaitazama familia ya kikristo, linalodhihirishwa
nayo katika uhalisia”.[59]
68. Baadaye, “mwenye heri Paulo VI, tokana na Mataguso wa II wa Vatikano ametoa mafundisho
ya ndani juu ya ndoa na familia. Kwa namna ya pekee, katika Ensiklika Humanae Vitae, ameweka
wazi uhusiano uliopo kati ya upendo wa wanandoa na uzazi. “Upendo kati ya wanandoa
unawataka wautambue utume wao wa kuwa wazazi wanaowajibika, jambo ambalo siku hizi kwa
usahihi kabisa kinakaziwa na ambalo lingetakiwa lieleweke kwa usahihi. [...] Uzazi unaowajibika
kwa hiyo unamaanisha kwamba wanandoa wanatakiwa kuzijua wajibu zao kwa Mungu, kwao
wenyewe, kwa familia na kwa jamii, kwa kuzingatia ngazi sahihi ya tunu” (na. 10). Katika Wosia
wa Kitume Evangelii nuntiandi, Paulo VI ameeleza uhusiano uliopo kati ya familia na Kanisa".[60]
69. “Mt. Yohane Paulo II katika katekesi zake juu ya upendo wa kibinadamu, Barua kwa familia
Gratissimam sane na hasa katika Wosia wa Kitume Familiaris consortio, ametoa nafasi kubwa
kwa familia. Katika hati hizo, Baba Mtakatifu ameitaja familia kuwa “njia ya Kanisa”; ametoa
mtazamo wa ujumla juu ya wito wa upendo wa mwanaume na mwanamke; amependekeza

3.6 Page 26

▲back to top
26
misingi elekezi ya uchungaji wa familia na kwa uwepo wa familia katika jamii. Kwa namna ya
pekee, akiongelea mapendo ya kindoa (taz. Familiaris Consortio, 13), ameieleza namna ambayo
wanandoa, katika kupendana, wanapokea zawadi ya Roho wa Kristo na wanauishi wito wao wa
kuwa watakatifu”.[61]
70. “Benedikto XVI, katika Ensiklika Deus caritas est, ameileta tena mada ya ukweli wa upendo
kati ya mume na mke, unaoangazwa kikamilifu na upendo wa Kristo msulibiwa (taz. na. 2). Yeye
anarudia kusisitiza kuwa “ndoa ambayo msingi wake ni upendo kati ya mume mmoja na mke
mmoja na wa kudumu inakuwa ikona ya uhusiano wa Mungu na taifa lake na pia kinyume chake:
namna ya kupenda ya Mungu inakuwa kipimo cha upendo wa kibinadamu” (na. 11). Zaidi ya hayo,
katika Ensiklika Caritas in veritate, anaeleza umuhimu wa upendo kama chimbuko la uhai katika
jamii (taz. na. 44), mahali ambapo watu hujifunza kuzoea mafaa ya pamoja”.[62]
Sakramenti ya ndoa
71. “Maandiko Matakatifu na Mapokeo hutufungulia mlango wa kuweza kuufahamu Utatu
Mtakatifu unaojifunua kwa sura ya kifamilia. Familia ni mfano wa Mungu, ambaye ni [...] ushirika
wa nafsi. Katika Ubatizo, sauti ya Baba inamtaja Yesu kama Mwanae mpendwa, na katika upendo
huu tunaweza kutambua uwepo wa Roho Mtakatifu (taz. Mk 1:10-11). Yesu, aliyepatanisha kila
kitu katika Yeye na amemkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi, si tu kwamba ameirudisha
ndoa na familia katika hali yake ya asili, bali pia ameikuza ndoa na kuifanya ishara ya
kisakramenti ya upendo wake kwa Kanisa (taz. Mt 19:1-12; Mk 10:1-12; Efe 5:21-32). Katika
familia ya kibinadamu, iliyokusanywa na Kristo, imerudishwa “sura na mfano” ya Utatu Mtakatifu
(taz. Mwa 1:26), fumbo ambalo toka kwalo unatoka kila upendo wa kweli. Toka kwa Kristo, kupitia
Kanisa, ndoa na familia hupokea neema ya Roho Mtakatifu, ili kushuhudia Injili ya upendo wa
Mungu”.[63]
72. Sakramenti ya ndoa si desturi ya kijamii, ibada tupu au ishara ya nje tu ya wajibu fulani.
Sakramenti ni zawadi kwa ajili ya kutakatifuza wanandoa na ya wokovu wao, kwa sababu "ukweli
kwamba kila mmoja ni wa mwingine, unaonyesha kwa ishara ya kisakramenti uhusiano wa Kristo
na Kanisa. Wanandoa kwa hiyo wanalikumbusha Kanisa juu ya kile kilichotokea juu ya Msalaba;
wanaishi mmoja kwa ajili ya mwingine, na kwa ajili ya watoto, mashahidi wa wokovu, ambao kwa
sakramenti wanafanywa waushiriki".[64] Ndoa ni wito, kwani ni jibu kwa mwito maalum wa kuuishi
upendo kati ya wanandoa kama ishara isiyo kamili ya upendo kati Kristo na Kanisa. Kwa hiyo,
uamuzi wa kuoana na kuunda familia ni lazima utokane na upambanuzi wa kimwito.
73. “Kujitoa kila mmoja kwa mwenzake ambako ni sifa ya msingi ya ndoa ya kisakramenti, kuna
mizizi yake katika neema ya ubatizo unaoweka agano la msingi la kila mtu na Kristo ndani ya
Kanisa. Katika kupokeana na kwa neema ya Kristo wanaofunga ndoa wanaahidiana kila mmoja
kujitoa kikamilifu kwa mwingine, pia wanaahidiana uaminifu na utayari wa kupokea uhai, yaani
kuzaa, wanatambua kuwa zawadi wanazopewa na Mungu ni msingi wa ndoa yenyewe,

3.7 Page 27

▲back to top
27
wanazichukua kwa umakini wajibu zao, katika jina lake na mbele ya Kanisa. Sasa, katika imani
inawezekana kuyapokea mema ya ndoa kama wajibu ambazo zinabebeka kirahisi zaidi kwa
msaada wa neema ya sakramenti. [...] Kwa hiyo, Kanisa linawatazama wanandoa kama moyo wa
familia nzima ambayo nayo inamtazama Yesu”.[65] Sakramenti si “kitu” fulani au “ nguvu” fulani,
kwa sababu kwa kweli Kristo mwenyewe “anakuja kukutana na wanandoa wakristo kwa njia ya
sakramenti ya ndoa. Yeye anabaki nao, anawapa nguvu ya kumfuasa wakichukua msalaba wao,
nguvu ya kuinuka wakianguka, ya kusameheana, ya kuchukuliana mizigo kila mmoja ya
mwenzake".[66] Ndoa ya kikristo ni ishara ambayo si tu kwamba inaonyesha jinsi Kristo
alivyolipenda Kanisa lake katika Agano lililowekwa msalabani, bali inaufanya upendo huo uwepo
katika ushirika wa wanandoa. Wakiungana katika mwili mmoja, wanakuwa ishara ya ndoa ya
Mwana wa Mungu na ubinadamu. Kwa sababu hii, "katika furaha za upendo wao na za maisha
yao ya kifamilia, Yeye huwapa, tayari hapa duniani, nafasi ya kuonja karamu ijayo ya arusi ya
Mwanakondoo".[67] Hata kama “mfano wa jozi mume-mke na Kristo-Kanisa” ni “mfano usio
kamili”,[68] unasaidia kumwomba Bwana amimine upendo wake kati ya wanandoa pamoja na
mapungufu yao.
74. Muungano wa kijinsia, unaofuata taratibu za kibinadamu na uliotakatifuzwa na sakramenti ya
ndoa, unawasaidia wanandoa kukua katika maisha ya neema. Ndilo "fumbo la ndoa".[69] Thamani
ya muungano wa miili inaonyeshwa katika maneno ya makubaliano, pale ambapo wanandoa
wanapokeana na kujitoa kila mmoja kwa mwingine ili kushirikiana kwa maisha yao yote. Maneno
haya yanatia maana kwa ujinsia, na yanauondolea utata wote. Hata hivyo, kwa kweli, maisha yote
ya pamoja ya wanandoa, mtandao wote wa mahusiano watakaoutengeneza kati yao, pamoja na
watoto wao na kwa ulimwengu, utajengwa na kuimarishwa na neema ya sakramenti inayobubujika
toka fumbo la Umwilisho na la Pasaka, ambamo Mungu ameonyesha upendo wake wote kwa
ubinadamu na akajiunganisha nao kabisa. Hawatakuwa kamwe peke yao kukabiliana na
changamoto zitakazotokea. Wao wanatakiwa kupokea zawadi ya Mungu kwa kuwajibika, kwa
ubunifu wao, kwa uvumilivu na mapambano ya kila siku, lakini wataweza daima kumwomba Roho
Mtakatifu aliyeweka wakfu muungano wao, ili neema waliyopokea iweze kudhihirika upya katika
kila hali.
75. Kadiri ya mapokeo ya kilatini ya Kanisa, katika sakramenti ya ndoa wahudumu ni mume na
mke wanaooana,[70] ambao kwa kutamka wazi makubaliano yao na kuyadhihirisha katika kujitoa
kimwili kila mmoja kwa mwenzake, wanapokea zawadi kubwa. Makubaliano yao na muungano wa
miili ni nyenzo ambazo kwazo Mungu anawafanya kuwa mwili mmoja. Katika ubatizo uliwekwa
wakfu uwezo wao wa kuungana katika ndoa kama wahudumu wa Bwana ili kuitikia wito wa
Mungu. Kwa hiyo, wanandoa wasio wakristo wanapobatizwa, si lazima kwao kurudia viapo vya
ndoa na inatosha kwamba hawavikatai, kwani, kutokana na Ubatizo wanaopokea, muungano wao
unakuwa papo hapo wa kisakramenti. Sheria za Kanisa zinazitambua kuwa ni halali hata ndoa
zilizoadhimishwa bila uwepo wa mhudumu mwenye daraja takatifu.[71] Maana, utaratibu wa asili
umechukuliwa na ukombozi wa Yesu Kristo, kwa namna ya kwamba “kati ya wabatizwa hapawezi
kuwepo mkataba halali wa kindoa, usio kwa wenyewe sakramenti”.[72] Kanisa linaweza kutaka

3.8 Page 28

▲back to top
28
tendo lifanyike hadharini, wawepo mashahidi, na mambo mengine ambayo yamebadilika katika
historia, lakini hili haliondoi kwa wanandoa ile hali yao ya kuwa wahudumu wa sakramenti, wala
halipunguzi umuhimu wa makubaliano ya mume na mke, ambayo ndiyo yanayoweka kifungo cha
kisakramenti. Kwa vyovyote vile, tunahitaji kutafakari zaidi juu ya tendo la kimungu katika
madhehebu ya ndoa, jambo ambalo linakaziwa zaidi katika Makanisa ya Mashariki, hasa kwa
kuonyesha umuhimu wa pekee kwa baraka ya wafunga ndoa kama ishara ya zawadi ya Roho.
Mbegu za Neno na hali zenye mapungufu
76. "Injili ya familia inazilisha pia zile mbegu ambazo bado zinasubiri kukomaa, nayo inapaswa
kuitunza miti ile iliyokauka na inayohitaji kutotelekezwa",[73] kiasi kwamba, kwa kuanzia na
zawadi ya Kristo katika sakramenti, “[watu] waongozwe kwa uvumilivu mbele zaidi, hadi kufikia
ufahamu mkubwa zaidi na hata kulizamisha kabisa Fumbo hili katika maisha yao”.[74]
77. Mababa wa sinodi wakizingatia mafundisho ya kibiblia, ambayo kadiri yake kila kitu
kimeumbwa kwa njia ya Kristo na kwa ajili ya Kristo, (taz. Kol 1:16), wamekumbusha kuwa
“mpango wa ukombozi unauangaza na kuukamilisha ule wa uumbaji. Ndoa ya asili, kwa hiyo,
inaeleweka kwa ukamilifu katika mwanga wa utimilifu wake wa kisakramenti: kwa njia tu ya
kumtazama Kristo inawezekana kuuelewa kwa undani kabisa ukweli juu ya mahusiano ya
kibinadamu. “Kwa kweli fumbo la binadamu linapata mwanga wa kweli katika fumbo la Neno
aliyetwaa mwili. […] Kristo, ambaye ni Adamu mpya, akifunua fumbo la Baba na la upendo wake,
anamfunua pia kikamilifu mtu kwa mtu mwenyewe na anamwonyesha wito wake wa juu kabisa”
(Gaudium et spes, 22). Inakuja kwamba ni muhimu kwa namna ya pekee kuzielewa kwa mtazamo
wa Kristokati tabia asili za ndoa, zile zinazounda mafaa ya wanandoa (bonum
coniugum)”,[75] ambayo ni umoja, utayari wa kuwa wazazi, uaminifu na kutovunjika kwa ndoa, na
ndani ya ndoa ya kikristo hata kusaidiana katika safari ya kuelekea kwenye ukamilifu wa urafiki na
Bwana. "Upambanuzi wa uwepo wa mbegu za Neno hata katika tamaduni nyingine (rej. Ad
gentes, 11) unaweza kufanyika hata katika masuala ya ndoa na familia. Zaidi ya ndoa ya kweli ya
asili kuna vitu chanya katika aina nyingine za ndoa zinazopatikana katika tamaduni za kidini tofauti
tofauti”,[76] hata kama vinapatikana pia vivuli. Tunaweza kutamka kuwa "kila mtu anayetaka
kuiunda katika ulimwengu huu familia inayofundisha watoto kufurahia kila tendo linalonuia
kushinda uovu – familia inayoonyesha kuwa Roho ni hai na anafanya kazi –, atapata shukrani na
heshima, awe ni mtu wa taifa lolote lile, au dini au kanda".[77]
78. “Mtazamo wa Kristo, ambao mwanga wake unamwangaza kila mtu (taz. Yn 1:9; Gaudium et
spes, 22), unalivuvia Kanisa katika uchungaji wake kwa waamini wanaoishi pamoja bila kufunga
ndoa au waliofunga ndoa za kiserikali tu au wametalikiana na kufunga ndoa nyingine. Katika
mtazamo wa malezi ya kimungu, Kanisa linawaangalia kwa upendo wale wanaoshiriki maisha
yake kwa namna isiyo kamilifu: linaomba pamoja nao neema ya wongofu, linawahamasisha
kutenda mema, kutunzana kwa upendo na kutoa huduma kwenye jumuiya wanamoishi na
wanamofanya kazi. […] Muungano usio rasmi unapofikia hatua thabiti kwa njia ya kifungo cha

3.9 Page 29

▲back to top
29
hadharani – na unaonyesha mapendo makubwa, unawajibika kwa watoto, una uwezo wa
kushinda magumu – unaweza kuwa fursa ya kuwasindikiza kuelekea sakramenti ya ndoa, pale
inapowezekana".[78]
79. “Mbele ya hali ngumu na familia zilizojeruhiwa, inatakiwa kukumbuka kanuni hii ya jumla:
‘Wachungaji watambue kuwa, kwa ajili ya ukweli, wanatakiwa kuzipambanua vyema hali
mbalimbali” (Familiaris consortio, 84). Kiasi cha wajibu hakilingani katika kila hali, na inawezekana
ziwepo sababu zinazopunguza uwezo wa kuamua. Kwa hiyo, wakati mafundisho yanatakiwa
yaelezwe kwa uwazi, tunatakiwa tuepukane na hukumu zisizozingatia ugumu wa hali tofauti, na ni
muhimu pia kuzingatia hali tofauti wanazoishi watu na maumivu waliyo nayo kutokana na hali
zao".[79]
Uzazi na malezi ya watoto
80. Ndoa, kwanza kabisa ni “jumuiya ya undani ya maisha na ya mapendo ya kindoa"[80] ambayo
ndiyo hasa mafaa kwa wanandoa wenyewe,[81] na ujinsia “unalenga kudhihirisha upendo wa
kindoa wa mwanamke na mwanaume”.[82] Kwa hiyo hata “wanandoa ambao Mungu hakuwajalia
watoto, wanaweza kuwa na maisha ya kindoa yenye maana, kiutu na kikristo”.[83] Pamoja na
hayo, muungano huu “kwa asili yake unalenga uzazi”.[84] Mtoto anayezaliwa “si kwamba
anajiongeza kutoka nje ya mapendo ya wanandoa; anachipua kutoka kwenye moyo wenyewe wa
majitoleo ya kila mmoja kwa mwingine, na anakuwa tunda na utimilifu wake".[85] Hafiki kama
hitimisho la mchakato, bali ni kwamba tayari yupo tangu mwanzo wa mapendo yao kama kiini
ambacho hakiwezi kukataliwa bila kuudhuru upendo wenyewe. Tangu mwanzo upendo unagoma
kujifungia ndani yake wenyewe na hivi unajifunua katika uzaaji ambao unaendeleza uwepo wake.
Hivyo, hakuna tendo la ndoa la wanandoa ambalo laweza kuikataa maana hii,[86] hata kama kwa
sababu mbalimbali si daima maisha mapya yanaweza kuzaliwa.
81. Mtoto anahitaji kuzaliwa kutokana na upendo wa mtindo huo na si katika mtindo mwingine
wowote, kwa vile yeye “si kitu kinachodaiwa, bali ni zawadi”,[87] ni “tunda la tendo maalum la
upendo wa kindoa wa wazazi wake”.[88] Kwa sababu “kadiri ya mpango wa uumbaji, upendo wa
kindoa kati ya mume na mke na uzazi hutegemezana (taz. Mwa 1:27-28). Kwa namna hii Muumba
amewashirikisha mwanaume na mwanamke katika kazi ya uumbaji wake na wakati huohuo
akawafanya kuwa vyombo vya upendo wake, akiwawajibisha kuhusu mustakabali wa wanadamu
kwa njia ya kuendeleza uhai ulimwenguni”.[89]
82. Mababa wa sinodi wametamka kuwa “si haba kuona watu wanavyozidi kuwa na mtazamo
unaodunisha uzazi kuwa ni jambo mojawapo tu la mipango ya mtu au jozi".[90] Mafundisho ya
Kanisa “yanasaidia kuishi kwa utulivu na uelewa ushirika kati ya wanandoa, katika nyanja zake
zote, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kuzaa. Inafaa kurudi kwenye ujumbe wa Ensiklika Humanae
vitae ya Paulo VI, unaokazia hitaji la kustahi hadhi ya mtu wakati wa kuzitathmini kimaadili njia za
kupanga uzazi [...]. Chaguo la kumwasilisha mtoto au kuwapokea watoto wasio wa wanandoa –

3.10 Page 30

▲back to top
30
hata ikiwa ni kwa muda – na kuwatunza ni namna nyingine ya pekee ya kuuishi uzazi katika
maisha ya wanandoa.[91] Kwa shukrani ya pekee, Kanisa “linaziunga mkono familia
zinazowapokea, zinazowalea na kuwaonyesha upendo watoto wao walemavu”.[92]
83. Katika muktadha huo, siwezi kutotamka kuwa, ikiwa familia ni hekalu la uhai, mahala ambapo
uhai huzalishwa na kutunzwa, ni mkanganyiko mkubwa kuona kwamba mahala hapohapo uhai
unakataliwa na kuharibiwa. Uhai wa binadamu una thamani kubwa hivi, na haki ya kuishi ya
mtoto, ambaye hana kosa, hainyang’anyiki hivi akingali anakua katika tumbo la uzazi la mama,
kiasi kwamba kwa namna yoyote haiwezekani kufanya hivyo, eti, kwa hoja ya haki binafsi ya
mwili, yaani kufanya maamuzi yanayodhulumu uhai huo, ambao kwa wenyewe unajitegemea na
usingetakiwa utawaliwe na binadamu mwingine. Familia hulinda uhai katika kila hatua yake na
hata katika mwisho wake. Kwa hiyo "wale wanaotoa huduma kwenye taasisi za afya
wanakumbushwa wajibu wa kimaadili wa kufuata ukinzani wa dhamiri. Hali kadhalika, Kanisa si tu
linaona ulazima wa kusisitiza haki ya kukutwa na kifo cha kawaida, bila kulazimisha matibabu ya
ghali sana wala kukubali kifo laini”, lakini pia "linapinga kwa dhati adhabu ya kifo".[93]
84. Mababa wa sinodi wametaka kusisitiza pia kwamba "changamoto mojawapo ya msingi
ambayo familia leo zinakabiliwa nayo bila shaka ni malezi, ambayo imekuwa ngumu na yenye
utata zaidi kutokana na mabadiliko ya kitamaduni na mvuto wa vyombo vya habari".[94] “Kanisa
linafanya kazi yenye thamani kubwa ya kuzisaidia familia, kuanzia na mafundisho ya kuwaingiza
katika ukristo, kwa kupitia jumuiya zenye ukarimu wa ukaribishaji”.[95] Hata hivyo naona muhimu
sana kukumbusha kuwa malezi kamili ya watoto “ni wajibu mkubwa mno” na wakati huohuo "ni
haki msingi” ya wazazi.[96] Si suala la wajibu au mzigo tu, bali pia haki msingi ya wazazi
isiyoweza kukasimishwa, nao wanatakiwa kuitetea na hakuna mtu anayeweza kudai kuiondoa
toka kwao. Serikali inaweza kuwasaidia tu wazazi katika kutoa huduma ya elimu kwa watoto,
ikiwasindikiza wazazi katika jukumu lao la kimalezi pasipo kuchukua nafasi yao, ambao wanayo
haki na uhuru wa kuchagua aina ya elimu – iliyo rahisi na bora – wanaopenda kutoa kwa watoto
wao kadiri ya fikra na imani yao. Shule haiwezi kuchukua nafasi ya wazazi, ila huduma inayotoa
inakamilishana na wajibu wa wazazi. Hii ni kanuni msingi: "Mshiriki yeyote mwingine katika
mchakato wa kutoa elimu kwa watoto ni lazima afanye hivyo kwa niaba ya wazazi, kwa ridhaa yao
na, kwa kiasi fulani, ni lazima wazazi wampe mamlaka".[97] Lakini "umetokea mpasuko kati ya
familia na jamii, kati ya familia na shule; mkataba wa kimalezi leo hii umevunjika; na hivi, agano la
kimalezi la jamii na familia limeingia katika mvurugiko”.[98]
85. Kanisa linaalikwa kushiriki, kwa tendo la kichungaji stahiki, ili wazazi wenyewe waweze
kutekeleza utume wao wa kulea. Linatakiwa liwasaidie kuthamini nafasi yao ya pekee, na
kutambua kuwa wale waliopokea sakramenti ya ndoa hufanyika kuwa wahudumu hasa wa malezi,
kwa sababu katika kuwalea watoto wao wazazi wanalijenga Kanisa,[99] na kwa kufanya hivyo
wanaitikia wito ambao kwao Mungu amewaita.[100]
Familia na Kanisa

4 Pages 31-40

▲back to top

4.1 Page 31

▲back to top
31
86. “Kanisa huzitazama kwa furaha ya dhati na faraja kubwa familia zinazodumu aminifu kwa
mafundisho ya Injili, likizishukuru na kuzitia moyo kwa ushuhuda unaooneshwa nazo. Kwa njia
yao, kwa kweli, uzuri wa ndoa isiyovunjika na aminifu daima unashuhudiwa kama jambo la
kuaminika. Katika familia, “inayoweza kuitwa Kanisa la nyumbani” (Lumen Gentium, 11), ndimo
tunaanza kujifunza kuuishi ushirika wa kikanisa, ambamo, kwa neema, fumbo la Utatu Mtakatifu
unaakisiwa. “Hapa ndipo mmoja anapojifunza ugumu na furaha ya kazi, upendo wa kidugu,
msamaha mkarimu, unaofanywa upya tena na tena, na hasa ibada takatifu kwa njia ya sala na
toleo la maisha yake” (Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 1657)”.[101]
87. Kanisa ni familia ya familia nyingi, ambalo daima hutajirishwa na maisha ya Makanisa yote ya
nyumbani. Kwa hiyo, "kwa njia ya sakramenti ya ndoa kila familia inakuwa kwa ukamilifu faida kwa
Kanisa. Kwa mtazamo huu, hakika itakuwa zawadi ya thamani kwa Kanisa la leo, kuzingatia hata
uhusiano wa kusaidiana uliopo kati ya familia na Kanisa: Kanisa ni faida kwa familia, familia ni
faida kwa Kanisa. Kuilinda zawadi ya sakramenti ya Bwana hakuihusishi familia moja pekee, bali
jumuiya nzima ya kikristo”.[102]
88. Upendo uliopo kwenye familia ni nguvu ya kudumu kwa uhai wa Kanisa. "Hatima ya ndoa ya
kudumisha umoja ni mwito wa daima wa kukua na kujikita katika upendo huu. Katika muungano
wao wa upendo wanandoa wanang’amua uzuri wa kuwa baba na mama; wanashirikishana
mipango na uchovu, matamanio na mahangaiko; wanajifunza kutunzana na kusameheana. Katika
upendo huu wanaadhimisha nyakati zao za furaha na wanasaidiana katika hatua ngumu za
maisha yao [...]. Uzuri wa kuwa mmoja zawadi kwa mwingine, furaha kwa watoto wanaozaliwa, na
matunzo yenye upendo kwa wanafamilia wote, kuanzia watoto hadi wazee, ni baadhi ya matunda
yanayofanya jibu kwa wito wa familia liwe pekee na lisilobadilishika",[103] kwa ajili ya Kanisa na
vilevile kwa jamii nzima.
SURA YA NNE
UPENDO KATIKA NDOA
89. Hayo yote yaliyosemwa hayajitoshelezi ili kuelezea Injili ya ndoa na ya familia kama
hatuchukui nafasi ili kunena kwa namna maalumu juu ya upendo. Kwani hatuwezi kuhimiza
mwendo wa uaminifu na wa kujitoa kila mmoja kwa mwenzake ikiwa hatuchochei ukuaji,
udumishaji na uimarishaji wa upendo kati ya wanandoa na katika familia. Kwa kweli, neema ya
sakramenti ya ndoa inaelekea kwanza kabisa "kukamilisha upendo kati ya wanandoa".[104] Katika
uwanja huo pia ni sahihi ule msemo, kwamba, hata “nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza
kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha
maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu" (1Kor 13:2-
3). Neno "upendo" lakini, ambalo ni mojawapo ya maneno yanayotumiwa zaidi, mara nyingi
linaonekana kurembuka.[105]

4.2 Page 32

▲back to top
32
Upendo wetu wa kila siku
90. Katika ule utenzi tuliozoea kuuita ‘wa upendo’, ulioandikwa na mtakatifu Paulo, tunakuta sifa
kadha wa kadha za upendo wa kweli:
"Upendo huvumilia,
upendo hufadhili,
hauhusudu,
upendo hautakabari,
haujivuni,
haukosi kuwa na adabu,
hautafuti mambo yake,
hauoni uchungu;
hauhesabu mabaya;
haufurahii udhalimu,
bali hufurahi pamoja na kweli.
Huvumilia yote,
huamini yote,
hutumaini yote,
hustahimili yote (1Kor 13:4-7).
Upendo huo unaonjwa na unasitawishwa katika maisha ambayo wanayashiriki kila siku
wanandoa, kati yao na pamoja na watoto wao. Kwa hiyo inasaidia kutafakari kwa kina maana ya
maneno haya [ya Paulo], ili kujaribu kuona namna yanavyoweza kuwa kweli kwa maisha halisi ya
kila familia.
Uvumilivu
91. Neno la kwanza linalotumika ni makrothimei. Tafsiri sahihi si moja kwa moja “wenye
kustahimili yote”, kwa sababu wazo hilo linatolewa mwishoni mwa aya ya 7. Maana yake inaweza
kupatikana katika tafsiri ya Kigriki ya Agano la Kale, pale ambapo inasema kwamba Mungu “si
mwepesi wa hasira” [, au ni “mpole wa hasira”] (Kut 34:6; Hes 14:18). Inajionyesha pale ambapo
mtu hakubali kuongozwa na misukumo ya hasira na anakwepa kuwashambulia wengine. Ni sifa
bainifu ya Mungu wa Agano anayeita kumwiga pia katika maisha ya kifamilia. Matini ambamo
Paulo ametumia neno hilo zinapaswa kusoma katika muktadha wa kitabu cha Hekima (taz. 11:23;
12:2,15-18): wakati sifa inapotolewa kwa upole wa Mungu anayetaka kuacha nafasi kwa toba,
hapohapo husisitizwa uweza wake unaodhihirika anapotenda kwa huruma. Uvumilivu wa Mungu
ni zoezi la huruma kwa mwenye dhambi, nao hudhihirisha uweza halisi.
92. Kuwa wavumilivu maana yake si kukubali wengine watutese mara kwa mara, au kuvumilia
kupigwa au kutendewa ukatili, au kuacha watuhesabu kama vitu. Tatizo linaanza pale ambapo

4.3 Page 33

▲back to top
33
tunadai kwamba mahusiano yawe kama hadithi tamu au kwamba watu wawe wakamilifu, au
tunapojiweka katikati na kunasubiri tu kwamba mapenzi yetu yatimizwe. Hapo kila kitu kinavunja
uvumilivu wetu, kila jambo linatusukuma tusisimue kwa ukali. Ikiwa hatusitawishi uvumilivu,
tutakuwa daima na sababu ya kujibu kwa hasira, na hatimaye tutakuwa watu ambao hawajui
kuishi pamoja na wengine, watu wanaochukia jumuiya, wasioweza kutawala mihemko, na familia
itapindua kuwa kiwanja cha vita. Ndiyo sababu Neno la Mungu linatuhimiza: "Uchungu wote na
ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu" (Efe 4:31). Uvumilivu huo
unaimarika ninapotambua kwamba pia mwingine huyu anayo haki ya kuishi duniani humu pamoja
na mimi, hivi alivyo. Haidhuru kama yeye huleta usumbufu kwangu, kama anabadili mipango
yangu, kama namna yake ya kuishi au mawazo yake hunisumbua, kama hawi katika yote kadiri
nilivyotegemea. Upendo unaendana daima na hisia ya kina ya huruma, inayoongoza kumpokea
mwingine kama sehemu ya dunia hii, pia anapotenda tofauti na nilivyotamani.
Moyo wa ufadhili
93. Linafuata neno krestevetai, ambalo ni pekee katika Biblia nzima, likitokana na krestos (mtu
mwema, anayeonyesha wema wake katika matendo). Lakini, kwa kuzingatia mahali hapa
linapopatikana, yaani sambamba kabisa na kitenzi kinachotangulia, linakuwa shamirisho yake.
Kwa namna hiyo, Paulo anataka kuweka dhahiri kwamba "uvumilivu" uliotajwa awali si hali ya
kutendwa tu, bali unaendana na utendaji maalumu, na marejesho yenye juhudi na ubunifu kuhusu
wengine. Unamaanisha kwamba upendo unawatendea wema wengine na unawaendeleza. Kwa
hiyo, tafsiri yake ni "wa fadhili".
94. Katika ujumla wa matini hii, inaonekana kwamba Paulo anataka kusisitiza ukweli wa kwamba
upendo si hisia tu, bali unatakiwa kufasiriwa katika maana ambayo kitenzi "kupenda" kinayo katika
lugha ya Kiebrania, yaani: "kutenda wema". Kama alivyosema mtakatifu Ignasi wa Loyola,
"upendo lazima utiwe katika matendo kuliko maneno".[106] Kwa namna hiyo, unaweza kuonyesha
uwezo wake mkuu wa kuzaa matunda, na unatuwezesha kung'amua furaha ya kutoa, ubora na
ukuu wa kujitolea kupita kiasi, bila kipimo, bila kudai thawabu, kwa ajili tu ya kutoa na kutumikia.
Kuponya husuda
95. Kwa hiyo inakataliwa kama kinyume cha upendo ule msimamo unaoelezwa na neno zelos
(wivu au husuda). Ina maana kwamba katika upendo hakuna nafasi ya kuchukizwa kwa sababu
ya mema anayopata mwingine (taz. Mdo 7:9; 17:5). Husuda ni uchungu kwa sababu ya mema
wanayopata wengine, unaodhihirisha kwamba sisi hatujali furaha ya wengine, kwani tunatafuta tu
manufaa yetu. Upendo unatutoa nje na sisi wenyewe, husuda inatusukuma kujikusanya ndani ya
umimi wetu binafsi. Upendo wa kweli unafurahia mafanikio ya wengine, bila kuwaona kama
kitisho, nao unajiokoa na uchungu wa husuda. Unakubali kwamba vipawa na njia ya maisha ya
kila mmoja hutofautiana. Kwa hiyo, unajitahidi kugundua njia yake pekee ili kuwa na furaha, na
kuwaachia wengine nao waione ya kwao.

4.4 Page 34

▲back to top
34
96. Kimsingi ni suala la kutimiza kilichoagizwa na amri mbili za mwisho za Sheria ya Mungu:
"Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala
mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako"
(Kut 20:17). Upendo unatuongoza kumthamini kwa dhati kila mwanadamu, kwa kutambua haki
yake ya kuwa na furaha. Ninampenda mtu yule, ninamtazama kwa mtazamo wa Mungu Baba,
atupaye vitu vyote "ili tuvitumie kwa furaha" (1Tim 6:17), na ndiyo sababu ninakubali ndani yangu
kwamba aweze kuifurahia nafasi njema. Kwa vyovyote, mzizi huuhuu wa upendo ni ule
unaoniongoza kukataa utovu wa haki ambao kwao wengine wana vitu vingi mno na wengine
hawana kitu, au ule unaonisukuma kutenda ili pia wale wanaotupwa na jamii waweze kuishi kwa
furaha walau kidogo. Hili lakini si husuda, bali ni hamu ya haki sawa.
Bila kutakabari wala kujivuna
97. Linafuata neno perperevetai, linalomaanisha majivuno, hamasa ya kujionyesha wakubwa
kuliko wengine na kuwashangaza kwa msimamo wa kisomi na mkali hasa. Mwenye kupenda, si tu
anajinyima kusema habari zake mwenyewe, lakini pia, kwa vile ametia wengine kama kiini cha
maisha yake, anajua kujitia katika nafasi yake, bila kudai kuwa kiini yeye mwenyewe. Neno
linalofuata – fisioutai – linafanana sana, kwa sababu linamaanisha kwamba upendo hauna kiburi.
Kwa fasiri sisisi linaelezea kwamba "haujikuzi" mbele ya wengine, na linadokeza jambo penyevu
zaidi. Si tu shauku isiyotulizika ya mtu kuonyesha sifa zake, lakini hupotezesha pia hisia ya
uhalisia wa mambo. Ni mtu kujihesabu mkubwa zaidi kuliko alivyo kwa sababu anaamini kuwa
yeye ni "wa rohoni" au "mwenye busara" zaidi. Paulo anatumia kitenzi hiki mara nyingine pia, kwa
mfano anaposema kwamba "ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga" (1Kor 8:1). Ndiyo
kusema kwamba wengine wanaamini kuwa ni wakubwa kwa sababu wanajua zaidi kuliko
wengine, na wanafanya bidii kudai mambo kutoka kwao na kuwadhibiti, wakati kile kinachotufanya
kuwa kweli wakubwa ni upendo unaowaelewa, kuwatunza na kuwategemeza walio dhaifu. Katika
aya nyingine analitumia ili kuwalaumu wale ambao "wanajivuna" (rej. 1Kor 4:18), lakini kiukweli
wanayo maneno tu kuliko "nguvu" ya kweli ya Roho (rej. 1Kor 4:19).
98. Ni muhimu wakristo waishi kwa msimamo huo katika namna yao ya kuwatendea ndugu zao
wasio na imani thabiti, au walio dhaifu au hawana uhakika katika fikra zao. Mara nyingine lililo
kinyume linatokea: wale ambao, ndani ya familia yao, inadhaniwa kwamba wamekua zaidi,
wanageuka kuwa watu wenye kiburi na wasiostahimilika. Moyo wa unyenyekevu unaonekana
hapa kama sehemu ya upendo, kwa sababu ili mtu aweze kuwaelewa, kuwasamehe na
kuwatumikia wengine kutoka moyoni, anapaswa kuponya kiburi na kusitawisha unyenyekevu.
Yesu alikuwa akiwakumbusha wanafunzi wake kwamba katika ulimwengu wa ukuu na mamlaka
kila mmoja anajitahidi kuwatawala wengine, na ndiyo maana anawaambia: "Haitakuwa hivyo
kwenu" (Mt 20:26). Mantiki ya upendo wa kikristo si ile ya mwenye kujisikia mkubwa kuliko
wengine na anahitaji kuwaonjesha uzito wa mamlaka yake, bali ni ile ambayo kwayo "mtu yeyote
anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu" (Mt 20:27). Katika maisha ya kifamilia
haiwezi kumiliki mantiki ya utawala wa mmoja juu ya mwingine, wala mashindano ili kuona ni nani

4.5 Page 35

▲back to top
35
aliye na akili zaidi au mwenye nguvu, kwani mantiki hiyo hufutilia mbali upendo. Pia kuhusu familia
lina nguvu himizo hili: "Ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu
Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema" (1Pet 5:5).
Adabu
99. Kupenda maana yake kutaka kupendeza pia, na hapo ndipo neno askemonei linapopata
maana yake. Linataka kuonyesha kwamba upendo hautendi kwa ufidhuli, haukosi kuwa na
heshima, sio mkali wa tabia. Matendo yake, maneno yake, ishara zake vina neema, wala si
vyenye kuchubua au ugumu. Huchukia kuwaumiza wengine. Uungwana "ni shule ya kuheshimu
hisia za wengine na ya kutotafuta faida ya binafsi" inayomdai mtu "achunge mawazo yake na hisia
zake, ajifunze kusikiliza, kunena na – wakati mwingine – kunyamaza".[107] Tabia ya kupendeza si
mtindo ambao mkristo aweza kuchagua au kukataa: ni sehemu ya masharti yasiyoepukika ya
upendo, kwa sababu "kila mwanadamu anapaswa kuwa na adabu mbele ya wale
wanaomzunguka".[108] Kila siku, “kuyaingilia maisha ya mwingine, hata kama yeye ni sehemu ya
maisha yetu, kunahitaji msimamo mpole na mvumilivu, unaompa upya daima imani na heshima.
[...] Na upendo, kwa kadiri unavyozidi kuwa wa ndani na wa kina, kwa kadiri hiyohiyo huzidi kudai
kuheshimu uhuru wa mwingine na kuweza kusubiri hadi mwingine atakapofungua mlango wa
moyo wake".[109]
100. Ili kujiandaa kukutana na mwingine katika ukweli, inatakiwa kuwa na mtazamo mpendevu juu
yake. Jambo hilo halitawezekana iwapo inatawala tabia ya kukosa rajua, inayosisitiza makasoro
na makosa ya mwingine, kana kwamba mtu ataka kufidia hisia zake za kuonewa. Mtazamo
mpendevu unatuwezesha kutobaki sana kutazama mapungufu wa mwingine, na hivyo tunaweza
kumvumilia na kuungana naye katika mradi wa pamoja, hata kama tuko tofauti. Upendo
mpendevu unazalisha vifungo, unasitawisha miungano, unaunda mitandao mipya ya
mtangamano, unajenga mfumo thabiti wa kijamii. Kwa namna hiyo unajilinda, kwa sababu bila
kujisikia kuwa wa mwingine mtu hawezi kustahimili hali ya kujitolea kwa wengine, na hatima ya
kila mmoja ni kutafuta tu maslahi yake binafsi, na kuishi pamoja kunakuwa jambo lisilo na
uwezekano. Mtu anayechukia jumuiya anaamini kwamba wengine wapo kwa ajili ya kutimiza
mahitaji yake, na kwamba wanapofanya hivyo ndipo wautimiza wajibu wao tu. Kwa hiyo hakuna
nafasi kwa upendevu wa upendo na wa misamiati yake. Mwenye kupenda anaweza kutamka
maneno ya kutia moyo, yenye kutuliza, yanayotia nguvu, yenye kufariji na kuhimiza. Tutazame,
kwa mfano, maneno machache ambayo Yesu alikuwa akiwaambia watu: "Jipe moyo mkuu,
mwanangu!" (Mt 9:2). “Imani yako ni kubwa!” (Mt 15:28). "Inuka!" (Mk 5:41). "Enenda zako kwa
amani" (Lk 7:50). "Msiogope" (Mt 14:27). Hayo si maneno yanayodhalilisha au kuhuzunisha,
yanayofadhaisha au yenye kudharau. Katika familia inatakiwa kujifunza lugha hii pendevu ya
Yesu.
Kujibandua na ubinafsi kwa ukarimu

4.6 Page 36

▲back to top
36
101. Tumewahi kusema mara nyingi kwamba tukitaka kuwapenda wengine inabidi kwanza
kujipenda wenyewe. Lakini, utenzi huu wa upendo unatamka kwamba upendo "hautafuti mambo
yake", au kwamba "hautafuti maslahi yake". Usemi huo unatumika pia katika sehemu nyingine:
"Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine" (Flp 2:4).
Mbele ya kauli hiyo ya Maandiko iliyo wazi namna hii, ni lazima tusiweke kipaumbele katika
kujipenda wenyewe kana kwamba ni jambo bora kuliko tendo la kujitolea kwa wengine. Kwa
namna fulani tu kuweka kipaumbele katika kujipenda ni sawa ikiwa kunaeleweka kama hali ya
kisaikolojia tu, kwa maana ya kwamba asiyeweza kujipenda anaona ugumu kuwapenda wengine.
"Aliye mbaya kwa nafsi yake, atakuwa mwema kwa nani? […] Hakuna mbaya zaidi kuliko yeye
anayejihusudu mwenyewe" (YbS 14:5-6).
102. Lakini Tomaso wa Akwino mwenyewe alieleza kwamba “ni sifa maalumu ya mapendo kutaka
zaidi kupenda kuliko kupendwa”[110] na kwamba, katika hali halisi, “kina mama, ambao ni wale
wanaopenda zaidi, wanatafuta zaidi kupenda kuliko kupendwa”.[111] Kwa hiyo upendo unaweza
kuvuka mipaka ya haki na kufurika bure, “bila kutumaini kupata malipo” (Lk 6:35), hadi kufikia
kilele cha upendo, ambao ni “kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine” (taz. Yn 15:13). Je, ukarimu
huu unawezekana bado, unaofanya tutoe bila kutumaini kupata malipo, na kutoa mpaka mwisho?
Bila shaka unawezekana, kwa sababu ndicho Injili inachodai: "Mmepata bure, toeni bure" (Mt
10:8).
Bila ukatili wa ndani
103. Ikiwa neno la kwanza la utenzi lilitualika kuwa na uvumilivu ule usiorejesha kwa hasira mbele
ya udhaifu au makosa ya wengine, sasa linaonekana neno jingine – paroksinetai – linaloelekeza
rejesho la ndani la uchungu linalosababishwa na tukio fulani la nje. Ni suala la ukatili wa ndani, la
hali ya kuchukizwa isiyodhihirika ambayo inatufanya tuwe na hisia ya kujihami mbele ya wengine,
kana kwamba watu ni maadui wachokozi ambao ni lazima kuepukana nao. Kulisha ujeuri huo wa
ndani haikusaidii kitu. Kunatudhoofisha, na hatima yake ni kututenga na wengine. Uchungu ni
mzuri pale ambapo unatusukuma kutenda lolote dhidi ya uonevu mkubwa, lakini ni hasara ukiathiri
kila namna yetu ya kuhusiana na wengine.
104. Injili inatualika kuangalia kwanza boriti iliyo ndani ya jicho letu (taz. Mt 7:5), na kama wakristo
hatuwezi kusahau kuwa Neno la Mungu mara nyingi linatualika kutochochea hasira: "Usishindwe
na ubaya" (Rum 12:21). "Tena tusichoke katika kutenda mema" (Gal 6:9). Kitu kimoja ni kuhisi
nguvu ya ujeuri unaotaka kujitokeza, na kitu kingine ni kuukubali, kuruhusu ukawe msimamo wa
daima. "Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka"
(Efe 4:26). Ndiyo sababu, haitakiwi kuacha iishe bila kuleta amani katika familia. "Na nilete amani
kwa namna gani? Kwa kupiga magoti? Hapana! Tendo dogo tu, kitu kidogo hivi, na amani inarudi
katika familia. Inatosha busu moja, si lazoma kusema neno. Lakini siku isiishe kamwe bila kuleta
amani katika familia!"[112] Kishindo cha ndani mbele ya usumbufu uliosababishwa na wengine
kingetakiwa kuwa hasa kubariki moyoni, kutamani wema wa mwingine, kumwomba Mungu

4.7 Page 37

▲back to top
37
amwokoe na kumponya: "Mwe watu wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa na Mungu
ili mrithi baraka" (1Pet 3:9). Tukitakiwa kushindana na uovu, tushindane, lakini kwa kusema daima
"hapana" mbele ya ukatili wa ndani.
Msamaha
105. Tunaporuhusu hisia mbaya ipenye nafsini mwetu, tunatoa nafasi kwa chuki ile kuvimba
moyoni. Maneno logizetai to kakon, maana yake ni "kuhesabu mabaya", "kuendelea
kuyakumbuka", yaani kutunza chuki. Kinyume chake ni msamaha. Msamaha wenye msingi katika
msimamo chanya, unaojaribu kuelewa udhaifu wa wengine na kutafuta udhuru kwa mtu mwingine,
kama vile Yesu alivyosema: "Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo" (Lk 23:34). Lakini
mara nyingi mwelekeo ni ule wa kutafuta zaidi na zaidi hatia [za mwingine], kuwaza zaidi mambo
maovu, kudhania kila namna ya nia mbaya, na kwa namna hiyo chuki inaongezeka na kutia mizizi.
Hivyo, kosa au kwazo lolote la mwenzi wa ndoa laweza kudhuru kifungo cha upendo na uthabiti
wa familia. Shida ni kwamba mara nyingine mtu anahesabu kila jambo kuwa na uzito sawa, kwa
hatari ya kuwa mkatili mbele ya kosa lolote la mwenzie. Jitihada iliyo halali ya mtu ya kudai haki
zake inageuka kuwa uchu wa daima na wa kudumu wa kulipa kisasi kuliko kuwa utetezi mzuri wa
hadhi ya mtu.
106. Baada ya kudharauliwa au kutahayarika, tendo la kusamehe linawezekana na linatamaniwa;
lakini hakuna asemaye kwamba li rahisi. Ukweli ni kwamba "umoja katika familia unaweza
kuhifadhiwa na kukamilishwa tu kwa moyo mkuu wa kujisadaka. Maana, unadai kwa wote na kwa
kila mmoja utayari mwepesi na mkarimu kwa maelewano, stahamala, msamaha na upatanisho.
Hakuna familia yoyote ambayo haijui kwamba ubinafsi, mabishano, mivutano, magomvi
hushambulia vikali na mara nyingine huupiga hadi kuufisha umoja wake: namna nyingi na
mbalimbali za mafarakano katika maisha ya kifamilia zinatokana na haya".[113]
107. Leo tunajua kwamba ili tuweze kusamehe tunahitaji kufanya kwanza mang'amuzi
yanayotuweka huru ya kujielewa na kujisamehe sisi wenyewe. Mara nyingi makosa yetu, au
mtazamo mkali wa watu tunaowapenda, vimetuondolea nia ya kujiheshimu. Na hilo linatuongoza
hatimaye kusita kuwakaribia wengine, kukimbia upendo, kujaa hofu katika mahusiano na watu
wengine. Na hivyo, kuwahukumu wengine kunageuka kuwa tulizo la uongo. Tunahitaji kusali
pamoja na historia ya maisha yetu, kujipokea jinsi tulivyo, kujua kuishi pamoja na makasoro yetu,
pia kujisamehe, ili kuweza kuwa na msimamo huohuo juu ya wengine.
108. Lakini kinachotakiwa kabla ya hayo ni mang'amuzi ya kuwa tumesamehewa na Mungu,
kuhesabiwa haki bure wala si kwa mastahili yetu. Tumefikiwa na upendo unaokuja kabla ya kila
tendo letu, unaotoa daima fursa mpya, unaohimiza na kuendeleza. Tukikubali kwamba upendo wa
Mungu hauna masharti, kwamba mahaba ya Baba hayanunuliwi wala kulipwa, hapo basi tutaweza
kupenda upeo, kuwasamehe wengine hata pale watakapokuwa wametutendea bila haki. La sivyo,
maisha yetu katika familia hayatakuwa tena nafasi ya kuelewana, kusindikizana na kuhimizana,

4.8 Page 38

▲back to top
38
bali yatakuwa tu kiwanja cha mizozo ya sikuzote na ya kupeana adhabu.
Kufurahi pamoja na wengine
109. Maneno hairei epi ti adikia yanamaanisha chochote kiovu kilichomo mtimani mwa moyo wa
mtu. Ni msimamo wenye sumu wa mtu anayefurahi anapoona kwamba wengine wanatendewa
pasipo haki. Sentensi hiyo inakamilishwa na maneno yanayofuata, yanayoelezea kwa jinsi
chanya: sinhairei ti alithia: hufurahi pamoja na kweli. Yaani, hufurahi mwingine anapopata mema,
inapotambuliwa hadhi yake, unapothaminiwa uwezo wake na matendo yake mema. Kufanya hivyo
haiwezekani kwa mtu anayetaka daima kujilinganisha na kushindana na wengine, hata na mwenzi
wake wa ndoa, kiasi cha kufurahi moyoni kila wanaposhindwa.
110. Kila mara mtu anayempenda mwingine anapoweza kumtendea mema, au anapoona kwamba
kwake yule mwingine mambo yote ni salama, na anafurahi kwa hayo na kwa namna hiyo
anamtukuza Mungu, kwani "Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo ya ukunjufu" (2Kor 9:7),
basi, Bwana wetu anapendezwa kwa namna ya pekee na yule mtu anayefurahi kwa furaha ya
mwingine. Tusipokuza uwezo wetu wa kufurahi kila mara mwingine apatapo mema na
tunazingatia hasa mahitaji yetu binafsi tu, tunajihukumia adhabu ya kuishi kwa furaha haba, kwa
vile Yesu alivyosema kwamba "Ni heri kutoa kuliko kupokea!" (Mdo 20:35). Familia inapaswa
kuwa daima mahali ambamo mmoja akitenda mema yoyote katika maisha, anajua kuwa humo
watayasherehekea pamoja naye.
Huvumilia yote
111. Orodha [ya sifa] inatimilizwa kwa maneno manne yanayosema ukamilifu: yanafuatwa na
neno “yote". Huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. Kwa namna hiyo,
unasisitizwa kwa nguvu uwezo wa upendo kama utamaduni kinzani, uwezao kukabili chochote
kinachoutishia.
112. Kwanza hutamkwa kwamba upendo "huvumilia yote" (panta stegi). Ni tofauti na usemi
"hauhesabu mabaya", kwa sababu neno hili linahusiana na matumizi ya ulimi; laweza kumaanisha
pia "kuutunza ukimya" juu ya mabaya yanayoweza kuwepo katika mtu mwingine. Pia linadokeza
nia ya kupunguza kuhukumu, kuzuia mwelekeo wa kulaumu kwa hasira kali na isiyo na huruma.
"Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa" (Lk 6:37). Ingawa linakwenda kinyume na matumizi yetu ya
kawaida ya ulimi, Neno la Mungu linatuagiza: "Ndugu, msisingiziane" (Yak 4:11). Kukazia
kuchafua sifa ya mwingine ni namna ya kujitukuza mwenyewe, ya kumtupia hasira na husuda zote
bila kujali madhara tunayosababisha. Mara nyingi tunasahau kwamba kusengenya huweza kuwa
dhambi kubwa, na kosa zito mbele ya Mungu, pale kunapoathiri vibaya sifa ya wengine na
kuwaletea madhara ambayo ni vigumu sana kuyaondoa baadaye. Ndiyo sababu Neno la Mungu
ni kali kiasi gani kuhusu ulimi, hadi kuusema kwamba ni "ulimwengu wa uovu" ambao "ndio uutiao
mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile" (Yak 3:6), "ni uovu usiotulia, umejaa

4.9 Page 39

▲back to top
39
sumu iletayo mauti" (Yak 3:8). Na iwapo "kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano
wa Mungu" (Yak 3:9), upendo huitunza sifa ya wengine, kwa ujazo wa uangalifu unaoweza kulinda
hata sifa njema ya walio adui. Katika kutetea sheria ya Mungu tunapaswa tusisahau kamwe sharti
hili la upendo.
113. Wanandoa wanaopendana na kuwa kila mmoja mali ya mwenzake, husema mema juu ya
mwingine, hujaribu kuonyesha sura njema ya mwenzi wa ndoa, licha ya udhaifu wake na makosa
yake. Kwa vyovyote, hutunza ukimya ili wasiidhuru sifa yake. Lakini si suala la tendo la nje, bali
latokana na msimamo wa ndani. Wala si ujinga wa mtu anayedai kutokuona magumu na
mapungufu wa mwingine, bali ni mtazamo mpana wa mwenye uwezo wa kuweka mapungufu na
makosa yale katika muktadha wake, mwenye kukumbuka kwamba makasoro hayo ni sehemu tu,
wala si ujumla wa nafsi ya mwingine. Kasoro moja katika uhusiano fulani si ujumla wa uhusiano
ule. Kwa hiyo twaweza kukubali kwa urahisi kwamba sote ni ambatano changamani la mianga na
vivuli. Mwenzangu si tu yule mwenye kunisumbua. Ni zaidi sana kuliko hilo. Kwa sababu hiyohiyo,
siwezi kudai kwamba upendo wake uwe mkamilifu ili nianze kuuthamini. Ananipenda kama alivyo
na kama awezavyo, kwa mapungufu yake, lakini upendo wake usipokuwa mkamilifu haimaanishi
kwamba si kweli au si halisi. Ni halisi, lakini una mipaka, ni wa duniani. Kwa hiyo, nikidai mno
kwake, kwa namna fulani atanifahamisha hilo, kwa sababu hataweza wala hatakubali kujielewa
kana kwamba yeye ni kiumbe cha mbinguni, wala hatavumilia kunitumikia katika mahitaji yangu
yote. Upendo unadumu pamoja na kutokamilika kwake, huvumilia, na hujua kubaki kimya mbele
ya mapungufu wa mwenzi mpendwa.
Unaamini
114. Panta pistevi: "huamini yote". Katika muktadha huu, "imani" hiyo haitakiwi kueleweka kwa
maana ya kiteolojia, bali kwa maana ya kawaida ya "kuwa na imani na mtu". Si tu suala la
kutokuwa na mashaka kwamba mwingine anaongopa au kudanganya. Imani hii ya msingi
inatambua ule mwanga uliowashwa na Mungu unaofichika ndani ya giza, au kinga kinachowaka
bado chini ya majivu.
115. Imani hiihii inawezesha kuwepo kwa uhusiano wenye uhuru. Hakuna haja ya kumdhibiti
mwenzi, ya kuchungulia kila hatua anakoenda, kwa lengo la kuzuia asitoke mikononi mwetu.
Upendo una imani, unaacha huru, hautaki kudhibiti kila kitu, kukamata, kutawala. Uhuru huo,
unaowezekanisha kuwepo kwa kila mmoja nafasi ya kujiamulia kwa hiari, kuwa wazi kwa
ulimwengu unaotuzunguka na kwa mang'amuzi mapya, unaruhusu uhusiano kati ya wenzi wa
ndoa utajirishwe wala ile isibaki kuwa ndoa ijifungayo ndani bila upeo wa fikra. Kwa namna hiyo,
wenzi wa ndoa, kila wanapokutana, waweza kuishi furaha ya kushirikishana yale waliyopokea na
kujifunza walipokuwa nje ya duru ya familia. Wakati huohuo unawezekanisha ukweli na uwazi,
kwa sababu pale ambapo mmoja ajua kwamba wengine wana imani naye na wanathamini wema
wake wa ndani, papo hapo yeye anajionyesha kama alivyo, bila kuficha lolote. Kama mmoja
anajua kwamba kila dakika wana mashaka juu yake, kwamba wanamhukumu bila huruma,

4.10 Page 40

▲back to top
40
wanashindwa kumpenda bila kudai lolote, atapendelea kutunza siri zake, kuficha maanguko na
udhaifu wake, kujisingizia kuwa tofauti na alivyo. Kinyume chake, familia ambamo imani thabiti na
yenye upendo inatawala, na ambamo kila mmoja daima anarudia kuwa na imani na wengine licha
ya tukio lolote, inawezesha kuchanua tabia ya kweli ya kila mwanafamilia na inajenga moyo wa
kukataa moja kwa moja udanganyifu, uongo na ulaghai.
Hutumaini
116. Panta elpizi: haukati moyo juu ya mustakabali. Kwa kuungana na neno linalotangulia,
linadokeza tumaini la yeye ambaye anajua kwamba mwenzie anaweza kubadilika. Unatumaini
daima ukomavu uweze kuwepo, kuchanua uzuri kama kwa namna ya ajabu, na kwamba vipaji vya
ndani zaidi vya maumbile yake vifunuke siku moja. Si kusema kwamba mambo yote yatabadilika
katika maisha haya. Inadokeza kukubali kwamba mambo mengine hayaendi sawa kama mmoja
anavyotazamia, lakini kwamba labda Mungu ananyosha yaliyopotoka ya mwingine na kuzalisha
mema fulani kutoka kwa maovu ambayo huyo hawezi kushinda katika dunia hii.
117. Hapa linajitokeza tumaini katika maana yake timilifu, kwa sababu linahusisha uhakika wa
kuwepo maisha baada ya kifo. Mtu yule, pamoja na udhaifu wake wote, anaitwa kwenye utimilifu
wa Mbinguni. Huko, akiisha kugeuzwa kikamilifu na ufufuko wa Kristo, hakutakuwepo tena udhaifu
yake, giza lake wala makasoro yake. Kule, nafsi halisi ya mtu huyo itang'aa kwa uwezo wake wote
wa wema na uzuri. Aidha, hilo litatuwezesha kumtazama mtu yule, kati ya masumbufu ya dunia
hii, kwa mtazamo wa kimbingu, kwenye mwanga wa tumaini, na kusubiri ule utimilifu ambao siku
moja ataupokea katika Ufalme wa mbinguni, ingawa kwa sasa hauonekani.
Hustahimili yote
118. Panta ipomeni, maana yake ni kwamba inastahimili kwa roho chanya yote yaliyo kinzani.
Inamaanisha kudumu imara katika mazingira yenye uadui. Si tu kuyastahimili mambo machache
yanayoleta usumbufu, ila ni msimamo wenye mtazamo mpana zaidi: ni upinzani wa kimkikimkiki
na wa kudumu, unaoweza kushinda changamoto yoyote. Ni upendo licha ya yote, hata pale
mazingira yanaposhauri kuwa na hisia nyingine. Unaonyesha kiasi cha uhodari thabiti, cha nguvu
dhidi ya mkondo wowote wa ubaya, chaguo la wema ambalo hakuna kitu kinachoweza kulipindua.
Hayo yananikumbusha maneno ya Martin Luther King, alipokuwa akisisitiza chaguo la upendo wa
kindugu hata kati ya madhulumu na madhalilisho mabaya sana. "Mtu anayekuchukia kuliko wote,
anacho walau kitu kilicho chema ndani yake; hata taifa linalochukia zaidi, lina chochote chema
ndani yake; pia kabila lenye kuchukia zaidi, lina chochote chema ndani yake. Na unapofikia
kwenye hatua ya kumtazama usoni kila mwanadamu na kuona sana ndani yake kile ambacho dini
inakiita "mfano wa Mungu", ndipo unapoanza kumpenda licha ya yote. Haidhuru anachofanya,
wewe unaona ndani yake mfano wa Mungu. Kuna punje ya wema ambayo huwezi kuifutulia mbali
kamwe [...]. Namna nyingine ya kumpenda adui wako ndiyo hii: unapopata fursa ya kumshinda
adui wako, ndipo wakati wa kuamua usitende hivyo [...]. Unapojiinua kwenye upeo wa upendo, wa

5 Pages 41-50

▲back to top

5.1 Page 41

▲back to top
41
uzuri na uwezo wake mkubwa, kitu pekee unachotaka kukishinda ni mifumo miovu. Watu
walionaswa na mfumo ule wewe unawapenda, lakini unajaribu kushinda mfumo ule [...]. Kulipa
chuki kwa chuki kunakuza tu kuwepo kwa chuki na uovu ulimwenguni. Kama mimi ninakupiga
wewe, na wewe unanipiga mimi, nami ninakurudishia pigo nawe unanirudishia pigo, na hivyo
kadhalika, ni wazi kuwa tutaendelea bila mwisho. Yaani hatutamaliza kamwe. Kwa upande fulani,
mmoja lazima awe na busara walau kidogo, naye ndiye mtu mwenye nguvu. Mtu mwenye nguvu
ni mtu awezaye kuvunja mnyororo wa chuki, mnyororo wa uovu [...]. Inapaswa apatikane ambaye
anayo imani na maadili ya kutosha ili kuuvunja na kupenyeza kwenye mfumo wenyewe wa
ulimwengu kipengere chenye nguvu na uweza cha upendo”.[114]
119. Katika maisha ya kifamilia kuna hitaji ya kusitawisha nguvu hiyo ya upendo, inayowezesha
kushindana dhidi ya uovu unaoyatishia. Upendo haukubali kutawaliwa na chuki, na dharau dhidi
ya watu, na hamu ya kujeruhi au kulipiza chochote. Lengo la Ukristo, na kwa namna ya pekee
katika familia, ni upendo licha ya yote. Inatokea kwamba ninaguswa, kwa mfano, na msimamo wa
watu waliolazimishwa kuachana na mwenzi wa ndoa ili kujilinda na ukatili wa kimwili, na hata
hivyo, kutokana na mapendo ya kindoa yanayojua kuvuka hisia, wameweza kumtendea mema,
ijapokuwa kwa kupitia wengine, katika nafasi za ugonjwa, za mateso au za shida. Hata huo ni
upendo licha ya yote.
Kukua katika mapendo ya kindoa
120. Utenzi wa mtakatifu Paulo, tuliouchambua, unatuwezesha kuelekea sasa kwenye mapendo
ya kindoa. Hayo ndio upendo unaowaunganisha wanandoa,[115] uliotakatifuzwa, kutajirishwa na
kuangazwa na neema ya sakramenti ya ndoa. Ni “muungano wa kimahaba”,[116] wa kiroho na wa
kujisadaka, ambao lakini unakusanya ndani yake upole wa urafiki na nyege ya kiashiki, ingawa
unaweza kuendelea kuwepo hata wakati ambapo hisia na hamu zitakuwa zimedhoofika. Papa
Pius XI alifundisha kuwa upendo wa namna hii unapenya katika kila wajibu wa maisha ya
wanandoa na "unashika kama nafasi ya kwanza katika ubora".[117] Kwani, huo upendo thabiti,
uliomiminwa na Roho Mtakatifu, ni kioo cha Agano lisilovunjika baina ya Kristo na wanadamu,
lililotimilika katika kujitoa mpaka mwisho, juu ya msalaba: "Roho, ambaye Bwana anamimina,
analeta kipaji cha moyo mpya na anawafanya mwanamume na mwanamke waweze kupendana
kama Kristo alivyotupenda. Upendo kati ya wanandoa unafikia ule utimilifu ambao ndio shabaha
yake ya ndani, yaani mapendo ya kindoa".[118]
121. Ndoa ni ishara yenye thamani, kwa sababu "kila mara mwanamume na mwanamke
wanaadhimisha sakramenti ya Ndoa, ni kana kwamba Mungu ‘angejiakisi’ ndani yao, inachora
ndani yao sura yake na tabia isiyofutika ya upendo wake. Ndoa ni ikona ya upendo wa Mungu
kwetu. Maana, pia Mungu ni ushirika: nafsi tatu ya Baba, ya Mwana na ya Roho Mtakatifu huishi
tangu milele na hata milele katika umoja kamili. Nalo ndilo fumbo la Ndoa: Mungu anawafanya
wanandoa wale wawili wawe ni umoja wa maisha".[119] Hilo lina matokeo yanayoonekana katika
maisha ya kila siku, kwa sababu wanandoa, “kwa nguvu ya Sakramenti, wanakabidhiwa utume

5.2 Page 42

▲back to top
42
halisi na maalumu, ili weweze kuonyesha, kutokana na mambo ya kawaida na rahisi, ule upendo
ambao Kristo amelipenda Kanisa lake, akiendelea kutoa uhai wake kwa ajili yake”.[120]
122. Lakini, si vema kuchanganya mambo ya viwango tofauti: haitakiwi kuwabebesha watu wawili
wenye udhaifu mzigo unaotisha wa kulazimika kunakili umoja kamili uliopo baina ya Kristo na
Kanisa lake, kwani ndoa kama ishara inajumuisha pia "safari ya maisha ambayo inaendelea,
hatua kwa hatua, katika kujaliwa na kupokea zaidi na zaidi karama za Mungu".[121]
Kwa maisha yote, mambo yote katika umoja
123. Baada ya upendo unaotuunganisha na Mungu, upendo kati ya wanandoa ni "aina ya urafiki
iliyo kubwa kuliko zote".[122] Ni muungano wenye sifa zote za urafiki mwema: kutafuta mema ya
mwingine, kutendeana kwa usawa, ukaribu sana, tulizo, udumifu, na mfanano kati ya rafiki
unaojengeka katika kushiriki maisha ya pamoja. Lakini ndoa inaongeza juu ya hayo yote umoja
usiochanganyikana na wengine na usiovunjika, unaojionyesha katika mpango thabiti wa kushiriki
na kujenga pamoja maisha yote. Tuwe wakweli na tutambue ishara ya hali halisi: anayemchumbia
mtu hapangi kwamba uhusiano huo uweze kudumu kwa muda tu, anayeishi kwa ari furaha ya
kufunga ndoa haidhanii itakuwa jambo la kupita; wanaosindikiza adhimisho la muungano uliojaa
upendo, ijapo dhaifu, watumai uweze kudumu sikuzote; watoto si tu wanatamani wazazi wao
wapendane, lakini pia wawe waaminifu na wadumu umoja daima. Ishara hizi, na nyingine pia,
zinaonyesha kwamba upo katika maumbile yenyewe ya upendo wa kindoa utayari wa kuutambua
kuwa ndio jambo la daima. Muungano unaothibitishwa kwa ahadi ya daima ya ndoa, ni zaidi ya
utaratibu wa kijamii au mapokeo, kwa sababu mizizi yake imo katika maelekeo ya dhati ya
binadamu; na, kwa waamini, ni agano mbele ya Mungu linalodai uaminifu: "Bwana amekuwa
shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni
mwenzako, na mke wa agano lako: […] mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo
ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana" (Mal 2:14,15,16).
124. Upendo ulio dhaifu au mlegevu, usioweza kupokea ndoa kama changamoto inayohitaji
wanandoa wawe tayari kupambana na magumu, kuhuishwa tena na tena, kujibuni na kuanza
upya daima hadi kifo, hauwezi kustahimili juhudi za hali ya juu. Unashindwa na utamaduni wa
yaliyo ya muda tu, unaozuia mchakato endelevu wa ukuzi. Lakini "kuahidi upendo wa daima
kunawezekana pale unapovumbuliwa mpango ulio mkuu zaidi kuliko miradi yetu binafsi,
unaotutegemeza na kutuwezesha kutoa maisha yetu yote ya mbeleni kwa yule
tunayempenda".[123] Ili upendo wa namna hiyo uweze kushinda majaribu yote na kudumu kuwa
mwaminifu licha ya yote, inatakiwa iombwe zawadi ya neema yenye kuuimarisha na kuuinua.
Kama alivyosema mtakatifu Roberto Belarmino, "tukio la kwamba mwanamume na mwanamke
wanaungana na mwenzi mmoja tu kwa kifungo kisichovunjika, kwa namna ambavyo hawataweza
kutengana, licha ya magumu yoyote yatakayojitokeza, na hata likipotea tumaini la kupata watoto,
jambo hilo haliwezi kutokea pasipo fumbo kubwa".[124]

5.3 Page 43

▲back to top
43
125. Aidha, ndoa ni urafiki wenye sifa zile zilizo maalumu za tamaa, lakini inayoelekea daima
kwenye muungano ulio zaidi na zaidi thabiti na wenye mhemuko. Kwani ndoa “haikuwekwa kwa
ajili ya uzazi tu”, lakini pia ili upendo wa mmoja kwa mwenzie “uwe na madhihirisho yake ya haki,
usitawi na kufikia kwenye ukomavu”[125]. Urafiki huo wa pekee kati ya mwanamume na
mwanamke unapata tabia ya kujumuisha yote ambayo ni maalumu katika muungano wa
wanandoa. Na kwa vile muungano huo unajumuisha yote, ndiyo sababu ni pia wa mwenzi mmoja,
una uaminifu na uko wazi kupokea watoto. Kwao, kila kitu ni cha kushirikishana, ikiwa ni pamoja
na ujinsia, daima katika kuheshimiana. Mtaguso Mkuu wa Vatikano II ulisisitiza jambo hilo kwa
kusema kwamba "upendo wa namna hiyo, unaounganisha pamoja tunu za kibinadamu na za
kimungu, huwaongoza wanandoa kujitoa kwa hiari kila mmoja kwa mwenzie; kadhalika,
unathibitishwa na hisia na vitendo vya upendo mtamu na kupenya vipengele vyote vya maisha ya
wanandoa".[126]
Furaha na uzuri
126. Katika ndoa ni vema kusitawisha furaha ya upendo. Pale ambapo kusaka ashiki kunashikilia
kila tamaa, kunawafunga wanandoa katika uwanja mmoja tu wala hakuruhusu kuona namna
nyingine za ridhaa. Kinyume chake, furaha inapanua uwezo wa kustarehe na inaruhusu
kuyafurahia mambo mbalimbali, hata katika awamu za maisha ambapo ashiki hufifia. Ndiyo
sababu mtakatifu Tomaso alisema kwamba neno "furaha" latumika ili kuelezea kuongeza kwa
kimo cha moyo.[127] Furaha ya ndoa, inayoweza kung'amuliwa hata katika mateso, inajumuisha
pia kukubali kwamba ndoa lazima iwe ni mseto wa furaha na uchungu, wa mivutano na utulivu, wa
mateso na uhuru, wa kuridhika na kutafuta, wa masumbufu na matulizo, daima katika mwendo wa
urafiki, unaosukuma kila mwanandoa kumtunza mwenzake: "wakisaidiana na kutumikiana".[128]
127. Upendo wa kirafiki unaitwa "mapendo" pale ambapo panahisiwa na kuheshimiwa "thamani
kuu" ya mwingine.[129] Uzuri, yaani “thamani kuu” ya mwingine ambayo si moja kwa moja vivutio
vya mwili wake au vya saikolojia yake, unatuwezesha kuonja utakatifu wa nafsi yake bila hitaji la
nguvu la kummiliki. Katika jamii ya ulaji hisia ya ujumi hudhoofika na hivyo furaha huzimika. Kila
kitu kipo ili kinunuliwe, kimilikiwe na kuliwa; hata watu. Kinyume chake, urafiki mwanana ni
dhihirisho la upendo huo unaojinasua na tamaa ya kiumimi ya kumiliki kila kitu kibinafsi.
Unatusukuma kuhamanika mbele ya mtu kwa heshima kuu na kwa hofu fulani ya kumdhuru au ya
kumwibia uhuru wake. Upendo kwa mwenzio unajumuisha pia faraja hii ya kutazama na
kupendezewa na kila chema na kitakatifu cha nafsi yake, ambayo ipo licha ya ujumla wa kumhitaji
kwangu. Hayo yananiwezesha kutafuta mema kwa ajili yake pia ninapojua kwamba hawezi kuwa
wangu, au mwili wake utakapokuwa haupendezi tena, au yeye amekuwa mkali au msumbufu.
Kwa hiyo, "kutokana na upendo ambao kwao mmoja anapendezwa na mwingine, unategemea
ukweli wa kwamba atampatia chochote kwa bure".[130]
128. Mang'amuzi ya kiujumi ya upendo yanadhihirika katika mtazamo ule unaomwangalia
mwingine kwa heshima, kama mwenye kikomo katika yeye mwenyewe, hata endapo yu mgonjwa,

5.4 Page 44

▲back to top
44
mzee au hana tena mivutio ya kihisia. Mtazamo unaoweza kuthamini una umuhimu mkubwa sana,
na, kwa kawaida, kuupunguza unaleta madhara. Wanandoa na watoto wao mara nyingine
wanafanya mambo mangapi ili kutazamwa na kuhesabiwa kwamba wapo! Majeraha mengi na
migogoro mingi asili yake ndiyo pale tunapoacha kutazamana kwa heshima. Hilo ndilo jambo
ambalo manung'uniko na malalamiko mengine yanayosikika katika familia yanalitokeza. "Mume
wangu haniangalii, mimi kwake ni kama mtu asiyeonekana". "Tafadhali, uniangalie ninapoongea
nawe". "Mke wangu haniangalii tena, sasa macho yake ni kwa watoto tu". "Nyumbani hakuna
anayenijali, wala hawanioni, ni kama mimi singalikuwepo". Upendo huyafumbua macho na
kutuwezesha kuona thamani ya binadamu, licha ya yote.
129. Furaha ya upendo wa namna hii uwezao kutazama inapaswa kusitawishwa. Kwa vile sisi
tulivyoumbwa ili kupenda, tunajua kwamba hakuna furaha iliyo kubwa zaidi kuliko kushirikishana
mema: "Toa na kupokea, na ujiburudishe roho yako" (YbS 14:16). Furaha kali zaidi katika maisha
zinatokea pale ambapo mtu anaweza kusababisha furaha kwa wengine, kama malimbuko ya
Mbinguni. Inafaa kukumbusha onyesho lile zuri la filamu "Karamu ya Babette", ambamo yeye
mpishi mkarimu anakumbatiwa kwa nia ya kumshukuru na kumsifu: "Utawapendeza namna gani
hata malaika!". Ni tamu na yenye kuleta faraja ile furaha inayotokana na kuwapatia wengine tulizo,
kuwaona wanafurahi. Furaha hiyo, tunda la upendo wa kindugu, si ile ya majisifu ya mwenye
kujitazama yeye tu, bali ni ile ya mwenye kupenda na kufurahia mema ya mpendwa, unaoelekea
mwenzi na unakuwa wenye kuzaa matunda ndani yake.
130. Kwa upande mwingine, furaha hufanywa upya katika huzuni. Kama alivyosema mtakatifu
Augustino, "kadiri ilivyokuwa kubwa hatari ya mapigano, ndivyo inavyokuwa kubwa furaha ya
ushindi".[131] Baada ya kuteseka na kushindana kwa pamoja, wenzi wa ndoa wanaweza
kung'amua kwamba ilikuwa muhimu kufanya hivyo, kwa sababu wamejipatia chochote kilicho
chema, wamejifunza chochote kwa pamoja, au kwa sababu wanaweza kufurahia zaidi kile
ambacho tayari wanacho. Kuna furaha chache za kibinadamu ambazo ni za kina na heri kama
pale ambapo watu wawili wanaopendana wamefanikisha kwa pamoja kitu ambacho kilihitaji juhudi
kubwa ya kushirikishana.
Kufunga ndoa kwa upendo
131. Ninataka kuwaambia vijana kwamba hakuna lolote la hayo linalohatarishwa iwapo upendo
unachukua taratibu za taasisi ya ndoa. Muungano unapata katika taasisi hiyo namna ya kuwa na
dira kwa uthabiti wake na kwa ukuzi halisi na kweli. Ni kweli kwamba upendo ni zaidi kuliko
ukubaliano wa nje au kuliko aina fulani ya mkataba wa ndoa, lakini vilevile ni kweli kwamba
uamuzi wa kuipa ndoa muundo unaoonekana katika jamii, ambao una wajibu maalumu,
unadhihirisha umuhimu wake: unaonyesha umakini wa kujitambua kitu kimoja na mwenzi,
unaashiria kuachana na ile tabia ya ubinafsi wa ujanani, na kuelezea uamuzi mkataa wa kuwa kila
mmoja mali ya mwenzie. Kufunga ndoa ni namna ya kuonyesha wazi kwamba kweli mtu ameacha
kiota cha wazazi ili kufunga mahusiano mengine thabiti na kushika wajibu mpya mbele ya mtu

5.5 Page 45

▲back to top
45
mwingine. Hilo lina thamani kubwa zaidi kuliko ushirikiano tu wa hiari kwa ajili ya kupendezana,
ambao ungekuwa ubinafsishaji wa ndoa. Ndoa kama taasisi ya kijamii ni ulinzi na chombo kwa ajili
ya ahadi waliyopeana, kwa kukomaza upendo, ili uamuzi kwa mwingine ukue katika uthabiti,
ukweli na kina, na wakati huohuo ili uweze kutimiza utume wake katika jamii. Ndiyo sababu ndoa
unashinda kila mtindo wa mpito na inadumu. Uwamo wake unatokana moja kwa moja na
maumbile yenyewe ya binadamu na tabia yake ya kijamii. Ndoa inajumuisha masharti kadhaa,
yanayotokana lakini na upendo wenyewe, na upendo ulioamua kabisa na unataka kujitolea na
unaweza kukabiliana na changamoto za mbeleni.
132. Kuchagua ndoa kwa namna hiyo kunaonyesha uamuzi halisi na kweli wa kufanya kwamba
njia mbili zigeuke kuwa njia moja tu, liwalo na liwe na licha ya changamoto yoyote. Kutokana na
ukweli wa ahadi hiyo ya hadharani ya kupendana, uamuzi huo hauwezi kuwa wa haraka, lakini
kwa sababu hiyohiyo hauwezi kuahirishwa bila mwisho. Kuweka ahadi ya kuishi na mwenzi
mmoja kwa namna ya kudumu kuna daima kiwango cha hatari na cha kamari hodari. Kukataa
kufanya uamuzi huo kunaonyesha tabia ya ubinafsi, yenye kutafuta maslahi yake tu, finyu, ya mtu
asiyeweza kutambua haki za mwenzie wala hafikii kamwe kwenye hatua ya kumtambulisha kwa
jamii kama anayestahili kupendwa bila mwisho. Kwa upande mwingine, wale ambao
wanachumbiana kwelikweli, wanataka kwamba upendo wao ujulikane kwa wengine. Upendo
unaokuwa thabiti katika ndoa ifungwayo mbele ya watu, pamoja na masharti yote yanayotokana
na kujifunga kwa taasisi hiyo, ni dhihirisho na ulinzi wa ile "ndiyo" inayotamkwa kwa hiari na bila
mipaka. Ile "ndiyo" inamaanisha nia ya kumwambia mwenzi kwamba ataweza kuwa daima na
imani nami, kwamba hatatelekezwa iwapo atapoteza mvuto, kama atakutwa na magumu, au kama
zitapatikana kwangu fursa nyingine za kujipendezesha au maslahi ya kibinafsi.
Upendo unaojidhihirisha na kukua
133. Upendo wa urafiki unaunganisha vipengele vyote vya maisha ya ndoa na kuwasaidia
wanafamilia wote kuendelea mbele katika awamu zake zote. Kwa hiyo, vitendo vinavyoonyesha
upendo wa namna hiyo vinatakiwa vistawishwe siku kwa siku, bila ubahili, vikiwa vimejaa maneno
ya ukarimu. Katika familia "ni lazima kutumia maneno matatu. Ningependa kusisitiza tena.
Maneno matatu: tafadhali, asante, samahani. Maneno matatu ya msingi!"[132] Pale ambapo
katika familia hakuna mwenye kutiisha na wote wanaomba kwa kusema ‘tafadhali’, pale ambapo
katika familia hakuna ubinafsi na wote hujifunza kusema ‘asante’, na kila mara mmojawapo
anapogundua kwamba ametenda jambo baya na anajua kusema ‘samahani’, katika familia ile
kuna amani na furaha”.[133] Tusiwe wanyimifu katika kutumia maneno hayo, tuwe wepesi katika
kuyarudia siku baada ya siku, kwa sababu “kuna namna za ukimya zinazolemea, mara nyingine
hata katika familia, baina ya mume na mke, kati ya wazazi na watoto, kati ya
ndugu”.[134] Kinyume chake, maneno yanayofaa, ya kusemwa wakati muafaka, yanatunza na
kukuza upendo siku baada ya siku.
134. Haya yote yanatekelezwa katika mwendo wa ukuzi endelevu. Aina hii ya pekee ya upendo

5.6 Page 46

▲back to top
46
iliyo ndoa, huitwa kukomazwa siku kwa siku, kwani inatakiwa kutumika kwa ajili yake usemi
ambao mtakatifu Tomaso wa Akwino alisema kuhusu mapendo: "Mapendo, kutokana na
maumbile yake, hayana kikomo katika ukuzi wake, kwa vile yanavyoshiriki maumbile ya mapendo
yale yasiyo na mipaka, yaani ya Roho Mtakatifu. […] Wala hayawezi kutiwa mipaka na mwenye
kuwa nayo, kwa sababu kwa njia ya kukua mapendo, hukua zaidi na zaidi pia uwezo wa kuyakuza
hata zaidi."[135] Mtakatifu Paulo alihimiza kwa nguvu: "Bwana na awaongeze na kuwazidisha
katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote" (1The 3:12); na akaongeza: “Katika habari ya
upendano [...] twawasihi, ndugu, mzidi sana” (1The 4:9-10). Zaidi sana. Upendo wa ndoa
haulindwi kabla ya yote kwa kutaja tabia yake ya kutokuvunjika kama ya sharti, au kwa kukariri
mafundisho fulani, bali kwa kuuimarisha kwa njia ya ukuzi wa daima kwa msukumu wa neema.
Upendo usiokua unaanza kuhatarika, na twaweza kukua tu kwa kuiitikia neema ya Mungu kwa
njia ya matendo mengi zaidi ya upendo, kwa vitendo vya mahaba vya mara kwa mara, vyenye
mhemuko zaidi, vyenye ukarimu zaidi, vya kutuliza zaidi, vyenye uchangamfu zaidi. Mume na mke
"wanang'amua maana ya umoja kati yao na wanazidi kuufikia kwa ukamilifu zaidi".[136] Zawadi ya
upendo wa Mungu unaowajaza wanandoa ni wakati huohuo mwito wa kuisitawisha daima zawadi
hii ya neema.
135. Hazifai njozi nyingine juu ya upendo wa hadithi tamu na ulio kamili, unaonyimwa kwa namna
hiyo kila changamoto ya kuukuza. Dhana ya kimbinguni ya upendo wa kidunia husahau kwamba
hali iliyo bora ndiyo ile ambayo bado haijafikiwa, ni divai inayoivishwa na miaka. Kama
walivyokumbusha Maaskofu wa Chile, "Familia zilizo kamili kama yanavyotuonyesha matangazo
ya kibiashara na ya kiulaji hazipo. Kwa familia hizo miaka haipiti, wala hayapo magonjwa, wala
huzuni, wala kifo [...]. Matangazo ya kiulaji yanaonyesha ndoto mazingaombwe isiyolingana katu
na hali halisi ambayo kina baba na kina mama wa familia zetu wanapaswa kukabiliana nayo siku
kwa siku.[137] Ni sahihi zaidi kuyakubali kwa dhana halisi mapungufu, changamoto na makasoro,
na kusikiliza miito ya kukua pamoja, ya kukomaza upendo na kusitawisha uthabiti wa muungano,
licha ya lolote linaloweza kutokea.
Mazungumzano
136. Mazungumzano ni namna bora na isiyoepukika ya kuishi, kuonyesha na kukomaza upendo
katika maisha ya ndoa na ya familia. Lakini yanahitaji uanagenzi mrefu na mzito. Wanaume kwa
wanawake, wazee kwa vijana, wana namna tofauti za kuwasiliana, wanatumia misamiati tofauti,
wanaishi kadiri ya kanuni nyingine nyingine. Namna ya kuuliza maswali, namna ya kutoa majibu,
sauti inayotumika, wakati na mambo mengine mengi yaweza kuathiri mawasiliano. Aidha, daima
ni muhimu kuchochea misimamo ambayo inaonyesha upendo na kuwezesha mazungumzano ya
kweli.
137. Kujipatia muda, na muda ulio bora, wa kusikiliza kwa uvumilivu na umakini, hadi mwingine
amesema yote aliyohitaji kusema. Hayo yanadai mtu afanye bidii ya kutoanza kusema kabla ya
wakati mwafaka. Badala ya kuanza kutoa maoni au mashauri, inatakiwa kuhakikisha kuwa

5.7 Page 47

▲back to top
47
tumesikiliza yote ambayo mwingine anahitaji kusema. Hilo linahitaji pia kutunza ukimya wa ndani
ili kusikiliza bila kelele moyoni na akilini: kuvua kila haraka, kuweka pembeni mahitaji na
vipaumbele vyetu binafsi, na kuwapatia wengine nafasi. Mara nyingi mwenzi hahitaji utatuzi wa
matatizo yake, ila tu anachotafuta ni kusikilizwa. Anahitaji kuhisi kwamba uchungu wake
umegunduliwa, au kushindwa kwake, au hofu, au hasira, au tumaini lake, au matarajio yake.
Lakini mara nyingi husikika malalamiko kama haya: "Hanisikilizi. Inapoonekana kwamba labda
ananisikiliza, kwa kweli anawaza kitu kingine". "Ninaongea; lakini ninahisi kwamba anasubiri tu
hatimaye nimalize kunena". "Ninapoongea mimi, anajaribu kuanza kuongea kitu kingine, au
ananijibu haraka haraka ili kufunga mazungumzo".
138. Kuchochea mazoea ya kumjali kweli mwenzio. Yaani, kuthamini nafsi yake, kutambua
kwamba yeye anayo haki ya kuwepo, ya kuwa na mawazo yake, ya kuwa na furaha. Lazima
yasipuuzwe yale anayosema au kudai, ingawa inafaa kuelezea mtazamo wako pia. Chini ya
dhana hiyo kuna imani ya kwamba kila mmoja anao mchango wake wa kutoa, kwa sababu wote
wana mang'amuzi mbalimbali ya maisha, kila mmoja anayaangalia mambo kwa mtazamo
mwingine, amegundua wasiwasi tofauti na kuwa na ustadi au uvumbuzi wake. Inawezekana
kutambua ukweli wa mwenzio, umuhimu wa kero zake za ndani zaidi na maana ya chinichini ya
yale anayoyatamka, hata yakiwa yamefichwa na maneno ya ukali. Kwa sababu hiyo inabidi
kujaribu kujiweka katika nafasi yake na kufasiri kina cha moyo wake, kufumbua ni nini
kinachompendeza zaidi na kuchukua kitu kile anachokitamani kama chanzo cha kuanzisha na
kuendeleza mazungumzano.
139. Upana wa mawazo, kusudi la kutojifungia katika dhana chache kwa hofu isiyotulia, na utayari
wa kubadili au kukamilisha maoni yangu: haya ni mambo ya muhimu. Inawezekana kwamba
kutokana na mawazo yangu na mawazo ya mwenzangu upatikane usanisi unaotutajirisha wote
wawili. Umoja ambao tunahitaji kutarajia si wote kuwa sawa, bali ni "umoja katika utofauti" au
"utofauti uliopatanishwa". Katika mtindo huo unaotajirisha ushirika wa kindugu, walio tofauti
wanakutana, wanaheshimiana na kuthaminiana, pamoja na kutunza kila mmoja vidokezo na
misisitizo yake pekee ambayo inatajirisha manufaa ya wote. Tunahitaji kujiokoa na faradhi ya
kudhani kwamba tunapaswa wote kufanana. Pia unatakiwa werevu ili kugundua mapema "kelele"
zinazoweza kujipenyeza, zisije zikaharibu mchakato wa mazungumzano. Kwa mfano, ni muhimu
kutambua hisia mbaya zinazozuka na kuweza kuzipunguza ili zisiathiri mawasiliano. Ni muhimu
kuweza kutamka yale ninayohisi, bila kujeruhi, kutumia lugha na namna ya kuongea ambazo
zaweza kupokelewa au kuvumiliwa kwa urahisi zaidi na mwenzangu, ingawa maudhui huenda ni
mazito; kueleza malalamiko yangu lakini bila kufoka kwa hasira kama kwa kulipa kisasi, na
kuachana kabisa na kutumia lugha ya kudhalilisha inayotafuta tu kushambulia, kuzomea,
kulaumu, kuumiza. Magomvi mengi katika jozi yanatokea kwa sababu zisizo nzito sana. Mara
nyingine ni mambo madogo, yasiyo na maana sana; lakini kinachoozesha mioyo ni ile namna ya
kuyatamka au msimamo ambao kila mmoja anachukua katika mazungumzano.
140. Kuwa na vitendo vya kumjali mwenzio na kumwonyesha mahaba. Upendo hushinda vizuizi

5.8 Page 48

▲back to top
48
vyote, hata vilivyo vikubwa mno. Inapotokea kwamba twampenda mtu au twajisikia kwamba yeye
anatupenda, twaweza kuelewa kwa urahisi zaidi anachotaka kusema na kutueleza. Twaweza
kushinda udhaifu unaotufanya tuwe na hofu mbele ya mwenzi kana kwamba ni "mshindani"
wangu. Ni muhimu sana mtu ajenge msimamo wake thabiti juu ya machaguo yaliyofanywa kwa
makini, juu ya imani na tunu, wala si juu ya kushinda katika mjadala mmoja au kwa sababu ataka
akukubaliwe kuwa na haki.
141. Hatimaye, tunatambua kwamba ili mazungumzano yawe na mafanikio inatakiwa kuwa na
chochote cha kusema, na jambo hilo linahitaji tuwe na utajiri wa ndani unaojilisha kwa kusoma,
kutafakari binafsi, kusali na kuwa wazi kwa jamii. Vinginevyo, mazungumzo yanakuwa ya
kuchosha na yasiyo na maana. Inapotokea kwamba kila mwenzi wa ndoa hailishi roho yake wala
hakuna mahusiano ya namna nyingi na watu wengine, maisha ya kifamilia yanakuwa ya ndoa
ijifungayo ndani na mazungumzano yanakuwa hafifu.
Upendo wa tamaa
142. Mtaguso wa Vatikano wa II ulifundisha kwamba upendo huo kati ya wanandoa "unauhusu
wema wa mtu mzima. Kwa sababu hiyo, upendo huo unaweza kuzitajirisha hisia za rohoni na
matendo yake ya kimwili kwa heshima ya pekee; na pia yaweza kuzitukuza hisia na matendo hayo
kama ishara na alama mahsusi za urafiki wa kindoa".[138] Lazima viwepo visa fulani
vinavyosababisha kwamba upendo usio na faraja wala tamaa hautoshi ili kuashiria muungano kati
ya moyo wa binadamu na Mungu: "Wamistiki wote wamesisitiza kwamba upendo wa kimungu na
upendo wa kimbingu unatafuta ishara zake na kuzipata tu katika upendo kati ya wanandoa, kuliko
kwenye urafiki, au kuliko hisia ya kimwana, au kuliko kufanya juhudi kwa kusudi maalum. Na
sababu yake kwa haki ipo katika utimilifu wake”.[139] Kwa nini, basi, tusichukue muda kusema
kuhusu hisia na ujinsia katika ndoa?
Ulimwengu wa mihemuko
143. Hamu, hisia, mihemuko, mambo haya ambayo wasomi wa zamani walikuwa wanaita
"tamaa", yanachukua nafasi muhimu katika ndoa. Yanazaliwa pale ambapo "mwingine" anatokea
na kujionyesha katika maisha ya mtu. Ni kawaida ya kila kiumbe chenye uhai kuvutwa kwenye kitu
kingine, na mvuto huo unaonyesha kila mara ishara za msingi za huba: faraja au huzuni, furaha
au uchungu, tulizo au hofu. Haya ni sababu za utendaji wa msingi wa kisaikolojia. Binadamu ni
kiumbe hai katika dunia hii na kila anachokifanya na kukitafuta kimejaa tamaa.
144. Yesu, kwa jinsi alivyokuwa binadamu kwelikweli, alikuwa anayaishi mambo yote kwa ujazo
wa mihemuko. Ndiyo sababu, alijaa huzuni alipokataliwa na Yerusalemu (rej. Mt 23:37), na hali
hiyo ilimsababisha alie machozi (rej. Lk 19:41). Hali kadhalika, yeye alikuwa anaona huruma
mbele ya mateso ya watu (rej. Mk 6:34). Alipoona wengine wanalia machozi, yeye aliugua rohoni
akafadhaika (rej. Yn 11:33); na Yeye mwenyewe akalia machozi kwa sababu ya kifo cha rafiki (rej.

5.9 Page 49

▲back to top
49
Yn 11:35). Madhihirisho haya ya hisia zake yalionyesha kwa kiasi gani moyo wake ulikuwa wazi
kwa wengine.
145. Kupata mhemuko si jambo ambalo kimaadili ni jema au baya kwa lenyewe.[140] Kuanza
kuona hamu au chuki si jambo lenye dhambi au la kulaumiwa. Lililo jema au baya ni tendo ambalo
mtu analitenda akisukumwa au akiambaa na tamaa fulani. Lakini, ikiwa hisia zinachochewa,
zinatafutwa na kwa sababu ya hizo tunatenda matendo maovu, uovu umo katika uamuzi wa
kuzichochea na katika matendo maovu yanayotokana nazo. Kwa maana hiyohiyo, kupendezwa na
mtu si moja kwa moja jambo jema. Ikiwa kwa kupendezwa naye mimi ninatenda ili mtu yule akawe
mtumwa wangu, hisia ile itakuwa kwa ajili ya ubinafsi wangu. Kuamini kwamba sisi ni wema kwa
sababu tu "tunahisi kitu fulani" ni kujidanganya vibaya. Kuna watu ambao wanajihisi kuweza kuwa
na upendo mkubwa kwa sababu tu wana hitaji kubwa la kupendwa, lakini hawawezi kuipigania
furaha ya wengine, nao wanaishi wamejifungia katika tamaa zao. Kwa namna hiyo, hisia
zinapeleka mbali na tunu zilizo kuu na zinaficha ndani yake umimi usiowezesha kuyasitawisha
maisha katika familia yaliyo mazuri na yenye furaha.
146. Kinyume chake, ikiwa tamaa inaendana na tendo huru, inaweza kudhihirisha kina cha
chaguo lile. Upendo wa kindoa unaelekeza kujitahidi ili maisha yote ya kimihemuko yawe jambo
jema kwa familia, nayo yaweze kusaidia maisha ya pamoja. Familia unafikia ukomavu pale
ambapo maisha ya kimihemuko ya wanafamilia wake yanageuka kuwa tabia yenye kukataa
kutawala au kufunika machaguo makuu na tunu, na – kinyume chake – huhakikisha uhuru
wake,[141] inayatajirisha, inayapamba na kuyafanya mwanana zaidi kwa mema ya wote.
Mungu anapenda furaha ya watoto wake
147. Hayo yanahitaji mwendo wa kipedagojia, mchakato unaosababisha kiasi fulani cha kujinyima.
Hilo ni sehemu ya imani ya Kanisa ambayo mara nyingi haikukubaliwa, kana kwamba i adui ya
furaha ya binadamu. Benedikto XVI alipokea swali hilo kwa wazi kabisa: "Kanisa kwa njia ya amri
zake na marufuku linayoweka si kwamba pengine linageuza kuwa uchungu kile kitu kizuri kuliko
vyote vya maisha? Je, si kwamba huenda limeweka alama za makatazo pale penyewe ambapo
furaha, iliyoandaliwa na Muumba kwa ajili yetu, inatupatia faraja inayotuonjesha tayari kitu kilicho
cha Kimungu?"[142] Lakini yeye alikuwa akijibu kwamba, ijapo havikukosekana katika Ukristo amri
ya kupita kiasi au kujinyima kupotovu, mafundisho rasmi ya Kanisa, yaliyo aminifu kwa Maandiko
Matakatifu, hayakukataa “mapenzi kwa yenyewe, lakini yamepiga vita dhidi ya tabia ya
kuyaumbua na kuyatia uharibifu, kwani juhudi ya kuyageuza mapenzi kuwa kama miungu ya
uongo [...] inayanyima hadhi yake, na kuyafanya kuwa ni kitu kisichomstahili binadamu”.[143]
148. Kulea mihemuko na silika ya mtu ni lazima, na kwa lengo hilo mara nyingine ni lazima
kujiwekea mipaka fulani. Kuzidisha kiasi, kukosa kujidhibiti, kufuatilia kwa pupa aina moja tu ya
anasa, mwisho wake ni kudhoofisha na kuozesha anasa na tamaa yenyewe,[144] na kuyadhuru
maisha ya familia. Kwa kweli inawezekana kutimiza mwendo mzuri na tamaa, maana yake

5.10 Page 50

▲back to top
50
kuzielekeza zaidi na zaidi kwenye mpango wa kujitolea na kujitimiliza unaotajirisha mahusiano ya
watu ndani ya familia. Hilo halimaanishi kujikatalia vipindi vya furaha kubwa,[145] lakini kuvipokea
katika mfumo wa vipindi vingine vya kujitolea kwa ukarimu, vya tumaini lenye kuvumia, vya
uchovu usioepukika, vya juhudi kwa lengo maalumu. Maisha katika familia ndivyo hivyo vyote,
nayo yanastahili tuyaishi kwa utimilifu.
149. Kuna madhehebu ya kitasaufi yanayosisitiza umuhimu wa kufuta kila hamu ili kuepukana na
huzuni. Lakini sisi tunaamini kwamba Mungu anapenda furaha ya binadamu, na kwamba Yeye
ameviumba vitu vyote "ili tuvitumie kwa furaha" (1Tim 6:17). Tuache furaha ifurike mbele ya
upendo wake mwanana anapotuambia: "Mwanangu, ujifanyizie mema [...]. Usijinyime siku ya
furaha” (YbS 14:11,14). Pia jozi la wanandoa linaitikia mapenzi ya Mungu kwa kufuata mwaliko
huu wa Biblia: "Siku ya kufanikiwa ufurahi" (Mhu 7:14). Suala ni kuwa na uhuru wa kukubali
kwamba mapenzi yapate namna nyingine ya kujidhihirisha katika nafasi mbalimbali za maisha,
kadiri ya mahitaji ya upendo wa kila mmoja kwa mwenzie. Kwa maana hiyo, inawezekana
kupokea shauri la walimu wengine wa Mashariki ambao wanasisitiza juu ya kupanua dhamiri, ili
kutonaswa katika mazoea yaliyo finyu mno ambayo yangebana matazamio yetu. Kupanua huko
kwa dhamiri si kukatalia au kuteketeza hamu, bali ni kutanuliwa na kukamilishwa kwake.
Upendo kama mapenzi
150. Hayo yote yanatuelekeza kutaja maisha ya kimapenzi ya wenzi wa ndoa. Mungu mwenyewe
ndiye aliyeumba ujinsia, ambao ni zawadi nzuri ajabu kwa viumbe vyake. Kwa kuyaheshimu na
kuachana na kukosa kuyadhibiti, tunazuia isitokee "udhalilishaji wa tunu hiyo
halisi".[146] Mtakatifu Yohane Paulo II alifukuzia mbali dhana ya kwamba mafundisho ya Kanisa
yanaleta kwenye "kukataa thamani ya ujinsia wa binadamu” au kwamba yanauvumilia tu “kwa
hitaji lenyewe ya kuzaa watoto”.[147] Hitaji la kijinsia la wenzi wa ndoa si suala linalodharaulika
wala “kwa vyovyote si hoja kulitilia mashaka hitaji hilo”.[148]
151. Kwa wale wanaohofia kwamba kwa njia ya malezi ya tamaa na ujinsia huweza kuhatarishwa
uhiari wa upendo wa kujamiiana, mtakatifu Yohane Paulo II alijibu kwamba binadamu "huitwa
kufikia uhiari kamilifu na mkomavu wa mahusiano", ambao ni "tunda linalopatikana hatua kwa
hatua la upambanuzi wa misukumo ya mioyo ya mtu".[149] Ni kitu kinachopatikana kwa
kukipigania, kwa vila kila binadamu “anapaswa kujifunza kwa subira na msimamo maana ya kweli
ya mwili”.[150] Ujinsia si mali yenye lengo la kupendezesha au kuburudisha, kwa sababu ni lugha
baina ya watu wawili, pale ambapo mwenzi anajali mwenzake, ikiwa ni pamoja na thamani yake
takatifu na isiyonyakuliwa. Kwa namna hiyo, "moyo wa binadamu anashiriki, tuseme hivi, uhiari wa
mwingine".[151] Katika muktadha huu, mapenzi yanaonekana kuwa dhihirisho la ujinsia lililo
maalum kwa binadamu. Ndani yake inawezekana kukuta ile "maana ya kindoa ya mwili, na hadhi
halisi ya kuwa zawadi".[152] Katika katekesi zake juu ya teolojia ya mwili wa binadamu, mtakatifu
Yohane Paulo II amefundisha kwamba hali ya mwili kuwa na ujinsia “si tu chimbuko la uwezo wa
kuzaa matunda na wa uzaaji wa watoto”, bali inao ndani yake “uwezo wa kudhihirisha upendo:

6 Pages 51-60

▲back to top

6.1 Page 51

▲back to top
51
yaani, upendo ule ambao kwao mtu-nafsi anakuwa zawadi".[153] Mapenzi yaliyo safi zaidi, ijapo
yameungana na hamu ya kutafuta ashiki, inatangulizwa na ushangao, na kwa hiyo yaweza
kuzifanya tamaa ziwe za kiutu.
152. Kwa hiyo, kwa namna yoyote ile hatuwezi kufasiri hali ya kimapenzi ya upendo kama uovu
ulioruhusiwa au kama mzigo wa kubebwa kwa ajili ya mema ya familia, bali kama zawadi ya
Mungu inayotia nakshi kwenye kukutana kwa wenzi wa ndoa. Kwa vile ni tamaa iliyoboreshwa na
upendo unaoheshimu hadhi ya mwenzi, inakuwa "dhihirisho kamilifu na angavu la upendo" lenye
kutuonyesha jinsi moyo wa binadamu unavyoweza maajabu, na hivyo kwa kitambo "huonjwa
kwamba maisha ya binadamu yamekuwa mafanikio".[154]
Ukatili na ulaghai
153. Katika muktadha ya mtazamo huo chanya ya ujinsia, inafaa kulitazama suala hili katika
ujumla wake na kwa utambuzi halisi ulio sahihi. Maana, hatuwezi kusahau kwamba mara nyingi
ujinsia unatenganishwa na utu, pia unajaa magonjwa, kwa jinsi ya kwamba "unakuwa zaidi na
zaidi nafasi na chombo cha kutawaza umimi wa mtu na cha kujiridhisha kibinafsi katika tamaa na
mivuto".[155] Katika nyakati hizi imekuwa kubwa ile hatari ya kwamba hata ujinsia unatawaliwa na
roho yenye sumu ya "tumia ukatupe”. Mwili wa mwenzi mara nyingi hufanywa kana kwamba ni kitu
cha kutwaa hadi hapo unapokuridhisha na cha kutupa hapo unapopoteza mvuto. Itawezekanaje
kuzisahau au kuficha zile namna endelevu za kutawala, kuonea, kunyanyasa, za ufasiki na ukatili
wa kijinsia, ambazo ndiyo matunda ya ughoshaji wa maana ya ujinsia na ambazo zinafukia hadhi
ya wengine na wito wa upendo chini ya hamu ya kigiza ya kusaka ridhaa za binafsi?
154. Si ya ziada kukumbusha kwamba pia katika ndoa ujinsia unaweza kugeuka kuwa asili ya
mateso na vurugu. Ndiyo sababu ni lazima tusisitize kwa wazi kwamba "kumshurutisha mwenzi
wa ndoa kufanya tendo la ndoa bila kujali hali yake na hamu zake za haki si tendo halisi la upendo
na kwa hiyo kunaenda kinyume na madai ya utaratibu wenye haki wa kimaadili mintarafu
mahusiano baina ya wenzi wa ndoa."[156] Matendo maalumu ya muungano wa kijinsia wa wenzi
wa ndoa yanaendana na maumbile ya ujinsia alivyopanga Mungu ikiwa “yametekelezwa kwa
namna iliyo ya kibinadamu kwelikweli”.[157] Ndiyo sababu mtakatifu Paulo alihimiza: "Mtu
asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili" (1The 4:6). Ingawa yeye aliandika katika
zama ambapo ulikuwa ukitawala utamaduni wa kibabe, ambamo mwanamke alihesabiwa mwenye
hali ya chini kabisa kulingana na mwanamume, hata hivyo alifundisha kwamba ujinsia ni suala
ambalo lahitaji mawasiliano baina ya wenzi wa ndoa: alidokeza uwezekano wa kunyimana kwa
muda mahusiano ya kijinsia, lakini "isipokuwa mmepatana" (1Kor 7:5).
155. Mtakatifu Yohane Paulo II alitoa tahadhari ya busara sana aliposema kwamba mwanamume
na mwanamke "wanatiishwa na hali ya kutoshiba".[158] Maana yake, wanaitwa kwenye
muungano unaokuwa mkubwa zaidi na zaidi, lakini hatari ni kudai kufuta tofauti zilizopo na ule
umbali usioepukika uliopo kati ya hao wenzi wawili. Kwa sababu kila mmoja anayo hadhi yake

6.2 Page 52

▲back to top
52
isiyo kifani. Pale ambapo ile hali yenye thamani ya kuwa kila mmoja mali ya mwenzie inageuka
kuwa unyanyaso, "muundo wa ushirika katika uhusiano baina ya watu unabadilika
kimsingi".[159] Katika mantiki ya kutaka kutawala, pia yule anayetawala mwisho wake ni kukataza
hadhi yake mwenyewe[160] na kuachana na “kujitambua kibinafsi kitu kimoja na mwili
wake”,[161] kwa kadiri anavyounyima maana yoyote. Anaishi ngono kama kukimbia mbali naye
mwenyewe na kama katazo kwa uzuri wa muungano.
156. Ni muhimu kuwa wazi katika kukataa kila namna ya unyanyasaji wa kijinsia. Kwa hiyo inafaa
kuepukana na kila aina ya ufasiri usio sahihi wa maneno ya Waraka kwa Waefeso yanayoagiza
kwamba “wake watii waume zao” (Efe 5:22). Mtakatifu Paulo hapa anaandika kwa kufuata dhana
za kitamaduni zilizo maalum kwa wakati wake, lakini sisi hatupaswi kujivika utamaduni huo, bali
kupokea ujumbe uliofunuliwa ndani ya ujumla wa matini hiyo. Tuchukue tena maelezo yenye
busara aliyotoa mtakatifu Yohane Paulo II: "Upendo unazuia kila aina ya unyanyasaji, ambao
kwao mke angekuwa mtumishi au mtumwa wa mume [...]. Jumuiya au umoja ambao wao
wanatakiwa kuunda kwa sababu ya ndoa, unafanyika kwa njia ya kujitoa kila mmoja kama zawadi
kwa mwenzie, tendo ambalo ni pia kila mmoja kujiweka chini ya mwenzie".[162] Ndiyo sababu
inasemwa pia kwamba “inawapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe” (Efe
5:28). Kihalisi maneno haya ya Biblia yanaalika kushinda ustarehe wa ubinafsi ili kuishi kwa
kuwaelekea wengine: "Mnyenyekeane katika kicho cha Kristo" (Efe 5:21). Kati ya wenzi wa ndoa
"kunyenyekeana" huku kunapata maana maalumu na kunaeleweka kama uamuzi wa hiari wa
kuwa kila mmoja mali ya mwenzie, ikiwa ni pamoja na sifa ya uaminifu, heshima na matunzo.
Ujinsia ni kwa namna isiyofutika msaada kwa urafiki wa namna hiyo kati ya wenzi wa ndoa, kwa
sababu unaelekea kufanya mwingine aweze kuishi kwa utimilifu.
157. Lakini, kuukataa ughushaji wa ujinsia na mapenzi kusingetakiwa kutuongoza kamwe
kuvidharau au kuvipuuzia. Lengo bora la ndoa haliwezi kuelezwa tu kama kujitoa kwa ukarimu na
kujisadaka, ambako kila mmoja anajikatalia hitaji lolote la kibinafsi na anajali tu kutenda kwa ajili
ya mema ya mwenzie bila ridhaa yoyote kwake binafsi. Inafaa tukumbuke kwamba upendo wa
kweli unajua pia kupokea mema kutoka kwa mwingine, unaweza kujitambua kama wenye vidonda
na mahitaji, haukatai kupokea kwa shukrani zenye furaha na ukweli vitendo vya kimwili vya
upendo katika bembelezo, katika kumbatio, katika busu na katika muungano wa kijinsia.
Benedikto XVI alikuwa wazi kuhusu jambo hilo: "Ikiwa binadamu anatarajia kuwa roho tu, na
kukataa mwili kama urithi ulio wa kinyama tu, hapo roho na mwili hupoteza hadhi yake".[163] Kwa
sababu hiyo “binadamu wala hawezi kuishi katika upendo tu wa kujisadaka na kujishusha. Hawezi
daima kutoa zawadi tu, anapaswa pia kupokea zawadi. Anayetaka kutoa upendo, lazima yeye
mwenyewe aupokee kama zawadi".[164] Jambo hilo linadai, kwa vyovyote, kwamba tukumbuke
kuwa msimamo wa mtu ni dhaifu, kwamba daima kuna chochote kinachokataa kufanywa kuwa
cha kiutu na kwamba wakati wowote hicho chaweza kulipuka upya, na kuchukua tena mielekeo
yake ya kiasili na kibinafsi zaidi.
Ndoa na ubikira

6.3 Page 53

▲back to top
53
158. "Watu wengi wanaoishi bila kufunga ndoa sio tu wanajitolea kwa ajili ya familia yao ya asili,
lakini pia hutoa huduma nyingi katika duru ya marafiki zao, katika jumuiya ya kikanisa na katika
maisha ya kitaaluma. [...] Zaidi ya hayo, wengi wanatumia talanta zao kwa kuitumikia jumuiya ya
kikristo katika ishara ya matendo ya huruma na ya kujitolea. Halafu wapo wasiofunga ndoa kwa
sababu wanaweka wakfu maisha yao kwa kumpenda Kristo na ndugu zao. Kwa njia ya juhudi zao
familia, katika Kanisa na katika jamii, hutajirishwa sana".[165]
159. Kuishi katika ubikira ni aina ya upendo. Kama ishara, unatukumbusha moyo wa
kujishughulisha kwa ajili ya Ufalme, utayari wa kujitolea bila mipaka kwa utumishi wa uinjilishaji
(rej. 1Kor 7:32), pia ni kioo cha utimilifu wa Mbinguni, ambapo "hawaoi wala hawaolewi" (Mt
22:30). Mtakatifu Paulo aliupendekeza sana kwa sababu alikuwa akitazamia kuwa Yesu atarudi
mara na alitaka wote wapate kuwa makini juu ya uinjilishaji pekee: "Muda ubakio si mwingi" (1Kor
7:29). Lakini ilikuwa wazi kwamba hilo lilikuwa oni lake binafsi na matamanio yake (rej. 1Kor 7:6-8)
wala si agizo la Kristo: "Sina amri ya Bwana" (1Kor 7:25). Wakati huohuo, alikiri thamani ya miito
mbalimbali: "Kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi"
(1Kor 7:7). Kwa maana hiyo mtakatifu Yohane Paulo II alisema kwamba Maandiko Matakatifu
“hayatoi sababu ya kutegemeza wazo la kuwa ndoa 'ina mapungufu', wala kuwa ubikira au useja
'ni bora zaidi'”[166] kwa sababu ya kujinyima tendo la ndoa. Zaidi kuliko kunena juu ya ukuu wa
ubikira kwa hali zote, inaonekana kufaa zaidi kuonyesha kwamba hali mbalimbali za maisha
zinakamilishana, kwa namna ya kwamba hali moja inaweza kuwa kamili zaidi kwa sehemu fulani,
na ile hali nyingine inaweza kuwa kamili zaidi kwa mtazamo mwingine. Aleksanda wa Hales, kwa
mfano, alisema kwamba kwa namna fulani ndoa inaweza kuhesabiwa kubwa kuliko sakramenti
nyinginezo: kwa sababu inaisharisha kitu kilicho kikubwa sana, yaani "muungano wa Kristo na
Kanisa au umoja wa tabia ya kimungu na maumbile ya kibinadamu".[167]
160. Kwa hiyo, “si suala la kupunguza hadhi ya ndoa ili kuongeza thamani ya kujinyima tendo la
ndoa”[168] na “kinyume chake hakuna msingi wowote wa kutegemeza ushindani kati yake [...].
Endapo, kufuatana na mapokeo fulani ya kiteolojia, inawezekana kutaja hali ya ukamilifu (status
perfectionis), hutajwa hivyo si kwa sababu tu ya kujinyima tendo la ndoa, bali kuhusiana na ujumla
wa maisha yenye misingi juu ya mashauri wa kiinjili".[169] Hata hivyo, mtu wa ndoa anaweza
kuishi mapendo kwa kiwango cha juu kabisa. Na hivyo "anaufikilia ule ukamilifu unaotokana na
mapendo, kwa njia ya kuwa mwaminifu kwa roho ya mashauri yale. Ukamilifu huo unawezekana,
nao u karibu na kila mtu".[170]
161. Ubikira unayo thamani ya kiishara ya upendo usiohitaji kummiliki mwenzi, na unaakisi kwa
namna hiyo uhuru wa Ufalme wa Mbinguni. Ni mwaliko kwa wanandoa ili waishi upendo wao wa
ndoa katika mtazamo wa upendo kamili kwa Kristo, kama mwendo wa pamoja kuelekea utimilifu
wa Ufalme. Kwa upande wake, upendo wa wanandoa unaonyesha tunu nyingine za kiishara: kwa
upande mmoja, ni kioo mahsusi cha Utatu Mtakatifu. Maana Utatu Mtakatifu ni umoja kamili,
ambamo ndani yake unaendelea kuwepo pia utofauti. Zaidi ya hayo, familia ni ishara ya Kristo,
kwa sababu inadhihirisha ukaribu wa Mungu anayeshiriki maisha ya binadamu kwa kuungana

6.4 Page 54

▲back to top
54
naye katika Umwilisho, katika Msalaba na katika Ufufuko. Na kila mwanandoa anakuwa "mwili
mmoja" na mwenzie wa ndoa, na anajitoa mwenyewe ili kushirikishana na mwenzie mpaka
mwisho. Wakati ubikira ni ishara ya "kieskatolojia" ya Kristo mfufuka, ndoa ni ishara "katika
historia" kwa ajili ya wale wanaosafiri duniani, ishara ya Kristo wa duniani aliyekubali kuungana
nasi na kujitoa hadi kumwaga damu yake. Ubikira na ndoa ni, kama ilivyo lazima viwe, namna
tofauti za kupenda, kwa sababu "binadamu hawezi kuishi bila upendo. Maana, mtu anaendelea
kuwa kwa mwenyewe kiumbe kisichoeleweka, na maisha yake hayana maana, kama upendo
haufunuliwi kwake”.[171]
162. Useja una hatari ya kuwa upweke wenye mustarehe, unaojalia uhuru wa kujitegemea, wa
kuhama mahali wajibu na machaguo, wa kuweza kutumia pesa binafsi, wa kuhusiana na watu
mbalimbali kadiri ya mvuto wa kila muda. Ikiwa hivyo, unang'aa zaidi ushuhuda wa watu wa ndoa.
Walioitwa kuishi ubikira waweza kuona katika majozi mengine ya wanandoa ishara wazi ya
uaminifu wenye ukarimu na usioharibika wa Mungu kwa Agano lake, inayoweza kuchochea mioyo
yao kujitolea na kujisadaka kimatendo hata zaidi. Na kwa kweli wapo watu wa ndoa ambao
wanadumisha uaminifu wao pale ambapo mwenzi ameumbuka kimwili, au asipoweza kuridhisha
mahitaji yao, hata ikiwa mara nyingi mazingira yanawaalika kukosa uaminifu au kumtelekeza
mwenzi. Mwanamke aweza kumwuguza mume wake aliye mgonjwa, na huko, karibu na Msalaba,
anarudia ile "ndiyo" ya upendo wake hadi kufa. Katika upendo wa jinsi hii inadhihirishwa kwa
namna angavu hadhi ya mwenye kupenda, hadhi iliyo kama kioo cha mapendo, kwa sababu ni
sifa ya mapendo kupenda kuliko kupendwa.[172] Twaweza pia kushuhudia katika familia nyingi
uwezo wa kujitoa kuwatumikia kwa upendo mwanana wana ambao ni wagumu au hata
wanaokosa shukrani. Kuishi hivi kunawafanya wazazi kuwa ishara ya upendo wa Yesu ulio wa
hiari na usiotafuta shukrani. Hayo yote yanakuwa mwaliko kwa waseja ili waishi juhudi zao kwa
ajili ya Ufalme kwa utayari na ukarimu zaidi. Leo mfumo wa kutukuza malimwengu umeutilia giza
muungano wenye kudumu kwa maisha yote, na umepunguza utajiri wa juhudi katika ndoa, na kwa
sababu hiyo "inapasa kuyahimiza yale mambo mazuri ya upendo kati ya wanandoa".[173]
Mabadiliko ya upendo
163. Maisha yarefuka, na hivyo inatokea kisichokuwa kawaida zamani: uhusiano wa ndani na hali
ya kuwa kila mmoja mali ya mwenzie hupaswa kudumishwa kwa miongo minne, mitano au sita,
nalo ladai kurudia kuchaguana tena na tena. Labda mtu wa ndoa havutwi tena na ashiki kali
inayomleta karibu na mwenzie, lakini husikia faraja ya kuwa mali yake na kwamba mwenzie ni
mali yake, ya kujua kwamba yeye siye peke yake, kwamba anaye "mwananjama" anayejua yote
ya maisha yake na ya historia yake, na ambaye anashiriki kila kitu naye. Ni yule mwenzi katika
mwendo wa maisha ambaye pamoja naye huwezekana kukabili mambo magumu na kufurahia
yaliyo mazuri. Pia hayo yanazalisha ridhaa inayoendana na hamu iliyo pekee ya upendo kati ya
wanandoa. Hatuwezi kudai kuwa na hisia zilezile kwa maisha yetu yote. Lakini bila shaka twaweza
kuwa na mpango wa pamoja ulio thabiti, kujitahidi kupendana na kuishi pamoja hadi hapo kifo
kitakapotutenganisha, na kuishi sikuzote kwa upendo mpevu wa ukaribu sana. Upendo

6.5 Page 55

▲back to top
55
tunaoahidiana unashinda kila mhemuko, hisia au hali ya moyo, hata kama huweza kuvihusisha. Ni
kupenda upeo, kwa uamuzi wa moyo unaoathiri kila siku ya maisha. Na hivyo, katika mgogoro
usiotulizwa, na ingawa hisia nyingi zinachangamana moyoni bila utaratibu, linadumu hai kila siku
azimio la kupenda, la kuwa kila mmoja mali ya mwenzie, la kushiriki maisha yote na kuendelea
kupendana na kusameheana. Kila mmoja katika jozi anatimiza mwendo wa ukuzi na ubadiliko wa
nafsi yake. Katika mkondo wa mwendo huo, upendo unaadhimisha kila hatua na kila mede mpya.
164. Katika historia ya kila ndoa, sura ya kimwili hubadilika, lakini hilo si sababu ya mvuto wa
kimapenzi kupotea. Mtu anamchumbia mtu mzima mwenye tabia na maumbile yake pekee, si tu
mwili, ingawa mwili huo, licha ya uchakavu unaosababishwa na wakati, haumalizi kamwe
kuonyesha kwa namna fulani ile tabia ya pekee iliyologa moyo wake. Wengine watakaposhindwa
kutambua tena uzuri wa tabia ile, mwenzie apendanaye anaendelea kuweza kuuona kwa hisi ya
upendo, na mahaba hayatoweki. Anasisitiza tena azimio lake la kuwa mali ya mwenzie,
anamchagua tena na kuonyesha uamuzi wake kwa kuwa karibu naye kwa uaminifu na kwa
upendo uliojaa tulizo. Ubora wa uamuzi wake kwa ajili ya mwenzie, kwa vile ulivyo na nguvu na
wa kina, unaamsha namna mpya ya mhemuko katika kutimiza utume wa mwanandoa. Kwani
"mhemuko uliosababishwa na binadamu mwingine kama nafsi [...] hauelekezi moja kwa moja
kwenye tendo la ndoa".[174] Unajipatia namna nyingine za kujionyesha kwa sababu upendo “ni
uhalisia mmoja, ingawa una hali mbalimbali; kila mara, hali moja au nyingine inajitokeza
zaidi”.[175] Kifungo kinapata namna nyingi mpya na kinadai ufanyike uamuzi wa kuanza tena na
tena kukiweka. Lakini si tu ili kukihifadhi, bali ili kikuzwe. Ni mwendo wa kujengana siku kwa siku.
Lakini hakuna lolote la haya ambalo linawezekana bila kumwomba Roho Mtakatifu, na bila kulia
kila siku na kuomba atujalie neema yake, bila kutafuta nguvu zake za kimbingu, na bila kumsihi
kwa nguvu ili amimine moto wake juu ya upendo wetu ili kuutilia nguvu, kuuelekeza na kuufanya
upya katika kila hali mpya inayojitokeza.
SURA YA TANO
UPENDO UZAAO MATUNDA
165. Upendo huleta uhai daima. Kwa hiyo, upendo wa kindoa “hauishii ndani ya jozi […].
Wanandoa wanapojizatiti hujitoa kila mmoja kwa mwenzie, hutoa - zaidi ya wao wenyewe - hata
uwepo wa mtoto wao, ambaye ni kielelezo halisi cha upendo kati yao, ishara ya kudumu ya umoja
wao kindoa na ni muhtasari halisi usiogawanyika ya kuwa wao baba na mama”.[176]
Kuukaribisha uhai mpya
166. Familia si tu mahali ambapo uhai mpya unazaliwa, bali pia ni pale ambapo uhai mpya
unapokelewa kama zawadi ya Mungu Kila uhai mpya “unatuwezesha kukitambua kipimo cha
upendo kisicho na gharama, ambacho hakiishi kutustaajabisha. Huo ni uzuri wa kupendwa kabla:
watoto hupendwa kabla ya kuzaliwa kwao”.[177] Hiyo inaonyesha upendo wa awali wa Mungu

6.6 Page 56

▲back to top
56
ambaye daima ndiye mwanzilishi, kwa maana watoto “hupendwa kabla ya kutenda tendo lolote la
kuwafanya wastahili”.[178] Hata hivyo, “watoto wengi tangu awali huwa wanakataliwa,
wanatelekezwa, wananyang’anywa haki yao ya utoto na ile ya maisha yao ya baadaye. Kuna watu
wanaothubutu kusema, labda wakijaribu kujihesabia haki, kuwa watoto hao walikuja duniani kwa
bahati mbaya. Aibu iliyoje! […] Je, tunawajibika vipi na haki za binadamu au haki za watoto, ilhali
baadaye tunawaadhibu watoto kwa ajili ya makosa ya watu wazima?[179] Kama mtoto anazaliwa
katika mazingira yasiyofaa, wazazi wake au wanafamilia wengine yawapasa wampokee kwa hali
na mali, kama zawadi ya Mungu, na wakubali kuwajibika kumkaribisha kwa utayari na upendo
Kwa maana, “inapowahusu watoto waliozaliwa duniani, hakuna majitoleo ya wazazi yatakayozidi
kipimo, ili kuepuka mtoto afikirie kuwa amekuja duniani kimakosa, hana thamani yoyote na
amebwagwa katika mahangaiko ya maisha kutokana na kiburi cha binadamu”.[180] Zawadi ya
mtoto mpya ambaye Bwana anawatunukia baba na mama, inaanza na mapokezi, kisha
inaendelea na malezi katika maisha ya hapa duniani, na mwisho inalenga ile furaha ya uzima wa
milele. Mtazamo mtulivu juu ya hatima ya binadamu utawafanya wazazi waitambue vema zawadi
madhubuti waliyotunukiwa na Mungu. Kwa hakika, Mungu amewapa wazazi ridhaa ya kumpa kila
mtoto wao jina wanalotaka ambalo Mungu pia atalitumia milele yote.[181]
167. Familia zenye watoto wengi ni furaha kwa Kanisa. Katika familia hizo upendo huonyesha
uzaaji wake wenye heri. Hilo halimaanishi kupuuzia ilani ya mtakatifu Yohane Paulo II alipokuwa
akieleza kuwa uzazi wa busara si ule wa “kuzaa watoto lukuki bila mpango ama kutozingatia
matunzo yao, isipokuwa ni utashi wa wanandoa kuzingatia kwa busara na uwajibikaji uhuru wao
usionyakulika, kwa kujali hali halisi ya kijamii na ya takwimu za idadi ya watu, pamoja na maisha
na mapendekezo halali yao wenyewe.[182]
Upendo wakati wa kusubiri ujauzito
168. Ujauzito ni kipindi kigumu, lakini pia ni wakati mwafaka ajabu. Mama anamsaidia Mungu ili
ufanyike mwujiza wa uhai mpya. Hali ya uzazi inatokana na “uwezo asilia wa mwili wa
mwanamke, ambao kutokana na sifa yake ya kipekee ya kutoa kiumbe kipya unawezesha utungaji
wa mimba na hatimaye kuzaliwa kwa binadamu”.[183] Kila mwanamke hushiriki “katika fumbo la
uumbaji, ambalo linajirudia katika kuzaliwa kwa binadamu”.[184] Ni kama isemavyo zaburi:
“Ulinitunga tumboni mwa mama yangu” (139:13). Kila mtoto anayetungwa ndani ya mamaye ni
mpango wa milele wa Mungu Baba na wa upendo wake wa milele. “Kabla sijakuumba katika
tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa” (Yer 1:5). Kila mtoto yupo katika moyo
wa Mungu tangu sikuzote, na wakati anapotungwa mimba inatimilika ndoto ya milele ya Muumbaji.
Na sasa tufikiri, je, huyu kiumbe anayetungwa mimba ana thamani gani! Yatupasa tumtazame
kwa macho hayohayo yenye upendo ya Mungu Baba, yaonayo mbali zaidi ya mwonekano wa nje.
169. Mwanamke mjamzito anaweza kushiriki katika mpango huo wa Mungu huku akiota juu ya
mtoto wake: "Kila mama na kila baba amekuwa akiota juu ya mwanawe kwa kipindi chote cha
miezi tisa. […] Haiwezekani iwepo familia isiyo na ndoto. Uwezo wa kuota ndoto unapotoweka

6.7 Page 57

▲back to top
57
katika familia, watoto hawakui tena, upendo pia hauongezeki, maisha yananyongea na
kutoweka”.[185] Katika ndoto hiyo, kwa jozi la wanandoa wa kikristo, Ubatizo ndipo unapochukua
nafasi. Wazazi wanauandaa kwa njia ya sala, wakimkabidhi mtoto wao kwa Yesu kabla hata ya
kuzaliwa kwake.
170. Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia leo hii inawezekana kujua hata rangi ya nywele za
mtoto ama ugonjwa atakaougua hapo baadaye, kabla hata hajazaliwa, kwa sababu sifa zote za
mwili wa mtu yule zinakuwa zimeshaandikwa kwenye mfumo wa kijenetiki wa kiumbe hicho kikiwa
bado tumboni. Lakini ni Baba tu aliyemwumba ambaye anamfahamu kwa undani. Ni yeye tu
anayejua thamani na umuhimu, maana ndiye pekee anayemjua huyu mtoto, na maumbile yake
kiundani. Mama ambaye anambeba huyu mtoto tumboni mwake anahitaji kuomba aangaziwe na
Mungu ili aweze kumjua kiundani mtoto wake na kumsubiri jinsi alivyo. Baadhi ya wazazi hujisikia
kwamba mtoto wao hafiki muda unaofaa. Wanahitaji kumwomba Mungu ili awaponye na awape
nguvu ili waweze kumpokea kikamilifu huyu mtoto, ili waweze kumsubiri kwa moyo. Ni muhimu
huyu mtoto ajisikie kwamba anasubiriwa. Mtoto haji kutatua mahitaji binafsi, wala yeye siyo ziada.
Mtoto ni binadamu, mwenye thamani kubwa sana na hawezi kutumiwa kwa faida binafsi. Kwa hiyo
suala hapa si kwamba huyu mtoto ana maana kwako au la, kama ana sifa zinazokupendeza au la,
kama atatimiza mipango na ndoto zako au la. Kwa sababu “watoto ni zawadi. Kila mtoto ni pekee
na hajirudii […]. Mtoto anapendwa kwa sababu ni mwana, si kwa sababu ni mzuri au yupo hivi au
vile; hapana, kwa sababu ni mwana wangu! Si kwa sababu anafikiri kama mimi, au matakwa
yangu nayaona kwake. Mwana ni mwana”.[186] Upendo wa wazazi ni chombo cha upendo wa
Mungu Baba ambaye anasubiri kwa mapendo kuzaliwa kwa kila mtoto, anampokea bila masharti
na kumkaribisha kwa shukrani.
171. Napenda kumwomba kwa upendo kila mwanamke mjamzito: ilinde furaha yako, na yeyote
asikunyang’anye furaha ya ndani ya umama. Huyu mtoto anastahili furaha yako. Usiruhusu hofu,
wasiwasi, maneno mabaya wanayosema watu au matatizo yoyote yale yaizime furaha ya kuwa
chombo cha Mungu cha kuleta uhai mpya duniani. Jibidiishe na yale ambayo unapaswa
kuyafanya au kuandaa, lakini bila kutingwa kwa wasiwasi na hilo tu, na umtukuze Mungu kama
Maria: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi
wangu, kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake” (Lk 1:46-48). Hata katika usumbufu,
uishi huu utulivu wa ndani, ukimwomba Bwana ailinde furaha yako ili uweze kumrithisha mtoto
wako.
Upendo wa mama na wa baba
172. “Mara baada ya kuzaliwa, pamoja na kula chakula na kutunzwa, watoto huanza kupokea
thibitisho la vipaji vya kiroho vya upendo. Matendo ya upendo hupokelewa kupitia zawadi ya jina
binafsi, lugha inayowaunganisha, madhumuni ya mitazamo, minururisho ya tabasamu. Kujifunza
kwamba uzuri wa muunganiko kati ya binadamu unaelekezwa kwenye roho yetu, hutafuta uhuru
wetu, hupokea utofauti wa mwingine, unamtambua na kumheshimu kama mshiriki katika

6.8 Page 58

▲back to top
58
mazungumzo. […] Na huo ndio upendo ambao huleta cheche ya upendo wa Mungu!”.[187] Kila
mtoto ana haki ya kupokea upendo wa mama na baba, wote wawili wakiwa muhimu kwa ajili ya
ukomavu mtulivu kiujumla wa mtoto. Kama walivyosema maaskofu wa Australia, wote wawili
“wanachangia, kila mmoja kwa namna yake, katika ukuaji wa mtoto. Kuuheshimu utu wa mtoto
kuna maana ya kusisitiza mahitaji yake na haki ya asili ya kuwa na baba na
mama”.[188] Hatuongelei kuhusu upendo wa baba na wa mama tu kila mmoja binafsi, ila pia
upendo kati yao, ambao unatambuliwa kuwa ni chemchemi ya uhai wake mtoto, kama kioto
kipokeacho na kama msingi wa familia. Bila hilo mtoto anaweza kudhilika kuwa kitu
kinachochezewa. Wote wawili, mume na mke, baba na mama, ni “washiriki wa upendo wa Mungu
Muumba na kwa namna fulani ni wahariri wake”.[189] Wanathibitisha kwa watoto wao sura ya
upendo wa kimama na wa kibaba wa Bwana Mungu. Pamoja na hayo, wote kwa pamoja
wanawafundisha tunu ya kushirikishana, kukutana kwa walio tofauti, ambako kila mmoja
huchangia kulingana na nafsi yake na anajua pia kupokea kutoka kwa mwingine. Endapo, kwa
sababu isiyozuilika, angekosekana mmojawapo wa wazazi, ni muhimu kutafuta kama kuna namna
inayoweza kuziba pengo, ili kumwezesha mtoto akue kwa hekima na busara za kibinadamu.
173. Kujisikia kama yatima ambayo ni hisia wanayong’amua watoto na vijana wengi leo hii, ni kitu
kinachowaathiri kwa undani zaidi kuliko tufikirivyo. Leo hii tunatambua kuwa ni haki halali kabisa,
pamoja na kuwa matamanio pia, kwamba wanawake watake kusoma, kufanya kazi, kuendeleza
vipaji vyao na kuwa na malengo yao. Wakati huohuo hatuwezi kukana mahitaji waliyo nayo watoto
ya uwepo wa mama, hasa kwa miezi ya mwanzoni ya maisha yao. Ukweli ni kwamba “mwanamke
yupo mbele ya mwanamume kama mama, chombo kinacholeta uhai mpya wa kibinadamu ambao
umetungwa mimba na unakua ndani yake, na kutokana naye unazaliwa
ulimwenguni”.[190] Udhaifu wa uwepo wa mama pamoja na mawaidha na vipaji vyake vya kike ni
hatari kubwa kwa hii dunia yetu. Nathamini harakati ya kutetea haki ya wanawake iwapo haidai
kusawazisha jinsia wala kukana hali ya uzazi. Kwani ukuu wa mwanamke unajumuisha haki zote
zinazotokana na hadhi yake ya kibinadamu isiyonyang’anyika, lakini pia na vipaji vyake vya kike,
ambavyo ni vya lazima kwa jamii. Upekee wao kama wanawake – hasa hali yao ya umama –
huwapa pia majukumu maalumu. Kwa sababu akina mama wana majukumu hapa duniani ambayo
yanawakabili wao tu, ambayo jamii inapasika kuyalinda na kuyaendeleza kwa manufaa ya
wote.[191]
174. Kusema kweli, “akina mama ni dawa inayofaa zaidi dhidi ya kusambaa kwa ubinafsi usiojali.
[…] Ni wao ambao wanahakikisha uzuri wa maisha”.[192] Bila shaka, “jamii bila akina mama
ingekuwa ni jamii mfu, isio na ubinadamu, kwa sababu akina mama daima, hata katika wakati
mgumu, hujua kushuhudia wema, majitoleo na hamasa ijengayo. Akina mama mara nyingi
hurithisha pia maana ya ndani ya uchaji wa Mungu: katika sala za kwanza, na katika ishara za
kwanza za ibada ambazo mtoto hujifunza toka kwao […]. Bila akina mama, siyo tu
kungekosekana waamini wapya, lakini pia imani yenyewe ingepoteza sehemu yake kubwa ya ari
nyofu na ya ndani. […] Wapendwa akina mama: Asanteni! Asanteni, kwa jinsi mlivyo katika familia
na kwa yote myatoayo kwa Kanisa na kwa ulimwengu”.[193]

6.9 Page 59

▲back to top
59
175. Mama ambaye humtunza mwanae kwa ukarimu na huruma humsaidia mtoto kukua katika
imani, na kutambua kwamba ulimwengu ni mahali pema ambapo anapokelewa vizuri. Hilo
linamsaidia mtoto kukua katika hali ya kujienzi, na kama matokeo linaendeleza uwezo wa
kupenda na kushirikiana na wengine. Na baba, katika nafasi yake, humsaidia mtoto kuyatambua
mapungufu katika maisha, na msaada wake hulenga hasa kumpa mtoto mwelekeo, uhodari wa
kutoka na kupambana na ulimwengu na changamoto zake, himizo la kufanya kazi kwa bidii na
kuwa na ujasiri mkuu. Baba mwenye kuionyesha furaha na amani ya kuwa mwanaume, na
ambaye anaidhihirisha pamoja na kuonyesha mapenzi kwa mke wake katika kumhudumia na
kumjali, ni muhimu sawasawa na matunzo ya mama. Hapo huweza kuweko matazamo tofauti
katika wajibu na majukumu mbalimbali, yaendanayo na hali na uwezo wa kila familia. Lakini
uwepo wa ngao zote mbili katika familia, ya kike na kiume, ni wa muhimu sana katika kujenga
mazingira bora yenye kuwezesha ukuaji bora wa watoto.
176. Husemekana mara kwa mara kuwa jamii yetu ni “jamii bila akina baba”. Katika utamaduni wa
watu wa Magharibi, ishara ya akina baba inakosekana, imepotea, imedhoofika. Hata uume
wenyewe leo upo katika mahojiano. Kimatokeo hayo yalileta fujo inayoeleweka, kwani “hapo
awali, jambo hili lilionekana kuwa ni uhuru: uhuru kutoka kwa baba kama mwenye mamlaka, baba
kama mwakilishi wa sheria inayotubana kutoka kwa nje, baba kama mwamuzi wa furaha ya
watoto na kikwazo kwa maendeleo na kujitegemea kwa vijana. Zamani, katika baadhi ya nyumba
ilitawala hali ya mabavu, na wakati mwingine hata ya ukandamizaji”.[194] Lakini, “kama
inavyotokea mara nyingi, matokeo ni kufikia hali iliyo kinyume kabisa. Shida ya siku hizi zetu siyo
tena ni uwepo wa kimabavu wa akina baba, bali zaidi kutokuwepo kwao, kuwa mbali na familia.
Akina baba hujikita zaidi katika kujitunza wenyewe au katika shughuli zao na wakati mwingine
katika miradi yao binafsi, kiasi cha kuwasahau hata familia zao. Nao huwaacha peke yao watoto
wadogo na vijana”.[195] Uwepo wa baba, na pia mamlaka yake, unadhoofishwa pia na muda
mwingi zaidi unaotumiwa kwa vyombo vya mawasiliano na kwa teknolojia ya maburudisho. Zaidi
ya hayo, siku hizi mamlaka inaonekana kutiliwa mashaka, na wazee hujadiliwa vikali. Hao
wenyewe wanakosa uhakika na hivyo hushindwa kutoa kwa watoto wao maongozi thabiti na
yenye misingi bora. Haifai kuchanganya majukumu ya wazazi na ya watoto: hilo linaharibu
mchakato mwafaka wa ukuaji ambao watoto wenyewe wanahitaji kuutimiza, na linawanyima
upendo uwezao kuwapa dira na kuwasaidia katika kukomaa kwao.[196]
177. Mungu anamweka baba katika familia ili, kwa tunu zake za kiume, “aweze kuwa karibu na
mke wake na kushirikishana kila kitu, furaha na huzuni, matumaini na magumu ya maisha. Na
kuwa karibu na watoto katika kukua kwao, katika michezo yao na katika juhudi zao, katika wakati
wa furaha, wasiwasi na mashaka, wakati wazungumzapo na wakati wa unyamavu, wanapojaribu
na wanapokuwa na woga wa kujaribu, wanapoteleza na wanapoona tena njia iliyo sahihi. Kuwa
baba ambaye yupo, daima. Kusema yupo si kusema kuwepo kama mnyapara. Kwa sababu akina
baba ambao wanafuatilia yote kama wanyapara, huwa kizuizi na kivuli katika ukuaji wa watoto, na
watoto huwa hawaendelei mbele”.[197] Baadhi ya akina baba hujisikia si wa muhimu na kwamba
hawahitajiki, lakini ukweli ni kwamba “watoto warudipo nyumbani na matatizo yao wanahitaji

6.10 Page 60

▲back to top
60
kumkuta baba akiwasubiri”. Wanaweza kujitahidi kutoonyesha au hata kutokubali, lakini kiukweli ni
kwamba wanahitaji”.[198] Sio jambo jema kwa watoto kuwakosa baba zao na kukuzwa kabla ya
wakati wao.
Kupanuka kwa uzaaji
178. Wanandoa wengine hawana uwezo wa kupata watoto. Tunafahamu kuwa hili laweza kuwa
sababu kubwa ya huzuni. Wakati huohuo tunafahamu kuwa “maisha ya ndoa hayakuanzishwa
kwa jukumu wa kuzaa watoto tu […]. Hasa katika hali zile ambazo wanandoa wanapenda
kuwapata watoto, na watoto hawapo, ndoa inabaki kuwa imara na yenye lengo la umoja na
ushirika wa maisha yote na inalinda thamani yake na hadhi yake ya muungano
usiovunjika".[199] Aidha “umama hauji tu kwa kuzaa watoto, kuna njia nyingine pia za kuwa
mama”.[200]
179. Kuasili mtoto (adoption) ni njia mojawapo ya kutimiza umama na ubaba kwa namna iliyo na
ukarimu mkuu. Nami ninapenda kuwatia moyo wale wasiokuwa na uwezekano kwa kuwazaa
watoto wao wenyewe, wapanue na kufungua wazi upendo wao wa kindoa ili kuwapokea watoto
ambao wanakosa hali za kifamilia zifaazo. Hawatajilaumu kamwe kwa kuwa wakarimu. Kumwasili
mtoto ni tendo la upendo la kumzawadia familia yule asiyekuwa nayo. Ni muhimu kusisitiza kuwa
vyombo vya sheria vihusikavyo viweze kurahisisha taratibu za kuasili watoto, hasa katika hali za
watoto wasiotakikana, ili kuzuia utoaji mimba au kutelekezwa kwa watoto wachanga. Wale wote
wanaoikabili changamoto ya kumwasili mtoto na wanampokea mtu bila masharti bali kwa ukarimu,
hawa ni njia pekee ya upendo wa Mungu. Maana anasema “ Hata kaka mama yako atakusahau,
lakini mimi sitakusahau kamwe” (taz. Isa 49:15).
180. “Uamuzi wa kumwasili mtoto au wa kumpokea kama walezi kwa muda maalumu ni
udhihirisho wa uzaaji mahsusi wa maisha ya kindoa, hata pale ambapo hayaathiriwi na huzuni wa
utasa. […] Mbele ya hali zile ambazo kwa udi na uvumba mtoto anatakikana kama haki ya
kujitimiliza na wanandoa, kuasili mtoto au kumpokea kama walezi ni hali ambayo, ikieleweka
katika udhati wake, inadhihirisha maana muhimu ya kuwa wazazi na kuwa watoto, kwa vile
inavyosaidia kutambua kwamba watoto, wa kuzaa wenyewe au wa kuasiliwa, ni watu wengine
muhimu mbali na mimi, na wanahitaji kupokelewa, kupendwa, kuhudumiwa, na siyo tu kuletwa
duniani. Haki za watoto lazima zilindwe na zipewe kipaumbele daima pale inapofanyika uamuzi
kuhusu kuasili mtoto au kumpokea kama walezi”.[201] Kwa upande mwingine “utekwaji na uuzaji
wa watoto katika nchi na mabara mbalimbali unahitaji kuzuiliwa kwa njia ya sheria zinazofaa na
kwa usimamizi makini ya Serikali.[202]
181. Tunawakumbusha tena kuwa kuzaa na kuasili mtoto si njia pekee za kuishi uwezo wa kuzaa
wa upendo. Hata familia kubwa lazima idhihirishe uwepo wake katika jamii inamoishi, ili
kuendeleza aina nyinginezo za uzaaji ambazo ni kama mwendelezo wa pendo unaozitegemeza.
Familia za kikristo zisisahau kuwa “imani haitutoi ulimwenguni, bali inatuingiza hata zaidi katika

7 Pages 61-70

▲back to top

7.1 Page 61

▲back to top
61
ulimwengu. […] Maana, kila mmoja wetu ana jukumu lake maalumu katika kuuandaa ujio wa
Ufalme wa Mungu”.[203] Familia isijione kama wigo wa kujikinga dhidi ya jamii. Badala yake,
inasonga mbele na kutoka nyumbani, inakwenda katika roho ya mshikamano na wengine. Kwa
njia hii inakuwa mahali pa kuwatangamanisha watu na jamii, na chombo cha kuunganisha maisha
ya binafsi na yale ya jumuiya Wanandoa lazima wawe na ufahamu wazi na wa hakika juu ya
majukumu yao ya kijamii. Hilo likitokea, mapenzi yao yanayowaunganisha hayapungui bali
yanastawishwa katika mwanga mpya, kama ushairi huu unavyoelezea:
“Mikono yako ni kumbatio langu
tuni tamu zineemeshazo siku zangu
ninakupenda kwa sababu mikono yako
inajibidisha kwa ajili ya haki.
Kama nakupenda, ni kwa sababu ya wewe kuwa
mpenzi wangu, mwenzi wangu, yote niliyo nayo
na mitaani, bega kwa bega
tu zaidi sana ya wawili”.[204]
182. Hakuna familia inayoweza kuzaa matunda mema ikiwa inajiona tofauti mno na wengine au
“kujitenga”. Ili kuzuia hatari hizi, lazima tuikumbuke familia yake Yesu. Imejaa neema na hekima,
haikuonekana kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida, kama nyumba ya kigeni na mbali na watu
wengine. Ndiyo sababu watu waliona vigumu kuitambua hekima ya Yesu na kusema: “Huyu
ameyapata wapi haya? […] Huyu si yule seremala, mwana wa Maria?” (Mk 6:2-3). “Huyu si
mwana wa seremala?” (Mt 13:55). Maswali haya yanaonyesha kuwa familia ya Yesu ilikuwa ni
familia ya kawaida, yenye ujirani mwema na mshikamano na familia nyingine, familia ambayo ni
sehemu ya jumuiya yake. Yesu hakukua na kulelewa katika mahusiano finyu ya Yosefu na Maria,
bali alishirikiana na kujihusisha kwa furaha na ujamaa mpana wa ndugu, jamaa na marafiki. Hilo
linaeleza kwa nini, katika kurudi kwao toka Yerusalemu, Maria na Yosefu walifikiria kuwa mtoto
wao wa miaka kumi na miwili alikuwa ndani ya msafara kwa siku nzima, akisikiliza hadithi na
kushirikishana mahangaiko ya wote: “Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda
mwendo wa kutwa” (Lk 2:44). Badala yake, mara nyingine inatokea kwamba baadhi ya familia za
kikristo, kwa sababu ya lugha waitumiayo, na jinsi watamkavyo mambo, au kwa watendavyo, kwa
jinsi wanavyorudia mara nyingi mambo yaleyale, wanatazamwa kama za mbali, kama zimejitenga
na jamii, na hata ndugu zao wenyewe wanajisikia kufedheheshwa au kuhukumiwa nao.
183. Wanandoa wanaoonja nguvu ya upendo wanafahamu kuwa upendo huo unaitwa kuponya
majeraha ya waliotelekezwa, na kukuza utamaduni wa kukutana kati ya watu, na kuipigania haki.
Mungu ameipatia familia jukumu la kuufanya ulimwengu kuwa nyumba ya wote,[205] ili wote
wafikie hatua ya kuwaona binadamu wote kama ndugu: “Mtazamo wa makini katika maisha ya kila
siku ya wanaume na wanawake wa leo unaonyesha mara moja hitaji lililopo popote la kupatiwa
sindano maridhawa ya roho ya kifamilia. […] Sio tu mipangilio ya maisha ya pamoja inazidi

7.2 Page 62

▲back to top
62
kukwama katika urasimu ulio geni kabisa kwa vifungu vya misingi vya kibinadamu, lakini hata
desturi na mwenendo wa kijamii na kisiasa unaonyesha mara nyingi dalili za
kumomonyoka”.[206] Kwa upendo wake, familia zilizo wazi na zinazoshikamana na wengine ili
kuwapa nafasi maskini, zinaweza kujenga urafiki na wale wenye hali mbaya kuliko ya kwao. Ikiwa
wanaheshimu kwelikweli Injili, hawawezi kusahau aliyosema Yesu: “Kadiri mlivyomtendea
mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mt 25:40). Kwa ujumla,
wanaishi kile ambacho, kwa wazi kabisa, tunaagizwa kufanya na maneno haya: “Ufanyapo
chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala
jirani zako wenye mali, wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu
waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri” (Lk 14:12-14). Utakuwa heri! Hapa ndipo
ilipo siri ya familia yenye furaha.
184. Kwa ushuhuda wao na kwa maneno yao familia zinatangaza kwa familia nyingine habari za
Yesu, wanapitisha imani yao, wanaamsha hamu ya Mungu, na kuonyesha uzuri wa Injili na wa
jinsi ya kuiishi. Kwa namna hiyo wanandoa wakristo wanaihamasisha jamii iliyokaa kivulini na
kuipaka rangi za undugu, za kujali mshikamano wa kijamii, za kutetea haki na kujali mahitaji ya
wale wenye hali duni, za imani inayoangaza, ya matumaini hai na tendaji. Uwezo wao wa kuzaa
hukua na kupanuka katika namna nyingi zisizohesabika za kudhihirisha uwepo wa upendo wa
Mungu katika jamii.
Kuutambua mwili
185. Katika mstari huo wa fikra ni muhimu kuitilia mkazo sehemu ile ya Biblia ambayo kwa
kawaida inafasiriwa mbali na muktadha wake, au hata kwa juujuu sana, hali ambayo inasababisha
kupoteza maana yake halisi na kamili zaidi, ambayo ni ya kijamii hasa. Ninaongelea juu ya 1Kor
11:17-34, ambako mtakatifu Paulo anapambana na hali ya aibu ya jumuiya. Matajiri wa jumuiya
wanawakandamiza na kuwatenga maskini, na utengano huu unapelekwa hata katika karamu ya
kijumuiya ambayo yaliambatana na adhimisho la Ekaristi Wakati matajiri wanaifurahia vyakula
vyao bora, maskini wanaachwa wabaki na njaa. “Hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. Je,
hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau Kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao
wasio na kitu?” (a. 21-22).
186. Ekaristi inatudai tuwe tunatangamana katika mwili mmoja wa Kanisa Mwenye kuijongea
meza ya Bwana ili kupokea Mwili na Damu ya Kristo hawezi wakati huohuo kuujeruhi Mwili huo
kwa kusababisha matengano ya aibu na ubaguzi katika viungo vyake. Hii ndiyo maana ya
“kupambanua” Mwili wa Bwana: kuutambua kwa imani na mapendo katika ishara ya sakramenti
na vilevile katika jumuiya, na yule asiyetimiza hilo, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake (taz. a.
29). Maneno hayo ya Biblia ni tahadhari nzito kwa familia ambazo zinajifunga ndani ya starehe
yao binafsi na wanajitenga, lakini hasa kwa familia zisizojali mateso ya familia zilizo maskini na
wahitaji. Maadhimisho ya Ekaristi yanakuwa hivi wakati mwafaka kwa kila mmoja “kujihoji
mwenyewe” (a. 28), ili kufungua milango ya familia kwa ushirika mpana zaidi na wale waliotupwa

7.3 Page 63

▲back to top
63
na jamii na hivyo kuipokea kwelikweli Sakramenti ya upendo wa kiekaristi inayotufanya sote tuwe
mwili mmoja. Tunapaswa tusisahau kwamba “fumbo la Sakramenti hii lina kipengele kinachohusu
tabia ya kijamii”.[207] Wakati wale wanaokomunika wanageuka vipofu kwa maskini na wenye
shida, au kutenda vitendo mbalimbali viigawanyavyo jamii, vya dharau na visivyo haki, Ekaristi
walioipokea hupokelewa isivyostahili. Kwa upande mwingine, familia zinazojilisha Ekaristi baada
ya kujiweka tayari, hawa wanaimarisha hamu yao ya kuishi kindugu, utayari wa kuwajibika kijamii
na majitoleo yao ya kuwasaidia wenye shida.
Maisha katika familia pana
187. Familia ndogo inapaswa kuchangamana na familia pana, ambapo wapo wazazi, akina
mashangazi na wajomba, binamu wote na hata majirani. Katika familia hii pana inawezekana
wawepo wengine ambao wanahitaji msaada au walau ujirani na upendo, au yaweza kuwepo
mateso makali yanayohitaji kufarijiwa.[208] Ubinafsi unaoshamiri leo unasababisha mara nyingine
familia zijifungie katika viota vya ulinzi, na kuwasikia wengine kama hatari yenye kuzibughudhi.
Lakini, kujitenga huko, kweli hakuwezi kumpatia yeyote amani kubwa au furaha, bali inapunguza
moyo wa familia na kuyadogoza maisha ya familia.
Kuwa wana
188. Kwanza, tuseme neno juu ya wazazi. Yesu aliwaambia Mafarisayo kuwa kumtelekeza mzazi
ni kinyume cha sheria ya Mungu (taz. Mk 7:8-13). Haimfai yeyote kujisahau kuwa mwana. Ndani
ya kila mtu, “hata kama mmoja anaufikia utu uzima, au ni mzee, hata kama mtu anafikia hali ya
kuwa mzazi, hata ukishika nafasi yenye wadhifa wowote ule, chini ya hayo yote inabaki hali ya
kuwa mwana. Sisi sote tu wana. Hili kila wakati huturudisha nyuma ili kukumbuka kuwa
hatukujipatia uhai, bali tuliupokea Zawadi kubwa ya uhai ni zawadi ya kwanza tuliyopokea”.[209]
189. Ndiyo sababu “amri ya nne inatutaka watoto […] tuwaheshimu baba na mama (taz. Kut
20:12). Amri hii inakuja mara baada ya zile zimhusuzo Mungu mwenyewe. Kwa kweli, hii
inahisisha kitu kitakatifu, kitu cha kimungu, kitu ambacho ni shina la mambo yote yahusuyo
heshima kati ya wanadamu. Na katika utungo wa kibiblia wa amri ya nne ya Mungu inaendelea
kusema: “siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako”. Kifungu cha
kifadhila kati ya vizazi ni uhakika wa kuwa na mustakabali, nacho ni dhamana ya historia iliyo ya
kiutu kwelikweli. Jamii yenye watoto wasiowaheshimu wazazi ni jamii bila heshima […]. Ni jamii
iliyoachwa mikononi mwa vijana wakali na wenye uroho”.[210]
190. Lakini kuna upande wa pili wa sarafu: “Mwanamume atamwacha baba yake na mama yake”
(Mwa 2:24), linatuambia Neno la Mungu. Hili halitokei kila wakati, na ndoa haipokelewi katika
thamani yake yote kwa sababu mtu hajatimiliza tendo hili la kuacha na kujitoa. Wazazi hawapaswi
kuachwa na kutelekezwa, hata hivyo, ili kufunga ndoa inabidi kuwaacha, ili familia mpya iweze
kuwa makazi, mahali pa usalama, jukwaa na mpango, na iwe inawezekana kuwa kweli "mwili

7.4 Page 64

▲back to top
64
mmoja” (ibid.) Katika baadhi ya ndoa, mwanandoa huwa msiri kwa mwenzie, na kuwa wazi zaidi
kwa wazazi kuliko kwa mwenzi. Na matokeo yake mawazo ya wazazi huwa ya thamani zaidi
kuliko hisia na rai ya mwenzi. Hali hii huwa haiendi mbali na hata kama ikienda, wanandoa
wanapaswa kufanya jitihada ili kukuza uaminifu na mawasiliano kati yao. Ndoa hutoa changamoto
kwa mke na mume kutafuta namna mpya ya kuwa wana.
Wazee
191. “Usinitupe wakati wa uzee, nguvu zangu zipungukapo usiniache" (Zab 71:9). Hili ni dua la
mzee ambaye anaogopa kusahauliwa na kudharauliwa. Kama vile Mungu anavyotuomba kuwa
wajumbe wake wenye kusikia kilio cha maskini, vivyo hivyo anatutaka sisi pia tusikilize mlio wa
wazee.[211] Hilo ni changamoto kwa familia na jumuiya, kwa sababu “Kanisa haliwezi na halitaki
kujikita katika fikra ya kukosa uvumilivu, wala ya kutojali au kudharau, mbele ya hali ya uzeeni.
Lazima kufufua hali ya pamoja ya shukrani, ya kuenzi, ya ukarimu, ambayo itamfanya mzee
ajisikie kuwa ni sehemu hai ya jumuiya yake. Wazee ni wanaume na wanawake, akina mama na
akina baba, ambao walitembea kabla yetu katika njia yetu hiihii, waliishi kabla yetu katika nyumba
yetu, katika mapambano kama yetu ya kila siku ili kuishi maisha yaliyo bora”.[212] Kwa hivyo,
“ningetamani namna gani Kanisa ambalo linapambana na utamaduni wa kutupatupa kwa njia ya
furaha ifurikayo katika kukutana na kukumbatiana upya vijana na wazee!”[213]
192. Mtakatifu Yohane Paulo II alitualika kuwa makini katika kutambua majukumu ya wazee katika
familia zetu, kwa sababu kuna tamaduni nyingine ambazo “kwa sababu ya maendeleo ya viwanda
na ya miji yasiyo na utaratibu, katika kipindi cha zamani na cha sasa wamewasahau na kuwaweka
kando wazee kwa namna zisizokubalika”.[214] Wazee wanatusaidia kuyathamini “mwendo wa
kizazi kimoja hadi kingine”, kwa “karama yao ya kuunganisha tena yaliyoraruka”.[215] Mara nyingi
ni akina babu na bibi ambao huhakiki kuwa tunu kuu za mila na desturi zimepishwa kwa wajukuu
na vitukuu, na “wengi wetu twaweza kuthibitisha kuwa imani tuliyo nayo tumerithishwa kweli toka
kwa babu au bibi”.[216] Maneno yao, makumbatio yao au hata uwepo wao tu, unawasaidia watoto
kutambua kuwa historia haikuanza na wao. Na kwamba wao ni warithi wa mwendo mrefu wa watu
na kwamba wanapaswa kuheshimu yote yaliyotokea kabla yao. Wale watakaovunja vifungo na
historia ya zamani watapata shida kujenga mahusiano imara na watashindwa kutambua kuwa
uhalisia ni mkubwa zaidi kuliko wao nao hawautawali. Kwa hiyo, “kuwaheshimu wazee ndiko
kunakofanya jamii na utamaduni wake kuwa bora. Jamii huonyesha kuwajali wazee? Kuna nafasi
kwa wazee? Jamii hii itaendelea kama itajua kuheshimu hekima na busara ya wazee”[217]
193. Ukosefu wa kumbukumbu ya kihistoria ni pungufu kubwa katika jamii zetu. Ni fikra
isiyopevuka ya "yaliyopita ni ya kale, na ya sasa ni ya sasa”. Kuyajua matukio ya zamani na
kuweza kuyapambanua ni njia pekee ya kujenga mustakabali wenye maana. Haiwezekani kulea
bila kukumbuka: “Zikumbukeni siku za kwanza” (Ebr 10:32). Kusikiliza wazee wasimuliapo historia
zao kunawafaa sana watoto na vijana, kwani inawafanya wajisikie wameunganishwa na historia
hai ya familia yao, pia ya majirani zao na nchi yao. Familia ambayo inashindwa kuheshimu na

7.5 Page 65

▲back to top
65
kuwaenzi babu na bibi zao, ambao ni historia hai yao, hiyo familia tayari imevunjika. Lakini familia
yenye kukumbuka, hiyo ina uhakika ya uendelevu wa maisha. Kwa hiyo, “jamii ambayo haiwapi
nafasi wazee au imewatupa kwa sababu huleta matatizo, jamii hiyo tayari ina ndani yake virusi
viletavyo kifo”,[218] kwa vile “inajikata na mizizi yake yenyewe”.[219] Mang’amuzi yetu ya kujisikia
yatima, kwa sababu ya kukosa mwendelezo wa mila na tamaduni kati ya vizazi, ya kung’olewa
mbali na mazingira ya asili na ya kupotelea mbali kwa uhakika unaofanya maisha yaumbike,
yanatupatia changamoto ya kuzifanya familia zetu ziwe mahali ambapo watoto waweze kutia
mizizi katika rotuba ya historia iliyo ya kijumuiya.
Kuwa ndugu
194. Uhusiano kati ya ndugu unaendelea kukua katika mwendo wa muda, na “muungano wa
ujamaa ambao huundwa katika familia kati ya watoto, kama ikiimarishwa katika hali ya kimalezi
iliyo wazi kuwaheshimu wengine, ni shule kuu ya uhuru na amani. Katika familia, kaka na dada
wajifunza maana ya kuishi pamoja wanadamu […]. Labda si wakati wote tunagundua hilo, lakini
ndiyo familia inayoingiza udugu duniani! Kutoka mwanzo huu wa mang’amuzi ya udugu,
unaoimarishwa na upendo na malezi ya nyumbani, mtindo wa udugu huangaza kama ahadi juu ya
jamii nzima”.[220]
195. Kukua pamoja na kaka na dada kunaleta mang’amuzi mazuri sana ya kujaliana, ya kusaidia
na kusaidiwa. Kwa hiyo, “udugu katika familia inapendeza kwa njia ya pekee tunapoona roho wa
kujaliana, uvumilivu, upendo ambao unadhihirishwa kwa kaka mdogo na dada mdogo ambaye ni
dhaifu zaidi, au mgonjwa, au ana ulemavu fulani”.[221] Tunapaswa kutambua kwamba “kuwa na
kaka au dada anayekupenda ni zawadi ya pekee, isiyoweza kulipwa na isiyo na kifani”.[222] Lakini
watoto wanapaswa kufundishwa kwa uvumilivu thamani ya kujaliana kama kaka na dada.
Mafunzo haya, ambayo mara nyingine yaweza kuwa magumu, ni shule halisi ya majumuisho.
Katika nchi fulani, ambako imekuwa ni hali ya kawaida kuwa na mtoto mmoja tu, mang’amuzi ya
kuwa na kaka au dada siyo tena ya kawaida. Ikiwa imetokea kwamba haikuwezekana kuwa na
watoto zaidi ya mmoja, lazima zitafutwe mbinu ili kuhakikisha kuwa huyu mtoto halelewi au kukua
peke yake au katika mazingira ya upweke.
Moyo mkuu
196. Zaidi ya duru ndogo ya wanandoa na watoto wao, kuna familia pana ambayo haiwezi
kusahauliwa. Maana, “upendo kati ya mume na mke katika ndoa na, kutokana na huo na kwa
upana zaidi, upendo kati ya wanafamilia wote – kati ya wazazi na watoto, kati ya akina kaka na
akina dada, kati ya ndugu na jamaa - unapewa uhai na unahimizwa kwa njia ya mkikimkiki
usiokoma, wenye kuiongoza familia kwenye ushirika wa ndani na wa kina zaidi na zaidi, ulio
msingi na roho ya jumuiya ya kindoa na ya kifamilia”.[223] Marafiki na familia nyingine ni sehemu
ya hii familia kubwa, hali kadhalika jumuiya za familia wanaoungana mkono katika shida, na katika
majukumu yao ya kijamii na katika maisha ya imani.

7.6 Page 66

▲back to top
66
197. Familia hii pana inatamaniwa ipokee kwa upendo mkuu kina mama vijana, na watoto wasio
na wazazi, akina mama wasio na waume, ambao wameachiwa jukumu la kulea watoto peke yao,
watu wenye ulemavu, ambao wanahitaji mapendo ya hali ya pekee na ukaribu, vijana
wanaopambana na hali tegemezi ya kulevya, watu wasioolewa au kuoa, waliotengana au
kutalakiana, wajane wanaohangaika katika upweke, wazee na wagonjwa wasio na huduma toka
kwa watoto. Hadi kuchukua majukumu ya kuwapokea ndani yake “hata wale waliopotoka zaidi
katika mienendo ya maisha yao”.[224] Hii familia pana yaweza kujihusisha katika kusaidia, eti,
hata udhaifu wa wazazi, au kufichua na kushtaki mapema hali ya ukatili, ikiwa pamoja na
unyanyasaji wa watoto, na kuwapatia upendo safi na tegemeo ya kifamilia pale ambapo wazazi
wao wanashindwa kuyatimiza haya.
198. Hatimaye, hatuwezi kusahau kuwa familia pana hii inajumuisha pia akina baba wakwe,
mama wakwe na ndugu wote wa mwenzi wa ndoa. Sifa ya upendo mwanana ni kujifunza
kutowatazama hawa ndugu kama washindani, watu wa hatari au wavamizi. Muungano wa
wanandoa unadai mila na desturi za ndugu hao ziheshimiwe, zifanyike juhudi katika kuelewa
misamiati yao, kupunguza mateto, kuwajali na kuwapa nafasi moyoni, hata pale ambapo
ingekuwa lazima kulinda uhuru halali ya jozi na hali ya undani wao. Kuwa tayari kufanya hivyo ni
pia njia bora ya kuonyesha unyofu na ukarimu wa upendo kwa mwenzi wa ndoa.
SURA YA SITA
BAADHI YA MITIZAMO YA KICHUNGAJI
199. Majadiliano wakati wa Sinodi yaliibua uhitaji wa kubuni mbinu mpya za kichungaji. Nitajaribu
kuorodhesha baadhi yao kwa jumla. Jumuiya tofauti ziandae mikakati ya utendaji na ya kufaa,
ambayo iendane na mafundisho ya Kanisa na mahitaji na changamoto za eneo mahalia. Pamoja
na kwamba sina nia ya kuelezea humu mpango wa uchungaji wa familia, ningependa kutafakari
juu ya baadhi ya changamoto za kichungaji zilizo muhimu zaidi.
Kuitangaza Injili ya familia leo
200. Mababa wa Sinodi walisisitiza kwamba familia za kikristo, kwa msaada wa neema ya
sakramenti ya ndoa, ni wahusika wa kwanza katika uchungaji wa familia, hasa kwa njia “ya
ushuhuda wa furaha ya wanandoa na familia, zilizo makanisa ya nyumbani”.[225] Kwa sababu
hiyo, walisisitiza kwamba “ni muhimu watu waguswe na Injili ya familia kama furaha ambayo
‘huijaza mioyo na maisha yote’, kwa sababu katika Kristo ‘tumekombolewa kutoka dhambi, huzuni,
utupu wa mioyo na upweke’ (Furaha ya Injili, 1). Katika mwanga wa mfano wa mpanzi (taz. Mt
13:3-9), wajibu wetu ni kushirikiana katika kupanda: mengine yote ni kazi ya Mungu. Wala
tusisahau kwamba Kanisa, ambalo linahubiri juu ya familia, ni ishara ya ukinzani”.[226]Waliofunga
ndoa wanashukuru kuwa wachungaji wao wanawahamasisha ili waelekeze kwa ushujaa maisha
yao kwenye upendo imara, wenye nguvu, wenye kudumu na wenye uwezo wa kuhimili katika

7.7 Page 67

▲back to top
67
mikikimikiki ya kila aina. Kanisa linatamani kwa unyenyekevu na mguso wa pekee, kuzifikia familia
na “kusindikiza kila familia kugundua njia nzuri zaidi ya kupambana na vikwazo inavyokumbana
navyo.”[227]Haitoshi kuonyesha mguso wa jumlajumla kwa familia katika mipango mikuu ya
kichungaji. Kuziwezesha familia kuchukua wajibu wao kama watu hai wa uchungaji wa familia
kunadai “juhudi za uinjilishaji na katekesi kwa ajili ya familia”,[228]inayoielekeza katika njia hiyo.
201. “Juhudi hii inalidai Kanisa zima kuongoka kimisionari: ni lazima kutosimama katika kutangaza
habari iliyo ya kinadharia tu, iliyotenganika na matatizo halisi ya watu.”[229]Uchungaji wa familia “
unapaswa kuwezesha kung’amua kwamba Injili ya familia inasaidia kujibu matarajio ya ndani
kabisa ya mwanadamu: ni jibu kwa utu wa kila mmoja na kwa utimilifu wake katika kusaidiana na
kukamilishana, katika ushirika na katika kuzaa matunda. Si suala tu la kutungwa kwa mlolongo wa
taratibu, bali ni kuonyesha tunu, ili kuitika hitaji la hizo linaloonekana leo, hata katika nchi
zinazofuata zaidi msimamo wa kidunia (most secularized).”[230]Sambamba, “imesisitizwa
kwamba unahitajika uinjilishaji unaoweza kukemea wazi athari za kitamaduni, kijamii, kisiasa na
kiuchumi, kama kwa mfano mitazamo ya kimasoko iliyotiliwa mkazo mkubwa, ambayo imekuwa
kikwazo kwa maisha ya familia na imesababisha ubaguzi, umaskini, unyanyapaa na ujeuri.”
Wakati huohuo, mazungumzano na ushirikiano na mifumo ya kijamii vinapaswa kukuzwa; na pia
inatakiwa kuwahamasisha na kuwategemeza waamini walei wanaojihusisha kama Wakristo katika
nyanja za kitamaduni na za kijamii-kisiasa.”[231]
202. “Mchango mkubwa kwa uchungaji wa familia unatolewa na parokia, ambayo ni familia ya
familia nyingi, ambapo jumuiya ndogondogo, vyama vya kitume na taasisi mbalimbali za kikanisa
zinaunganishwa pamoja.”[232]Pamoja na mpango wa kichungaji unaoelekezwa mahsusi kwa
familia, tunadhihirishiwa uhitaji wa “malezi madhubuti kwa mapadre, mashemasi, watawa wa kike
na wa kiume, makatekista na wadau wengine wa mambo ya kichungaji”.[233]Katika michango
kutoka kona mbalimbali ulimwenguni, inaonyeshwa wazi kuwa wahudumu wenye daraja takatifu
hawana mafunzo ya kutosha ili kukabiliana na changamoto nzito zinazozikabili familia leo hii.
Kuhusu shida hiyo, na desturi ya mapadre wenye ndoa inayopatikana katika hazina kubwa ya
mapokeo ya Makanisa ya mashariki, inafaa itazamwe.
203. Ingefaa waseminari wapate mafunzo yenye kuunganisha fani mbalimbali kuhusu mambo ya
uchumba na ndoa, yasihusu tu mafundisho ya Kanisa. Aidha, mafunzo yao hayatoshelezi daima
kuwasaidia wafunue mtima wao wa kisaikolojia na wa mahabahisia (affective). Wengine wanatoka
katika familia zenye matatizo, bila wazazi na zisizo na uthabiti wa mihemuko. Kuna haja ya
kuhakikisha kuwa mpango wa malezi unawawezesha kufikia ukomavu wa kiutu, ili wapate utulivu
mzuri ule wa kisaikolojia unaodaiwa na majukumu yao ya usoni. Mafungamano ya kifamilia ni
muhimu sana kwa ajili ya kukuza uwezo mzuri wa waseminari wa kutambua hadhi yao. Ni muhimu
kwa familia ziwe karibu nao katika mchakato mzima wa malezi ya seminari na maisha ya kipadre,
kwani zinachangia kuwatia nguvu kwa namna halisi. Inasaidia sana kwa waseminari kuishi muda
mwingine seminarini na muda mwingine maparokiani. Hapo parokiani wanapata kukutana na
mazingira halisi ya kifamilia; na ni kweli kwamba katika maisha yake yote ya kichungaji, padre

7.8 Page 68

▲back to top
68
hujihusisha hasa na familia. “Uwepo wa walei, familia na hasa uwepo wa wanawake katika malezi
ya kipadre, unakuza kutambua uzuri wa tofauti na mkamilishano wa miito mbalimbali ndani ya
Kanisa.”[234]
204. Majibu yaliyotolewa kwa mashauriano ya kabla ya Sinodi pia yamehimiza juu ya uhitaji wa
mafunzo kwa walei wanaotenda kazi katika uwanja wa uchungaji wa familia, kwa msaada wa
walezi wataalamu wa saikolojia, madaktari wa familia na madaktari wa jumuiya, maofisa wa ustawi
wa jamii, mawakili wa watoto na familia; pamoja na utayari wa kujifunza kutokana na michango ya
saikolojia, sosholojia, elimujinsia, na ushauri nasaha pia. Wataalamu, hasa wale wenye uzoefu wa
kusindikiza, wanasaidia kuweka mikakati ya kichungaji inayojikita katika hali halisi na mahangaiko
ya kweli ya familia. “Kozi na mipango mbalimbali zilizo maalumu kwa wadau wa mambo ya
kichungaji zaweza kuwa na msaada ili wamudu kujumuisha mpango wa maandalizi kabla ya ndoa
ndani ya mpango mkubwa endelevu wa maisha katika Kanisa.”[235]Mafunzo bora ya kichungaji ni
muhimu, “hasa kwa sababu ya hali maalumu zilizotokana na ukatili wa nyumbani na udhalilishaji
wa kijinsia”.[236]Mambo haya yote hayafifishi bali yanakamilisha thamani kubwa ya maongozi ya
kiroho, ya hazina kubwa za kiroho za Kanisa na ya sakramenti ya Upatanisho.
Kuwaandaa wachumba kwa ajili ya ndoa
205. Mababa wa Sinodi wamesema kwa namna mbalimbali kwamba tunapaswa kuwasaidia vijana
kutambua hadhi na uzuri wa ndoa.[237]Wanapaswa kusaidiwa kutambua mvuto wa muungano
kamili ambao hukuza na kutimiliza tabia ya kijamii ya maisha, huipa ujinsia maana bora zaidi, na
huwanufaisha watoto kwa kuwapatia mazingira bora ya makuzi na malezi.
206. “Mambo mengi ya jamii ya leo na changamoto zinazozikabili familia zinahitaji juhudi kubwa
kwa jumuiya nzima ya kikristo katika kuwaandaa kwa ajili ya ndoa wale wanaokaribia kuoana.
Umuhimu wa fadhila ni vema uonyeshwe. Kati ya hizo, usafi wa moyo hudhihirisha thamani ya
pekee katika kukua kwa upendo wa kweli baina ya watu. Katika mtazamo huu, Mababa wa Sinodi
wamekubali juu ya uhitaji wa kuihusisha jumuiya nzima kikamilifu zaidi kwa kutoa nafasi ya pekee
kwa ushuhuda wa familia zenyewe, na kujikita kwa maandalizi ya ndoa ndani ya mchakato wa
kuingizwa katika Ukristo, kwa kuonyesha uhusiano baina ya ndoa na ubatizo na sakramenti
nyingine. Mababa wamezungumzia pia juu ya uhitaji wa mipango mahsusi kwa ajili ya maandalizi
ya ndoa inayowapatia wachumba ushiriki mzuri katika maisha ya kikanisa, na kuangalia kwa
undani mambo mbalimbali ya maisha ya kifamilia.”[238]
207. Nazitia moyo jumuiya za Kikristo kutambua faida kubwa zinazopatikana kwao zenyewe kwa
kuwasaidia wachumba katika kukua katika upendo. Kama ambavyo imeshabainishwa na
Maaskofu wa Italia, kwa ajili ya jumuiya ya kikristo wanandoa ni “tunu ya thamani, jinsi
wanavyosaidiana kukua katika upendo na kujitolea kama zawadi kila mmoja kwa ajili ya mwingine,
wanachangia kuleta mwamko mpya katika Kanisa zima. Urafiki wao wa pekee waweza
“kuwaambukiza” wengine, na kukuza urafiki na udugu katika jumuiya yao ya Kikristo”.[239]Kuna

7.9 Page 69

▲back to top
69
namna nyingi za halali za kupanga maandalizi ya ndoa, na kila Kanisa mahalia litaamua namna ipi
ni bora zaidi, kwa kutoa malezi yanayofaa bila kuwaweka vijana mbali na sakramenti. Hawahitaji
kufundishwa Katekisimu yote, wala kupewa mafundisho mengi sana. Hata kuhusu hayo, ni kweli
kwamba “sio elimu kubwa inayojaza na kuridhisha roho, bali ni kuguswa na kufurahia mambo toka
moyoni”.[240]Ubora ni muhimu zaidi kuliko uwingi, na kipaumbele kiwekwe - pamoja na kuhubiri
tena mafundisho ya msingi ya Injili (kerigma) - katika kutoa mafundisho yenye mvuto na mguso wa
kuwasaidia wachumba kujiandaa kuishi pamoja daima “kwa moyo thabiti na
ukarimu”.[241]Maandalizi ya ndoa yanapaswa kuwa ni “mafunzo ya awali” kuelekea sakramenti ya
ndoa, yakiwasaidia wachumba kupokea sakramenti kwa nia nzuri na kufanya mwanzo imara wa
maisha ya kifamilia.
208. Kwa msaada wa familia za kimisionari, familia za wachumba wenyewe na mambo mbalimbali
ya kichungaji, njia mbalimbali zipangwe za kutoa maandalizi ya mapema, ili kwa kuwasindikiza
kwa mifano na ushauri mzuri, yawasaidie kukua katika kupendana. Majadiliano katika makundi ya
wachumba na mazungumzo juu ya mada mbalimbali zinazopendwa kweli na vijana mara nyingi
yanasaidia sana. Pia mikutano ya mmoja mmoja ni mizuri, kwani lengo la msingi ni kumsaidia kila
mmoja kujifunza kumpenda mtu ambaye ana mpango wa kuishi naye kwa maisha yote. Kujifunza
kumpenda mtu hakuji ghafla, wala hakufundishwi katika semina fupi kabla ya adhimisho la ndoa.
Kwa kweli, kwa kila mtu, maandalizi ya ndoa yanaanza baada ya kuzaliwa. Alichopokea katika
familia zake kingeweza kumsaidia ajifunze kutokana na maisha yake, na kumwezesha kufanya
uamuzi mkamilifu na wa daima. Walioandaliwa vizuri kwa ajili ya ndoa, pengine ni wale
waliofundishwa maana ya ndoa ya kikristo toka kwa wazazi wao, waliochaguana bila masharti na
kuzidi kuthibitisha uamuzi ule. Katika mtazamo huu, vipaumbele vya kichungaji vinavyoelekezwa
katika kuwasaidia wanandoa kukua katika upendo na kuishi Injili katika familia, ni msaada
usiopimika kwa watoto, ili wajiandae kwa maisha ya baadaye ya ndoa. Pia tusipuuze michango
mizuri inayotolewa na uchungaji wa kitamaduni. Nawaza kwa mfano juu ya siku ya Mtakatifu
Valentino; kwa baadhi ya nchi, malengo ya kibiashara yanatawala zaidi katika kujua umuhimu wa
siku hii kuliko malengo ya Kanisa.
209. Maandalizi ya wale walioweka hadharani uchumba wao, pale ambapo jumuiya ya parokiani
inafaulu kuwasaidia tangu awali, yaweza kuwapa pia nafasi ya kuona changamoto na hatari za
usoni. Kwa namna hii, wataweza kufikia hatua ya kutambua kwamba ni busara kuvunja uhusiano
ule, ili kuepukana na hatari ya kushindwa ambako kungeleta huzuni nyingi. Kwa sababu ya nguvu
ya upendo wa mwanzoni mwa mahusiano yao, wachumba wanaweza kuficha au kupunguza uzito
wa mambo mbalimbali na kuepusha migogoro baina yao; na kusukuma mbele tu matatizo,
ambayo baadaye huibuka. Kwa sababu hiyo, wahimizwe sana kujadiliana juu ya matarajio yao ya
baadaye katika ndoa, wanachojua juu ya upendo na kujitoa, nini kila mtu anataka toka kwa
mwenzie na aina gani ya maisha wanataka kujenga pamoja. Majadiliano hayo yatawasaidia
kutambua kama maafikiano si mengi, na kutambua kuwa mvuto wa nje hautoshelezi kuwaweka
pamoja. Hakuna chenye kudai, kisicho cha uthabiti na kisichoweza kutabiriwa kuliko shauku.
Uamuzi wa kuoa usikaziwe sana iwapo hakuna sababu na mazingira mazuri ya kuhakikisha

7.10 Page 70

▲back to top
70
uhalisia na uthabiti kwa mpango ule wa kufanya agano la kudumu.
210. Katika tukio lolote, ikiwa mwenza mmoja ametambua udhaifu wa mwenzake, basi anapaswa
kuwa na imani isiyo bandia juu ya uwezekano wa kumsaidia kusitawisha mema aliyo nayo ili
kuwiana na uzito wa udhaifu wake, akiwa na nia thabiti ya kuhamasisha maendeleo ya kiutu. Hali
hii inadai kukubali kwa utashi thabiti uwezekano wa kukabiliana na majikatalio na matatizo na
migogoro; inadai pia maamuzi mazito ya kuwa tayari kufanya hivyo. Wachumba wanapaswa kuwa
na uwezo wa kutambua ishara za hatari katika mahusiano yao, na kabla ya ndoa watafute njia
sahihi za kukabiliana nazo na kuzishinda. Kwa bahati mbaya, wachumba wengi hufunga ndoa
pasipo kujuana vema. Wamefurahia kuwa pamoja na kufanya mengi pamoja, lakini
hawakukabiliana na changamoto wa kujifunua walivyo na kujuana vizuri kwa undani.
211. Maandalizi yote ya ndoa, yawe ya muda mfupi au mrefu, yahakikishe kuwa wachumba
hawachukulii kuwa sherehe ya harusi ndio mwisho wa nia yao, bali kuichukulia ndoa kama wito
wa muda mrefu unaowataka wawe na maamuzi imara na halisi ili kukabiliana na changamoto
mbalimbali na magumu kwa pamoja. Msaada wa kichungaji kwa wachumba na wanandoa lazima
ujikite katika uchungaji juu ya kifungo cha ndoa, utakaowasaidia sio tu kukuza upendo baina yao
bali kukabiliana na matatizo na magumu mbalimbali. Msaada huo sio tu kuyapokea mafundisho ya
Kanisa, wala kuzitumia tunu za thamani za kiroho ambazo daima Kanisa linaweza kutoa, bali
lazima uwe kuwasaidia kwa vitendo, ushauri wenye nguvu, mikakati halisi inayotokana na uzoefu
wa maisha, na maelekezo ya kisaikolojia. Haya yote yanaunda malezi ya upendo, yanayojikita
katika hisia na mazingira ya vijana na uwezo wa kuwasaidia kukua kiundani. Maandalizi ya ndoa
yawapatie wachumba pia majina ya mahali na watu, pia taasisi au familia zinazoweza kuwapa
ushauri, ambapo wataweza kuzifikia ili kupata msaada mara wapatapo shida fulani. Pia ni muhimu
kuwakumbusha juu ya uwepo wa sakramenti ya upatanisho, ambayo itawasaidia kuungama
dhambi zao na makosa ya maisha yao, na hata ya mahusiano yao yenyewe, mbele ya Mungu, na
kupokea msamaha wa huruma yake na ya nguvu yake ya kuponya.
Maandalizi ya adhimisho
212. Maandalizi ya muda mfupi ya ndoa yanajikita katika mialiko, mavazi, sherehe na vitu vingi
ambavyo sio tu hugharimu pesa nyingi bali pia nguvu na hata furaha. Wachumba wanakuja
kwenye siku ya harusi wakiwa wachovu sana na wanaharakishwa, badala ya kuweka nguvu zao
zote katika kujiandaa kama jozi kwa hatua kubwa watakayopiga kwa pamoja. Mawazo kama hayo
pia huwaathiri wale wanaoishi pamoja, bila kufikia kamwe katika hatua ya kufunga ndoa, kwa
sababu ya kufikiria sherehe zenye gharama kubwa mno, badala ya kuiwekea kipaumbele hali yao
ya kupendana na kuidhihirisha rasmi mbele ya watu. Wachumba wapendwa, muwe na ujasiri wa
kuwa tofauti. Msitekwe na mambo ya jamii ya ulaji na muonekano. Kilicho muhimu ni upendo
unaowaunganisha, wenye kuimarishwa na kutakatifuzwa na neema. Mnaweza kuchagua sherehe
kuwa ya kawaida tu, ambapo upendo unatawala juu ya kila kitu. Wadau wa mambo ya kichungaji
na jumuiya kwa ujumla wanaweza kusaidia ili kipaumbele hiki kiwe jambo la kawaida wala si la

8 Pages 71-80

▲back to top

8.1 Page 71

▲back to top
71
kipekee.
213. Katika maandalizi yao ya siku ya ndoa, ni muhimu wachumba wasaidiwe kujiandaa ili
adhimisho la kiliturujia liwaguse ipasavyo, ili kila mmoja aone maana na thamani ya kila ishara.
Kwa wale ambao wote ni wabatizwa, nia inayoonyeshwa na mabadilishano ya ukubali wa ndoa,
na muungano wa miili ambao huifanya ndoa ikamilike, huweza kufasiriwa tu kama ishara ya
upendo wa Mwana wa Mungu aliyetwaa mwili na kuunganika na Kanisa lake katika agano la
upendo. Kwa wabatizwa, maneno na vitendo huwa lugha mwanana inayodhihirisha imani. Mwili,
pamoja na maana ambayo Mungu alipouumba akaiweka ndani yake, “huwa lugha ya wahudumu
wa sakramenti ya ndoa, wanaotambua kwamba katika makubaliano ya ndoa fumbo huonyeshwa
na kudhihirishwa ambalo hutoka kwa Mungu mwenyewe”.[242]
214. Wakati mwingine, wachumba hawapati maana nzuri ya kiteolojia na kiroho ya maneno ya
ukubaliano, ambayo huangaza maana ya vitendo vyote vinavyofuata. Ihimizwe kwamba maneno
yale hayahusu wakati wa sasa tu; bali ni kwa nyakati zote pamoja na wakati ujao: “mpaka kifo
kiwatenganishe”. Maneno ya ukubaliano yanaonyesha maana hii, kwamba “uhuru na uaminifu
hayakinzani, ila yanabebana, katika mahusiano ya mtu na mtu na mahusiano ya kijamii. Halafu,
tufikirie madhara yaliyosababishwa katika utamaduni wetu wa mawasiliano ya kiutandawazi, kwa
ongezeko kubwa la kutotimiza ahadi […]. Mtu kuheshimu maneno aliyotoa, na kuwa mwaminifu
kwa kile alichoahidi: haya ni mambo yasiyonunuliwa wala kuuzwa. Hayawezi kudaiwa kwa nguvu,
wala kuyatunza bila kujitoa sadaka.[243]
215. Maaskofu wa Kenya wamegundua kuwa “wanaotarajia kufunga ndoa, wakiwa wanaitazama
zaidi siku ya harusi, wanasahau kwamba wanajiandaa kwa jukumu ambalo watakuwa nalo kwa
maisha yote”.[244]Wanapaswa wasaidiwe kuona kuwa sakramenti si kitu cha mara moja tu na
kisha kusahaulika, bali inatia nguvu kwa maisha yote ya ndoa, kwa namna ya
kudumu.[245]Maana ya uumbaji shirikishi katika masuala ya kujamiiana, lugha ya mwili na alama
za upendo zinazojionyesha wakati wote wa maisha ya ndoa, zote zinakuwa “mwendelezo usio na
mwisho wa lugha ya kiliturujia” na “maisha ya ndoa yanakuwa, na namna fulani, liturujia”.[246]
216. Wachumba wanaweza pia kutafakari juu ya masomo ya Biblia, na maana ya pete
watakazobadilishana na ishara mbalimbali zinazopatikana katika madhehebu ya ndoa. Wala
haitakuwa vizuri kwao kuifikia siku ya kufunga ndoa huku hawakuwahi kusali pamoja, kuombeana,
kuomba msaada wa Mungu ili kuwa waaminifu na wakarimu, kumwuliza Bwana nini anataka
kutoka kwao, na kuweka wakfu pendo lao mbele ya taswira ya Bikira Maria. Wale
wanaowasindikiza katika maandalizi ya ndoa ingefaa wawaelekeze ili wapate uzoefu wa kusali
ambao utaweza kuwafaa sana. “Liturujia ya ndoa ni tukio la pekee, ambalo linaadhimishwa kwa
furaha katika mazingira ya kifamilia na kijamii. Ishara ya kwanza ya Yesu ilifanyika katika karamu
ya harusi ya Kana. Divai njema, iliyotokana na muujiza wa Bwana na kuleta furaha mwanzoni
mwa familia mpya, ni divai mpya ya agano la Kristo na waume kwa wake wa vizazi vyote. [...]
Mara nyingi, kiongozi wa ibada anapata fursa ya kuongea na kusanyiko la watu ambao si washiriki

8.2 Page 72

▲back to top
72
wa mara kwa mara wa maisha ya kikanisa, au ni Wakristo wa madhehebu mengine au dini tofauti.
Kumbe ni nafasi nzuri ya kutangaza Injili ya Kristo”.[247]
Kusindikiza mwanzoni mwa maisha ya ndoa
217. Ni muhimu ndoa ionekane kuwa ni suala la upendo, na kwamba wale tu ambao
wamechaguana kwa uhuru na wanapendana ndio wafunge ndoa. Lakini ikiwa upendo ni mvuto wa
kimwili au mahusiano ya juujuu tu, wanandoa wataingia katika hatari pale ambapo ukaribu au
mvuto wa sura utapungua. Kutokana na hali hii kutokea mara kwa mara, ni muhimu sana
wanandoa wasindikizwe katika miaka ya mwanzo ya maisha yao ya pamoja ili wazidi kusitawisha
na kuimarisha uamuzi wao wa dhati na huru wa kuwa kila mmoja wa mwenzake na wa kupendana
mpaka mwisho wa maisha. Mara nyingi kipindi cha uchumba hakitoshi, uamuzi wa kufunga ndoa
unaharakishwa kwa sababu mbalimbali, na mbaya zaidi vijana wanachelewa kukomaa. Basi,
matokeo yake wanandoa wapya wanalazimika kuendelea kumalizia ile safari ambayo ingetakiwa
kutimilika katika kipindi cha uchumba.
218. Kwa upande mwingine, napenda kusisitiza kwamba katika uchungaji wa familia changamoto
mojawapo ni kusaidia kutambua kwamba ndoa si jambo la siku moja tu basi. Muungano wa
wanandoa ni halisi na usioweza kuvunjika kamwe, umethibitishwa na kutakaswa na sakramenti ya
ndoa. Lakini katika kuungana kwao, wanandoa wanajikita katika wajibu wa kuendesha maisha yao
na katika kubuni mpango wa maisha wa kutimiliza kwa pamoja. Mtazamo wao unaelekezwa
kwenye mambo ya mbele yapasayo kujengwa siku kwa siku kwa msaada wa neema ya Mungu.
Kwa sababu hiyo, kila mmoja asitegemee mwenzie kuwa mkamilifu. Kila mmoja anapaswa
kuweka kando mawazo yasiyo halisi na kumkubali mwenzake kama alivyo: kuwa ni mtu
anayeendelea kutimilika na kukua. Ukosoaji mkali wa mara kwa mara kwa mwenzi wa ndoa ni
ishara ya kuwa ndoa imefungwa kwa kukosa wazo la kwamba yenyewe ni mpango wa kujenga
pamoja maisha, kwa uvumilivu, kuelewana, msamaha na ukarimu. Taratibu upendo utafifia kiasi
cha kuanza kukosoana vikali, kuishi kwa kupimana madai na haki, kukaripiana, kushindana na
kujitetea. Kisha wanandoa wanajiona kushindwa kusaidiana katika kukomaa kwao na katika
kukuza muungano wao. Hali hii inapaswa kudhihirishwa wazi mapema kwa wanandoa wapya, ili
watambue kuwa harusi ni “mwanzo tu” wa maisha yao ya pamoja. Kwa kuambiana “ndiyo” wakati
wa ibada wameanza safari inayowataka kukabiliana na kushinda magumu na vikwazo vyote
vitakavyokuwepo mbele yao. Baraka ya ndoa wanayoipokea ni neema na kichocheo kwa safari hii
iliyo mbele yao. Mara nyingi kuketi na kujadili kuhusu mpango wa maisha, kupanga malengo, njia
na hatua mbalimbali kunasaidia.
219. Nakumbuka msemo wa zamani: maji yanayotuama yanakuwa mgando na kuharibika. Ni kile
kinachotokea endapo katika miaka ya mwanzo ya maisha ya ndoa pendo litapoa, litakosa kuwa
kichocheo bora cha kuyakuza na kuyasukuma mbele. Ngoma ya kusonga mbele inayochezwa na
upendo mchanga, ngoma ya mshangao uliojaa tumaini isikome kamwe. Wakati wa uchumba na
katika miaka ya mwanzo ya maisha ya ndoa matumaini ndiyo kama kichocheo kinachosukuma

8.3 Page 73

▲back to top
73
kutazama mbali zaidi kwa kushinda migogoro, magomvi, mazingira magumu, na kinachowezesha
kuona daima mbele. Matumaini ndiyo yanayochochea kila matarajio yetu ili kuendelea katika
kukua. Matumaini yenyewe yanatutaka tuishi kikamilifu muda wa sasa, kwa kujitoa kikamilifu kwa
maisha ya familia, kwa sababu njia bora ya kuandaa maisha bora ya baadaye ni kuishi vizuri sasa.
220. Safari hii ina hatua mbalimbali ambazo zinatudai kujitoa kwa ukarimu: Hisia za nguvu za
kwanza za mvuto zinafungua njia ya kudhihirisha kuwa sasa mwenzangu ni sehemu ya maisha
yangu. Kutoka hapa tunaingia katika hatua ya utamu wa kuwa kila mmoja mali ya mwenzie, na
baadaye kuyaelewa maisha yote kama mpango wa wote wawili, na uwezo wa kuhakikisha kwanza
furaha ya mwenzio, na furaha ya kuona kwamba ndoa hii inaifaidisha jamii. Pendo litakua ikiwa
wahusika watajifunza pia “namna ya kufikia mwafaka”. Majadiliano hayo yasipohusishwa na
ubinafsi au mchezo wa nipe nikupe, ni njia nzuri ya kuonyeshana upendo, kwa sababu ni mfumo
wa kupeana na kujinyima, kwa manufaa ya familia. Katika kila hatua mpya ya maisha ya ndoa,
kuna kila haja ya kuketi chini na kurudia makubaliano, ili asiwepo anayeshinda na anayeshindwa,
bali wote wawili wawe washindi. Nyumbani, maamuzi yasifanywe na upande mmoja tu, kwani
wanandoa wote wawili wana wajibu kwa familia; hata hivyo kila familia ni ya pekee na kila ndoa
itatafuta namna bora zaidi itakayowafaa.
221. Miongoni mwa sababu za kuvunjika ndoa ni matarajio makubwa mno juu ya maisha ya ndoa.
Pale mambo yanapokwenda tofauti na mategemeo na kuleta changamoto kinyume na mtu
alivyotegemea, suluhisho si kufikiria haraka na bila busara kufikiria bora kutengana, bali ni
kutambua kuwa maisha ya ndoa ni safari ya ukomavu, ambapo kila mmoja ni njia ya Mungu ya
kumsaidia mwingine kukua. Mabadiliko, maendeleo, kushamiri kwa mambo mazuri yaliyoko kwa
kila mmoja - haya yote yanawezekana. Kila ndoa ni aina ya “historia ya wokovu”, nayo ina maana
kwamba inakubalika ianzie katika udhaifu fulani, na ambayo kutokana na zawadi ya Mungu na
itikio la wanandoa lenye ubunifu na ukarimu, polepole inageuka kuwa zaidi na zaidi kitu cha
thamani na cha kudumu. Tuseme kwa hakika kuwa mkakati mkubwa kati ya watu wawili katika
upendo ni kusaidiana na kuwa mwanaume hasa au mwanamke hasa. Kuchochea kukua maana
yake ni kumsaidia mtu kujitengeneza kadiri ya utambulisho wake mwenyewe. Kwa sababu hiyo
upendo ni jambo la kiufundi. Tunaposoma katika Biblia juu ya kuumbwa kwa mtu, tunamwona
Mungu akimwumba kwanza Adamu (Taz. Mwa 2:7); Halafu anatambua kuna kitu muhimu
kimepungua, na hivyo anamwumba Eva, na kisha anamsikia mwanaume akisema kwa hisia ya
mshangao, “Naam, huyu ndiye anayenifaa!”. Na baadaye ni kama twaweza kusikia yale
mazungumzo mazuri sana mwanaume na mwanamke wanapoanza kutambuana. Katika maisha
ya wanandoa, hata katika kipindi kigumu, mmoja aweza kumshangaza mwingine, na milango
mipya kufunguliwa ili kukutana tena; utadhani ndiyo wanakutana kwa mara ya kwanza. Katika kila
hatua mpya, wanarudia “kuundana” wao kwa wao. Upendo hufanya wavumiliane kwa subira kama
ile ya fundi, waliyoirithi kwa Mungu mwenyewe.
222. Kuwasindikiza kiuchungaji wanandoa wapya ni pamoja na kuwahimiza kuwa wakarimu katika
kurithisha uhai duniani. “Kadiri ya tabia ya ujumla na binafsi ya binadamu juu ya upendo wa

8.4 Page 74

▲back to top
74
kindoa, uzazi wa mpango hufaa kama ni maafikiano ya mazungumzano ya wanandoa,
ukizingatiwa muda na hadhi ya kila mmoja. Kwa maana hii, mafundisho ya Ensiklika Humanae
Vitae (taz. 10-14) na Wosia wa kitume Familiaris consortio (taz. 14; 28-35) lazima yaangaliwe
upya kwa lengo la kuamsha utayari wa kuzaa na kupambana na dhana mbaya dhidi ya uhai […].
Maamuzi yahusuyo uzazi wenye uwajibikaji yanategemea malezi ya dhamiri, ambayo “ndicho kiini
cha siri zaidi cha binadamu, na hekalu lake. Humo yeye yumo peke yake pamoja na Mungu,
ambaye sauti yake ndimo inamosikika” (Gaudium et spes, 16). Kadiri wanandoa wanavyojitahidi
kuisikiliza sauti ya Mungu katika dhamiri na sheria zake (taz. Rum 2:15), na kusindikizwa kiroho,
ndivyo maamuzi yao yatakuwa siyo ya kukurupuka na ya kufuata mkondo tu”.[248] Mafundisho
yaliyo wazi ya Mtaguso wa pili wa Vatikano bado yana uzito: “Wenzi wa ndoa [...]
watajitengenezea fikra zilizo nyofu kwa njia ya kutafakari na juhudi za pamoja, wakiyazingatia
manufaa yao wenyewe na ya watoto wao, wale waliokwisha zaliwa kama vile wanaotarajiwa
kuzaliwa. Wataipima hali ya maisha ya nyakati zao na ya wao wenyewe kwa upande wa kimwili na
wa kiroho. Na hatimaye watautunza utaratibu ulio bora wa manufaa ya familia, ya jamii, na ya
Kanisa. Wanandoa wenyewe tu wafanye maamuzi haya mbele ya Mungu.”[249] Kwa upande
mwingine, “matumizi ya njia zinazojikita katika ‘mfumo wa asili wa uzazi’ (Humanae Vitae, 11)
yakuzwe. Iwekwe wazi kwamba ‘njia hizi zinaheshimu miili ya wenzi, zinachochea kujaliana na
kukuza maadili ya uhuru wa kweli’ (Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2370)., Daima mkazo uwekwe
katika hoja kuwa watoto ni zawadi ya ajabu kutoka kwa Mungu, na furaha ya wazazi na ya Kanisa.
Kwa njia yao, Bwana huupyaisha ulimwengu.”[250]
Baadhi ya mbinu za kufanya
223. Mababa wa Sinodi walionelea kuwa “miaka ya mwanzo ya ndoa inahusu kipindi muhimu na
makini ambacho wanandoa hutambua changamoto na maana ya maisha ya ndoa. Kwa hiyo
msaada (usindikizaji) wa kichungaji unapaswa uendelee kutolewa hata baada ya adhimisho
lenyewe la sakramenti (Familiaris Consortio, Sehemu ya III). Katika hili, wanandoa wenye uzoefu
wana nafasi nzuri ya kusaidia. Parokia ni mahali ambapo wanandoa hao wenye uzoefu wanaweza
kuwasaidia wanandoa vijana, kwa kushirikiana na taasisi, vyama vya kitume na jumuiya mpya.
Wanandoa vijana wanahitaji kutiwa moyo kupokea zawadi kubwa ya watoto. Mkazo pia utolewe
juu ya umuhimu wa maisha ya kiroho ya familia, sala na ushiriki wa Ekaristi siku za Dominika;
wanandoa watiwe moyo kukutana mara kwa mara ili kusaidia maendeleo ya maisha ya kiroho na
mshikamano katika mahitaji halisi ya maisha. Liturujia, namna mbalimbali za kusali na adhimisho
la Ekaristi kwa ajili ya familia, hasa katika kumbukumbu ya siku ya kufunga ndoa, zimetajwa kama
nafasi muhimu sana katika kufanikisha uinjilishaji kupitia familia.”[251]
224. Safari hii huchukua muda. Upendo unahitaji muda ulio wazi na usio na madai; vingine vyote
hufuata baadaye. Unahitajika muda kwa kuzungumza, kwa kukumbatiana bila haraka, kwa
kushirikishana mipango, kwa kusikilizana, kwa kuangaliana usoni, kwa kutambua thamani ya kila
mmoja na kuimarisha uhusiano. Mara nyingine, mambo ya haraka haraka ndani ya jamii na
shinikizo la majukumu ya kazi vinaibua matatizo. Nyakati nyingine, tatizo ni kwamba watu

8.5 Page 75

▲back to top
75
hawaishi vizuri muda wanapokaa pamoja. Watu wanaweza kukaa mahali pamoja, lakini bila
kujaliana. Wahudumu wa mambo ya kichungaji na makundi ya watu wa ndoa ingetakiwa wasaidie
wanandoa wachanga au wanandoa walio hatarini kujifunza kukutana katika nafasi hizo, kutulia
mmoja mbele ya mwingine, na pia kushiriki katika nafasi za ukimya zinazomlazimisha kila mmoja
aelewe uwepo wa mwenzake.
225. Wanandoa waliojifunza kufanya hili vizuri wanaweza kupendekeza njia na mbinu halisi
walizoziona kuwa zinafaa: kupanga muda wa kuwa pamoja bila madai, nyakati za burudani na
watoto, namna mbalimbali za kusherehekea matukio muhimu, kushirikishana nafasi mbalimbali za
makuzi ya kiroho. Lakini wanaweza pia kufundisha mbinu zitakazosaidia nafasi hizo ziwe na uzito
na ziwe za maana zaidi, na hivyo kukuza mahusiano yao. Hii ni hatua muhimu sana wakati upya
wa uchumba unapopoa Ikifikia mmoja haoni thamani ya kuwa na muda na mwenzie, basi mmoja
au wote watatafuta njia mbadala, atakimbilia kwenye teknolojia, atabuni majukumu mengine,
atatafuta ukaribu na mwingine au kutafuta njia nyingine za kuwa mbali na yule ambaye ukaribu
wake umemchosha.
226. Wanandoa vijana watiwe moyo kuanzisha mazoea yao, ambayo yatawafanya wajisikie katika
hali ya uimara na salama, mazoea yanayojengwa kwa njia ya taratibu za kila siku zinazokubaliwa
nao. Ni jambo jema la kila wakati busu la asubuhi, baraka ya jioni, kusubiriana mlangoni na
kupokeana, matembezi ya pamoja na kufanya pamoja kazi za nyumbani. Lakini wakati huohuo ni
vizuri kusitisha mazoea kwa kufanya sherehe, bila kushindwa kusherehekea nyumbani, kufurahia
na kuadhimisha matukio mazuri. Wanahitaji nyakati hizi za kufurahia zawadi za Mungu, na
kuongeza kwa pamoja utamu na uchangamfu wa maisha. Tukijua kuadhimisha, uwezo huo
unafanya upya nguvu ya upendo, nao hautawaliwi tena na hali ya uchokevu wa kurudiarudia tu
bali utajaza mazoea ya kila siku kwa uchangamfu na tumaini.
227. Sisi wachungaji tunapaswa kuzitia moyo familia kukua katika imani. Hii ikihusisha
kuwashawishi kufanya mara kwa mara kitubio, kupata maongozi ya kiroho na kufanya mafungo.
Pia kushawishi kufanya sala za pamoja za wiki, kwani “familia inayosali pamoja hukaa pamoja”.
Tunapowatembelea watu makwao, tusali pamoja wanafamilia kwa ufupi na kuwaalika kuombeana
kila mmoja kwa wengine na kuikabidhi familia katika mikono ya Bwana. Wakati huohuo, inafaa
kuwatia moyo wanandoa, ili kila mmoja wao ajitafutie nafasi zake za sala peke yake mbele ya
Mungu, kwa sababu kila mmoja ana misalaba yake ya siri ya kuibeba. Kwa nini tusimwambie
Mungu shida zetu zinazotuhangaisha moyoni, na kumwomba atujalie nguvu za kuponya majeraha
yetu, na mwanga tunaohitaji ili kuyakabili majukumu yetu ? Mababa wa Sinodi wamesisitiza kuwa
“Neno la Mungu ni chemchemi ya uhai na ya mambo ya kiroho ya familia. Kazi zote za kichungaji
kwa ajili ya familia lazima ziruhusu kuundwa kiundani na kuwajenga wanafamilia kama washiriki
wa Kanisa la nyumbani kwa kupitia masomo ya tafakari na sala ya Maandiko Matakatifu kwa
mtazamo wa Kanisa. Neno la Mungu sio tu ni Habari Njema kwa maisha ya binafsi ya watu lakini
pia ni kigezo cha hukumu na mwanga unaopambanua changamoto mbalimbali zinazowakabili
wanandoa na familia.”[252]

8.6 Page 76

▲back to top
76
228. Katika baadhi ya mazingira, mmoja wa wanandoa hajabatizwa au hataki kuishi imani. Katika
hali hiyo, hamu ya mmojawapo kuishi na kukua kama mkristo inasababisha kwamba hali ya
kutojali ya mwenzake iwe sababu ya huzuni. Hata hivyo inawezekana kuwa na tunu za
kushirikishana pamoja na kuzikuza kwa dhati. Kwa vyovyote, kuonyesha upendo kwa mwenzi
asiye mwamini, kumfurahisha, kumfariji katika mateso yake, na kushirikishana maisha pamoja,
kunaashiria njia ya kweli ya utakatifu. Upendo, daima ni zawadi ya Mungu, na pale unapoenea
hudhihirisha nguvu yake ya kuleta mabadiliko, mara nyingine kwa namna ya kifumbo, hata “mume
asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe” (1Kor
7:14).
229. Maparokia, vyama, shule mbalimbali na taasisi nyingine za Kanisa zaweza kusaidia familia
kwa njia mbalimbali ili kuzitunza na kuzistawisha familia. Hii ni pamoja na: mikutano ya wanandoa
majirani au marafiki, mafungo ya muda mfupi kwa wanandoa; mafunzo ya wataalamu juu ya
mambo halisi yahusuyo maisha ya familia, vituo vya ushauri nasaha wa ndoa, wamisionari
walioandaliwa kuwasaidia wanandoa kujadili matatizo yao na shauku zao, huduma za kijamii
zinazohusu matatizo ya familia (kama ulevi wa kupindukia, kukosa uaminifu katika ndoa na ukatili
wa kinyumbani), nafasi za makuzi ya kiroho, semina kwa wazazi wenye watoto wenye matatizo,
na mikutano ya familia. Ofisi ya parokia inapaswa kujiandaa kusaidia na kuwa macho juu ya
mahitaji ya familia na kuwa tayari kuelekeza kwa urahisi penye mahali ambapo misaada
inapatikana. Pia kuna mchango wa kichungaji unaotolewa katika makundi ya wanandoa, kama
huduma na utume, sala, malezi na kusaidiana. Makundi hayo yanawawezesha wanandoa kuwa
wakarimu, kusaidia familia nyingine na kushirikishana imani; lakini wakati huohuo wanaziimarisha
ndoa na kuzisaidia kukua.
230. Ni kweli kwamba wanandoa wengi, mara baada ya ndoa, wanajitoa katika jumuiya ya
Kikristo. Lakini mara nyingi hatutumii fursa ya matukio ambapo hawa wanarudi tena, hapo
tungeweza kuwakumbusha juu ya mambo mazuri ya ndoa ya kikristo na kuwavuta katika nafasi
ambapo msaada wa usindikizaji huweza kupatikana: naongea, kwa mfano, juu ya Ubatizo na
Komunyo ya kwanza ya watoto wao, au mazishi au arusi za ndugu au marafiki. Karibu wanandoa
wote wanakuwepo katika matukio haya, na tungeweza kutumia vizuri zaidi fursa hizo. Njia
nyingine ya kuwa karibu ni zoezi la kubariki nyumba, au kutembeza manyumbani sanamu ya
Bikira Maria; nafasi hizi zinatoa fursa ya kuendeleza mazungumzo ya kichungaji kuhusu hali ya
kifamilia. Pia linaweza kuwa jambo linalofaa kuwakabidhi walio katika ndoa kwa muda mrefu
jukumu la kuwasaidia wanandoa wapya waishio maeneo ya jirani, kwa kuwatembelea na kuwapa
mwongozo wa ukuzi katika miaka yao ya awali ya ndoa. Kutokana na mwendo wa haraka wa
maisha ya kisasa, wanandoa walio wengi hawatakuwa tayari kushiriki mikutano ya mara kwa
mara; hata hivyo hatuwezi kukubali kuwa na huduma ya kichungaji kwa makundi ya watu wa
pekee wachache tu. Siku hizi, uchungaji wa familia unapaswa kuwa wa kimisionari, kuwafuata
walengwa mahali walipo. Hatuwezi kuendelea kuwa kama kiwanda cha kuandaa kozi ambazo
mahudhurio yake ni hafifu.

8.7 Page 77

▲back to top
77
Kutia mwanga kwenye migogoro, fadhaa na magumu
231. Neno moja lisemwe kwa wale ambao upendo wao, kama divai njema, baada ya uchumba
umefika mahali pake. Kama divai inavyoanza “kuwa nzuri” kadiri muda unavyoenda, pia uzoefu
wa kila siku wa uaminifu huyapatia maisha ya ndoa utajiri na utimilifu. Ni uaminifu wa subira na
uvumilivu Uaminifu huo uliojaa furaha na sadaka huzaa tunda kadiri miaka inavyoenda na yote
“yakomaa” nayo macho yao yanang’aa katika kuwatazama kwa furaha watoto wa watoto wao.
Uliokuwako tangu mwanzo, unazidi kudhihirika, kutulia na kukomaa, katika ushangao wa
kuugundua siku hadi siku zaidi, mwaka hadi mwaka. Kama alivyofundisha mtakatifu Yohane wa
Msalaba, kwamba “wapenzi wa muda mrefu wamejaribika na kuthibitika”. Wao hawatawaliwi tena
na “hisia zenye nguvu, na mihemko na moto wa vionjo vya nje, ila kwa sasa wanaonja utamu wa
divai ya upendo halisi, iliyochemka tayari na kutulia sasa mioyoni mwao.”[253] Hali hiyo
imepatikana kwa sababu wanandoa wamefanikiwa kukabiliana kwa pamoja na migogoro na
magumu, bila kuzikimbia changamoto au kuficha matatizo.
Changamoto ya migogoro
232. Maisha ya kila familia hupitia katika migogoro ya kila namna, nayo ni pia sehemu ya uzuri
wake. Wanandoa wasaidiwe kutambua kuwa kuushinda mgogoro sio sababu ya kudhoofisha
uhusiano wao; isipokuwa kunauboresha na kunautuliza, na kunaifanya divai ya umoja wao kuwa
mzuri zaidi. Maisha ya pamoja yasififishe furaha, bali yafundisha kufurahi kwa namna mpya; kila
hatua mpya yaweza kuwasaidia wanandoa kupata nafasi mpya ya kufurahi. Kila mgogoro
unakuwa ni njia ya kukua pamoja kwa karibu, au walau kuona maana mpya ya maisha ya ndoa.
Kamwe wasivumilie kukubali upendo wao upoe, maisha yao yaishie katika hali ya vuguvugu ya
kuvumiliana tu. Kinyume chake, pale ndoa inapoeleweka kama jukumu linalohusisha pia
kuvishinda vikwazo, kila mgogoro unakabiliwa kama fursa ya kufikia hatua ya kunywa pamoja
divai iliyo bora. Ni jambo jema kuwasindikiza wanandoa ili waweze kuikabili migogoro itakayokuja,
kupokea changamoto hizo na kutambua nafasi zao katika maisha ya familia. Wanandoa wazoefu
na waliokomaa wawe tayari kuwapa wengine msaada wa mwongozo, ili wanandoa wachanga
wasitishiwe na migogoro wala wasishawishike kufanya maamuzi ya kukurupuka. Kila mgogoro
unaficha habari njema inayopaswa kusikilizwa kwa kuboresha usikivu wa moyo.
233. Tunapokumbana na mgogoro, huwa tunajihami sana haraka, kwa kuwa tunadhani tutapoteza
mwelekeo, au tunadhani tuna matatizo katika namna yetu ya kuishi, na hii inatufanya tujisikie
vibaya. Tunawahi kulikimbia tatizo, kulificha au kulifanya lionekane dogo tukitumaini litayeyuka
kwa kuvuta muda. Lakini hii haisaidii; itafanya hali kuwa mbaya zaidi, kupoteza nguvu na
kuchelewesha suluhisho. Vifungo vinalegea na wanandoa wanajiimarisha katika upweke
unaoharibu mawasiliano yao ya ndani. Tunapokataa kulikabili tatizo, kinachoharibika zaidi ni
mawasiliano. Katika hali hiyo, polepole, upendo na ukaribu wa wanandoa hupungua: yule
aliyekuwa "mpenzi wangu” anakuwa "anayenisindikiza katika maisha yangu”, halafu si zaidi ya
"baba au mama wa watoto wangu”, na hatimaye ni mgeni tu.

8.8 Page 78

▲back to top
78
234. Migogoro ikabiliwe kwa pamoja. Hii ni muhimu kwa sababu wakati mwingine watu
wanajitenga ili kukwepa kueleza wanavyojisikia; wanakaa kimya tu, lakini ukimya huu si mzuri na
unajaa udanganyifu. Katika mazingira ya namna hii ni muhimu sana kutengeneza nafasi ya
mazungumzo ya wazi na ya ndani kati ya wote wawili. Tatizo ni kwamba kama wanandoa
hawajajifunza mfumo huo mapema, kuja kujifunza wakati migogoro imeshaanza ni vigumu sana.
Mtu hujifunza ufundi huo wa kweli wakati wa utulivu, ili usaidie katika kipindi kigumu. Lazima
kuwasaidia wanandoa wazitambue sababu zilizofichwa zaidi mioyoni mwao, na kuzikabili kama
kuzaa mtoto, hii ni hatua chungu inayoleta hazina mpya. Majibu yaliyotolewa kwenye maandalizi
ya sinodi yanaonyesha kuwa wengi wanapopata matatizo au changamoto huwa hawatafuti
msaada wa kichungaji kwa kuwa hawaoni kama ni wa msaada, wenye uhalisia, au hawaoni
ukaribu wa ndani wa wachungaji. Kwa sababu hiyo, sasa tutajitahidi kuyakabili migogoro ya ndoa
kwa umakini mkubwa unaojali uzito wa mateso na fadhaa.
235. Baadhi ya migogoro ni ya kawaida katika kila ndoa, kama kwa mfano migogoro ya mwanzoni,
ambapo wanandoa wapya wanapaswa kujifunza jinsi ya kupokea tofauti zao na kuachana na
wazazi. Au kama migogoro inayozuka wakati wa kupata mtoto, jambo liletalo changamoto za hisia
mpya. Kulea mtoto kunasababisha mabadiliko katika maisha ya wazazi, na kipindi mtoto
anapobalehe, kipindi kinachodai nguvu nyingi zitumike, huweza kuwasababishia wazazi shida
mbalimbali na hata mvutano kati yao. Mgogoro wa "kiota kitupu”, ambapo wazazi wanalazimishwa
kutafakari upya mahusiano yao; mgogoro wa kuwatunza wazazi wa wanandoa katika uzee wao,
matunzo hayo yanadai kuwa karibu nao zaidi, umakini zaidi na maamuzi magumu. Hali hizi zote
ngumu zaweza kumtisha mtu na kumsababisha kujisikia ana hatia fulani, kuwa na msongo wa
mawazo na uchovu wa akili, na hatimaye kusababisha matatizo makubwa kwenye ndoa.
236. Pia kuna migogoro binafsi ambayo huwaathiri wanandoa wote, na hasa inayohusu shida za
uchumi, matatizo ya kazini, ya kihisia, ya kijamii na ya kiroho. Mambo yasiyotegemewa yaweza
kuibuka na kuathiri maisha ya familia na yanahitaji kusameheana na kupatana. Katika kuwekana
sawa kwa njia ya kusameheana, kila mmoja ajiulize kwa unyenyekevu kama mwenyewe
hakuchangia kuandaa mazingira yaliyomsukuma mwingine atende makosa. Baadhi ya familia
zinaparaganyika kwa sababu ya kurushiana tuhuma, lakini “uzoefu unaonyesha palipo na msaada
wa kufaa na upatanisho utokanao na nguvu ya neema, ndoa nyingi zenye matatizo hupata
suluhisho muafaka. Kujua namna ya kusamehe na kujisikia umesamehewa ni mazoea msingi
katika maisha ya familia.”[254] “Ufundi mgumu wa upatanisho, ambao huhitaji msaada wa neema,
unahitaji ushirikiano mzuri wa ndugu na marafiki na hata msaada wa nje na msaada wa
wataalamu.”[255]
237. Imekuwa ni jambo la kawaida kufikiri kwamba, ikiwa mmoja hajaridhishwa, au matarajio yake
yameyeyuka, basi hii ni sababu tosha kwa kukomesha ndoa. Kama hali ndiyo hii, hakuna ndoa
itakayodumu. Wakati mwingine, kwa kuamua kwamba kila kitu kimekwisha inatosha siku moja
kutoridhishwa, au kutokuwepo kwa mwenzi wakati anapohitajika sana, au jeraha litokanalo na
majivuno (kuaibishwa), au hofu isiyoeleweka. Kuna hali zisizoepukika, zitokanazo na udhaifu wa

8.9 Page 79

▲back to top
79
kibinadamu, lakini zinachukuliwa kihisia kwa uzito mno. Kwa mfano, mmoja wa wanandoa
anaweza kujiona kama hachukuliwi kwa uzito kama anavyostahili, wivu na mivutano vinavyoweza
kuibuka kati yao, kuvutiwa na wengine, au vivutio vipya vinavyoelekea kuuteka moyo, mabadiliko
ya kimwili ya mwenzi. Mambo haya na mengine mengi, kuliko kuwa tishio kwa upendo, ni fursa
zinazoelekeza kuufanya upya tena.
238. Katika mazingira hayo, wengine wana ukomavu ule unaohitajika ili kumchagua tena
mwingine kama mwenzi katika safari ya maisha, licha ya madhaifu ya uhusiano kati yao, na
wanapokea kwa kukubali hali halisi ya kuwa mwenzi hataweza kutekeleza ndoto zote. Watu wa
namna hii hukwepa kujiona kama wahenga pekee; huwathamini uwezo wanaopewa na maisha
katika familia ingawa mdogo na wenye mipaka, na hufanya kila liwezekanalo kwa kuimarisha
kifungo kati yao, kazi ambayo itachukua muda na nguvu. Wanakiri kuwa kila mgogoro unakuwa
kama “ndiyo” mpya, inayouwezesha upendo kupyaishwa, kuimarishwa, kukomaa, kupata sura
mpya na kung’arishwa. Kutokana na mgogoro inawezekana kupata ujasiri wa kuchimbachimba ili
kupata mizizi ya yale yanayotokea, kujadili na kuelewana tena kuhusu makubaliano ya msingi,
kufikia muafaka mpya na kusonga mbele pamoja kuelekea hatua nyingine. Kwa msimamo huo wa
uwazi, wanaweza kukabiliana na mazingira magumu mengi. Kwa vyovyote, tukitambua kwamba
upatanisho unawezekana, tunagundua kwamba “kinachohitajika haraka leo hii ni huduma yenye
kuwashughulikia wale ambao uhusiano wao wa ndoa umevunjika.”[256]
Vidonda vya zamani
239. Inaeleweka kwamba familia hukumbana na matatizo mengi pale ambapo mmoja wa
wanafamilia hajakomaa katika namna yake ya kuhusiana na wengine, kutokana na majeraha
aliyoyapata maishani mwake kuchelewa kuponywa. Kukosa furaha utotoni au wakati wa kubalehe
huweza kusababisha matatizo binafsi yanayoathiri ndoa ya mtu. Ikiwa wote wangekuwa watu
waliokomaa kawaida, migogoro isingetokea mara kwa mara au isingeumiza sana. Lakini ukweli ni
kwamba mara nyingine ni katika miaka ya arobaini hivi, ambapo watu wanafikia kwa kuchelewa
ukomavu ambao wangeufikia kipindi cha kubalehe. Mara nyingine watu wanapenda na upendo ule
ulio wa mtoto ambao ni wa kibinafsi, umeganda katika hatua ambapo hushindwa kuelewa hali
halisi na hudai kwamba wote wamwangalie yeye na kila kitu ni chake. Ni upendo usioridhika
ambao huwa na kelele na majonzi pale usipotimiziwa matakwa yake. Mara nyingine upendo
umeganda katika kipindi cha kubalehe, ni wenye malumbano, wenye ukosoaji mkali na mazoea ya
lawama kwa wengine; unaoongozwa na hisia na ndoto, ambapo watu wa namna hii wanataka
wenzao kuwaridhisha kwa kila hitaji wanalotaka.
240. Watu wengi wanatoka utotoni bila kuonja upendo wa dhati. Hali hii inaathiri uwezo wao wa
kuwaamini na kujiaminisha kwa wengine, na kujitoa kwao. Mahusiano mabovu na wazazi na
ndugu, kama hayajarudi katika hali nzuri, madhara yake yatajitokeza na kuharibu maisha ya ndoa.
Basi, lazima kuwa na safari ya ukombozi ambayo haijawahi kufanyika. Kama kati ya wanandoa
uhusiano unaanza kuwa magumu, kabla ya maamuzi mazito kuchukuliwa, ni muhimu kuhakikisha

8.10 Page 80

▲back to top
80
kuwa kila mwanandoa ametimiza safari yake ya kuiponya historia yake. Safari hii inadai kutambua
uhitaji wa kuponywa, kuomba kwa mkazo kwa ajili ya neema ya kusamehe na kujisamehe, ukubali
wa kupokea msaada, na uamuzi wa kutokata tamaa bali kuendelea kujaribu. Kila mmoja lazima
awe mkweli kabisa kwa nafsi yake ili aweze kutambua kwamba namna yake ya kupenda ina
upungufu. Hata kama ni jambo lililo wazi kuwa mwenye kosa ni mwingine, mgogoro hauwezi
kutatuliwa kirahisi kwa kutegemea abadilike yeye mwenyewe tu. Tunapaswa kujiuliza katika
maisha yetu ni kipi kinahitaji kukua au kuponywa ili kurahisisha kushinda migogoro.
Kusindikiza baada ya kuvunjika uhusiano wa ndoa na baada ya talaka
241. Katika nafasi nyingine, kwa kuzingatia heshima ya mwenyewe na manufaa ya watoto lazima
kuyawekea mipaka thabiti madai ya ajabu ya mwingine, kuzuia ukiukwaji mkubwa wa haki, ukatili
au ukosefu wa heshima uliokuwa sugu. Lazima tukiri kwamba “zipo nafasi ambapo kutengana
hakuepukiki. Wakati mwingine, kimaadili hatua hii inalazimika, hasa pale inapolazimu
kumwepusha mwenzi mwenye hatari zaidi ya kuumia au watoto wadogo wasiumizwe vibaya kwa
sababu ya ubabe, ukatili, udhalilishaji na ukandamizaji, utelekezaji na kutokujali.”[257] Hata hivyo,
“kutengana kuchukuliwe kuwa ni hatua ya mwisho, baada ya jitihada zingine zote
kushindikana.”[258]
242. Mababa wa Sinodi wamegundua kuwa “upambanuzi maalumu ni muhimu sana kwa ajili ya
kuwasindikiza kichungaji wale waliotengana, waliopeana talaka na waliotelekezwa. Yapokelewe
na kuthaminiwa hasa maumivu ya wale ambao pasipo haki walitengwa, walipewa talaka au
kutelekezwa au ya wale ambao wameshinikizwa kuvunja maisha ya pamoja kutokana na
minyanyaso waliofanyiwa na mume au mke wao. Kusamehe ukatili huu sio kitu rahisi, ila ni safari
inayowezeshwa na neema. Kutokana na hilo kuna haja ya kuwa na huduma ya kichungaji
inayolenga upatanisho na mazungumzo kupitia vituo maalumu vya ushauri nasaha
majimboni.”[259] Wakati huohuo, “waliopewa talaka na hawajafunga ndoa nyingine, na ambao
mara nyingi ni mashahidi wa uaminifu wa ndoa, watiwe moyo kwa kushibishwa na Ekaristi ili
wasaidiwe katika hali waliyo nayo. Jumuiya mahalia na Wachungaji wawe karibu na kuwasindikiza
watu hawa, na hasa kukiwa na watoto au wanapobanwa sana na umaskini.”[260] Kuvunjika kwa
familia kunakuwa mbaya zaidi na kunaleta maumivu zaidi katika hali ya umaskini, kwani wana vitu
vichache vya kuweza kuanza maisha mapya. Mtu maskini, akiondolewa katika mazingira salama
ya familia, hali yake huwa mbaya mara mbili zaidi kutokana na upweke na hatari ya kila aina kwa
usalama wake.
243. Ni muhimu kwamba waliotalikiana na kuwa na mwenzi mpya waendelee kujiona ni sehemu
ya Kanisa. Kwamba “hawajatengwa na Kanisa” na wasifanywe kana kwamba wametengwa, kwani
wanaendelea kuwa sehemu ya ushirika wa Kanisa.[261] Hali hizi “zinahitaji upambanuzi makini na
ukaribu wenye heshima kubwa. Lugha au tabia yoyote itakayoashiria kuwadharau iepukwe, na
watiwe moyo kushiriki katika maisha ya jumuiya. Matunzo yanayotolewa na jumuiya ya Kikristo
kwa watu wa namna hiyo yasichukuliwe kuwa ni kudhoofisha imani na ushuhuda juu ya

9 Pages 81-90

▲back to top

9.1 Page 81

▲back to top
81
kutovunjika kwa ndoa; bali kwa njia ya matunzo hayo inadhihirisha mapendo yake.”[262]
244. Tena, idadi kubwa ya Mababa wa Sinodi “wamesisitiza ulazima wa kufanya taratibu za kesi
za kutangaza ubatili wa ndoa kuwa nyepesi zaidi na ikiwezekana ziendeshwe bila kudai
malipo.”[263] Mwendo wa polepole wa hukumu hizo unachosha na kuweka watu katika hali
mbaya. Nyaraka zangu mbili za hivi karibuni zinazojikita katika mambo haya[264] zimerahisisha
hatua za kutangaza ndoa batili. Kupitia nyaraka hizo, nilipenda “kuweka wazi kuwa askofu
mwenyewe, katika Kanisa analolichunga na kuliongoza, ni hakimu wa waamini waliokabidhiwa
kwake.”[265] Hivyo, “utekelezaji wa nyaraka hizi ni wajibu mkubwa wa maaskofu mahalia
majimboni, ambao wameitwa ili kutoa wenyewe hukumu katika baadhi ya kesi na kwa vyovyote
kuhakikisha waamini wanarahisishwa kupata haki zao. Hii inadai kuwaandaa watenda kazi wa
kutosha, waklero na walei, ambao katika utendaji wao wataweka kipaumbele kwa huduma hiyo ya
kikanisa. Huduma za taarifa, ushauri na mazungumzano zinazohusiana na uchungaji wa familia
zinapaswa ziwafikie wale waliotengana au walio katika mgogoro. Huduma hizi zaweza kuhusisha
mapokezi ya watu kwa uchunguzi wa awali wakati wa kuanzisha kesi ya ndoa. (taz. Mitis Iudex,
art. 2-3).”[266]
245. Mababa wa Sinodi pia waliangazia “madhara ya kutengana au kutalikiana kwa watoto,
ambao kwa vyovyote ni wahanga wasio na hatia”.[267] Pamoja na mambo mengine yote,
maendeleo ya watoto yapewe kipaumbele zaidi, na yasifunikwe kamwe na madai au malengo
mengine. Natoa ombi hili kwa wazazi waliotengana: “Kamwe, kamwe, kamwe msithubutu
kuwafanya watoto wenu mateka! Mlitengana kwa matatizo na sababu nyingi. Maisha yamewapa
haya majaribu, lakini watoto wenu wasiwe wahanga wa kutengana kwenu wala wasitumike kama
mateka dhidi ya mwenzi wa ndoa. Wakue wakimsikia mama yao akinena mazuri juu ya baba yao,
hata kama hawako pamoja, na baba akinena mazuri juu ya mama.”[268] Huwa sio sawa
kumdhalilisha mwenzi ili watoto wakupende zaidi wewe, au kumlipizia kisasi au kujifanya mwenye
haki. Kwa kufanya hivi, watoto wataumizwa kwa ndani, na vidonda hivi huwa vigumu kupona.
246. Kanisa, ingawa linaelewa mazingira ya migogoro ndani ya ndoa, haliwezi kukoma kuwa sauti
ya walio dhaifu zaidi ambao ni watoto wanaoumia, mara nyingi kimyakimya. Leo, “pamoja na
utaalamu na maendeleo yote ya kisaikolojia, najiuliza kama hatujapigwa ganzi ili tusijali majeraha
ya roho za watoto. […] Tunatambua mzigo mkubwa wa kisaikolojia unaowaangukia watoto katika
familia ambapo ndugu wanajeruhiana kiasi cha kuvunja uaminifu wa ndoa?”[269] Mazingira hayo
mabaya hayawasaidii watoto kukua vema kuelekea katika majukumu ya kudumu. Kwa sababu
hiyo, jumuiya za Kikristo zisiwatelekeze wazazi waliotalikiana na kuungana na mwenzi mpya, bali
wawakumbuke na kuwasaidia katika kazi yao ya malezi. Kwa kweli, “tutawezaje kuwatia moyo
wazazi hawa waendelee kuwalea watoto kikristo, na kuwaonyesha mfano wa maisha ya imani hai,
ikiwa tumewaweka mbali na maisha ya jumuiya kana kwamba wametengwa na Kanisa? Lazima
tuangalie namna ya kutozidisha mizigo ambayo tayari watoto, katika mazingira kama haya,
wameshaibeba!”[270] Kusaidia kutibu majeraha ya wazazi na kuwapokea kiroho, ni faida kwa
watoto pia, ambao wanahitaji kuuona uso wa kifamilia wa Kanisa katika kipindi hiki kigumu kwao.

9.2 Page 82

▲back to top
82
Talaka ni uovu, na ongezeko kubwa la talaka linahangaisha sana. Kumbe wajibu wetu muhimu wa
kichungaji juu ya familia ni kuuimarisha upendo, na kusaidia kutibu majeraha; kwa namna hiyo
tunaweza kuweka kinga dhidi ya uenezaji wa janga hilo la nyakati zetu
Baadhi ya mazingira magumu
247. “Masuala yahusuyo ndoa ya mseto yanahitaji jicho la pekee. Ndoa baina ya Wakatoliki na
wabatizwa wengine “ingawa ni za namna yake ya pekee, zina vitu vingi ambavyo vyaweza
kuthaminiwa na kuendelezwa, kutokana na thamani yake yenyewe, na pia kwa mchango ambao
zaweza kutoa kwa ajili ya mchakato wa kiekumeni”. Kwa lengo hili, “juhudi zifanywe kuimarisha
[...] mahusiano kati ya mhudumu mkatoliki na yule asiye mkatoliki, kuanzia kipindi cha maandalizi
ya ndoa mpaka siku ya ndoa yenyewe’ (Familiaris Consortio, 78). Kuhusu kushiriki Ekaristi,
“maamuzi ya wasio Wakatoliki katika ndoa kuweza kupokea Ekaristi yafuate taratibu zilizopo za
kisheria, kwa Wakristo wa Mashariki na Wakristo wengine, na hasa kwa kuzingatia hali hii ya
pekee, yaani kwamba wanapokea sakramenti ya ndoa ya kikristo wawili ambao ni wakristo
waliobatizwa. Ingawa wanandoa katika ndoa ya mseto wanashiriki sakramenti ya ubatizo na ya
ndoa, ushiriki katika Ekaristi ni jambo la pekee na, kwa vyovyote, taratibu zilizowekwa zifuatwe.”
(Baraza la Kipapa la ukuzaji wa Umoja wa Kikristo, Mwongozo wa matumizi ya kanuni na maadili
ya ekumeni, 25 Machi 1993, 159-160).”[271]
248. “Ndoa za watu wenye dini tofauti zinatoa fursa mahususi kwa mazungumzano kati ya dini
tofauti [...], zinaambatana na shida maalumu zinazohusu utambulisho wa Kikristo wa familia, na
malezi ya kidini ya watoto. [...] Idadi ya watu wanaofunga ndoa na watu wa dini nyingine
inaongezeka sana hasa katika maeneo ya kimisioni na hata katika nchi zenye utamaduni wa
Kikristo kwa muda mrefu. Familia hizo zinahitaji haraka iwezekanavyo, matunzo mbalimbali ya
kichungaji kadiri ya mitizamo ya kijamii na kitamaduni ya eneo mahalia. Katika baadhi ya nchi
ambazo hazitambui uhuru wa dini, mwenzi mkristo analazimishwa abadili dini ili aweze kufunga
ndoa, na hivyo hawezi kuadhimisha ndoa baina ya wenzi wa dini tofauti kadiri ya sheria ya Kanisa
na hata kubatiza watoto. Lazima tuhimize tena juu ya umuhimu wa uhuru wa dini kuheshimiwa
kwa watu wote.”[272] “Uangalizi maalumu uwekwe kwa wale ambao waingia ndoa za namna hiyo,
sio tu katika kipindi kabla ya ndoa. Changamoto za pekee huwakumba wanandoa na familia
ambazo mwanandoa mmoja ni mkatoliki na mwingine hana dini. Katika hali hiyo, ushuhuda wa
uwezo wa Injili kupenya katika mazingira hayo utawezesha malezi yanayofaa kwa watoto katika
imani ya Kikristo.”[273]
249. “Matatizo ya pekee huibuka pale ambapo watu walioko katika ndoa za aina yake wanataka
kubatizwa. Tunaongea kuhusu watu ambao wamefunga ndoa wakati walau mmoja kati yao
alikuwa hana ufahamu juu ya imani ya Kikristo. Katika hali hizo, Maaskofu wanatakiwa kufanya
upambanuzi wa kichungaji ambao yanaendana na manufaa ya roho zao.”[274]
250. Kanisa linaiga kwa dhati kabisa msimamo wa Bwana Yesu, ambaye kwa upendo usio na

9.3 Page 83

▲back to top
83
mipaka amejitoa afe kwa ajili ya kila mtu bila ubaguzi.[275] Pamoja na Mababa wa Sinodi
niliangalia hali za familia ambapo ndani yake wapo watu wenye mwelekeo wa ushoga, hali
ambayo ni mgumu kwa upande wa wazazi na wa watoto pia. Tungependa kwa mara nyingine tena
kusisitiza kuwa, pasipo kujali mwelekeo wake wa kijinsia, kila mtu anastahili kupewa heshima kwa
utu wake na anastahili kupokelewa kwa heshima na hivi “kila hali ya ubaguzi usio haki”[276]
iepukwe, na hasa kila aina ya mashambulizi na ukatili. Familia za namna hii lazima zipewe kwa
heshima huduma za kichungaji, ili wale wenye mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja wapate
msaada wanaouhitaji ili katika maisha yao wayatambue na kuyatekeleza kikamilifu mapenzi ya
Mungu.[277]
251. Katika kujadili hadhi na utume wa familia, Mababa wa Sinodi waliona kuwa “kuhusu mipango
ya kutambua muungano kati ya watu wa jinsia moja kuwa sawa na ndoa, hakuna sababu za
msingi za kuweka katika hadhi sawa au ya mfanano baina ya mapenzi ya jinsia moja na ndoa
katika mpango wa Mungu juu ya ndoa na familia”. Haikubaliki, “kwa Makanisa mahalia
kushinikizwa katika mambo haya, na mashirika ya kimataifa kupanga kutoa misaada kwa masharti
kwa nchi maskini ikiwa tu zinaweka sheria za uanzishwaji wa ‘ndoa’ za jinsia moja.”[278]
252. Familia za mzazi mmoja mara nyingi zinatokana na “kutokuwa tayari kwa baba na mama
halisi kuwa sehemu ya familia, mazingira ya ukatili ambapo mzazi mmoja analazimika kukimbia na
watoto; kifo cha mmoja wa wazazi; kutelekezwa kwa familia na mmoja wa wazazi, na mazingira
mengine. Kwa sababu yoyote ile, mzazi mmoja anayekaa na mtoto inabidi atiwe moyo na apate
msaada kutoka familia nyingine za jumuiya ya Kikristo, na kutoka taasisi za kichungaji za parokia.
Mara nyingi, familia hizi hukutana na magumu, kama matatizo mazito ya kiuchumi, ukosefu wa
ajira, shida katika kutunza watoto, ukosefu wa makazi.”[279]
Maumivu makali ya kifo
253. Wakati mwingine maisha ya familia yanapata changamoto kwa wanafamilia kuondokewa na
mpendwa wao. Tusiache kutoa mwanga wa imani kwa kuzisindikiza familia zilizo katika huzuni
kwa matukio kama haya.[280] Kuipa kisogo familia yenye majonzi kutokana na msiba ni
kutokuonyesha huruma, kukosa nafasi ya kichungaji, na hali hiyo inaweza kufunga milango kwa
juhudi za uinjilishaji.
254. Natambua maumivu ya aliyefiwa na mpendwa wake, mwenzi aliyeshiriki naye mengi. Yesu
mwenyewe aliguswa sana hadi alilia kwa kifo cha rafiki yake (taz.. Yn 11:33,35). Na tunawezaje
kushindwa kuelewa kilio cha wazazi waliopotewa na mtoto wao? Maana, “ni kama siku haziendi
kabisa: ni shimo linalomeza ya jana na ya kesho”, [...] na wakati mwingine tunaenda mbali zaidi,
hata kumshtaki Mungu. Wapo watu wengi tu - nawaelewa – ambao wana hasira na Mungu.”[281]
“Hali ya ujane ni vigumu kuuvumilia. [...] Wengine wana juhudi za kuelekeza nguvu zao zote katika
malezi ya watoto na wajukuu; na katika hali hii ya upendo wanakuta namna nyingine ya kuwa
walezi. Wale wasio na ndugu wa kukaa nao na kuwasaidia au kupata faraja kutoka ukaribu wao,

9.4 Page 84

▲back to top
84
wasaidiwe na jumuiya ya kikristo kwa jicho la pekee, na hasa wakiwa katika hali ngumu ya
umaskini.”[282]
255. Katika hali ya kawaida, msiba huchukua muda na pale mchungaji anapoungana nao wafiwa,
anapaswa kuendana na mahitaji ya kila hatua waliyofikia wafiwa. Safari nzima inagubikwa na
maswali: juu ya sababu za kuondokewa na mpendwa wao, juu ya yote ambayo yangaliweza
kufanyika, juu ya hali aliyo nayo mtu wakati wa kifo... Kwa moyo wa utulivu na uvumilivu kwa njia
ya sala kutoka moyoni, amani hupatikana. Kwenye msiba, tunafikia mahali ambapo tunapaswa
kuwasaidia wafiwa watambue kuwa, baada ya kumpoteza mpendwa wao, bado wana kazi za
kufanya, na haisaidii kurefusha muda wa uchungu, kana kwamba ni tendo la kumheshimu
marehemu. Mpendwa wetu marehemu hahitaji sisi tuteseke, wala hafurahi kuona tunaharibu
maisha yetu. Wala sio njia nzuri ya kuonyesha upendo kwa marehemu wetu kuendelea kumlilia
muda wote na kumtaja kwa jina muda wote, kwa sababu inamaanisha kwamba tumeganda katika
yaliyopita, badala ya kuonyesha upendo kwa mtu halisi ambaye tayari anaishi peponi. Hawezi
kuendelea kuwa nasi kimwili, lakini, ingawa mauti na kifo kina nguvu, “upendo una nguvu kama
mauti” (Wim 8:6). Upendo unatuwezesha kusikia na kuona visivyosikika na kuonekana. Hii
haimaanishi kuwaona wapendwa wetu kama walivyokuwa, bali kuwa tayari kupokea mabadiliko
yao, na hali kama walivyo sasa. Yesu mfufuka, wakati rafiki yake Maria alipotaka kumkumbatia,
alimwambia asimshike (taz. Yn 20:17), ili amwongoze katika namna nyingine ya kukutana naye.
256. Inatufariji kujua kuwa wale waliotangulia hawapotei kabisa, na imani inatuhakikishia kwamba
Bwana mfufuka hatatutelekeza kamwe. Kwa hiyo, tunaweza kufanya kifo na msiba usiue maisha
yetu, kutufanya tushindwe kuonyesha upendo na kutuzamisha katika giza nene ”.[283] Biblia
inatuambia kuwa Mungu alituumba kwa sababu ya upendo na kufanya maisha yetu yasiyeyushwe
na kifo (taz. Hek 3:2-3). Mtakatifu Paulo anazungumza nasi juu ya kukutana na Kristo mara baada
ya kufa: “Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo” (Flp 1:23). Pamoja na Kristo, baada ya kifo,
tunasubiria “yale Mungu aliyowaandalia wampendao” (taz. 1Kor 2:9). Utangulizi wa Liturujia ya
wafu unasema vizuri sana: “Sisi tunaosikitika kwa sababu tunajua kwamba lazima tutakufa,
tufarijiwe kwa ahadi ya uzima wa milele. Maana, uzima wa waamini wako, ee Bwana,
hauondolewi, ila unageuzwa tu”. Kimsingi, “wapendwa wetu hawajapotelea mahali pasipo na
maana; tumaini linatuhakikishia kuwa wako katika mikono iliyojaa mema na thabiti ya
Mungu”.[284]
257. Njia mojawapo ya kuendeleza mahusiano na wapendwa wetu waliofariki ni kuwaombea.[285]
Biblia inatuambia kuwa “kuwaombea marehemu” ni “tendo la uchaji na utakatifu” (taz. 2Mak 12:44-
45). Sala yetu kwao “ina nguvu siyo tu ya kuwasaidia, lakini pia ya kuwafanya kuwa waombezi
wetu wa dhati.”[286] Kitabu cha Ufunuo kinatoa taswira ya mashahidi wakiwaombea wale
walionyimwa haki hapa duniani (taz. Ufu 6:9-11), wakishikamana na ulimwengu huu ulio safarini.
Baadhi ya watakatifu, kabla ya kufa, waliwafariji wapendwa wao kwa kuwaahidi kwamba
watakuwa karibu nao na kuwasaidia. Mtakatifu Teresa wa Lisieux alijisikia kuendelea kuwatendea
mema tokea mbinguni wapenzi wake.[287] Mtakatifu Dominiko alisema kwamba “atatusaidia zaidi

9.5 Page 85

▲back to top
85
baada ya kufa, [...] mwenye nguvu zaidi wa kupatia neema”.[288] Ni vifungo vya upendo,[289] kwa
sababu “umoja wa wale wanaosafiri duniani na wa ndugu waliolala katika amani ya Kristo
haukatiki hata kidogo, kinyume chake, […] huimarishwa kwa kubadilishana mema ya kiroho”.[290]
258. Tukikubali kifo, tunaweza kujiandaa nacho. Njia yenyewe ni kukua katika upendo kwa wale
wanaotembea pamoja nasi, mpaka siku ambapo “mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo,
wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena” (Ufu 21:4). Hivyo tutajiandaa pia kukutana tena na
wapendwa wetu waliotutangulia. Kama vile Yesu alivyomrudisha kwa mama yake mtoto wake
aliyekuwa amekufa (taz. Lk 7:15), vivyo hivyo atafanya na sisi. Tusipoteze nguvu kwa kuwaza
sana yaliyopita. Kadiri tunavyoishi vema katika dunia hii, ndivyo tutakavyofurahia pamoja na
wapendwa wetu huko mbinguni. Kadiri tunavyokua vema na kusonga mbele katika dunia hii,
ndivyo tutakavyokuwa na vitu vizuri vya kutolea katika karamu ya mbinguni.
SURA YA SABA
KUIMARISHA MALEZI KWA WATOTO
259. Wazazi wana wajibu mkubwa siku zote katika mafundisho ya kimaadili ya watoto, kwa wema
na ubaya. Kwa hiyo, kitu cha msingi ni kupokea wajibu huo usiokwepeka na kuutekeleza kwa
dhamira, furaha, akili na uzuri. Na kwa sababu jukumu hili la familia la kulea ni la muhimu hivi na
linaendelea kuwa na changamoto nyingi, ningependelea nitumie fursa hii ya pekee kulijadili hilo.
Watoto wako wapi?
260. Familia haiwezi kamwe kujinyima kuwa mahali pa msaada, usindikizaji na uongozi, hata
kama itapaswa daima kutumia ubunifu ili kutafuta njia mbadala na maarifa mapya. Inahitaji
kuandaa mwelekeo mzima wa maisha ya watoto wake. Na kwa malengo hayo haiwezi kukwepa
kujiuliza juu ya wale wanaowashughulikia katika michezo na maburudisho, wale wanaoingia katika
makazi yao kupitia luninga, wale wanaokabidhiwa majukumu ya kuwaongoza wakati wa
mapumziko yao. Ni wakati ule hasa tunaokuwa nao, tukiongea lugha rahisi na yenye mapendo juu
ya mambo muhimu, na pia nafasi nzuri tunayojitengea ili wapate kutumia vyema muda wao,
ndivyo vitakavyoruhusu kukwepa nafasi zinazowapotosha. Kuna umuhimu sikuzote wa kuwa
macho. Kuwaacha hakusaidii hata kidogo. Wazazi wanatakiwa kuelekeza na kuandaa watoto na
vijana ili waweze kujua namna ya kukabiliana na mazingira hatarishi, kama vile hatari za
kushambuliwa, kudhalilishwa kingono au kupatiwa madawa ya kulevya.
261. Hata hivyo ufuatiliaji uliokithiri si malezi, na haiwezekani kufuatilia na kuhakiki kila mazingira
ambayo mtoto anayapitia. Hapa ni msingi kuzingatia kuwa “muda unazidi nafasi”.[291] Hii
inamaanisha kuandaa mifumo endelevu ya malezi kuliko kuyadhibiti mazingira. Kama mzazi ni
mfuatiliaji aliyekithiri na anataka kujua kila sehemu alipo mtoto wake na anahakiki chochote kile
atakachokifanya, atatafuta tu namna ya kudhibiti mahali pake binafsi pa kuishi. Na kwa namna

9.6 Page 86

▲back to top
86
hiyo hatamfundisha, hatamwimarisha, na hatamwandaa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto.
Cha msingi ni kuzalisha katika maisha ya mtoto, kwa mapendo makuu, michakato ya kukomaza
uhuru wake, ya kumwandaa kijana akue kijumla, na kumjengea mazingira ya uwajibikaji katika kila
analolifanya. Kwa namna hiyo tu yule mtoto atajijengea ndani yake ile hali anayoihitaji kwa ajili ya
kujilinda na kuamua kwa akili na busara katika mazingira magumu. Kwa hiyo swali la msingi siyo
tu mahali alipo mtoto wako, au yuko na nani, ila amefikia wapi katika mpango mzima wa kimaisha,
wapi anakoelekeza mawazo yake, malengo yake na matazamio yake katika utaratibu mzima wa
maisha yake. Ndiyo sababu maswali ninayowauliza wazazi ni haya: “Tujaribu kujiuliza ‘ni wapi’
watoto wetu wanakoelekea katika safari yao ya maisha? Tunafahamu kweli moyo wao uko wapi?
Na zaidi sana: je, tunataka kujua kwelikweli?”[292]
262. Kama kukua ingekuwa tu ni suala la maumbile ambalo lipo tayari kwenye mfumo wa jene,
hatungekuwa na cha kufanya. Busara, maamuzi sahihi na dhamira safi havitegemei kuongezeka
kwa miaka, bali ni ule mlolongo mzima wa hatua za kujilea zinazokuja kuunda utu wa ndani, na,
hasa, kiini cha uhuru wake. Haikwepeki kwamba kila mtoto hutushangaza kwa mipango
inayotokana na uhuru huo, kwamba anavunja taratibu zetu, na hilo ni jambo jema litokee. Malezi
ni pamoja na juhudi ya kuchochea matumizi ya uhuru kwa kuwajibika, ambao katika njia panda
uweze kuongoza kufanya maamuzi kwa busara na akili. Ni kuandaa watu wanaoelewa bila
vipingamizi kwamba maisha yao e yale ya jumuiya yao yapo mikononi mwao na kwamba uhuru
huo ni zawadi kubwa sana.
Mafundisho ya kimaadili kwa watoto
263. Haka kama wazazi wana uhitaji mkubwa wa shule ili kuhakikisha mafundisho ya msingi kwa
watoto wao, hawawezi kamwe kuukabidhi wajibu wa malezi ya kimaadili. Kukua kimapendo na
kimaadili kwa mtu kunategemea mang’amuzi haya ya msingi: kuamini kuwa wazazi wako
wanaweza kuaminika. Hilo linajumlisha wajibu wa kimalezi: kwa mapendo na mifano imani
hujengeka katika watoto, na kuamshwa ndani yao heshima yenye mapendo. Mtoto anapohisi
kutopendeka na wazazi wake kwa sababu ya mapungufu yake, au haonji kama wao kiukweli
wanahangaika juu yake, jambo hilo litamjengea madonda makubwa ndani yake yanayosababisha
magumu mengi katika makuzi yake. Kutokuwepo huko, kutelekezwa kimapendo, kunasababisha
machungu ya ndani makali zaidi kuliko karipio linalotolewa mbele ya tendo baya.
264. Wajibu wa wazazi unahusisha kuelimisha moyo, kusitawisha mazoea mazuri na desturi
njema ya kupenda kutenda mema. Hii inamaanisha kuonyesha kama za kutamaniwa desturi za
kujifunza na mielekeo ya kukomazwa. Lakini hayo daima ni mchakato unaoanza kwenye
mapungufu kuelekea kwenye ukamilifu. Hamu ya kulandana na jamii au mazoea ya kujinyima
ridhaa ya papo hapo, kwa lengo la kuheshimu taratibu zilizopo na kujihakikishia maisha mema ya
pamoja, hii ni dalili tosha kuwa ndani yake kuna thamani kianzio inayoandaa mazingira kwa ajili ya
kukua kuelekea tunu kubwa zaidi. Malezi ya kimaadili inabidi siku zote yatimilike na njia hai na
majadiliano ya kimalezi yanayohusisha hisia na lugha zilizo maalumu kwa watoto. Zaidi ya hayo,

9.7 Page 87

▲back to top
87
malezi hayo ni lazima yafanyike kwa mtindo wa dhamiri, kiasi cha kumfanya mtoto aweze kufikia
kutambua mwenyewe umuhimu wa maisha yanayoongozwa na maadili, kanuni misingi na sheria,
badala ya kumlazimisha azishike kama ukweli usiopingika.
265. Ili kutenda vema haitoshi “kuhukumu inavyotakiwa” au kuelewa wazi nini cha kufanya,
ingawa hayo ni utangulizi muhimu. Mara nyingi mienendo yetu ya maisha haiendani na mawazo
yetu, hata yakiwa thabiti kabisa. Hata kama dhamiri inatuongoza katika kufanya maamuzi ya
kimaadili, mara nyingine kinachochukua uzito zaidi ni vitu vingine tu vinavyotuvutia, ikiwa tutakuwa
hatujajijenga kuwa wema tuliouelewa kwa akili zetu lazima uote mizizi ndani yetu kama mwelekeo
wa hisia zetu, kama uzoefu wa kutamani utamu wa wema kuliko vivutio vingine na unaotufanya
tuhisi kwamba yale tuliyoyaona kama wema ni wema hata “kwa ajili yetu” hapahapa na sasa hivi.
Malezi mazuri ya kimaadili yanamwonyesha mtu jinsi ilivyo vyema kwake pia kutenda mema. Mara
nyingi siku hizi haisaidii kuagiza kitu kinachodai juhudi na sadaka, bila kuonyesha kwa uwazi
wema ambao ungeweza kupatikana kwa kutenda vile.
266. Ni muhimu kukomaa katika mazoea mazuri. Hata desturi za kurithi toka utotoni zina malengo
mazuri, kwani zinaruhusu maadili mazuri waliyojifunza yatafsiriwe katika matendo ya nje yaliyo
sahihi na thabiti. Mmoja anaweza kuwa mchangamfu na mwenye mwelekeo wa urahisi kwa
wengine, ila kama kwa muda mrefu hajajizoesha kupitia mafundisho ya wakubwa kusema,
“tafadhali”, “samahani”, “asante”, tabia yake njema ya ndani haiwezi kutafsiriwa vyema na
kuonekana. Kukomaza maamuzi na kurudia baadhi ya matendo kunatengeneza maisha ya
kimaadili, na bila marudio ya dhati, huru na yanayokubalika ya baadhi ya matendo mema
haiwezekani kutimiza malezi ya tabia njema kama hiyo. Shauku, au mvuto tunaosikia kwa tunu
fulani ya kimaadili, haviwezi kuwa fadhila bila ya kuwepo matendo hayo yanayosukumwa na
uthabiti.
267. Uhuru ni kitu cha thamani kubwa sana, ila tunaweza kuupoteza. Malezi ya kimaadili ni
kupalilia uhuru kupitia mapendekezo, maelezo, utendaji, vichocheo, zawadi, mifano, ishara,
alama, tafakari, maonyo, marudio ya mitindo ya kuishi na majadiliano yanayowasaidia watu
kuziendeleza zile kanunimsingi imara za ndani zinazoweza kusukuma ili wema utendeke kwa hiari
kabisa. Fadhila ni dhamiri fulani iliyogeuka kuwa sababu ya ndani na thabiti ya kutenda. Kwa hiyo,
maisha yenye fadhila yanajenga uhuru, yanauimarisha na kuulea, yakikwepa kumfanya mtu awe
mtumwa wa mielekeo iliyolazimishwa mbali na utu wake na yenye kuchukia kuishi kijamii.
Kiuhalisia hadhi yenyewe ya binadamu inamtaka kila mtu “atende kadiri ya chaguo lake kwa kujua
na kwa uhuru; yaani awe amesukumwa na kuhimizwa kutoka ndani”.[293]
Umuhimu wa adhabu kama kichocheo
268. Vivyo hivyo, ni lazima kuwahimiza watoto na vijana ili watambue kuwa matendo mabaya
yana madhara yake. Inafaa kuamsha ile ari ya kujiweka mahali pa mwingine na kujutia kwa ajili ya
uchungu tuliomsababishia kwa kumtendea mabaya. Adhabu nyingine - kwa ajili ya matendo ya

9.8 Page 88

▲back to top
88
ukatili dhidi ya jamii - zinaweza kusaidia ili kufikia malengo hayo. Ni muhimu kumwongoza mtoto
kwa msimamo ajifunze kuomba msamaha na kulipia fidia ya madhara aliyosababisha kwa
wengine. Pale ambapo utaratibu wa malezi unaonyesha matunda hasa katika kukua kwa uhuru
binafsi, mtoto mwenyewe ataanza kutambua kwa shukrani kwamba ilikuwa ni vizuri kwake kukua
katika familia na kuvumilia magumu aliyolazimishwa kuyatekeleza wakati wa malezi yake.
269. Kuonya ni kichocheo endapo papo hapo tunathamini na kufahamu juhudi za mtoto na
endapo yeye anagundua kwamba wazazi wake wanadumu kuwa na tumaini kwake kwa uvumilivu.
Mtoto anayeonywa kwa mapendo anajisikia kuthaminiwa, anajitambua kuwa wa maana, anahisi
kuwa wazazi wake wanatambua pia vipaji vyake. Hali hii haiwataki wazazi wasiwe na kosa, ila
kwamba watambue kwa unyenyekevu mapungufu yao na waonyeshe juhudi zao katika kuwa
wazazi wema. Ila ushuhuda ambao watoto wanahitaji kuona kutoka kwa wazazi wao ni kwamba
wasiongozwe na hasira. Mtoto anayetenda tendo ovu, anatakiwa kurekebishwa, ila kamwe kama
adui au kama mmoja wa kumtupia hasira binafsi. Zaidi ya hayo, mtu mzima anapaswa kutambua
kuwa baadhi ya matendo mabaya yanaendana na udhaifu na mapungufu ya umri wa utoto. Kwa
sababu hiyo tabia ya kutoa adhabu za mara kwa mara inaharibu, wala haisaidii kuelewa tofauti ya
uzito iliyopo katika matendo mbalimbali, nayo inaweza kusababisha kukata tamaa na uchungu:
’’Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu” (Efe 6:4; taz. Kol 3:21).
270. Kitu cha muhimu ni kwamba kanuni za nidhamu zisigeuzwe kukatisha matamanio, ila ziwe
kama kichocheo cha kwenda daima mbele zaidi. Ni namna gani tuunganishe kanuni za nidhamu
na mhemuko wa ndani? Kwa namna gani kuweza kuifanya sheria iwe ni kizingiti cha kujenga njia
ambayo mtoto anatakiwa kupitia na siyo ukuta wa kumpoteza au sehemu ya malezi
yanayomdhoofisha? Inafaa kutafuta uwiano kati ya mipaka hiyo miwili inayoharibu: Kwa upande
mmoja ni kule kudhani kwamba lazima kumtengenezea kijana ulimwengu unaoendana na
matamanio yake, mtoto anayekua akidhani kuwa yeye ndiye mwenye haki tu, wala si wajibu. Au
pia kumlea kijana aishi bila kutambua hadhi yake, upekee wake na haki zake, anayeteswa na
wajibu na anayetakiwa tu kutimiza matakwa ya wengine.
Kukubali hali halisi kwa uvumilivu
271. Malezi ya kimaadili ni pamoja na kuagiza kwa mtoto au kijana mambo yale tu ambayo kwake
siyo sadaka isiyowezekana, na kudai tu kiwango kile cha juhudi kisichomletea chuki au kufanya
matendo ya kulazimishwa tu. Njia ya kawaida ni kumshauri hatua ndogondogo ambazo
zinaeleweka, zinakubalika na kuthaminika, na zinazomsababishia sadaka inayowezekana. Tofauti
na hapo, kutaka zaidi ni kutopata kitu. Huyo mtu pale atakapoweza kujikomboa na mwenye
mamlaka, pengine ataacha kutenda vizuri.
272. Malezi ya kimaadili mara nyingine yanasababisha dharau inayotokana na mazoea ya
kutelekezwa, kukata tamaa, ufinyu wa upendo, au picha mbaya ya wazazi. Kuelekeza kwenye
tunu za kimaadili picha za ovyo za baba na mama, au mapungufu ya wakubwa. Ni kwa sababu

9.9 Page 89

▲back to top
89
hiyo lazima kusaidia vijana wanaokua kuweka kimatendo ulinganifu huu: tunu za kimaadili
zinatimilizwa hasa na baadhi ya watu maarufu, lakini pia zaweza kutekelezwa kwa namna zisizo
kamili na katika kiwango tofauti. Pia, kwa kuwa upinzani wa vijana unatokana na uzoefu mbaya,
inafaa kuwasaidia watembee katika njia ya uponyaji wa huo ulimwengu wa ndani uliojeruhiwa,
kusudi waweze kufikia hatua ya kuelewa na kupatana na watu na jamii.
273. Tunapofundisha juu ya maadili, ni vyema kuanza taratibu, na kuendelea kwa namna tofauti
kadiri ya umri na uwezo halisi walizo nazo watu, bila kulazimisha kutumia njia ngumu na
zisizobadilika. Michango mizuri ya saikolojia na ya sayansi ya ufundishaji inaonyesha kuwa
inatakiwa kwenda kwa hatua katika kuyafikia mabadiliko ya kitabia, lakini pia kuwa uhuru unahitaji
kuongozwa na kuchochewa, kwa sababu ukiachwa tu hivyo hauwezi kukomaa. Uhuru kamili, halisi
una mipaka yake na masharti yake. Uhuru si uwezo tu wa kuchagua lililo jema bila kubughudhiwa.
Si rahisi daima kutofautishwa kati ya tendo la “makusudi” na tendo “huru”. Mtu anaweza kutamani
kitu kibaya kwa makusudi yake yote, lakini kwa sababu ya tamaa isiyotawalika au malezi mabaya.
Katika mazingira hayo, anafanya maamuzi kwa makusudi yake kabisa, kwa sababu hayapingani
na mapenzi yake, lakini si huru, kwa sababu kwake inaonekana kuwa ni kama vile haiwezekani
kutochagua uovu. Nacho ndicho kinachotokea kwa walevi wa madawa ya kulevya. Anapoitamani
anafanya hivyo kwa nguvu zake zote, lakini analazimishwa hivi kwa sababu wakati huo hawezi
kuchukua maamuzi mengine. Hivyo maamuzi yake ni ya makusudi, lakini si huru. Haina maana
’kuacha mtu achague kwa uhuru’, kwa sababu kiuhalisia hawezi kuchagua, na kumwacha penye
madawa ya kulevya hakufanyi kingine zaidi ya kumwongezea utegemezi. Huyo anahitaji msaada
wa wengine na malezi endelevu.
Maisha ya familia kama mazingira ya malezi
274. Familia ni shule ya kwanza ya maadili ya kibinadamu, ndiko huko tunakojifunza matumizi
mazuri ya uhuru. Kuna mielekeo iliyokomaa katika utoto ambayo inasharabu maisha ya ndani ya
mtu na inabaki kwa maisha yake yote kama mvuto mwema kwa ajili ya tunu fulani, au kama
katazo la dhati la vitendo fulani vya kitabia. Watu wengi wanatenda kwa maisha yao yote kwa
mtindo fulani kwa sababu wanadhani kuwa ni sahihi kutenda vile kwani ndiyo walivyojifunza tangu
utoto wao, kama kwa osmosi: “Mimi nimefundishwa hivi”; “hivi ndivyo nilivyorithi”. Katika mazingira
ya familia mtu anaweza kujifunza namna ya kudadisi aina za taarifa za vyombo vya habari. Hata
kama, mara nyingi vyombo vya mawasiliano kama televisheni au aina fulani za matangazo
yanawaharibu na kupunguza nguvu za tunu za kimaadili zinazopatikana katika familia zenyewe.
275. Katika zama zetu hizi, ambapo tunatawaliwa na mfadhaiko na taharuki ya kiteknologia,
wajibu muhimu sana wa familia ni kufundisha umuhimu wa subira. Hii haimaanishi kuwazuia
vijana wasicheze na vifaa vya kielektroniki, bali kutafuta namna ya kuwajengea uwezo wa
kutofautisha mantiki tofauti na kutotumia huo mwendo kasi wa kidijitali katika kila sehemu za
maisha. Kusubiri si kukataza kuwa na tamaa, ila kuahirisha tu utimilizaji wake. Pale ambapo
watoto na vijana hawafundishwi kupokea kwamba vitu vingine lazima visubiri kwanza, wanakuwa

9.10 Page 90

▲back to top
90
na kiburi, wakilazimisha kila kitu kiweze kutekeleza matakwa binafsi ya sasa na hivyo wanakua
katika upotofu wa “kutaka kila kitu haraka haraka”. Huo ni udanganyifu mkubwa usiosababisha
uhuru, bali unautilia uhuru sumu. Isipokuwa, pale unapoelimishwa kuahirisha vitu vingine na
kusubiri muda muafaka, unajifunza maana halisi ya kujitawala, kuwa huru katika mihemko yako.
Na ndiyo pale ambapo mtoto anang’amua kwamba ana uwezo wa kuwajibika juu yake
mwenyewe, anazidi kujithamini. Na wakati huohuo, hii inamfundisha namna ya kuheshimu uhuru
wa wengine. Kwa vyovyote vile hii haimaanishi kuwataka watoto watende kama watu wazima,
lakini pia haitakiwi kudharau uwezo wao wa kuzidi kukomaza uhuru wenye kuwajibika. Katika
familia yenye malezi bora, ukufunzi huo unafanyika kwa kawaida kwa njia ya madai ya maisha ya
pamoja.
276. Familia ndiyo mazingira ya msingi ya kuishi kijamii, kwa sababu ndiyo mahali pa kwanza
kabisa ambapo mtu anajifunza namna na kukaa na wengine, namna ya kuwasikiliza,
kushirikishana, kuvumiliana, kuheshimiana, kusaidiana na kuishi pamoja. Kazi ya malezi ni
kufundisha kuhisi ulimwengu na jamii kama “mazingira ya kifamilia”, ni kuelimisha namna ya kujua
“kuishi”, nje ya mipaka ya nyumba yako. Katika muktadha wa familia tunafundishwa kutambua
tena umuhimu wa ujirani mwema, wa kuhudumiana, na wa kusalimiana. Na ndipo hapo ambapo
kwa mara ya kwanza ubinafsi unaoua unapopigwa vita, tupate kutambua kuwa tunaishi na
wengine, pamoja nao, hao ambao wanauhitaji usikivu wetu, ukarimu wetu na mapendo yetu.
Hakuna mahusiano ya kijamii bila sehemu hii ya maisha ya kila siku, ndogo ya kuonekana
isipokuwa kama kwa darubini tu: kukaa pamoja katika ujirani, kukutana katika nafasi mbalimbali za
kila siku, kujishughulisha katika yale yanayohusu wote, kusaidiana katika shida ndogondogo za
kila siku. Familia lazima ibuni kila siku njia mpya za kuendeleza kutambuana.
277. Katika mazingira na nyumbani mtu anaweza kujipanga na kubadili hata mazoea yake ya ulaji
ili kuacha nafasi kwa ajili ya jumuiya: Familia ndiyo mhusika mkuu wa ikolojia sahihi, kwa sababu
ndiyo mhusika wa kwanza katika jamii, ambayo ndani yake ina misingi miwili ya ustaarabu wa
binadamu duniani: msingi wa muungano na msingi wa uzaaji”.[294] Vivyo hivyo, wakati mgumu
wa maisha ya familia unaweza kuwa muda mzuri wa kujifunzia. Hicho ndicho kinachotokea, kwa
mfano, pale yanapoingia magonjwa, kwa sababu “mbele ya ugonjwa, hata ndani ya familia ndipo
yanapozaliwa matatizo, yanayoendana na udhaifu wa kibinadamu. Lakini, kwa kawaida, wakati wa
ugonjwa ndio wakati wa kuimarisha mahusiano ya kifamilia.. [...] Malezi yasiyojali sana mazingira
ya ugonjwa, yanaukandamiza moyo. Na yanawafanya vijana wawe kama wenye “ganzi” mbele ya
mahangaiko ya wengine, wasioweza kukabiliana na mateso na wasioweza kuishi hali yetu
pungufu ya kibinadamu.”[295]
278. Mkutano wa kimalezi kati ya wazazi na watoto wao unaweza kurahisishwa au kuharibiwa na
teknologia za mawasiliano na burudisho, ambazo kila siku zinakuwa tata zaidi. Pale ambapo
zitatumika vizuri zinaweza kusaidia kuwakutanisha wanafamilia hata kama wapo mbali.
Mawasiliano yanaweza kuwa ya mara kwa mara na kusaidia kutatua shida.[296] Lakini, lazima
tukubaliane kwamba umuhimu wa mawasiliano ya ana kwa ana na ya kina unabaki kuwa ya

10 Pages 91-100

▲back to top

10.1 Page 91

▲back to top
91
msingi, wala hayana mbadala, kwa vile inavyohitajika na hamu ya kuwa karibu, au walau, ya
kusikia sauti ya mwingine. Tunafahamu kuwa mara nyingine vyombo hivyo vya mawasiliano
vinawatenga badala ya kuwaweka pamoja ndugu, kama wakati wa chakula kila mmoja akijali simu
yake, au pale ambapo mmoja wa wanandoa analala akimngojea mwingine, anayeshinda muda
mwingi akitumia chombo cha kielektroniki. Katika familia, jambo hilo pia lazima liwe sababu ya
mazungumzano na makubaliano, yanayowezesha kuweka kipaumbele katika kukutana kwa
wanafamilia, bila kutia vizuizi visivyo na tija. Kwa vyovyote, tunapaswa tusisahau hatari za mitindo
mipya ya mawasiliano kwa watoto na vijana, ambao mara nyingine wanakuwa watepetevu,
wakijitenga na ulimwengu halisi. Hali hii ya “tawahudi (autism, yaani ugonjwa wa kujitenga) ya
kiteknolojia” inawaweka kwenye hatari ya kurubuniwa na wale wanaojaribu kupenya hisia za
mioyo yao kwa maslahi ya ubinafsi wao.
279. Wala si vizuri kwamba wazazi wanakuwa kama miungu kwa watoto wao, ambao wangeweza
kuwa na imani na wao tu peke yao, kwani kwa kufanya hivyo wangezuia ule mchakato unaofaa
wa kuzoea maisha ya kijamii na wa kukomaa katika mapendo. Ili kufanikisha kurefusha matumizi
sahihi ya hali ya ubaba na umama kwa ajili ya hali halisi iliyo mpana zaidi, “jumuiya za kikristo
zinaitwa kusaidia katika utume wa kimalezi wa familia”[297], hasa kwa kupitia katekesi za
kuingizwa [katika Ukristo]. Ili kurahisisha malezi sahihi lazima “kuimarisha mapatano kati ya familia
na jumuiya ya kikristo.”[298] Sinodi imeweka wazi umuhimu wa shule za kikatoliki, ambazo
“zinatekeleza dhima muhimu sana ya kuwasaidia wazazi katika wajibu wao wa kulea watoto. [...]
Shule za kikatoliki zinapaswa kutiwa moyo katika utume wao wa kuwasaidia wanafunzi ili wakue
kama watu wazima waliokomaa na wanaoweza kuuona ulimwengu kwa mtazamo wa mapendo ya
Yesu na kuelewa kuwa maisha ni wito wa kumtumikia Mungu.”[299] Katika maana hiyo, “lazima
kusisitiza kwa wazi juu ya uhuru wa Kanisa wa kufundisha imani yake na haki ya ukinzani wa
dhamiri kwa upande wa walezi.”[300]
Hitaji la elimu ya jinsia
280. Mtaguso mkuu wa pili wa Vatikano ulidokeza kwamba watoto na vijana, “kadiri wanavyokua,
lazima wapewe kwa busara elimu ya jinsia iliyo na tunu nzuri” kwa “kuthaminiwa sawasawa
maendeleo katika saikolojia, pedagojia na ufundishaji”.[301] Inabidi tujiulize kama taasisi zetu za
malezi zimeshaipokea changamoto hii. Ni vigumu kufikiri juu elimu ya jinsia katika zama ambapo
wengi wanapunguza uzito wa suala la ujinsia na kudhoofisha umuhimu wake. Tungeweza kuiweka
elimu hii katika mtaala tu wa malezi ya mapendo, ya kujitoa kila mmoja kwa mwenzake. Ni katika
hali hiyo kwamba muktadha wa ujinsia hauwezi kuwa na muonekano huu dhaifu, ila muonekano
wa mwanga. Ashiki ya kijinsia inaweza kupaliliwa katika utaratibu wa kujitambua na kukua katika
kujitawala, na hivyo kusaidia katika kuelekeza kwenye furaha ya kweli na kukutana katika
mapendo.
281. Elimu ya jinsia inatoa taarifa, bila kusahau kuwa watoto na vijana hawajafikia ule ukomavu
kamili. Taarifa lazima ifike katika wakati muafaka kwa namna inayoendana na hatua yao ya

10.2 Page 92

▲back to top
92
makuzi. Haisaidii kuwamezesha vijana na watoto taarifa hizo bila kuwapa mantiki au udadisi kwa
taarifa wanazozipokea, mbele ya picha za ponografia bila udhibiti, na msongamano wa taarifa za
vishawishi vinavyohaiharibu ujinsia. Vijana wawezeshwe kutambua kuwa wanarushiwa mno
taarifa ambazo haziwalei wala kuwaelekeza kwenye mema yao na ukomavu. Inatakiwa
kuwasaidia wajitambue na watafute mafundisho mazuri, na wakati huohuo wachukue hatua stahiki
dhidi ya yale yote yanayouharibu uwezo wao wa kupenda. Vilevile, inabidi tukubali kuwa “hitaji la
kuwa na lugha mpya na yenye kuwafaa zaidi linajitokeza kwanza wakati wa kuwaingiza watoto na
vijana kwenye mada ya ujinsia”.[302]
282. Elimu ya jinsia inayoheshimu soni sahihi ina thamani kubwa sana, hata kama siku hizi
wengine wanadhani ni suala la kizamani. Ni ngome ya asili ya mtu inayomlinda katika utu wa
ndani na kumwepusha asigeuke kuwa kitu cha kushikwa tu. Bila soni, tungepunguza thamani ya
upendo na ujinsia hadi kujifanya kama kupagawa na mapepo yanayotuvamia katika sehemu zetu
za siri, na ugonjwa sugu unaouharibu uwezo wetu wa kupenda kweli, na katika aina mbalimbali za
ubakaji zinazotupelekea kuwa kama si watu na kuwaumiza wengine.
283. Mara nyingi elimu ya jinsia inaelekezwa tu juu ya namna ya “kujikinga”, kwa kutafuta “ngono
salama”. Lugha hizi tata hazifundishi msimamo mwema juu ya lengo la asili la ujinsia, ambalo ni
kuzaa, kana kwamba mtoto atakayepatikana anatazamwa kama adui ambaye mtu anatakiwa
kujikinga naye. Na hivyo tunaendekeza ukatili wa ubinafsi badala ya ukaribu. Ni kukosa uwajibikaji
kila mafundisho yanayowalenga vijana kucheza na miili yao na hisia zao, kana kwamba
wangekuwa watu wakomavu, waadilifu, wenye kuweza kushika tayari masharti na malengo halisi
ya ndoa. Ndivyo wanavyoshawishiwa kwa furaha kumtumia mtu mwingine kama kitu cha
mang’amuzi yao ili kuridhisha upungufu na udhaifu wao. Kinyume chake, ni muhimu sana
kuwafundisha njia sahihi kuhusu sura halisi na pana za upendo, namna ya kuhudumiana,
kuhurumiana kwa kuheshimiana, na ya kuwasiliana juu ya mambo yenye maana. Kwani, hayo
yote yatamwandaa kijana katika kujitoa kikamilifu sadaka kwa upendo utakaojionyesha, baada ya
kuweka ahadi hadharani, katika kupeana sadaka ya miili yao. Muungano wa kijinsia katika ndoa
utaonekana wazi kuwa alama ya ahadi na wajibu kamili, ambayo imetajirishwa na safari nzima ya
mwanzo.
284. Haitakiwi kuwadanganya vijana kwa kuwapelekea kuchanganya hatua: kuvutiwa
“kunatengeneza, wakati huo, udanganyifu juu ya muungano, hata hivyo bila mapendo ‘muungano’
huo utawafanya hao wawili wabaki wageni na kuwatenga kama mwanzo.”[303] Lugha ya mwili
inahitaji uvumilivu wa msingi utakaoruhusu kutafsiri na kufundisha matamanio ya binafsi kwa ajili
ya kujitoa kweli. Unapodhani kujitoa kila kitu kimwili mara moja, ni rahisi kutojitoa hata kidogo
kama sadaka. Kitu kimoja ni kutambua udhaifu wa kiumri na mchanganyiko wake, kitu kingine ni
kuhimiza vijana waendelee katika kutokomaa kwa namna zao za kupenda. Lakini ni nani
anayeyazungumzia hayo leo hii? Ni nani anayewathamini kweli vijana? Ni nani anayewasaidia
vijana katika kujiandaa vizuri kupenda kweli na kwa kujisadaka? Inachukuliwa kirahisi mno elimu
ya jinsia.

10.3 Page 93

▲back to top
93
285. Elimu ya jinsia inatakiwa kuhusisha heshima e staha ya utofauti, inayomwonyesha kila
mmoja uwezekano wa kujikwamua katika mapungufu yako na kujifungua katika kumpokea
mwingine. Zaidi ya magumu yale ambayo kila mmoja anaweza kuyaishi, inatakiwa kusaidia
kuutambua mwili wako vile ulivyoumbwa, kwa sababu “mantiki ya kutaka kutawala mwili wako
unaweza kugeuka mara nyingine kuwa mantiki ya kutaka kutawala viumbe vyote pia [...]. Pia
kuuthamini mwili wako katika hali yake ya kike au kiume ni muhimu ili kuweza kujitambua
mwenyewe katika kukutana na mwingine ambaye ni tofauti nawe. Kwa mtindo huo itawezekana
kupokea kwa furaha sadaka maalumu ya mwingine, kazi ya Mungu muumbaji, na kujitajirisha kila
mmoja kwa mwingine.”[304] Katika kuondokana na hofu ya utofauti tu, ndipo itakapowezekana
kujikomboa katika kubaki kwenye umimi na kujipendelea wewe mwenyewe. Elimu ya jinsia lazima
isaidie katika kujipokea katika mwili wako, ili mtu asidhani “kufuta utofauti wa kijinsia kwa sababu
hawezi kabisa kukabiliana nao.”[305]
286. Na haiwezekani kutotambua kuwa katika kujitengenezea mtindo wako wa maisha, wa kike au
wa kiume, haziingii tu sababu za kibayolojia au kijenetiki, bali hata uwingi wa masuala
yahusianayo na hulka, historia ya kifamilia, utamaduni, mang’amuzi ya maisha, malezi na elimu,
ushawishi wa marafiki, wanafamilia au watu unaowajali, au hata mazingira halisi mengine
yanayotaka juhudi fulani ili kupatana nayo. Ni kweli kwamba hatuwezi kugawanya kile
kinachomhusu mwanamme na mwanamke na kazi ya Mungu, ambayo ipo kabla ya maamuzi na
mang’amuzi yetu na ambamo mna uhalisia wa kibayolojia ambao hatuwezi kuukataa. Hata hivyo
ni kweli pia kwamba vilivyo vya mwanamume au vya mwanamke si hali ambayo imeganda. Kwa
hiyo inawezekana, kwa mfano, kwamba mtindo wa kuwa mwanamume wa mume mtu unaweza
kujitengeneza ili endana na hali za kikazi ya mke wake. Kujishughulisha katika kazi za nyumbani
au katika fani fulani za kuwalea watoto hakumfanyi mwanamume kuwa si mwanamume, au
kumfanya ajisikie kama ameshindwa, amejidhalilisha au amejiaibisha. Inatakiwa kuwasaidia
watoto wawapokee wazazi wao katika mabadilishano haya mema kama jambo la kawaida, na
kwamba hayapunguzi heshima ya baba wa familia. Ugumu wa kubadilika unaleta hali unaosisitiza
mno hali ya kiume au ya kike, wala haisaidii watoto na vijana kutambua uzuri wa kupokezana
katika matendo ya kawaida ya hali halisi ya ndoa. Ugumu huo, kwa upande mwingine, unazuia
ukomavu wa vipaji vya kila mmoja, mpaka kumdhania kuwa huyu ni mwanamume nusu yule
anayejishughulisha na sanaa au ngoma na kwamba si mwanamke halisi yule anayeshika nafasi
za uongozi. Mtazamo huu, tumshukuru Mungu, umebadilika, ila katika baadhi ya mazingira dhana
hizi zisizofaa zinaendelea kudumishwa na hivyo kuathiri haki ya uhuru na kufifisha ukomavu wa
tabia thabiti ya watoto na wa vipaji vyao.
Kurithisha imani
287. Malezi ya watoto yanapaswa kuwa pamoja na mwendo wa kuirithisha imani, ambao
unafanywa kuwa mgumu na changamoto za maisha ya sasa, kama vile ratiba za kazi,
mchangamano wa ulimwengu wa leo, ambamo wengi wanajaribu kuishi wakikimbizana.[306] Hata
hivyo, familia lazima iendelee kuwa mahali pa kufunzia namna ya kupokea sababu na uzuri wa

10.4 Page 94

▲back to top
94
imani, kusali na kuhudumia jirani. Hilo linaanza kwa Ubatizo, ambamo, kama anavyosema
Mtakatifu Agustino, akina mama wanaowachukua watoto wao “wanashiriki katika uzazi
mtakatifu.”[307] Hapo ndipo inapoanza safari ya kukua kwa yale maisha mapya. Imani ni kipaji
cha Mungu, tunachopewa kwa sakramenti ya Ubatizo, wala si matokeo ya kazi za binadamu,
lakini wazazi ni vyombo ambavyo Mungu anavitumia kwa ajili ya kuikomaza na kuisitawisha. Kwa
hiyo “ni vizuri sana pale akina mama wanapowafundisha watoto wadogo kumbusu Yesu na Bikira
Maria kwa mbali. Ni upendo mkubwa namna gani katika kitendo kama hicho! Wakati huo moyo wa
watoto unabadilika na kuwa hazina ya sala.”[308] Kurithisha imani kunawataka wazazi waishi
kweli maisha ya kumwamini Mungu, kumtafuta na kumhitaji, kwa sababu kwa mtindo huo ndivyo
“kizazi kwa kizazi kitakavyoyasifu matendo yako, kitayatangaza matendo yako makuu” (Zab
145:4), na “baba atakavyowajulisha watoto kweli yako” (Isa 38:19). Hilo linatudai kumwomba
Mungu afanye kazi ndani ya mioyo, pale ambapo hatuwezi kwa nguvu zetu. Chembe ya haradali,
hata kama ni ndogo hukua na kuwa mmea mkubwa (taz. Mt 13:31-32), na hivi ndivyo
tunavyofahamu kutokuwiana kati ya tendo na matokeo yake. Ndiyo maana tunafahamu kuwa sisi
siyo wamiliki wa zawadi ya Mungu ila ni mawakili wenye uangalifu. Hata hivyo juhudi zetu za
kiuvumbuzi ni sehemu ya mchango wetu unaotuwezesha kushiriki katika kazi ya Mungu. Kwa
hiyo, “inabidi kuwathamini wazazi, akina mama kwa akina baba, kama waalimu wa kwanza wa
katekesi [...]. Ni msaada mkubwa sana katekesi ya kifamilia, kama njia salama ya kuandaa wazazi
vijana na kuwafanya wajitambue juu ya wajibu wao kama wainjilishaji wa familia zao.”[309]
288. Mafundisho ya imani yana tabia ya kuendana na kila mtoto, kwa sababu nyenzo zilizotumika
hapo zamani, au miiko, mara nyingine hazifanyi kazi. Watoto wanahitaji alama, ishara na hadithi.
Vijana wanaokua ni kawaida kuingia katika msukosuko na watu wenye madaraka na pia sheria,
kwa hiyo ina faida zaidi kuchochea mang’amuzi yao wenyewe ya imani na kuwapa ushuhuda
unaong’aa utakaopokelewa nao kutokana na uzuri wake wenyewe. Wazazi wanaotaka
kuwasindikiza watoto wao katika imani wa makini katika mabadiliko yao, kwa sababu wanafahamu
wazi kwamba maisha ya kiroho hayalazimishwi bali yanalelewa kwa uhuru kamili. Ni muhimu sana
kwa watoto kuona kwa mifano hai kwamba kwa wazazi wao kusali ni jambo la msingi kabisa. Kwa
sababu hiyo, wakati wa sala katika familia na vitendo vya ibada za watu vinaweza kuwa na nguvu
zaidi katika uinjilishaji kuliko katekesi zote na semina mbalimbali. Ninapenda kupongeza kwa
namna ya pekee akina mama wote wale wanaosali kwa moyo mkuu, kama alivyofanya Mtakatifu
Monika, kwa ajili ya watoto wao ambao wamejitenga na Kristo.
289. Kazi ya kurithisha imani kwa watoto, katika maana ya kurahisisha vitendo vyake na makuzi
yake, inaifanya familia kuwa mwinjilishaji, na kwamba – bila kujilazimisha – ianze kuitangaza kwa
wale wote wanaoikaribia, hata nje ya mazingira ya familia yenyewe. Watoto wanaokua katika
familia za kimisionari wanakuja kuwa wamisionari, kama wazazi wakiweza kuishi kazi hiyo kwa
namna ambayo hata wengine wanawaona karibu nao na marafiki zao, na hivyo watoto nao
wanakua katika msimamo huo wa kimahusiano na ulimwengu, bila kuacha imani yao e
mang’amuzi yao. Tukumbuke kuwa Yesu mwenyewe alikula na kunywa pamoja na wenye dhambi
(taz. Mk 2:16; Mt 11:19), aliweza kuzungumza na mwanamke msamaria (taz. Yn 4:7-26), na

10.5 Page 95

▲back to top
95
kumpokea Nikodemu usiku (taz. Yn 3:1-21), aliruhusu kupakwa mafuta na mwanamke mzinzi (taz.
Lk 7:36-50), na hakukwepa kuwashika wenye ugonjwa (taz. Mk 1:40-45; 7:33). Hivyo ndivyo
walivyofanya mitume wake, ambao hawakuwa watu waliowadharau wengine, waliojitenga kama
vikundi vya wateule, mbali na maisha ya jamii. Wakati wenye mamlaka walikuwa wakiwatesa, wao
walikuwa wakikubalika na watu wote (taz. Mdo 2:47; 4:21.33; 5:13).
290. “Familia inakuwa ni mlengwa mkuu wa kazi ya kichungaji kwa kupitia utangazaji wa Injili na
urithi wa aina mbalimbali za ushuhuda: mshikamano na maskini, uwazi katika kupokea watu wa
aina mbalimbali, hifadhi ya huluka, mshikamano wa hali na mali na familia nyingine hasa zile
zenye matatizo mengi zaidi, juhudi katika kusitawisha manufaa ya wote pia kwa njia ya
kurekebisha mifumo ya kijamii isiyo haki, kuanzia katika mazingira familia inamoishi, kwa kutenda
matendo ya huruma ya kimwili na ya kiroho”.[310] Hilo linapasika kulichukua katika muktadha wa
ile imani yenye thamani zaidi kwa wakristo: yaani upendo wa Mungu Baba unaotutegemeza ka
kukomaza, ulioonekana katika sadaka kamili ya Yesu, aliye hai kati yetu, anayetuwezesha
kupambana katika umoja na dhoruba zote na hatua zote za maisha. Hata ndani kabisa ya kila
familia inabidi usikike mwangwi wa kerigma, katika kila mazingira yanayofaa na yasiyofaa, ipate
kutumulikia njia. Wote tungetakiwa tuweze kusema, kutokana na maisha tunayoishi ndani ya
familia: “Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini” (1Yoh 4:16).
Kutokana na mazoea haya tu, uchungaji wa familia utaweza kufanikisha kwamba familia ziwe
Kanisa la nyumbani na, wakati huohuo, chachu ya uinjilishaji katika jamii.
SURA YA NANE
KUSINDIKIZA, KUPAMBANUA NA KUTEGEMEZA UDHAIFU
291. Mababa wa Sinodi walisema kwamba, ingawa Kanisa linahesabu kuwa kila tendo la
kukivunja kifungo cha ndoa “ni kwenda kinyume cha mapenzi ya Mungu, linaelewa pia kwamba
wanae wengi ni dhaifu”.[311] Likiangazwa na mtazamo wa Kristo, “Kanisa linawaangalia kwa
upendo wale wanaoshiriki maisha yake kwa namna isiyotimilika, likitambua kuwa neema ya
Mungu hufanya kazi pia katika maisha yao kwa kuwapa moyo wa kutenda mema, wa kutunzana
kwa upendo, na kuihudumia jumuiya yenyewe ambamo wanaishi na kufanya kazi”.[312] Kwa
upande mwingine, msimamo huo unaimarishwa na mazingira ya mwaka huu wa Jubilei ya
huruma. Ijapokuwa Kanisa linawaelekeza sikuzote wote kwenye ukamilifu na kuwaalika
wamwitikie Mungu zaidi na zaidi, “linapaswa kuwasindikiza kwa makini na kwa upendo wanae
dhaifu zaidi, walioathirika na upendo uliojeruhiwa na kupotewa, kwa kuwatia moyo na tumaini,
kama vile mwanga unaomulika juu ya mnara bandarini, au mwenge unaopelekwa kati ya watu ili
kuwaangaza waliopotea njia au wanaokumbwa na tufani”.[313] Tusisahau kuwa mara nyingi kazi
ya Kanisa inafanana na ile ya hospitali ya dharura.
292. Ndoa ya kikristo, iliyo kioo cha muungano wa Kristo na Kanisa lake, inatimilizwa kikamilifu
katika muungano kati ya mwanamume na mwanamke, ambao wanajitoa mmoja kwa mwenzake tu

10.6 Page 96

▲back to top
96
katika upendo maalum na uaminifu huru, na kila mmoja anakuwa ni mali ya mwenzie hadi siku ya
kufariki, na wote wawili wapo tayari kuzaa watoto, wakiwa wamewekwa wakfu kwa njia ya
sakramenti yenye kuwapa neema ili wawe Kanisa la nyumbani na chachu ya maisha mapya kwa
jamii. Mitindo mingine ya muungano inapinga kabisa makusudio haya, lakini mingine tena
inayatimiza walau kwa sehemu na kimfanano. Mababa wa Sinodi walisema kwamba Kanisa halina
budi kuyathamini mambo yanayoweza kujenga, katika hali ambazo haziwiani bado na mafundisho
yake juu ya ndoa au zimeacha kuwiana nayo.[314]
Kazi ya kichungaji hatua kwa hatua
293. Mababa wa Sinodi wameangalia pia hali maalum ya ndoa ya kiserikali tu; na hata ile hali ya
kuishi pamoja bila ndoa. Maana, ingawa tofauti zipo kati ya hali hizo, “pale ambapo huo
muungano unafikia uthabiti mkubwa wa kutosha kwa njia ya kifungo cha hadharani, ukiwa
unaonyesha kuwepo kwa upendo mkuu, uwajibikaji mbele ya watoto, uwezo wa kukabiliana na
magumu, huweza kutazamwa kama fursa ya kusindikizwa ili ichanue hadi kufikia hatua ya
kuadhimisha sakramenti ya ndoa”.[315] Kwa upande mwingine, inahangaisha kuona kwamba
nyakati hizi vijana wengi hawategemei ndoa na wanakaa pamoja wakiahirisha bila kikomo kifungo
cha ndoa, na tena kuna wengine ambao wanakatisha kifungo chao na mara wanafunga kingine
kipya. Wale “walio sehemu ya Kanisa, wanahitaji uangalizi wa kiuchungaji wenye huruma na wa
kutia moyo”.[316] Maana, wajibu wa Wachungaji si tu kuhamasisha ndoa ya kikristo, bali pia
“kufanya upambanuzi wa kichungaji juu ya hali za watu wengi ambao hawaishi tena hali hiyo”, ili
“kuanzisha mazungumzano ya kichungaji na watu hao kwa lengo la kuangalia mambo yaliyomo
kwenye maisha yao yanavyoweza kusaidia kuwaongoza kupokea Injili ya ndoa katika utimilifu
wake”.[317] Kwa ajili ya upambanuzi wa kichungaji yafaa “kujitahidi kugundua katika maisha ya
watu hao viashiria vya uwezekano wa uinjilishaji na ukuaji wa kibinadamu na kiroho”.[318]
294. “Uamuzi wa kufunga ndoa ya kiserikali au, katika hali nyingine, wa kuishi pamoja bila ndoa,
mara nyingi hausababishwi na kukadiria vibaya au kupinga muungano wa kisakramenti, ila na hali
za utamaduni au hali nyingine za dharura”.[319] Katika hali hizo zitaweza kuthaminiwa alama zile
za upendo ambazo, kwa namna fulani, zinaakisi upendo wa Mungu.[320] Tunajua kwamba
"inaendelea kukua idadi ya majozi ambayo baada ya kuishi pamoja kwa muda mrefu, wanaomba
kuadhimisha ndoa kanisani. Kuchagua kuishi pamoja bila ndoa mara nyingi hutokana na kasumba
ya jumla iliyozoea kupingana na wajibu wowote ulio rasmi na wa kudumu, lakini pia unatokana na
kusubiri kuwa na uhakika wa maisha kiuchumi (kazi na mshahara wa kudumu). Mwisho, miungano
isiyo rasmi katika baadhi ya nchi ni mingi si tu kutokana na kukataa tunu za familia na ndoa, bali
hasa kutokana na ukweli kwamba, kwa wanaoishi katika hali ya chini kijamii, kufunga ndoa
kunatazamwa kama starehe ya matajiri, kiasi kwamba umaskini wa mali unawasukuma kuiishi
miungano isiyo rasmi”.[321] Lakini, "hali zote hizi zishughulikiwe kwa mtindo wa kujenga, kwa
kujaribu kuzigeuza ziwe fursa za makuzi kuelekea utimilifu wa ndoa na wa familia katika mwanga
wa Injili. Yaani, inatakiwa kuzipokea hali hizo na kuzisindikiza kwa uvumilivu na umakini”.[322]
Ndivyo alivyofanya Yesu na mwanamke Msamaria (taz. Yn 4:1-26): alimwambia neno la kugusa

10.7 Page 97

▲back to top
97
hamu yake ya upendo wa kweli, ili amponye na yote yaliyokuwa yanatia giza maishani mwake, na
kumwongoza kwenye furaha kamili ya Injili.
295. Kwa mtazamo kama huo, mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa akishauri kutumia utaratibu ule
unaoitwa “sheria ya hatua kwa hatua”, kwa kutambua kwamba binadamu “hufahamu, hupenda na
kutimiza wema wa kimaadili kwa kupitia hatua mbalimbali za ukuaji”.[323]. Si kwamba sheria
yenyewe ina hatua nyingi ndani yake; bali ni kwamba watu wasio katika hali ya kuelewa, kukubali
na kutekeleza kikamilifu madai halisi ya sheria, wafikie hatua kwa hatua kutenda kwa busara
matendo huru. Maana, pia sheria ni zawadi ya Mungu yenye kuelekeza njia, zawadi kwa ajili ya
wote bila ubaguzi, inayoweza kupokelewa maishani kwa nguvu ya neema, ingawa kila
mwanadamu “anaendelea hatua kwa hatua katika mwendo wake kwa kutangamanisha kwa
utaratibu vipawa vya Mungu na madai ya upendo wake wa kudumu na usio na mipaka katika
maisha mazima ya kibinafsi na ya kijamii ya mtu”.[324]
Upambanuzi wa hali zinazoitwa “zisizo kadiri ya kanuni”[325]
296. Sinodi imezungumza juu ya hali mbalimbali za udhaifu au za kukosa ukamilifu. Kuhusu hilo,
napenda hapa kukumbusha kile nilichotaka kubainisha wazi kwa Kanisa lote, tusije tukakosa njia:
"Mantiki mbili huelekeza historia nzima ya Kanisa: ile ya kutenga, na ile ya kukaribisha tena [...].
Njia ya Kanisa, kuanzia Mtaguso wa Yerusalemu na kuendelea, ndiyo daima ileile ya Yesu: yaani,
ya kuhurumia na kutangamanisha [...]. Njia ya Kanisa siyo ile ya kumhukumu mtu hata milele; bali
ni ile ya kuwatolea huruma ya Mungu watu wote wanaoiomba kwa moyo mnyofu [...]. Kwa maana
mapendo ya kweli daima hayastahiliwi, hayana sharti yoyote, ni bure!”.[326] Kwa hiyo, “lazima
kuachana na hukumu ambazo hazizingatii ugumu wa mazingira mbalimbali, na inabidi kuangalia
kwa makini jinsi watu wanavyoishi na kuumia kwa sababu ya hali yao”.[327]
297. Ni suala la kuwatangamanisha wote; ni lazima kumsaidia kila mmoja kupata namna yake wa
kushiriki katika jumuiya ya kikanisa, ili ajisikie amejaliwa huruma "isiyostahiliwa, bila masharti, na
ya bure". Hakuna mtu anayeweza kuhukumiwa kwa daima, kwa maana hiyo siyo mantiki ya Injili!
Siwaongelei tu wenye talaka wanaoishi muungano mpya, bali wote, katika mazingira yoyote
wanamoishi. Ni dhahiri kwamba endapo mtu mmoja anaringa kuishi katika dhambi halisi kana
kwamba hiyo inayo makusudio ya kikristo, ama hutaka kulazimisha kitu kilicho tofauti na
linachofundisha Kanisa, hawezi kudai kufundisha katekesi au kuhubiri, na, kwa maana hiyo, kuna
kitu fulani kinachomtenganisha na jumuiya (taz. Mt 18:17). Anahitaji kusikiliza upya ujumbe wa
Injili na mwaliko kwa wongofu. Lakini hata kwa mtu huyo inaweza kupatikana njia fulani ya
kushiriki maisha ya jumuiya: katika shughuli za kijamii, katika mikutano ya sala, au kadiri
anavyomsukumwa na moyo wake, pamoja na upambanuzi wa Mchungaji. Kuhusu namna ya
kuyashughulikia hali mbalimbali zilizoitwa “zisizo kadiri ya kanuni”, Mababa wa Sinodi
wameyafikilia makubaliano ya kijumla, ambayo nayategemeza: “Kwa lengo la kuwashughulikia
kiuchungaji watu waliofunga ndoa kiserikali, au wenye talaka waliofunga ndoa tena, au wale
ambao wanaishi tu pamoja, ni juu ya Kanisa kuwafunulia malezi ya kimungu yanayohusu kazi ya

10.8 Page 98

▲back to top
98
neema katika maisha yao, na kuwasaidia kuufikia utimilifu wa mpango wa Mungu ndani yao”,[328]
unaowezekana sikuzote kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.
298. Wenye talaka ambao wanaishi muungano mpya, kwa mfano, wanaweza kujikuta katika hali
ya maisha zinazotofautiana sana kati yao, ambazo si halali ziainishwe au kufungwa katika
matamko yaliyo magumu mno bila kuacha nafasi ya upambanuzi wa kufaa wa kadhia moja moja
na wa kichungaji. Kitu kimoja ni muungano wa pili ambao umeimarika baada ya muda mrefu wa
kuishi pamoja, ulioleta na watoto wapya, ambao una uaminifu uliohakikishwa, majitoleo yenye
ukarimu, bidii ya kikristo, utambuzi wa hali yao isiyo kadiri ya kanuni na ugumu mkubwa wa kurudi
nyuma bila kuhisi katika dhamiri kwamba huko kungesababisha kuingia katika makosa mengine.
Kanisa linatambua hali zile ambazo “mwanamume na mwanamke, kwa sababu nzito – kama, kwa
mfano, malezi ya watoto wao – hawawezi kutekeleza sharti la mafarakano”.[329] Wapo pia wale
ambao walifanya juhudi kubwa kusudi waokoe ndoa ya kwanza, nao wametelekezwa bila haki, au
wengine “ambao walifunga muungano wa pili, kwa ajili ya malezi ya watoto, na pengine wanayo
hakika katika dhamiri yao ya kwamba ndoa ya kwanza, iliyovunjika moja kwa moja, ilikuwa si halali
tangu mwanzo”.[330] Lakini ni kitu kingine muungano mpya unaotokana na talaka ya karibuni,
pamoja na yatokanayo yote ya mateso na mahangaiko yawapatayo watoto na familia zote husika,
ama hali ya mtu ambaye, mara kwa mara, amekosa kuyashika majukumu yake ya kifamilia.
Lazima iwe dhahiri kwamba hayo siyo makusudio ambayo Injili inashauri kwa ndoa na familia.
Mababa wa Sinodi walisema pia kwamba upambanuzi wa Wachungaji inabidi ufanyike daima
“kwa kuzibainisha inavyotakiwa hali mbalimbali za watu”,[331] kwa mtazamo wenye “kuelewa
vizuri utofauti wa hali mbalimbali”.[332] Tunajua kuwa hazipo “mbinu rahisi”.[333]
299. Nipokee maoni ya Mababa wengi wa Sinodi, ambao wamekubaliana kutamka kwamba
“wabatizwa wenye talaka ambao wamefunga ndoa tena kiserikali lazima washirikishwe zaidi katika
jumuiya za kikristo kwa mbinu zote zinazowezekana, kwa kukwepa kila nafasi ya kusababisha
kikwazo. Mantiki ya tangamano ndiyo ufunguo wa juhudi ya kuwasindikiza kiuchungaji, kusudi
wajue kuwa ni viungo vya Mwili wa Kristo ulio Kanisa, ila si hilo tu, bali pia kwamba waweze
kung’amua kwa furaha ukweli huo na kutoa matunda mema. Hao ndio wabatizwa, ndio kaka na
dada zetu, naye Roho Mtakatifu anawamiminia mapaji na karama kwa manufaa ya wote. Kushiriki
kwao kunaweza kuchukua sura za huduma mbalimbali za kikanisa: kwa hiyo inabidi kupambanua,
kati ya aina mbalimbali za kutenga watu zinazotumiwa mpaka wakati huu katika liturujia,
uchungaji, malezi na mambo ya taasisi, ni zipi zile ambazo zinaweza kufutwa. Hao hawatakiwi
kujisikia wametengwa na Kanisa, lakini si hilo tu, bali pia waweza kuishi na kukua kama viungo hai
vya Kanisa, wakilihisi ni kama Mama mwenye kuwakaribisha daima, kuwatunza kwa upendo na
kuwapa moyo katika njia ya maisha na ya Injili. Tangamano hii inahitajika pia ili kuwatunza na
kuwalea kikristo watoto wao, wanaopaswa kuhesabiwa wa muhimu kuliko wote”.[334]
300. Kama tukizingatia idadi kubwa sana ya namna tofauti za hali halisi ya watu, kama yale
tuliyotaja hapo juu, inaeleweka wazi kwamba isingetarajiwa kupata, kutokana na Sinodi au Wosia
huu, sheria mpya za jumla za mtindo wa kikanoni, zenye kufaa kwa hali zote. Inawezekana kutoa

10.9 Page 99

▲back to top
99
tu himizo jipya lenye kutia moyo ili ifanyike upambanuzi wa wahusika na wa kichungaji, ambao
utasaidia kuzishughulikia kwa uwajibikaji kila kadhia maalumu; upambanuzi huo ungetakiwa
kutambua kwamba, kwa vile “kiwango cha wajibu si sawasawa kwa kadhia zote”,[335] yatokanayo
au matokeo ya kanuni fulani haibidi yawe daima yaleyale.[336] Mapadre kazi yao ni
“kuwasindikiza wahusika katika njia ya upambanuzi kadiri ya mafundisho ya Kanisa na maelekezo
ya Askofu. Katika mchakato huu itafaa kufanya uchunguzi wa dhamiri, kwa njia ya vipindi vya
matafakari na vya toba. Wenye talaka waliofunga ndoa tena wangepaswa kujiuliza jinsi
walivyowatendea watoto wao wakati muungano wa ndoa ulipoingia kwenye mgogoro; ikiwa
walitafuta njia ya kupatana tena; ikoje hali ya mwenzi aliyeachwa; uhusiano mpya una athari gani
kwa ajili ya ndugu wengine wa familia na ya jumuiya ya waamini; nao unatoa mfano gani kwa
vijana wanaotakiwa kujiandaa kwa ndoa. Tafakuri ya dhati inaweza kuiimarisha imani juu ya
huruma ya Mungu ambayo hapana mtu anayenyimwa”.[337] Ndio utaratibu wa usindikizaji na
upambanuzi ambao “unawaelekeza waamini hawa wafahamu ukweli wa hali yao mbele ya Mungu.
Mazungumzo na padre, faraghani, yanachangia katika kupata utambuzi sahihi juu ya kinachozuia
uwezekano wa kushiriki kikamilifu zaidi maisha ya Kanisa, na juu ya hatua zinazoweza kuusaidia
na kuuendeleza ushiriki huo. Kwa vile katika sheria yenyewe hamna utaratibu wa kwenda hatua
kwa hatua (gradualness, taz. Familiaris consortio, 34), upambanuzi huo hautaweza kamwe
kusahau masharti ya ukweli na ya upendo ya Injili yanayopendekezwa na Kanisa. Kusudi hilo
litokee, inabidi yahakikishwe masharti ya lazima ya unyenyekevu, usiri, upendo kwa Kanisa na
kwa mafundisho yake, katika kuyatafuta kiadilifu matakwa ya Mungu, na katika matamanio ya
kufikia kuyaitikia kwa ukamilifu zaidi”.[338] Msimamo wa namna hii ni ya msingi ili kuepukana na
hatari nzito ya kueneza taarifa zisizo sahihi, kama vile wazo la kwamba mapadre wengine waweze
kutoa haraka “ruhusa zisizo kawaida”, au la kwamba wawepo watu wanaostahili kupata
mapendeleo kuhusu sakramenti baada ya kutoa ufadhili. Mtu mtaratibu na wa busara, asiyedai
kuweka tamaa zake juu ya manufaa ya wote katika Kanisa, anapokutana na Mchungaji ambaye
anajua kutambua uzito wa suala analopambana nalo, inakwepwa hatari ya kwamba aina fulani ya
upambanuzi isababishe wazo la kwamba Kanisa linashika maadili mawili.
Mambo tetezi katika upambanuzi wa kichungaji
301. Kusudi tuelewe jinsi ipasavyo kwa nini upambanuzi maalum unawezekana na kuhitajika
katika kuzishughulikia hali zile “zisizo kadiri ya kanuni”, kama zinavyoitwa, pana suala ambalo
inabidi daima kulitilia maanani, ili mtu asifikiri kamwe kuwepo lengo la kupunguza masharti ya
Injili. Kanisa limetafakari kwa kina kuhusu athari zinazosababisha matendo na juu ya mambo
tetezi. Ndiyo maana haiwezekani tena kusema kwamba wale wote wanaojikuta katika hali fulani
inayosemwa “isiyo kadiri ya kanuni” wanaishi katika hali ya dhambi ya mauti, na wamenyimwa
neema ya utakaso. Mapungufu hayatokani tu na kutokujua sheria. Mtu, hata akijua vizuri sheria,
anaweza kuona ugumu mkubwa katika kuelewa “tunu zilizomo ndani ya kanuni ya kimaadili”[339]
au anaweza kujikuta katika hali halisi ambazo hazimruhusu kutenda kwa mtindo tofauti na kufanya
maamuzi mengine bila kukosa tena. Kadiri walivyojieleza vema Mababa wa Sinodi “inawezekana
ziwepo sababu zinazopunguza uwezo wa kuamua”.[340] Mtakatifu Tomaso wa Aquino tayari alikiri

10.10 Page 100

▲back to top
100
kwamba wengine wanaweza kuwa na neema na upendo, ila hawawezi kutekeleza vizuri
mojawapo ya fadhila,[341] kwa namna ya kwamba, hata ingawa wanazo moyoni fadhila zote za
kimaadili, hawaonyeshi kidhahiri uwepo wa mojawapo, kwa sababu matendo ya nje ya fadhila hiyo
yanapatwa na magumu: “Husemwa kuwa watakatifu wengine hawana fadhila fulani, kwa sababu
ya magumu wang'amuayo katika kuzitenda, [...] ijapokuwa hao wanayo tabia ya fadhila zote”.[342]
302. Kuhusu athari hizo Katekisimu ya Kanisa Katoliki inajieleza kwa jinsi isiyoweza kupingwa:
“Shutuma na uwajibikaji juu ya tendo fulani huweza kupunguzwa au kuondolewa kwa sababu ya
ujinga, kupitiwa, kutendwa ukatili, hofu, mazoea, mapenzi yasiyo na taratibu na vitu vingine vya
kisaikolojia na kijamii”.[343] Katika kipengele chake kingine inazidokeza tena hali zinazopunguza
uwajibikaji wa kimaadili na inataja, kwa upana sana, “kutokomaa kihisia, nguvu ya mazoea
yaliyojijenga, hali za fadhaa na mambo mengine ya kisaikolojia au kijamii.[344] Kwa sababu hiyo,
kuihukumu hali fulani halisi kuwa ni kosa hakusababishi hukumu juu ya kushutumiwa na uhalifu
wake mtu anayehusika.[345] Katika muktadha wa mambo hayo, naona kwamba yana maana sana
waliyotaka kusema Mababa wengi wa Sinodi: “Katika hali fulani, watu wanakutana na magumu
makubwa katika kuamua kutenda vinginevyo. [...] Upambanuzi wa kichungaji, ijapokuwa unaitia
maanani dhamiri ya watu iliyolelewa kiadilifu, lazima ujitwike hali hizo. Pia matokeo ya matendo
yalilofanyika, siyo yaleyale bila shaka katika kila hali”.[346]
303. Tunapokumbuka athari ya hali halisi ya mambo kama haya, tunaweza kuongeza kusema
kuwa dhamiri ya mtu binafsi yatakiwa ishikamanishwe vizuri zaidi ndani ya desturi ya utendaji wa
Kanisa katika mazingira fulani yale yasiyojumuisha uelewa wetu wa ndoa. Ama hakika, nguvu zote
zitumike kuongeza makuzi ya dhamiri yenye uelewa sahihi, iliyoundwa na kusindikizwa na
upambanuzi makini na unaowajibika wa Mchungaji, na kuhimiza ili kuiaminia zaidi na zaidi neema
ya Mungu. Hata hivyo, dhamiri inaweza kutenda zaidi ya kule kutambua kwamba mazingira fulani
maalum hayapatani kiukweli na madai ya jumla ya Injili. Inaweza pia kutambua kwa unyofu na
moyo safi kuwa ni mwitiko upi kwa sasa unaonyesha moyo wa ukarimu unaoweza kuelekezwa
kwa Mungu, na kuweza kutambua kwa uhakika wa kiwango fulani cha uadilifu kwamba hili ndilo
analolitaka Mungu katikati ya mwingiliano huu wa mapungufu ya mtu binafsi, ijapo siyo bado hali
ile timilifu inayotazamiwa. Kwa vyovyote, tukumbuke kuwa upambanuzi unaendelea kufanyika, na
ni lazima uwe tayari kuingia hatua nyingine ya makuzi na kuwa tayari kufanya maamuzi mapya
yanayowezesha litekelezwe vizuri zaidi lengo timilifu.
Kanuni na upambanuzi
304. Ni kidogo mno kufikiria tu ikiwa matendo ya mtu mmoja yanapatana na sheria ama kanuni ya
jumla au la, kwa sababu hilo halitoshi kwa ajili ya kupambanua na kuthibitisha uaminifu kamili kwa
Mungu katika maisha halisi ya mwanadamu. Naomba kwa moyo kabisa tulikumbuke fundisho la
mtakatifu Tomaso wa Akwino na tujifunze ili tuliunganishe na upambanuzi wetu wa kichungaji:
“Hata kama kuna ulazima katika kanuni za jumla, tunavyozidi kutelemka na kusogelea vipengee
vya kinaganaga, ndivyo mara nyingi zaidi tunakutana na mapungufu. [...] Kuhusu hali za tendo,

11 Pages 101-110

▲back to top

11.1 Page 101

▲back to top
101
ukweli au kanuni ya utendaji siyo sawa kwa wote unapoangalia kwa kinaganaga, ila tu inapohusu
kanuni za jumla; na hata palipo na makubaliano kuhusu kanuni ya utendaji unapoangalia kwa
kinaganaga, hiyo kanuni haijulikani kwa namna ileile na wote. [...] Kanuni itaonekana kuzidi
kutoeleweka kadiri tunavyoelekea katika hali ya kinaganaga zaidi”.[347] Ni kweli kwamba kanuni
za jumla zinaonyesha jambo jema ambalo haliwezi kupuuzwa ama kudharauliwa, lakini katika
kutamkwa kwake haiwezekani kuonyesha vipengele vya mazingira yote. Na wakati huohuo,
inabidi kusema kwamba, hasa kwa sababu hiyohiyo, jambo linalohusu upambanuzi wa kiutendaji
katika hali ya mazingira maalumu haliwezi kuwekwa katika kiwango cha kuwa kanuni ya jumla.
Kufanya hivyo kungaliishia siyo tu katika mkanganyiko usiovumilika wa hoja za kutetea mambo
yasiyo ya kweli, bali pia kungalihatarisha tunu na thamani zinazopaswa kutunzwa kwa uangalifu
wa pekee.[348]
305. Kwa sababu hiyo, Mchungaji hawezi kuchukulia kuwa inatosha kutumia tu kanuni za maadili
juu ya wale wanaoishi katika hali “isiyo kadiri ya kanuni”, kana kwamba zingalikuwa ni mawe ya
kuwatupia watu. Hii ingedhihirisha moyo uliojifungia wa mtu aliyefichama nyuma ya mafundisho ya
Kanisa, “akikalia kiti cha Musa akitoa hukumu, mara nyingine kwa kujiaminia ukuu na kwa
kurashia tu, juu ya matatizo mazito ya familia zilizojeruhiwa”.[349] Kwa mtiririko huohuo, Tume ya
Kimataifa ya Teolojia imetamka hivi: “Sheria asilia haingeelezwa kuwa tayari ni orodha ya kanuni
zinazolazimika kuwapo na kutumia awali ya yote (a priori) wakati wa kuhukumu mambo ya
maadili; bali ni chemchemi ya mshituo halisi kwa mchakato wa hiyo hukumu, ambao hasa ni wa
binafsi, ya kufikia uamuzi”.[350] Kutokana na mambo yanayomweka mtu katika hali ya maelekeo
ya kufanya jambo, na mambo yanayopunguza makali ya lawama, inawezekana kwamba mtu
akiwa katika hali ambayo kwa yenyewe ni hali ya dhambi – lakini yeye asiwe na lawama, ama
asiweze kulaumiwa kikamilifu – aweze kuishi katika hali ya neema ya Mungu, akawa na upendo
na pia akaongezeke katika maisha ya neema na upendo, huku akipokea msaada wa Kanisa kwa
nia hiyo.[351] Upambanuzi lazima usaidie kupata njia zinazowezekana za kumwitikia Mungu na
kukua katikati ya mapungufu. Kwa kuamini kuwa kila kitu kinakuwa ama cheupe ama cheusi,
nyakati nyingine tunafungia mbali njia za neema na makuzi, na hivyo kuziponda moyo safari za
utakaso zinazomtukuza Mungu. Ebu tukumbuke kuwa “hatua moja katikati ya mapungufu
makubwa ya kibinadamu, inaweza ikampendeza zaidi Mungu kuliko maisha yanayoonekana kwa
nje kuwa ni mazuri, lakini yanatiririka kwa siku nzima bila kuyashinda magumu yoyote
mazito”.[352] Utekelezaji wa kazi ya uchungaji wa wahudumu na jumuiya za kikristo lazima
uzingatie ukweli wa hali hii.
306. Katika kila hali, mbele ya wale wenye shida ya kushika kikamilifu sheria ya Mungu, mwaliko
wa kufanya bidii ya kufuata njia ya upendo (via caritatis) usikike wazi kabisa. Upendo wa kindugu
ndiyo sheria ya kwanza ya Wakristo (Yn 15:12; Gal 5:14). Na tusisahau maneno ya kitulizo
yaliyoahidi Maandiko Matakatifu: “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana, kwa
sababu upendano husitiri wingi wa dhambi” (1Pet 4:8); “ukaache dhambi zako kwa kutenda haki,
ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa
raha” (Dan 4:27); “Maji huuzimisha moto uwakao, na sadaka huwa upatanisho wa dhambi” (YbS

11.2 Page 102

▲back to top
102
3:29). Hivi ndivyo pia alivyofundisha mtakatifu Agustino akiandika: “Kama vile tungalikuwa katika
hatari kwa sababu ya moto, tungekimbia mara moja kwenda kuchota maji ili tuuzimishe, [...]
ndivyo pia, iwapo miali ya dhambi inalipuka katika manyasi ya tamaa zetu na tunatikiswa, kama
tunapata fursa ya kufanya tendo la huruma, ebu tulifurahie kana kwamba ingalikuwa chemchemi
ya maji tuliyopewa ili kuuzimisha moto huo mkali”.[353]
Mantiki ya huruma ya kichungaji.
307. Ili kuepusha uelewa mbaya, ninasisitiza kwamba kwa namna yoyote ile Kanisa lisisitize
kufundisha hali ya ndoa timilifu inayotamaniwa, ambayo ndiyo mpango wa Mungu katika utakatifu
wake: “Vijana waliobatizwa wahimizwe kuelewa kwamba sakramenti ya ndoa ina uwezo wa
kutimiliza matumaini yao ya kufanikiwa katika upendo wao na kwamba wanaweza kupata nguvu
kwa neema ya Kristo katika sakramenti na kwa uwezekano wa kutumia fursa nyingi za kushiriki
kikamilifu katika maisha ya Kanisa”.[354] Msimamo usio na mwelekeo, ama aina yoyote ya
kuamini kuwa ukweli na uadilifu unategemea mazingira, ama kuona aibu wakati wa kuitangaza,
ingekuwa ni kukosa uaminifu kwa Injili na kwa upande wa Kanisa ni kukosa pia upendo kwa vijana
wenyewe. Kuonyesha uelewa kwa mazingira ya pekee hakumaanishi hata kidogo kuficha nuru ya
kusudio timilifu, ama kupunguza yale ambayo Yesu anataka kuwajalia binadamu. Leo, kazi
muhimu zaidi kuliko kuchunga ndoa zilizoshindwa, ni kufanya juhudi za kiuchungaji ili kuimarisha
ndoa na hivyo kuzuia zisivunjike.
308. Lakini, kutokana na kutambua uzito wa vitendo na hali zinazopunguza uzito wa kulaumiwa -
yaani hali ya kisaikolojia, kihistoria na hata kimaumbile – inafuata kwamba “bila kupunguza lengo
timilifu la kiinjili, kuna haja ya kuzisindikiza kwa huruma na uvumilivu hatua za kukua binafsi
kuelekea lengo hilo zinavyojitokeza moja baada ya nyingine”, tukiachia nafasi kwa ajili ya “huruma
ya Mungu, inayotuhimiza tutende mema yanayowezekana”.[355] Ninawaelewa wale
wanaopendelea kuchukua hatua kali zaidi za kichungaji ambazo haziruhusu mwanya wa
kutoeleweka vizuri. Lakini ninaamini kwa unyofu wote kwamba Yesu analitaka Kanisa
linalotambua uzuri anaoupanda Roho Mtakatifu katikati ya udhaifu wa kibinadamu: Kanisa ambalo
ni Mama ambaye kwa upande mmoja anaonyesha mafundisho yake jinsi yalivyo, na upande
mwingine “linafanya kila jema linalowezekana, hata kama katika utendaji huo lina hatari ya
kuchafuka kwa matope ya njiani”.[356] Wachungaji wa Kanisa, wanapowafundisha waamini ukweli
kamili wa Injili na mafundisho ya Kanisa, yawapasa pia kuwaelekeza jinsi ya kuwasaidia wadhaifu
kwa huruma, wakiepuka kuongeza maumivu ama kutoa hukumu kali ama za haraka haraka. Injili
yenyewe inatufundisha tusihukumu wala kulaumu (Mt 7:1; Lk 6:37). Yesu “anatutazamia kuwa
tuache kutafuta vijishimo vya kufichama binafsi ama kama jumuiya, vinavyotukinga na mafuriko ya
majanga ya kidinadamu, na badala yake tuingie katika ukweli wa mambo ya maisha ya watu na
kutambua nguvu ya upendo upole. Kila tunapofanya hivyo, maisha yetu yanakuwa yana
mchangamano mzuri wa kustaajabisha”.[357]
309. Ni maongozi ya Mungu kwamba tafakari hii inafanyika katika Mwaka Mtakatifu

11.3 Page 103

▲back to top
103
unaosherehekea Huruma ya Mungu, kwa sababu hata mbele ya hali mbalimbali zinazohusu
familia, “Kanisa limeagizwa kazi ya kuitangaza huruma ya Mungu, iliyo moyo hai wa Injili, ambayo
kwa njia ya Kanisa lazima ipenye akili na moyo wa kila mtu. Kanisa, lililo Bibi Harusi wa Kristo,
linapanga mwenendo wake kumwiga Mwana wa Mungu anayemwendea kila mmoja bila
kubagua”.[358] Kanisa linajua kuwa Yesu mwenyewe ni Mchungaji wa kondoo wote mia moja, na
siyo wa tisini na tisa tu. Anawapenda wote. Kwa msingi wa kutambua hilo, sasa itawezekana
“marhamu ya huruma ya Mungu kumfikia kila mmoja, mwamini na yule aliye mbali kabisa, iwe ni
ishara kwamba ufalme wa Mungu tayari u katikati yetu”.[359]
310. Hatuwezi kusahau kuwa “huruma si utendaji wa Baba tu; inakuwa ni kipimo cha kutambua ni
akina nani ambao ni wanae wa kweli. Kifupi, tunaitwa tuishi kwa huruma, kwa sababu sisi tulipewa
huruma kwanza”.[360] Hili si swala la hisia tupu ama mwitiko vuguvugu kwa upendo wa Mungu,
ambao daima unatafuta kilicho bora kabisa kwa ajili yetu, kwa sababu “huruma ndiyo msingi
wenyewe wa maisha ya Kanisa. Kazi zake zote za kichungaji zinatakiwa ziunganishwe mara na
upendo mpole ambao Kanisa linawaonyesha waamini; huruma isikosekane popote katika
mahubiri yake na ushuhuda wake kwa ulimwengu”.[361] Ni kweli kwamba wakati mwingine
“tunatenda kama wadhibiti wa neema kuliko kuwa wawezeshaji. Lakini Kanisa siyo nyumba ya
ushuru; ni nyumba ya Baba, ambamo kuna nafasi kwa kila mmoja, licha ya kuwa na matatizo
yake”.[362]
311. Ufundishaji wa somo la teolojia ya maadili usiache kujumuisha vipengele hivi, kwa sababu
ingawa ni kweli kabisa kuwa yapasa kuwajibika ili kufundisha kikamilifu maadili ya Kanisa,
uangalifu wa pekee uonyeshwe ili kusisitiza na kutengeneza mazingira ya usitawi wa mafundisho
makuu na ya kina juu ya tunu za Injili,[363] hasa kuhusu nafasi ya kwanza ya upendo kama
mwitiko kwa zawadi tusiyostahili ya upendo wa Mungu. Wakati mwingine, katika kazi zetu za
kichungaji, tunaona vigumu kutoa nafasi kwa upendo wa Mungu usio na masharti.[364] Tunaweka
masharti mengi sana ya kupata huruma na msamaha, kiasi kwamba tunafuja maana yake
inayolingana na ukweli wa mambo na makusudio yake halisi. Hii ndiyo njia mbaya kabisa ya
kuichujua Injili. Ni kweli, kwa mfano, kwamba huruma haijitengi na haki pamoja na ukweli, lakini
kwanza juu ya yote lazima tuseme kwamba huruma ni utimilifu wa haki na ndiyo ushahidi
unaong’ara kabisa wa ukweli wa Mungu. Kwa sababu hii, tunapaswa kutambua kuwa “ni uelewa
usiotosha wa kiteolojia ule ambao mwishoni unatilia mashaka kuhusu uwezo mkuu wa Mungu, na
hasa kuhusu huruma yake”.[365]
312. Hii inatupatia kipimo na mpangilio ambavyo hutusaidia kuepuka ubaridi na urasimu wa
kimaadili tunaposhughulikia maswala nyeti. Badala yake, yanatuweka katika mazingira ya
upambanuzi wa kichungaji, uliojaa upendo wenye huruma, ambao upo tayari daima kuelewa
mambo, kusamehe, kusindikiza, kutumainia, na zaidi ya yote kuwakaribisha na kutangamanisha
wote. Hii ndiyo namna ya mtazamo wa mambo ambao yapasa utawale katika Kanisa na kutufanya
“tufungue mioyo yetu na kuwaelekea wale wanaoishi pembezoni kabisa mwa jamii”.[366]
Nawahimiza waamini wanaojikuta katika hali ya mkanganyiko wazungumze na wachungaji wao

11.4 Page 104

▲back to top
104
kwa matumaini ama na walei wengine wenye maisha yaliyoshikamana na Bwana. Yawezekana
wasikute daima ndani yao uthibitisho wa mawazo na hamu zao, lakini kwa hakika watapata nuru
fulani itakayowasaidia kuielewa vizuri zaidi hali yao na kugundua njia ya kukomaa binafsi. Pia
nawahimiza wachungaji wa Kanisa kuwasikiliza kwa moyo wa uelewa na utulivu, kwa nia nyofu ya
kuielewa hali yao ngumu na mtazamo wao, ili kuwasaidia waishi maisha mema zaidi na watambue
nafasi yao husika katika Kanisa.
SURA YA TISA
TASAUFI (MAISHA YA KIROHO) KATIKA NDOA NA FAMILIA
313. Mapendo yana namna mbalimbali ya kujidhihirisha, kwa kadiri ya hali tofauti ya maisha
ambayo kila mtu ameitwa kuishika. Hata miongo kadhaa iliyopita, Mtaguso Mkuu wa Vatikano II,
katika Dikrii juu ya utume wa walei, ulisisitiza tasaufi itokayo katika maisha ya kifamilia. Mtaguso
Mkuu ulisema kwamba tasaufi ya walei “inatakiwa kuwa na sura ya pekee kutokana na hali ya
ndoa na ya familia”[367], na kwamba “mahangaiko kwa ajili ya familia ... hayatakiwi kuwa mbali na
mwelekeo wa kiroho wa maisha”.[368] Kwa hiyo inafaa tueleze kwa kifupi sifa chache za msingi
za tasaufi hii ya pekee inayositawi kwenye mahusiano hai yaliyomo katika maisha ya familia.
Tasaufi ya ushirika wenye kupita maumbile
314. Tumesema daima juu ya Mungu kukaa moyoni mwa mtu anayeishi katika neema yake. Leo
tunaweza kuongeza kusema kwamba Utatu Mtakatifu umo katika hekalu la ushirika wa kindoa.
Kama Utatu Mtakatifu unavyokaa juu ya sifa za watu wake (taz. Zab 22:4), ndivyo unavyoishi kwa
undani katika mapendo ya wanandoa yanayoutukuza.
315. Uwepo wa Bwana hukaa katika familia halisi, na kama ilivyo katika hali yake, pamoja na
taabu zake, mapambano yake, furaha zake na azma zake za kila siku. Tunapoishi katika familia,
ni vigumu kwetu kujisingizia au kusema uongo; hatuwezi kujificha nyuma ya kinyago. Iwapo
upendo ni moyo wa juhudi hiyo ya kutenda kiukweli, ndipo Bwana anapotamalaki huko kwa furaha
yake na amani yake. Tasaufi ya upendo wa kifamilia inajumuisha maelfu ya vitendo halisi na vya
kweli. Mungu ana makao yake katika wingi huu wa vipawa na mahusiano mbalimbali vinavyokuza
ushirika. “Upendo wa namna hii unaunganisha pamoja tunu za kibinadamu na za kimungu”,[369]
kwa sababu umejaa upendo wa Mungu. Kwa jumla, tasaufi ya ndoa ni tasaufi ya kifungo (cha
kindoa) ambacho katika hicho upendo wa Mungu hukaa.
316. Ushirika wa kifamilia, mtu anapouishi vizuri, ni mwendo halisi wa kutakatifuzwa katika maisha
ya kawaida, na wa kukua katika maisha ya kifumbo; tena ni namna ya kuunganishwa kwa ndani
na Mungu. Maana, haja zinazoibuka katika maisha ya familia, ziwe za kindugu au za kijumuiya,
zinakuwa ni nafasi ya kufungua moyo zaidi na zaidi; na hilo linawezesha uhusiano na Bwana
unaotimilika zaidi na zaidi. Neno la Mungu linasema kwamba, “Yeye amchukiaye ndugu yake, yu

11.5 Page 105

▲back to top
105
katika giza; ... akaa katika mauti; ... hakumjua Mungu” (taz. 1Yoh 2:11, 3:14, 4:8). Mtangulizi
wangu Benedikto XVI alisema kwamba “kufumba macho mbele ya jirani, kunafanya mtu awe
kipofu hata mbele ya Mungu”,[370] na kwamba, kwa msingi, upendo ni nuru pekee “inayoangaza
upya sikuzote ulimwengu uliomo gizani”.[371] Kama tu “tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na
pendo lake limekamilika ndani yetu” (1Yoh 4:12). “Kwa asili na maumbile yake, binadamu ana
tabia ya kijamii”,[372] na “dhihirisho la kwanza na la asili la tabia ya kijamii ya mtu ni jozi la mume
na mke na familia”.[373] Kwa hiyo, tasaufi inapata umbo katika ushirika wa kifamilia. Kwa hiyo,
watu wenye hamu za kiroho za undani wasifikiri kuwa familia inawazuia wasikue kiroho; kinyume
chake, familia ni njia anayotumia Bwana ili awaongoze kwenye kilele che muungano wa kifumbo
naye.
Kuungana katika sala kwa mwanga wa Pasaka
317. Endapo familia ina kiini chake katika Kristo, Yeye anaunganisha na kuangaza maisha yote ya
kifamilia. Mateso na matata yanavumiliwa kwa kushiriki Msalaba wa Bwana; na kukumbatiana
naye kunawezesha kustahimili magumu yanapoibuka nyakati fulani. Katika siku za uchungu za
familia, pana muungano na Yesu ulio na nguvu ya kuzuia familia isivunjike. Familia zinafikia kwa
utaratibu, na “kwa neema ya Roho Mtakatifu, utakatifu wao kwa njia ya maisha ya ndoa, kwa
kushiriki pia fumbo la msalaba wa Kristo, linalogeuza shida na mateso viwe sadaka ya
upendo.”[374] Na, kwa upande mwingine, siku za furaha, pumziko, sherehe, na ujinsia pia,
vinakuwa namna ya kushiriki uhai kamili wa Ufufuko wake. Wenzi wa ndoa wanajenga kwa
vitendo vyao mbalimbali vya kila siku “nafasi hii ya kuangazwa na Mungu (spazio teologale)
ambapo uwepo wa kifumbo wa Bwana mfufuka unahisika.[375]
318. Kusali katika familia ni njia ya pekee ya kuonyesha na kuimarisha imani hii ya kipasaka.[376]
Dakika chache kila siku zipatikane ili wanafamilia wakae kwa pamoja mbele ya Bwana aliye hai,
na kumwambia mahangaiko yao, kumwomba kwa mahitaji ya familia, kumwomba kwa ajili ya
mwanafamilia aliye katika hali ngumu, kumwomba awasaidie kupendana, kumshukuru kwa
maisha waliyojaliwa na kwa mambo mema yote, kumwomba Bikira awalinde kwa ulinzi wake wa
mama. Kwa kutumia maneno machache, kipindi hiki cha sala kinaweza kuleta mema mengi sana
kwa familia. Aina mbalimbali za ibada za watu ni hazina ya kiroho kwa familia nyingi. Mwendo wa
pamoja wa sala una kilele chake katika kushiriki kwa pamoja Ekaristi Takatifu, hasa siku za
Dominika, iliyo siku ya mapumziko . Yesu anabisha hodi mlangoni kwa familia ili kushirikishana
nayo karamu ya Ekaristi (taz. Ufu 3:20). Hapo, wanandoa wanaweza daima kuthibitisha agano la
kipasaka lililowaunganisha, linaloakisi kama kioo Agano alilofunga Mungu na wanadamu
msalabani.[377] Ekaristi ni sakramenti ya Agano Jipya ambapo tendo la ukombozi la Kristo
linafanya kazi hadi sasa (taz. Lk 22:20). Hivyo, vifungo vya undani kati ya maisha ya ndoa na
Ekaristi vinaonekana wazi.[378] Chakula cha Ekaristi ni nguvu na kichocheo ili kuishi kila siku
agano la ndoa kama “Kanisa la nyumbani”.[379]
Tasaufi ya upendo unaojitoa kwa mwenzake tu kwa uhuru

11.6 Page 106

▲back to top
106
319. Katika ndoa mtu anaishi ukweli wa kuwa kabisa wa mwingine mmoja tu. Wanandoa
wanakubali changamoto na tarajio la kuzeeka na kujisadaka kwa pamoja; na hivyo wanakuwa ni
mfano wa uaminifu wa Mungu. Uamuzi thabiti huu, unaoathiri mtindo wa kuishi, ni “haja ya ndani
ya agano la upendo kati ya wanandoa”,[380] kwa sababu “mtu asiyeamua kwamba atapenda kwa
daima, ni vigumu aweze kupenda kwa dhati hata siku moja tu”.[381] Lakini uaminifu huu
usingekuwa na maana kiroho kama ungekuwa tu sheria iliyoshikwa kama jambo lililopaswa
kuvumiliwa tu. Kinyume chake, hali ya kuwa wa mtu mwingine inapaswa kukaa moyoni, ambamo
Mungu tu anaweza kuona (taz. Mt 5:28). Kila asubuhi, tunapoamka, tunachukua tena mbele ya
Mungu uamuzi huu wa kuwa waaminifu, licha ya mambo yoyote yatakayotokea baadaye. Na kila
mtu, anapokwenda kulala, anatarajia aamke tena ili kuendelea katika safari hiyo, kwa kutegemea
msaada wa Bwana. Hivyo, kila mwenzi wa ndoa ni kwa mwingine ishara ya Bwana aliye karibu
naye, ambaye hatuachi peke yetu: “Mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari”
(Mt 28:20).
320. Pana wakati maalumu ambapo upendo wa jozi unapata kuwa huru kwa namna kuu, na
unakuwa nafasi ya uhuru safi: ni hapo kila mwanandoa anapogundua kwamba mwenzie si mali
yake, bali ni wa mwingine aliye muhimu kabisa kuliko yeye: Bwana wake pekee. Hakuna mtu
anayeweza kudai kuwa anamiliki undani wa nafsi ya mpenzi wake, ule wa siri zaidi. Bwana tu
anaweza kukaa katika kiini cha maisha yake. Wakati huohuo, kanuni ya uhalisia wa kiroho
inafanya mwenzi wa ndoa asiweze kudai mwenzie aridhishe kikamilifu haja zake. Kama
alivyoeleza vizuri Dietrich Bonhoeffer, mwendo wa kiroho wa kila mtu unatakiwa kumsaidia
kutambua kuwa mwingine si kama ambavyo angalimtaka yeye,[382] na kumsaidia kuacha
kutarajia kutoka kwake mambo yaliyo ya pekee ya upendo wa Mungu tu. Hayo yanadai mtu
ajinyenyekeze kwa ndani. Nafasi ya pekee ambayo kila mwenzi wa ndoa huitenga kwa ajili ya
uhusiano wake wa binafsi na Mungu, haisaidii tu majeraha ya maisha ya pamoja yaponywe, bali
pia inawawezesha wenzi wa ndoa kuona maana ya maisha yao katika upendo wa Mungu.
Tunahitaji kuomba kila siku Roho Mtakatifu atende kazi ili tupate kuwa na uhuru huu wa ndani.
Tasaufi ya kujali, kufariji na kuhamasisha
321. “Wanandoa wakristo ni washiriki wa neema na mashahidi wa imani, mwenzi mmoja kwa
mwenzie, kwa watoto wao na kwa jamaa zao wengine wote”.[383] Mungu anawaita kuzaa na
kutunza. Ndiyo sababu familia “imekuwa ni daima ’hospitali’ iliyo jirani zaidi”.[384] Tutunzane,
tutegemezane, tuhamasishane, na tufikirie hayo yote kama sehemu ya maisha yetu ya kiroho
katika familia. Maisha ya pamoja ya jozi ni kushiriki tendo lenye kuzaa la Mungu; na kila mwenzi ni
kwa mwenzie kichocheo cha kudumu cha Roho. Upendo wa Mungu unadhihirika “kupitia maneno
hai na halisi ambayo kwayo mume na mke wanaambiana upendo wao wa kindoa”.[385] Hivyo,
hao wawili, kila mmoja kwa mwenzie, ni kama kioo cha upendo wa kimungu unaofariji kwa neno,
kwa mtazamo au mguso wa mapendo, kwa kusaidia na kwa kukumbatia. Kwa hiyo, “kutaka
kuunda familia ni kuwa na ushujaa wa kushiriki ndoto ya Mungu, ushujaa ya kuota ndoto pamoja
naye, ushujaa wa kujenga pamoja naye, ushujaa wa kujishughulisha pamoja naye katika maisha

11.7 Page 107

▲back to top
107
haya, wa kujenga ulimwengu ambapo hakuna mtu anayejisikia peke yake”.[386]
322. Maisha yote ya familia ni kama “malisho” ya huruma. Kila mwenzi “anachora” na “anaandika”
kwa mapendo katika maisha ya mwenzie. “Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu
[...] si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai” (taz. 2Kor 3:2.3). Kila mtu ni “mvuvi wa watu”
(taz. Mt 4:19) ambaye “anawashushia wengine nyavu” (taz. Lk 5:5) kwa jina la Yesu, au mkulima
anayelima ardhi yenye rutuba, yaani wapendwa wake, kwa kustawisha mambo bora waliyo nayo.
Ndoa kuzaa matunda ni jambo linalotegemea kazi ya kustawisha, kwa sababu “kumpenda mtu ni
kutarajia toka kwake mambo yasiyotabirika wala kupangika, na wakati huohuo ni kwa namna
fulani kumwezesha atimize matarajio hayo”.[387] Nayo ni ibada kwa Mungu, kwa sababu yeye
ndiye aliyepanda mambo mema mengi ndani ya wengine; naye anatumaini kwamba sisi
tutayakuza.
323. Kumtazama mtu mpendwa kwa macho ya Mungu, na kumtambua Kristo katika yeye, ni
mang’amuzi ya kiroho ya kina. Hayo yanadai kuwa tayari kujitolea kwa hiari, na hivyo kuthamini
hadhi yake. Unaweza kuwa na mahusiano makamilifu na mwenzio endapo tu unajitolea bila
kutafuta sababu, na kusahau mambo mengine yote yanayokuzunguka. Mpenzi wako anastahili
wewe umjali kwa nafsi yako yote. Yesu ni mfano, kwa sababu, mtu alipomkaribia aongee naye,
yeye alikuwa anamkazia macho na kumwangalia kwa upendo (taz. Mk 10:21). Mbele ya Yesu,
hapakuwa na mtu aliyejisikia amesahauliwa, kwa sababu maneno yake na vitendo vyake vilikuwa
vikidokeza swali hili, “Wataka nikufanyie nini?” (Mk 10:51). Nalo ndilo tunaloonja katika maisha ya
kila siku ya familia. Katika familia twakumbuka kwamba mtu anayeishi pamoja nasi anastahili yote,
kwa sababu hadhi yake haina mipaka, kwa kuwa Mungu anampenda kwa upendo usiopimika.
Hivyo, upendo mwororo unastawi, ulio na nguvu ya “kuamsha moyoni mwa mwenzi furaha ya
kujisikia mtu mwenye kupendwa. Upendo mwororo hudhihirika kwa namna ya pekee mmoja
anapogeuka kuangalia kwa hisani mapungufu ya mwingine, hasa yanapoibuka wazi”.[388]
324. Kwa msukumo wa Roho, familia haiwapokei tu watoto ndani yake kwa kuwazaa, bali pia
inafungua milango yake, inatoka nje ya mazingira yake ili kuwagawia wengine wema wake,
kuwajali na kuwasaidia wawe na furaha. Huko kufungua milango yake kunaonyeshwa hasa kwa
kukaribisha,[389] kama linavyohamasisha Neno la Mungu kwa namna nzuri, “Msisahau
kuwafadhili wageni; kwa maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika bila kujua” (Ebr
13:2). Familia inapowakaribisha na iko tayari kuwasaidia wengine, hasa watu maskini na
waliotelekezwa, inakuwa ni “ishara na ushuhuda wa umama wa Kanisa, na inaushiriki nalo.”[390]
Upendo wa kijamii, ulio kioo cha Utatu Mtakatifu, ndio unaounganisha maana ya kiroho ya familia
na utume ambao familia hutoa nje yake, kwa sababu upendo huo hutimiza “kerigma” na sharti
zake za kijumuiya. Familia huishi tasaufi yake maalumu huku ikiwa, wakati huohuo, Kanisa la
nyumbani na chembe hai ya kugeuza ulimwengu.[391]
****

11.8 Page 108

▲back to top
108
325. Maneno ya Yesu, Mwalimu wetu (taz. Mt 22:30), na yale ya mtakatifu Paulo kuhusu ndoa
(taz. 1Kor 7:29-31), – kwa kusudi maalumu – yanahusianishwa na kweli ya mwisho na ya kudumu
ya kuishi kwetu, ambayo tunahitaji kurudi kuizingatia. Hivyo, wanandoa wataweza kuitambua
maana ya kweli ya mwendo wao. Kwani, kama tulivyokumbuka mara nyingi katika Wosia huu,
hakuna familia iliyo timilifu na kuwekwa tayari kabisa, bali kila familia inahitaji kukuza kwa
utaratibu uwezo wake wa kupenda. Pana wito endelevu unaotokana na ushirika kamili wa Utatu
Mtakatifu, na umoja wa ajabu wa Kristo na Kanisa lake, na jumuiya nzuri sana ile iliyo familia ya
Nazareti, na undugu usio na doa wa watakatifu wa mbinguni. Kutazama ukamilifu ambao
hatujaupata bado, kunatufanya tuangalie mwendo wetu wa kifamilia katika maisha haya kwa
mtazamo wenye uwiano, ili tuache kudai kwamba katika mahusiano kati ya watu pawepo utimilifu,
usafi wa nia na msimamo thabiti vitakavyopatikana tu katika Ufalme wa milele. Tena, kunatuzuia
tusihukumu kwa ukali watu wale wanaoishi katika hali ya udhaifu mkubwa wa kiroho. Tunaitwa
sote kuendelea kuelekeza mioyo yetu kwenye mambo yanayopita nafsi zetu wenyewe na
mapungufu yetu; na kila familia inapaswa kuishi kulingana na msukumo endelevu huu. Enyi
familia, tusonge mbele, naam, tuzidi kusonga mbele! Mambo tuliyoahidiwa yapita daima fikra zetu.
Tusikate tamaa kwa sababu ya mapungufu yetu; lakini pia tusiache kutafuta utimilifu wa upendo
na wa ushirika tulioahidiwa.
Sala kwa Familia Takatifu
Yesu, Maria na Yosefu,
katika ninyi tunatazama
mwangaza wa upendo wa kweli;
tunajikabidhi kwenu tukiwategemea.
Familia Takatifu ya Nazareti,
zifanye familia zetu pia ziwe
mahali pa kushirikiana, na nyumba za sala,
shule halisi za Injili
na Makanisa madogo ya nyumbani.
Familia Takatifu ya Nazareti,
katika familia visiwepo tena
visa vya ukatili, unyanyapaa, matengano;
mtu yeyote aliyejeruhiwa rohoni au kukashifiwa
afarijiwe na kuponywa mara.
Familia Takatifu ya Nazareti,
utujalie tutambue sote
tabia ya wakfu na isiyodhurika ya familia,
na uzuri wake katika mpango wa Mungu.

11.9 Page 109

▲back to top
109
Yesu, Maria na Yosefu,
mtusikie na kupokea dua yetu.
Amina.
Imetolewa Roma, penye kanisa la Mtakatifu Petro, katika Jubilei isiyo ya kawaida ya Huruma,
tarehe 19 ya mwezi wa Machi, sherehe ya Mtakatifu Yosefu, ya mwaka 2016, wa nne wa Upapa
wangu.
Fransisko
[1] Mkutano wa Dharura wa Tatu wa Sinodi ya Maaskofu, Relatio Synodi, 18 Oktoba 2014, 2.
[2] Mkutano wa Kawaida wa Kumi na Nne wa Sinodi ya Maaskofu, Relatio finalis, 24 Oktoba 2015,
3.
[3] Hotuba ya kuuhitimisha Mkutano wa Kawaida wa Kumi na Nne wa Sinodi ya Maaskofu (24
Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 26-27 Oktoba 2015, uk. 13; taz. Tume ya Kipapa ya Biblia,
Imani na utamaduni katika mwanga wa Biblia. Hati za Kikao cha jumla cha mwaka 1979 cha Tume
ya Kipapa ya Biblia, Turin, 1981; Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et
Spes, 44; Yohane Paulo II, Waraka Ensiklika Redemptoris Missio (7 Desemba 1990), 52; AAS 83
(1991), 300; Wosia wa Kitume Evangelii gaudium (24 Novemba 2013), 69, 117: AAS 105 (2013),
1049, 1068-1069.
[4] Hotuba katika mkutano wa familia uliofanyika huko Santiago wa Cuba (22 Septemba 2015):
L’Osservatore Romano, 24 Septemba 2015, uk. 7.
[5] Jorge Luis Borges, “Calle desconocida”, katika Fervor de Buenos Aires, Buenos Aires 2011,
23.
[6] Homilia katika Misa huko Puebla de los Ángeles (28 Januari 1979), 2: AAS 71 (1979), 184.
[7] Taz. ilivyotangulia.
[8] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 4: AAS 74 (1982),
84.

11.10 Page 110

▲back to top
110
[9] Relatio Synodi 2014, 5.
[10] Baraza la Maaskofu la Uhispania, Matrimonio y familia (6 Julai 1979), 3, 16, 23.
[11] Relatio finalis 2015, 5.
[12] Relatio Synodi 2014, 5.
[13] Relatio finalis 2015, 8.
[14] Hotuba kwenye Bunge la Marekani (24 Septemba 2015): L’Osservatore Romano, 26
Septemba 2015, uk. 7.
[15] Relatio finalis 2015, 29.
[16] Relatio Synodi 2014, 10.
[17] Mkutano wa Dharura wa Tatu wa Sinodi ya Maaskofu, Ujumbe, 18 Oktoba 2014.
[18] Relatio Synodi 2014, 10.
[19] Relatio finalis 2015, 7.
[20] Taz. ilivyotangulia, 63.
[21] Baraza la Maaskofu la Korea, Towards a culture of life! – Kuelekea utamaduni wa uhai! (15
Machi 2007).
[22] Relatio Synodi 2014, 6.
[23] Baraza la Kipapa la Familia, Hati ya haki za familia (22 Oktoba 1983), 11.
[24] Taz. Relatio finalis 2015, 11-12.
[25] Baraza la Kipapa la Familia, Hati ya haki za familia (22 Oktoba 1983), Utangulizi.
[26] Taz. ilivyotangulia, 9.
[27] Relatio finalis 2015, 14.
[28] Relatio Synodi 2014, 8.

12 Pages 111-120

▲back to top

12.1 Page 111

▲back to top
111
[29] Taz. Relatio finalis 2015, 78.
[30] Relatio Synodi 2014, 8.
[31] Relatio finalis 2015, 23; taz. Ujumbe kwa Siku ya Dunia kwa ajili ya Wahamiaji na Wakimbizi
2016 (12 Septemba 2015): L’Osservatore Romano, 2 Septemba 2015, uk. 8.
[32] Relatio finalis 2015, 24;
[33] Taz. ilivyotangulia, 21.
[34] Taz. ilivyotangulia, 17.
[35] Taz. ilivyotangulia, 20.
[36] Taz. kama ilivyotangulia, 15.
[37] Hotuba ya kuuhitimisha Mkutano wa Kawaida wa Kumi na Nne wa Sinodi ya Maaskofu (24
Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 26-27 Septemba 2015, uk. 13.
[38] Baraza la Maaskofu la Argentina, Navega mar adentro (31 Mei 2003), 42.
[39] Baraza la Maaskofu la Meksiko, Que en Cristo Nuestra Paz México tenga vida digna (15
Februari 2009), 67.
[40] Relatio finalis 2015, 25.
[41] Taz. ilivyotangulia, 10.
[42] Katekesi (22 Aprili 2015): L’Osservatore Romano, 23 Aprili 2015, uk. 7.
[43] Katekesi (29 Aprili 2015): L’Osservatore Romano, 30 Aprili 2015, uk. 8.
[44] Relatio finalis 2015, 28.
[45] Taz. ilivyotangulia, 8.
[46] Taz. ilivyotangulia, 58.
[47] Taz. ilivyotangulia, 33.
[48] Relatio Synodi 2014, 11.

12.2 Page 112

▲back to top
112
[49] Baraza la Maaskofu la Kolumbia, A tiempos difíciles, colombianos nuevos (13 Februari 2003),
3.
[50] Wosia wa Kitume Evangelii gaudium (24 Novemba 2013), 69, 117: AAS 105 (2013), 1049,
1068-1069.
[51] Taz. ilivyotangulia, 164: AAS 105 (2013), 1088.
[52] Taz. ilivyotangulia.
[53] Taz. ilivyotangulia, 165: AAS 105 (2013), 1089.
[54] Relatio Synodi 2014, 12.
[55] Taz. ilivyotangulia, 14.
[56] Taz. ilivyotangulia, 16.
[57] Relatio finalis 2015, 41.
[58] Taz. ilivyotangulia, 38.
[59] Relatio Synodi 2014, 17.
[60] Relatio finalis 2015, 43.
[61] Relatio Synodi 2014, 18.
[62] Taz. ilivyotangulia, 19.
[63] Relatio finalis 2015, 38.
[64] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 13: AAS 74
(1982), 94.
[65] Relatio Synodi 2014, 21.
[66] Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 1642.
[67] Taz. ilivyotangulia.
[68] Katekesi (6 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 7 Mei 2015, uk. 8.

12.3 Page 113

▲back to top
113
[69] Leo Mkuu, Epistola Rustico narbonensi episcopo, inquis. IV: PL 54, 1205A; taz. Inkmaro wa
Reims, Waraka 22: PL 126, 142.
[70] Taz. Pius XII, Waraka Ensiklika Mystici Corporis Christi (29 Juni 1943): AAS 35 (1943), 202:
“Kwenye [sakramenti ya] Ndoa kila mmoja wa wana harusi ni mhudumu wa neema kwa ajili ya
mwenzie”.
[71] Taz. Mkusanyo wa Sheria Kanoni, kann. 1116; 1161-1165; Mkusanyo wa Kanoni za
Makanisa ya Mashariki, 832; 848-852.
[72] Mkusanyo wa Sheria Kanoni, kan. 1055 § 2.
[73] Relatio Synodi 2014, 23.
[74] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 9: AAS 74
(1982), 90.
[75] Relatio finalis 2015, 47.
[76] Taz. ilivyotangulia.
[77] Homilia katika Misa ya kuhitimisha Mkutano wa Nane wa Dunia wa familia, Philadelphia (27
Septemba 2015): L’Osservatore Romano, 28-29 Septemba 2015, uk. 7.
[78] Relatio finalis 2015, 53-54.
[79] Taz. ilivyotangulia, 51.
[80] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 48.
[81] Mkusanyo wa Sheria Kanoni, kan. 1055 § 1: “imewekwa kwa ajili ya mema ya wanandoa na
ya uzazi na malezi ya watoto”.
[82] Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2360.
[83] Taz. ilivyotangulia, 1654.
[84] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 48.
[85] Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2366.
[86] Taz. Paulo VI, Waraka Ensiklika Humanae vitae (25 Julai 1968), 11-12: AAS 60 (1968), 488-

12.4 Page 114

▲back to top
114
489.
[87] Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2378.
[88] Idara Takatifu ya Mafundisho ya Imani, Maelek. Donum vitae (22 Februari 1987), II, 8: AAS 80
(1988), 97.
[89] Relatio finalis 2015, 63.
[90] Relatio Synodi 2014, 57.
[91] Taz. ilivyotangulia, 58.
[92] Taz. ilivyotangulia, 57.
[93] Relatio finalis 2015, 64.
[94] Relatio Synodi 2014, 60.
[95] Taz. ilivyotangulia, 61.
[96] Mkusanyo wa Sheria Kanoni, kan. 1136; taz. Mkusanyo wa Kanoni za Makanisa ya Mashariki,
627.
[97] Baraza la Kipapa la Familia, Ujinsia wa binadamu: ukweli na maana yake (8 Desemba 1995),
23.
[98] Katekesi (20 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 21 Mei 2015, uk. 8.
[99] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 38: AAS 74
(1982), 129.
[100] Taz. Hotuba kwenye Mkutano wa kijimbo huko Roma (14 Juni 2015): L’Osservatore
Romano, 15-16 Juni 2015, uk. 8.
[101] Relatio Synodi 2014, 23.
[102] Relatio finalis 2015, 52.
[103] Taz. ilivyotangulia, 49-50.
[104] Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 1641.

12.5 Page 115

▲back to top
115
[105] Taz. Benedikto XVI, Waraka Ensiklika Deus caritas est (25 Desemba 2005), 2: AAS 98
(2006), 218.
[106] Mazoezi ya kiroho, Taamuli kwa ajili ya kupata upendo, 230.
[107] Octavio Paz, La llama doble, Barcelona 1993, 35.
[108] Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae II-II, q. 114, a. 2, ad 1.
[109] Katekesi (13 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 14 Mei 2015, uk. 8.
[110] Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae II-II, q. 27, a. 1, ad 2.
[111] Taz. ilivyotangulia, a. 1.
[112] Katekesi (13 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 14 Mei 2015, uk. 8.
[113] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 21: AAS 74
(1982), 106.
[114] Hotuba iliyotolewa kwenye Kanisa la Kibaptisti la Dexter Avenue, Montgomery, Alabama, 17
Novemba 1957.
[115] Mt. Tomaso wa Akwino anatambua upendo kama “nguvu inayounganisha” (Summa
Theologiae I, q. 20, a. 1, ad 3), akinukulu usemi liotumia kwanza Dionigi Ps.-Areopagita (De
divinis nominibus, IV, 12: PG 3, 709).
[116] Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae II-II, q. 27, a. 2.
[117] Waraka Ensiklika Casti connubii (31 Desemba 1930): AAS 22 (1930), 547-548.
[118] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 13: AAS 74
(1982), 94.
[119] Katekesi (2 Aprili 2014): L’Osservatore Romano, 3 Aprili 2014, uk. 8.
[120] Taz. ilivyotangulia.
[121] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 9: AAS 74
(1982), 90.
[122] Tomaso wa Akwino, Summa contra Gentiles, III, 123; taz. Aristotele, Etica Nic., 8, 12 (ed.

12.6 Page 116

▲back to top
116
Bywater, Oxford 1984, 174).
[123] Waraka Ensiklika Lumen Fidei (29 Juni 2013), 52: AAS 105 (2013), 590.
[124] De sacramento matrimonii, I, 2: in Id. Disputationes, III, 5, 3 (ed. Giuliano, Napoli 1858, 778).
[125] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 50.
[126] Taz. ilivyotangulia, 49.
[127] Taz. Summa Theologiae I-II, q. 31, a. 3, ad 3.
[128] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 48.
[129] Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae I-II, q. 26, a. 3.
[130] Taz. ilivyotangulia, q. 10, a. 1.
[131] Maungamo, VIII, 3, 7: PL 32, 752.
[132] Hotuba kwa familia za dunia nzima kwenye hija yao huko Roma katika Mwaka wa Imani (26
Oktoba 2013): AAS 105 (2013), 980.
[133] Malaika wa Bwana (29 Desemba 2013): L’Osservatore Romano, 30-31 Desemba 2013, uk.
7.
[134] Hotuba kwa familia za dunia nzima kwenye hija yao huko Roma katika Mwaka wa Imani (26
Oktoba 2013): AAS 105 (2013), 978.
[135] Summa Theologiae II-II, q. 24, a. 7.
[136] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 48.
[137] Baraza la Maaskofu la Chile, La vida y la familia: regalos de Dios para cada uno de nosotros
(21 Julai 2014).
[138] Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 49.
[139] A. Sertillanges, L’amour chrétien, Paris 1920, 174.
[140] Taz. Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae I-II, q. 24, a. 1.

12.7 Page 117

▲back to top
117
[141] Taz. ilivyotangulia, q. 59, a. 5.
[142] Waraka Ensiklika Deus caritas est (25 Desemba 2005), 3: AAS 98 (2006), 219-220.
[143] Taz. ilivyotangulia, 4 : AAS 98 (2006), 220.
[144] Taz. Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae I-II, q. 32, a. 7.
[145] Taz. ilivyotangulia, II-II, q. 153, a. 2, ad 2: “Utele wa furaha uliopo katika tendo la kujamiiana
linalofanyika kadiri ya akili, haukinzani na utaratibu wa kiasi wa fadhila”.
[146] Yohane Paulo II, Katekesi (22 Oktoba 1980), 5: Mafundisho III, 2 (1980), 951.
[147] Taz. ilivyotangulia, 3.
[148] Yohane Paulo II, Katekesi (24 Septemba 1980), 4: Mafundisho III, 2 (1980), 719.
[149] Katekesi (12 Novemba 1980), 2: Mafundisho III, 2 (1980), 1133.
[150] Taz. ilivyotangulia, 4.
[151] Taz. ilivyotangulia, 5.
[152] Taz. ilivyotangulia, 1: 1132.
[153] Katekesi (16 Januari 1980), 1: Mafundisho III, 1 (1980), 151.
[154] Josef Pieper, Über die Liebe, München 2014, 174.
[155] Yohane Paulo II, Waraka Insiklika Evangelium vitae (25 Machi 1995), 23: AAS 87 (1995),
427.
[156] Taz. Paulo VI, Waraka Insiklika Humanae vitae (25 Julai 1968), 13: AAS 60 (1968), 489.
[157] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 49.
[158] Katekesi (18 Juni 1980), 5: Mafundisho III, 1 (1980), 1778.
[159] Taz. ilivyotangulia, 6.
[160] Taz. Katekesi (30 Julai 1980), 1: Mafundisho III, 2 (1980), 311.

12.8 Page 118

▲back to top
118
[161] Katekesi (8 Aprili 1981), 3: Mafundisho IV, 1 (1981), 904.
[162] Katekesi (11 Agosti 1982), 4: Mafundisho V, 3 (1982), 205-206.
[163] Waraka Ensiklika Deus caritas est (25 Desemba 2005), 5: AAS 98 (2006), 221.
[164] Taz. ilivyotangulia, 7.
[165] Relatio finalis 2015, 22.
[166] Katekesi (14 Aprili 1982), 1: Mafundisho V, 1 (1982), 1176.
[167] Glossa in quatuor libros sententiarum Petri Lombardi, IV, XXVI, 2 (Quaracchi 1957, 446).
[168] Yohane Paulo II, Katekesi (7 Aprili 1982), 2: Mafundisho V, 1 (1982), 1127.
[169] Kama ilivyotangulia, Katekesi (14 Aprili 1982), 3: Mafundisho V, 1 (1982), 1177.
[170] Taz. ilivyotangulia.
[171] Yohane Paulo II, Waraka Ensiklika Redemptor hominis (4 Machi 1979), 10: AAS 71 (1979),
274.
[172] Taz. Tomaso wa Akwino, Summa Theologiae II-II, q. 27, a. 1.
[173] Baraza la Kipapa la Familia, Familia, ndoa na “miungano isiyo rasmi” (26 Julai 2000), 40.
[174] Yohane Paulo II, Katekesi (31 Oktoba 1984), 6: Mafundisho VII, 2 (1984), 1072.
[175] Benedikto XVI, Waraka Ensiklika Deus caritas est (25 Desemba 2005), 8: AAS 98 (2006),
224.
[176] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 14: AAS 74
(1982), 96.
[177] Katekesi (11 Februari 2015): L’Osservatore Romano, 12 Februari 2015, uk. 8.
[178] Taz. ilivyotangulia.
[179] Katekesi (8 Aprili 2015): L’Osservatore Romano, 9 Aprili 2015, uk. 8.
[180] Taz. ilivyotangulia.

12.9 Page 119

▲back to top
119
[181] Taz. Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 51: Ni “wazi
kwa wote kwamba uhai wa binadamu na jukumu la kuuendeleza uhai huo havifungwi katika
mipaka ya maisha ya hapa duniani, wala haviwezi kupimwa na kueleweka katika ulimwengu huu
tu, bali vinahusu daima kikomo cha milele cha wanadamu.”
[182] Waraka kwa Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu na
Maendeleo (18 Machi 1994): Mafundisho XVII, 1 (1994), 750-751.
[183] Yohane Paulo II, Katekesi (12 Machi 1980), 3: Mafundisho III, 1 (1980), 543.
[184] Taz. ilivyotangulia.
[185] Hotuba katika mkutano wa familia uliofanyika huko Manila (16 Januari 2015): AAS 107
(2015), 176.
[186] Katekesi (11 Februari 2015): L’Osservatore Romano, 12 Februari 2015, uk. 8.
[187] Katekesi (14 Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 15 Oktoba 2015, uk. 8.
[188] Baraza la Maaskofu Katoliki la Australia, Waraka wa kichungaji Don’t Mess with Marriage
(24 Novemba 2015), 11.
[189] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 50.
[190] Yohane Paulo II, Katekesi (12 Machi 1980), 2: Mafundisho III, 1 (1980), 542.
[191] Taz. Yohane Paulo II, Waraka wa kitume Mulieris dignitatem (15 Agosti 1988), 30-31: AAS
80 (1988), 1727-1729.
[192] Katekesi (7 Januari 2015):L’Osservatore Romano, 7-8 Januari 2015, uk. 8.
[193] Taz. ilivyotangulia.
[194] Katekesi (28 Januari 2015): L’Osservatore Romano, 29 Januari 2015, uk. 8.
[195] Taz. ilivyotangulia.
[196] Taz. Relatio finalis 2015, 28.
[197] Katekesi (4 Februari 2015): L’Osservatore Romano, 5 Februari 2015, uk. 8.
[198] Taz. ilivyotangulia.

12.10 Page 120

▲back to top
120
[199] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 50.
[200] Kongamano la Tano la Maaskofu wa Marekani ya Kusini na Kati na Karaibi, Hati ya
Aparecida (29 Juni 2007), 457.
[201] Relatio finalis 2015, 65.
[202] Taz. ilivyotangulia.
[203] Hotuba katika mkutano wa familia uliofanyika huko Manila (16 Januari 2015):AAS 107
(2015), 178.
[204] Mario Benedetti, “Te quiero”, in Poemas de otros, Buenos Aires 1993, 316: “Tus manos son
mi caricia / mis acordes cotidianos / te quiero porque tus manos / trabajan por la justicia. / Si te
quiero es porque sos / mi amor mi cómplice y todo / y en la calle codo a codo / somos mucho más
que dos”.
[205] Taz. Katekesi (16 Septemba 2015): L’Osservatore Romano, 17 Septemba 2015, uk. 8.
[206] Katekesi (7 Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 8 Oktoba 2015, uk. 8.
[207] Benedikto XVI, Waraka Ensiklika Deus caritas est (25 Desemba 2005), 14: AAS 98 (2006),
228.
[208] Taz. Relatio finalis 2015, 11.
[209] Katekesi (18 Machi 2015): L’Osservatore Romano, 19 Machi 2015, uk. 8.
[210] Katekesi (11 Februari 2015): L’Osservatore Romano, 12 Februari 2015, uk. 8.
[211] Taz. Relatio finalis 2015, 17-18.
[212] Katekesi (4 Machi 2015): L’Osservatore Romano, 5 Machi 2015, uk. 8.
[213] Katekesi (11 Machi 2015): L’Osservatore Romano, 12 Machi 2015, uk. 8.
[214] Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 27: AAS 74 (1982), 113.
[215] Yohane Paulo II, Hotuba kwa walioshiriki kwenye Jukwaa la kimataifa kuhusu kuzeeka hai (5
Septemba 1980), 5: Mafundisho III, 2 (1980), 539.
[216] Relatio finalis 2015, 18.

13 Pages 121-130

▲back to top

13.1 Page 121

▲back to top
121
[217] Katekesi (4 Machi 2015): L’Osservatore Romano, 5 Machi 2015, uk. 8.
[218] Taz. ilivyotangulia.
[219] Hotuba katika mkutano pamoja na wazee (28 Septemba 2014): L’Osservatore Romano, 29-
30 Septemba 2014, uk. 7.
[220] Katekesi (18 Februari 2015): L’Osservatore Romano, 19 Februari 2015, uk. 8.
[221] Taz. ilivyotangulia.
[222] Taz. ilivyotangulia.
[223] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 18: AAS 74
(1982), 101.
[224] Katekesi (7 Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 8 Oktoba 2015, uk. 8.
[225] Relatio Synodi 2014, 30.
[226] Taz. ilivyotangulia, 31.
[227] Relatio finalis 2015, 56.
[228] Taz. ilivyotangulia, 89.
[229] Relatio Synodi 2014, 32.
[230] Taz. ilivyotangulia, 33.
[231] Taz. ilivyotangulia, 38.
[232] Relatio finalis 2015, 77.
[233] Taz. ilivyotangulia, 61.
[234] Taz. ilivyotangulia.
[235] Taz. ilivyotangulia.
[236] Taz. ilivyotangulia.

13.2 Page 122

▲back to top
122
[237] Taz. Relatio Synodi 2014, 26.
[238] Taz. ilivyotangulia, 39.
[239] Baraza la Maaskofu la Italia. Tume ya Kiaskofu kwa ajili ya familia na uhai, Maelekezo ya
kichungaji kuhusu maandalizi kabla ya ndoa na kuunda familia (22 Oktoba 2012), 1.
[240] Ignasi wa Loyola, Mazoezi wa kiroho, maelezo na. 2.
[241] Taz. ilivyotangulia, na. 5.
[242] Yohane Paulo II, Katekesi (27 Juni 1984), 4: Mafundisho VII, 1 (1984), 1941.
[243] Katekesi (21 Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 22 Oktoba 2015, uk. 12.
[244] Baraza la Maaskofu la Kenya, Ujumbe wa Kwaresima (18 Februari 2015).
[245] Taz. Pius XI, Waraka Ensiklika Casti connubii (31 Desemba 1930): AAS 22 (1930), 583.
[246] Yohane Paulo II, Katekesi (4 Julai 1984), 3.6: Mafundisho VII, 2 (1984), 9.10.
[247] Relatio finalis 2015, 59.
[248] Taz. ilivyotangulia, 63.
[249] Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 50.
[250] Relatio finalis 2015, 63.
[251] Relatio Synodi 2014, 40.
[252] Taz. ilivyotangulia, 34.
[253] Cántico Espiritual, B, XXV, 11.
[254] Relatio Synodi 2014, 44.
[255] Relatio finalis 2015, 81.
[256] Taz. ilivyotangulia, 78.
[257] Katekesi (24 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 25 Juni 2015, uk. 8.

13.3 Page 123

▲back to top
123
[258] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 83: AAS 74
(1982), 184.
[259] Relatio Synodi 2014, 47.
[260] Taz. ilivyotangulia, 50.
[261] Taz. Katekesi (5 Agosti 2015): L’Osservatore Romano, 6 Agosti 2015, uk. 7.
[262] Relatio Synodi 2014, 51; taz. Relatio finalis 2015, 84.
[263] Relatio Synodi 2014, 48.
[264] Taz. Motu proprio Mitis Iudex Dominus Iesus (15 Agosti 2015): L’Osservatore Romano, 9
Septemba 2015, uk. 3-4; Motu proprio Mitis et Misericors Iesus (15 Agosti 2015): L’Osservatore
Romano, 9 Septemba 2015, uk. 5-6.
[265] Motu proprio Mitis Iudex Dominus Iesus (15 Agosti 2015), Dibaji, III: L’Osservatore Romano,
9 Septemba 2015, uk. 3.
[266] Relatio finalis 2015, 82.
[267] Relatio Synodi 2014, 47.
[268] Katekesi (20 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 21 Mei 2015, uk. 8.
[269] Katekesi (24 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 25 Juni 2015, uk. 8.
[270] Taz. Katekesi (5 Agosti 2015): L’Osservatore Romano, 6 Agosti 2015, uk. 7.
[271] Relatio finalis 2015, 72.
[272] Taz. ilivyotangulia, 73.
[273] Taz. ilivyotangulia, 74.
[274] Taz. ilivyotangulia, 75.
[275] Taz. Bula Uso wa Huruma (Misericordiae Vultus), 12: AAS 107 (2015), 409.
[276] Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2358; taz. Relatio finalis 2015, 76.

13.4 Page 124

▲back to top
124
[277] Taz. kama iliyotangulia.
[278] Relatio finalis 2015, 76; taz. Idara Takatifu ya Mafundisho ya Imani, Tafakari kuhusu
mipango ya kutambua kisheria muungano wa watu wa jinsia moja (3 Juni 2003), 4.
[279] Relatio finalis 2015, 80.
[280] Taz. kama ilivyotangulia, 20.
[281] Katekesi (17 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 18 Juni 2015, uk. 8.
[282] Relatio finalis 2015, 19.
[283] Katekesi (17 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 18 Juni 2015, uk. 8.
[284] Taz. ilivyotangulia.
[285] Taz. Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 958.
[286] Taz. ilivyotangulia.
[287] Taz. Maneno ya mwisho, “Daftari ya njano” ya Mama Mkuu Agnesi, 17 Julai 1897: Opere
complete, Città del Vaticano - Roma 1997, 1028. Kuhusu hilo, ni muhimu ushuhuda waliotoa
masista wenzake kuhusu ahadi ya mtakatifu Teresa kwamba kufariki kwake dunia hii kutakuwa
kama “mvua ya waridi” (taz. ilivyotangulia, 9 Juni, 991).
[288] Yordani wa Saksonia, Libellus de principiis Ordinis prædicatorum, 93: Monumenta Historica
Sancti Patris Nostri Dominici, XVI, Roma 1935, 69.
[289] Taz. Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 957.
[290] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kidogma Lumen Gentium, 49.
[291] Wosia wa Kitume Evangelii gaudium (24 Novemba 2013), 222: AAS 105 (2013), 1111.
[292] Katekesi (20 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 21 Mei 2015, uk. 8.
[293] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 17.
[294] Katekesi (30 Septemba 2015): L’Osservatore Romano, 1 Oktoba 2015, uk. 8.
[295] Katekesi (10 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 11 Juni 2015, uk. 8.

13.5 Page 125

▲back to top
125
[296] Taz. Relatio finalis 2015, 67.
[297] Katekesi (20 Mei 2015): L’Osservatore Romano, 21 Mei 2015, uk. 8.
[298] Katekesi (9 Septemba 2015): L’Osservatore Romano, 10 Septemba 2015, uk. 8.
[299] Relatio finalis 2015, 68.
[300] Taz. ilivyotangulia, 58.
[301] Tamko Gravissimum educationis, 1.
[302] Relatio finalis 2015, 56.
[303] Erich Fromm, The Art of Loving, New York 1956, uk. 54.
[304] Waraka Ensiklika Laudato si’ (24 Mei 2015), 155.
[305] Katekesi (15 Aprili 2015): L’Osservatore Romano, 16 Aprili 2015, uk. 8.
[306] Taz. Relatio finalis 2015, 13-14.
[307] De sancta virginitate, 7, 7: PL 40, 400.
[308] Taz. Katekesi (26 Agosti 2015): L’Osservatore Romano, 27 Agosti 2015, uk. 8.
[309] Relatio finalis 2015, 89.
[310] Taz. ilivyotangulia, 93.
[311] Relatio Synodi 2014, 24.
[312] Taz. ilivyotangulia, 25.
[313] Taz. ilivyotangulia, 28.
[314] Taz. ilivyotangulia, 41.43; Relatio finalis 2015, 70.
[315] Relatio Synodi 2014, 27.
[316] Taz. ilivyotangulia, 26.

13.6 Page 126

▲back to top
126
[317] Taz. ilivyotangulia, 41.
[318] Taz. ilivyotangulia.
[319] Relatio finalis 2015, 71.
[320] Taz. kama iliyotangulia.
[321] Relatio Synodi 2014, 42.
[322] Taz. ilivyotangulia, 43.
[323] Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 34: AAS 74 (1982), 123.
[324] Taz. ilivyotangulia, 9: 90.
[325] Katekesi (24 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 25 Juni 2015, uk. 8.
[326] Homilia katika Misa iliyoadhimishwa pamoja na Makardinali wapya (15 Februari 2015): AAS
107 (2015), 257.
[327] Relatio finalis 2015, 51.
[328] Relatio Synodi 2014, 25.
[329] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 84: AAS 74
(1982), 186. Katika hali kama hizi, wengi, wakijua na kuukubali uwezekano wa kuishi pamoja
kama “kaka na dada”, ambao Kanisa linaruhusu, wanagundua kwamba, ikiwa vitendo fulani vya
upendo wa ndani vinakosekana, “mara nyingi uaminifu huhatarishwa, na manufaa ya watoto
huathirika” (Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 51).
[330] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 84: AAS 74
(1982), 186.
[331] Relatio Synodi 2014, 26.
[332] Taz. ilivyotangulia, 45.
[333] Benedikto XVI, Hotuba kwenye Mkutano wa Saba wa Dunia wa familia, Milan (2 Juni 2012),
jibu na. 5: Mafundisho VIII, 1 (2012), 691.
[334] Relatio finalis 2015, 84.

13.7 Page 127

▲back to top
127
[335] Taz. ilivyotangulia, 51.
[336] Wala kwa yale yanayohusu nidhamu ya kisakramenti, kwa vile upambanuzi unavyoweza
kugundua kwamba katika kadhia mahususi hakuna hatia nzito. Hapa lifuatwe nililotamka katika
hati nyingine: taz. Wosia wa Kitume Evangelii gaudium (24 Novemba 2013), 44, 47: AAS 105
(2013), 1038, 1040.
[337] Relatio finalis 2015, 85.
[338] Taz. ilivyotangulia, 86.
[339] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 33: AAS 74
(1982), 121.
[340] Relatio finalis 2015, 51.
[341] Taz. Summa Theologiae II-II, q. 65, a. 3, ad 2; De malo, q. 2, a. 2.
[342] Taz. ilivyotangulia, ad 3.
[343] Na. 1735.
[344] Taz. ilivyotangulia, 2352; Idara Takatifu ya Mafundisho ya Imani, Tamko Iura et bona kuhusu
kifo laini (5 Mei 1980), II: AAS 72 (1980), 546. Yohane Paulo II, kwa kukosoa dhana ya “chaguo la
kimsingi”, alikubali kwamba “bila shaka inawezekana kuwepo hali changamani na za kigiza kwa
upande wa saikolojia, ambazo zinaathiri uwezo wa kumshutumu binafsi mtu aliyetenda dhambi”
(Wosia wa Kitume Reconciliatio et paenitentia (2 Desemba 1984), 17: AAS 77 (1985), 223.
[345] Taz. Baraza la Kipapa kwa ajili ya hati za Kisheria, Tamko kuhusu uwezekano wa kuruhusu
kupokea Ekaristi wenye talaka waliofunga ndoa nyingine (24 Juni 2000), 2.
[346] Relatio finalis 2015, 85.
[347] Summa Theologiae I-II, q. 94, a. 4.
[348] Akifafanua kuhusu ufahamu wa jumla wa sheria na ufahamu binafsi wa upambanuzi wa
kiutendaji, mtakatifu Tomaso anafikia kusema kwamba “ikiwa upo ufahamu wa aina moja tu kati
ya hizo, bora uwe ule ufahamu binafsi wa uhalisia, ambao unakaribia zaidi utendaji” (Sententia
libri Ethicorum, VI, 6 [ed. Leonina, t. XLVII, 354]).
[349] Hotuba ya kuuhitimisha Mkutano wa Kawaida wa Kumi na Nne wa Sinodi ya Maaskofu (24

13.8 Page 128

▲back to top
128
Oktoba 2015): L’Osservatore Romano, 26-27 Oktoba 2015, uk. 13.
[350] Tume ya Kimataifa ya Teolojia, Kutafuta kanuni za maadili kwa wote: mtazamo mpya kuhusu
sheria asilia (2009), 59.
[351] Katika kadhia fulani, ingeweza kuwa pia msaada wa Sakramenti. Kwa hiyo,
“ninawakumbusha mapadre kwamba sanduku la kitubio halipaswi kuwa chumba cha mateso, bali
mahali pa kuona huruma ya Bwana” (Wosia wa Kitume Evangelii Gaudium (24 Novemba 2013),
44: AAS 105 [2013], 1038). Vilevile, ninasisitiza kuwa Ekaristi “si tuzo kwa walio wakamilifu, bali ni
dawa na chakula kilichotolewa kwa ukarimu kwa wale walio dhaifu” (kama ilivyotangulia, 47:
1039).
[352] Wosia wa Kitume Evangelii Gaudium (24 Novemba 2013), 44: AAS 105 (2013), 1038-1039.
[353] De catechizandis rudibus, I, 14, 22: PL 40, 327; taz. Wosia wa Kitume Evangelii Gaudium
(24 Novemba 2013), 193: AAS 105 (2013), 1101.
[354] Relatio Synodi 2014, 26.
[355] Wosia wa Kitume Evangelii Gaudium (24 Novemba 2013), 44: AAS 105 (2013), 1038.
[356] Taz. ilivyotangulia, 45: AAS 105 (2013), 1039.
[357] Taz. ilivyotangulia, 270: AAS 105 (2013), 1128.
[358] Taz. Bula Uso wa Huruma (Misericordiae Vultus, 11 Aprili 2015), 12: AAS 107 (2015), 407.
[359] Taz. ilivyotangulia, 5: 402.
[360] Taz. ilivyotangulia, 9: 405.
[361] Taz. ilivyotangulia, 10: 406.
[362] Wosia wa Kitume Evangelii Gaudium (24 Novemba 2013), 47: AAS 105 (2013), 1040.
[363] Taz. ilivyotangulia, 36-37: AAS 105 (2013), 1035.
[364] Huenda kwa hofu ya kukosea, iliyofichwa nyuma ya hamu kubwa ya kuwa waaminifu katika
kushika ukweli, mapadre wengine wanadai kwamba wanaofanya kitubio waweke nia ya kutubu
pasipo mashaka yoyote, kiasi kwamba – kwa kudai hivyo – huruma hufifia chini ya utafutaji wa
haki kamili ambayo ni ya ndoto tu. Kwa hiyo, ni muhimu kukumbuka mafundisho ya mtakatifu
Yohane Paulo II, ambaye alitamka kuwa ukitazamiwa kuwa mtu ataanguka tena “hii si sababu ya

13.9 Page 129

▲back to top
129
kukataa ukweli wa nia iliyowekwa” (Waraka kwa Kard. William W. Baum kwenye nafasi ya semina
kuhusu medani ya ndani iliyoandaliwa na Penitensiari ya Kitume [22 Machi 1996], 5: Mafundisho
XIX, 1 [1996], 589).
[365] Tume ya Kimataifa ya Teolojia, Tumaini la wokovu kwa watoto waliokufa bila kubatizwa (19
Aprili 2007), 2.
[366] Bula Uso wa Huruma (Misericordiae Vultus, 11 Aprili 2015), 15: AAS 107 (2015), 409.
[367] Tamko Apostolicam actuositatem, 4.
[368] Taz. kama iliyotangulia.
[369] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kichungaji Gaudium et Spes, 49.
[370] Waraka Ensiklika Deus caritas est (25 Desemba 2005), 16: AAS 98 (2006), 230.
[371] Taz. ilivyotangulia, 39: AAS 98 (2006), 250.
[372] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume wa baada ya Sinodi Christifideles laici (30 Novemba
1988), 40: AAS 81 (1989), 468.
[373] Taz. ilivyotangulia.
[374] Relatio finalis 2015, 87.
[375] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume wa baada ya Sinodi Vita consecrata (25 Machi 1996), 42:
AAS 88 (1996), 416.
[376] Taz. Relatio finalis 2015, 87.
[377] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 57: AAS 74
(1982), 150.
[378] Tusisahau kwamba Agano la Mungu na watu wake linaonyeshwa kuwa kama uchumba (taz.
Eze 16:8.60; Isa 62:5; Hos 2:21-22), na Agano Jipya linachukua pia sura ya ndoa (taz. Ufu 19:7;
21:2; Efe 5:25).
[379] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Konstitusyo ya kidogma Lumen gentium, 11.
[380] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 11: AAS 74
(1982), 93.

13.10 Page 130

▲back to top
130
[381] Yohane Paulo II, Homilia katika Misa Takatifu iliyoadhimishwa kwa ajili ya familia za
Córdoba – Argentina (8 Aprili 1987), 4: Mafundisho X, 1 (1987), 1161-1162.
[382] Taz. Gemeinsames Leben, München 1973, 18 (tafsiri ya Kiing.: Life Together, New York,
1954, uk. 27)
[383] Mtaguso Mkuu Vatikano II, Tamko Apostolicam actuositatem, 11.
[384] Katekesi (10 Juni 2015): L’Osservatore Romano, 11 Juni 2015, uk. 8.
[385] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 12: AAS 74
(1982), 93.
[386] Hotuba kwenye Sherehe ya Familia na kesha la sala, Filadelfia (26 Septemba 2015):
L’Osservatore Romano, 28-29 Septemba 2015, uk. 6.
[387] Gabriel Marcel, Homo viator. Prolégomènes à une métaphysique de l´espérance, Paris
1944, 63.
[388] Relatio finalis 2015, 88.
[389] Yohane Paulo II, Wosia wa Kitume Familiaris consortio (22 Novemba 1981), 44: AAS 74
(1982), 136.
[390] Taz. ilivyotangulia, 49: AAS 74 (1982), 141.
[391] Kuhusu masuala ya kijamii ya familia, taz. Baraza la Kipapa linaloshughulikia masuala ya
Haki na Amani, Mkusanyiko wa Mafundisho ya Kanisa kuhusu jamii, 248-254.
Copyright © Dicastero per la Comunicazione - Libreria Editrice Vaticana