ADMA-swahili3 Regulations 2004


ADMA-swahili3 Regulations 2004



1 Page 1

▲back to top


KANUNI MPYA ZA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Julai 2003
DIREZIONE GENERALE OPERE DON BOSCO
Via della Pisana, 1111 - 00163 Roma
Gombera Mkuu
Kwa wanachama,
Utambulisho wa Kanuni mpya kwa wanachama wa ushirika.
Katika Sikukuu ya Mt. Yohane Bosko, baba na mwanzilishi wetu, ninafu-
raha kutambulisha kanuni hii mpya kwenu. Haya ni matokeo ya kazi ya
ziada kwa sehemu ya kila mmoja na vikundi – na sana kwa namna ya
pekee kwa kikundi cha kwanza huko Torino – nawashukuru nyote.
Kanuni hizi zimeidhinishwa na kitengo cha mashirika ya maisha ya wak-
fu na jumuiya za maisha ya utume, tarehe 7 Oktoba 2003.
Kwa kuwa kanuni hizo zimesharudiwa na kurekebishwa, ni ishara kuwa
ushirika huu upo hai, ambao una nia ya kuendelea katika kazi ya utume
na kiroho katika uhusiano mwema na Kanisa pamoja na Familia ya
Waselesiani. Ni pia ishara kweli ya kilelezo cha uwajibikaji wa nguvu na
uaminifu kwa Don Bosko, ambaye alitaka ushirika wa Maria Msaada wa
Wakristo kuwa alama ya shukrani kwa uwepo wa kimama wa Bikira Ma-
ria katika maisha yake na kazi zake, na mfano wa maisha ya Kikristo am-
bao kiini chake ni elimu, upendo na kumuenzi Bikira Maria.
Nimatumaini yangu ya dhati kuwa wanachama wote wa ushirika huu, wa-
taweza kusoma kwa undani maandishi haya mapya na kupata roho ya
Waselesiani iliyoelezwa ndani yake. Ninawakabidhi nyote kwa Mama
yetu, Msaada wa Wakristo.
Roma, 31 Januari 2004
Sikukuu ya Mt. Yohane Bosko
Fr Pascual Chávez V .
Mkuu wa Shirika
1

2 Page 2

▲back to top


AMRI
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo, ulianzishwa na Mt. Yohane
Bosko, kuendeleza heshima kwa Sakramenti Takatifu ya Ekaristi na
upendo kwa Maria Msaada wa Wakristo”, kisheria ilisimikwa katika
madhabahu ya Maria Msaada wa Wakristo huko Torino tarehe 18 Aprili
1869, na kuinuliwa na Mwenyeheri Pius IX tarehe 5 Aprili 1870 katika
daraja la jumuya kubwa, ambayo ni mali ya Familia ya Waselesiani.
Msaidizi wa Mkuu wa Shirika (The Vicar of the Rector Major) ametam-
bulisha kanuni hizi kwa ofisi kuu ya Utume kwa ajili ya kibali.
Kitengo cha mashirika ya maisha ya wakfu na jumuiya ya maisha ya
Utume, baada ya kutathimini kwa uangalifu, Kanuni zilizotajwa, na
kuidhinisha katika lugha ya Kitaliano iliyowekwa katika hifadhi, mashar-
ti yote ya sheria yalifuatwa. Kitu chochote kinyume hakikubaliki.
Ilitolewa Vatikani, 7 Oktoba 2003, Sikukuu ya Bikira wa Rozari.
Eduardo Card. Martinez Somalo
Mkaguzi
Piergiorgio bu
Sala ya shukrani kwa wanachama wa Maria Msaada wa Wakristu
Ee Mungu Baba Mwenyezi, tunakushukuru kwa neema na baraka
ulizotujalia siku ya leo, tuwe wafuasi wa Maria Msaada wa wakristo.
Ulimkingia Bikira Maria dhambi ya asili na kumteua awe Mama wa
Mkombozi na mama yetu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Nakuomba
unipe neema na baraka niwe mtakatifu, mwaminifu na mwenye bidii kati-
ka Imani; nifuate mfano wa Bikira Maria aliyekuwa mtii na mtakatifu.
Tunakuomba uwabariki wafuasi wote wa ushirika wa Maria Msaada wa
Wakristu. Kwa neema na baraka zako, tunajiweka chini ya ulinzi wa Biki-
ra Maria Msaada wa Wakristu. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana
wetu. Amina
Padre au askofu:
Ee Mungu Baba, ulimchagua Bikira Maria ashiriki katika mpango
wako wa ukombozi wa Mwanadamu, sikiliza sala na maombi yetu
ambayo tunakutolea katika imani, tunamwita yule ambaye umetupa-
tia awe Mama na Msaada. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
2
19

3 Page 3

▲back to top


SALA ZA WAAMINI
Padre au askofu:
Ndugu na dada, tumwombe Mungu Mwenyezi katika huruma yake, asikie
sala tunazomtolea kwa maombezi ya Maria msaada wa Wakristo.
Kiitikio: Bwana Utusikie
1. Tunaliombea Kanisa Takatifu la Mungu, ili Maria, Bikira mwenye
nguvu, mtetezi wa Kanisa”, alisaidie Kanisa kwa upendo wa kimama.
2. Tunaomba kwa ajili ya Baba Mtakatifu: Kama watangulizi wake Mt.
Pio V na Pio VII apate ulinzi kamili wa Maria Msaada wa Wakristo kati-
ka majaribu yote na magumu katika Kanisa.
3. Kwa ajili ya maaskofu, mapadre na watawa, ili katika ushirika na Baba
Mtakatifu, waongozwe katika imani na maisha ya Kikristo ambayo
wamepewa kwa ajili ya kutunza na kulilinda Kanisa la Mungu.
4. Kwa ajili ya recta meja mkuu wa Waselisiani, na kwa wakuu na kamati
mbalimbali za Familia ya Waselisiani, waweze kupata ulinzi wa Maria
Msaada wa Wakristo na Mt. Yohane Bosko katika shughuli zote za ku-
waongoza Waselisiani.
5. Kwa ajili ya wote tulio hapa, wafuasi wa ushirika wa Maria Msaada wa
Wkaristo, ulimwenguni kote na hasa kwa wale ambao wamekuwa wa-
fuasi leo, kwamba katika kusherehekea na kuheshimu Maria Msaada wa
Wakristo, tujisikie tumeungana katika sala na kuishi kwa kuendeleza iba-
da kwa Maria Msaada wa Wakristo, kwa ajili ya kutafuta miito mitakatifu
kwa ajili ya Kanisa na Familia ya Waselisiani.
KANUNI ZA JAMII YA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Masahisho ya Julai 2003
DIBAJI
Akisukumwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya mahitaji ya dharura na isha-
ra za nyakati, Don Bosko, alianzisha katika utume wake chama kikubwa
cha watu ambao wangefanya kazi kwa namna mbalimbali kwa ajili ya
faida ya vijana na kundi la wale wafanyikazi.Ushirika wa Maria Msaada
wa Wakristo ulianzishwa na Don Bosko kama chombo maalum cha
Kutangaza heshima kwa Sakramenti Takatifu ya Ekaristi na upendo kwa
Maria Msaada wa Wakristo”.
Ilizinduliwa kisheria katika madhabahu ya Maria Msaada wa Wa-
kristo huko Torino 18 Aprili 1868, na aliitazamia kuwa sehemu maalum
katika jumuiya ya Waselesiani(Fr Pietro Ricaldone, Maria Ausiliatrice,
Colle Don Bosco 1951, p. 83).
Katika mhutasari mfupi tarehe 5 Aprili 1870, Pius IX aliuinua
katika darala la Jumuiya kubwa, na ibada ya pamoja ya vyama ambavyo
vinaibuka katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa kijana na nia
hiyo.
5 Julai 1989, Mkuu wa Waselesiani, Pd. Egidio Viganò pamoja na
halmashauri yake, rasmi walitambua ushirika wa Maria Msaada wa Wa-
kristo kama mwanachama wa familia ya Waselesiani.
TESTUS APPROBATUS
Romae, die 7-10-2003
KANUNI YA
18
3

4 Page 4

▲back to top


USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
ASILI NA SABABU YA USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO [ADMA]
Kanuni 1
Tendo la Msingi
Baada ya Don Bosko kujenga madhabahu ya heshima ya Bikira Maria
ambayo yaliwekwa wakfu kwa ajili ya Msaada wa Wakristo [Torino
1868], kwa kufuatia ishara zake alizopata kutoka njozi, alielewa baada ya
mwaka ilikuwa hamu ya kujenga Basilika. Ushirika wa wafuasi wa Maria
Msaada wa Wakristo(18 April 1869) una wajibu wa kueneza ulimwengu-
ni mote ibada kwa Maria Maria kwa jina hilo.
Kanisa la Maria Msaada wa Wakristo, ndilo kiini cha kusambaza utume
huu, ulimwenguni pote, mahali hapa kwa Don Bosko ilikuwa ukamilifu
wa kazi zake zote, kisima cha neema na madhabahu ya ulimwengu.
Upendo wa Don Bosko kwa Maria Msaada wa Wakristo unapatikana
katika ushirika huu kwa namna ya maelezo ya kulinda na kutetea imani.
Sisi Wakristo ni lazima tuunganike katika nyakati ngumu. Kuwa miongo-
ni mwa wale wanaotenda wema, ni chemichemi inayochangamsha na ku-
chochea wema kwetu, bila kuelewa zaidi”[MB 7, 602)
Uzoefu, unatuoenyesha kuwa utume wa Maria kama mama wa
Kanisa na Msaada wa Wakristo, alioanza duniani, unaendelea kutoka
mbinguni kwa namna ya ajabu kwa ulimwengu wote”.
(G.BOSCO, Meraviglie della Madre di Dio invocata sotto il titolo
di Maria Ausiliatrice, Torino, 1868, p. 45).
Uwepo huu wa Kimama wa Bikira Maria ndio msingi wa Ushirika
na msukumo wa majukumu ya wafuasi kwa ajili ya huduma ya Ufalme
wa Mungu.
Kanuni 2
Asili na Sababu
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo unatoa nafasi ya kukutana kwa
waamini ambao hushiriki kazi maalumu ya Bikira Maria. Katika Kanisa,
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo ni ushirika wa hadharani wa
waamini tukirejelea Sheria za Kanisa [Kan. 298-320]. Tena ushirika huu
una sifa ya sheria za Kanisa.
Baraka juu ya Rosari na katiba ya uanachama:
Padre au askofu: Bwana unadhihirisha upendo wako ndani ya Bikira Ma-
ria, Mama yetu na msaada. Tunakuomba rozari hizi, ziwe, ishara ya
wokovu wako miongoni mwetu. Amina!
(padre au askofu ananyunyizia maji ya Baraka na kisha kufukisia ubani)
Padre au askofu: Katiba hizi zilizo na ishara picha ya Maria Msaada wa
Wakristo ikukumbushe uanachama wako wa Ushirika wa Maria Msaada
wa Wakristo ulionzishwa na Mt. Yohane Bosko. Maria Msaada wa Wa-
kristo akuwezeshe kukuwa katika Bwana Yesu Kristo, kwa yule ambaye
umechukua majukumu kuwa mfausi wake mwaminifu. Bikira Maria aku-
pe ulinzi na usaidizi wa Mama. Amina!
Kiapo wanachochukua Wakandidati
[Wakandidati wote hupiga magoti na kusema yafuatayo]
Bikira Maria, Msaada wa Wakristo na Mama wa Kanisa, kwa kuwa
mfuasi wa ushirika wako, ninaahidi kuwa shahidi mwaminifu wa Kristo
katika maisha yangu ya kila siku, hasa kwa familia yangu, sehemu ya ka-
zi, na katika jamii na Kanisa, kwa nguvu na uwezo unaotokana na sala, na
katika kuopkea Sakramenti ya Kitubio na Ekaristi mara kwa mara. Ni-
naahidi kuomba kwa ajili ya miito kwa ajili ya Kanisa na familia ya
Kiselesiani, kwa kufuata mafundisho na mifano ya Mt. Yohane Bosko na
kujiaminisha kwa msaada wa kimama utakao nipa.
Wakristo wote hujibu. Amina.
Basi kila mwanachama hupewa rosari na katiba, ya uanachama.
Padre au askofu: Sasa ninyi ni wanachama kamili wa Ushirika wa Maria
Msaada wa Wakristo, na mshiriki wa neema za kiroho za ushirika huu, na
kazi zote njema zinafanywa ndani ya familia ya Waselesiani iliyoanzish-
wa na Mt. Yohane Bosko.
Padre au askofu: Maria Msaada wa Wakristo.
Wote wanaitikia: Utuombee.
4
17

5 Page 5

▲back to top


kujiunga na ushirika huu?
Wakandidati: Kila mmoja binafsi atafanya maisha yake ya kiroho yawe
mfano wa Bikira Maria, kuyafanya maisha yetu yawe kama yake, kum-
wamini Mungu pekee, na kufanya hii kuwa jukumu la maisha yote.
Hivyo, kusikiliza Neno la Mungu kama Bikira alivyosikiliza, tutabaki
makini kwa kusikiliza Neno la Mungu, ambalo tutatangaza kwa neno na
mifano ya maisha yetu.
Kama vile bikira alivyosali, tutahakikisha kuwa maisha yetu yatanurishwa
na sala ya rohoni katika mawazo na shukrani mbele ya Baba. Kama Biki-
ra Maria, tutashirikiana na Papa, maaskofu na mapadre kwa ajili ya kukua
kwa watu wa Mungu. Kama vile Bikira alivyojitolea mwenyewe, tutafan-
ya maisha yetu matoleo kwa Mungu, kwa furaha ya kukamilishwa na
mapenzi ya Baba ambayo ndiyo njia ya kutakatifuzwa.
Padre au askofu: Ni majukumu yapi ya kipekee unayojiwekea kama
mwanachama wa ushirika huu?
Wakandidati: Kama tabia yetu ya kipekee na wajibu, tunatazamia kuene-
za ibada ya Maria Msaada wa Wakristo na kumwabudu Yesu katika
Ekaristi Takatifu katika jamii yetu. Hayo yote tutatimiza kwa maneno
yetu na matendo ambayo yanatokana na Injili na maisha ya kiroho na
utume wa Mtakatifu Yohane Bosko.
Katika nchi zote ushirika huu waweza fuata usajili wa kisheria,
hata hivyo ushirika huu si wa kisiasa, au wakutengeneza faida. Ushiriki
huu wa Maria Msaada wa wakristo unatoa mwongozo wa utakatifu kwa
ajili ya utume wa Waselesiani[ ni mapenzi yake Bikira Maria tumhesh-
imu kwa jina la Maria Msaada wa Wakristo. Nyakati zetu ni ngumu, twa-
hitaji huyu Bikira Mtakatifu kutusaidia kutunza na kulinda imani ya
KikristoMB 7,334]. Kwa njia ya pekee Don Bosko alianzisha ushirika
huu ili kuwashirikisha wafanya kazi katika maisha ya kiroho na utume wa
Shirika la Waselisiani, kama kikundi cha pili maalum katika kazi zake
[GC 24, 80].
Ushirika huu, unatoa nafasi ya pekee kabisa kwa ajili ya Ibada
kwa Ekaristi Takatifu na upendo kwa Maria Msaada wa Wakristo katika
kila namna, kwa matumizi ya binafsi au kwa ibada hadharani ambayo
imeidhinishwa na Kanisa. Inatimiza wajibu wake kwa ushirika na utii
kwa maaskofu wa Kanisa na ushirikiano na vyama vingine vya Kanisa,
hasa Familia ya Waselesiani.
Jina lake rasmi ni Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo au
ASSOCIATION OF MARY HELP OF CHRISTIANS (AMHC), au As-
sociation Di Maria Ausiliatrice (ADMA) na makao yake makuu yapo
Torino, via Maria Ausiliatrice 32, karibu na madhabahu ya Maria Msaada
wa Wakristo.
Kanuni 3.
Ushirika huu katika familia ya Waselesiani
Wafuasi wanaunda sehemu ya Familia ya Waselesiani, kwa njia ya
heshima kwa Msaada wa Wakristo kadiri Don Bosko alivyo weka msingi.
Kuwa mfuasi ni kujitolea kumheshimu Maria, msaada na Mama wa Kani-
sa, kwa kushiriki utume wa Don Bosko kwa watu, hasa, vijana na zaidi
katika kulinda na kuiteta imani ya Kikristo”.(Egidio Viganò, Lettera Al
Rettore del Santuario di Maria Ausiliatrice a Torino del 24/07/1989).
Katika Familia ya Waselesiani, ushirika huu unahamasisha na
kueneza ibada kwa Maria kama namna ya kuinjilisha na kuwasaidia wa-
tu, hasa vijana na wale maskini. Ushirika huu unatambua [Rector Ma-
jor] , mwandamizi wa Don Bosko, kama baba wa umoja wa Familia ya
Waselisiani wote.
16
5

6 Page 6

▲back to top


Kanuni 4
Wajibu wa kila mwanachama
Ufuasi kamili kwa ushirika huu, yadhihirisha kufuata na kuwajibika, hasa
katika familia na mahali unaishi, na sehemu za kazi na wale wote una-
shirikiana nao. Bidii na heshima ya kushiriki maisha ya Liturjia, kwa
kuungana na Kanisa ambalo Maria ni sura na mfano ; na hasa kwa namna
ya kipekee kwa Sakramenti ya Ekaristi na Sakramenti ya Kitubio, na jinsi
ya kuishi binafsi maisha ya Ukristo:
Kuishi na kueneza ibada ya Maria Msaada wa Wakristo kadiri ya roho ya
Don Bosko, hasa katika Famila ya Waselisiani(Egidio VIGANÒ, Circu-
lar Letter: Mary renews Don Boscos Salesian Family in ASC 289 Janu-
ary-June 1978);
- Kufanya upya, kuimarisha na kuishi ibada na maisha ya kiroho
kwa pamoja:
- Kumbukumbu ya Maria Msaada wa Wakristo kila Mwezi tarehe 24;
- Kusali rozari;
- Novena kwa maandalizi ya Sikukuku ya Maria Msaada wa Wakris-
to;
- Baraka ya Maria Msaada wa Wakristo;
-Hija kwa mahali patakatifu pa Maria;
- Maandamano ya sala;
- Kushiriki maisha ya parokia: Liturjia, Katekesi, kuwatembelea
wagonjwa na wazee, na mahitaji na huduma zingine katika Kanisa.
-Kumuenzi Maria kwa namna ya kuishi maisha ya Ukristo katika fa-
milia yako na pia kuwa mkarimu na yule ambaye anakaribisha;
- Kujihusisha na sala pamoja na matendo mema dhidi ya vijana masi-
kini na watu wengine wanaohitaji;
- Kusali na kuwaimarisha walei, watawa na wale amabo wana vyeo
ndani ya Kanisa na kwa namna ya pekee Familia ya Waselisiani;
- Kila siku kuishi maisha ya kiroho yenye mwelekeo wa fadhila za In-
jili, hasa kumshukuru Mungu kwa maajabu yanaoyoonekana katika
kazi zake, na kuwa mwaminifu kwake hata katika nyakati za mateso
na msalaba, kwa kufuata mfano wa Maria.
Kanuni 5
Kuwa mkarimu kwa zawadi za kiroho
Wafuasi hushirikishana faida ya neema na maisha ya kiroho ambayo
kwayo ni rasmi kwa ushirika na kwa wale wa familia ya Waselesiani
(Wafuasi hushiriki katika msamaha na faida ya kiroho ambayo ni ya
kipekee kwa chama na familia ya Waselesiani. Tumepewa katika Nyonge-
za II maelezo muhimu kwa ajili ya kutusaidia kuepuka matendo amabyo
6
tasema kwa heshima ya Sakramenti Takatifu: Isifiwe na itukuzwe sasa
na siku zote Sakramenti Takatifu sana ya Kimungu "; na kwa heshima
ya Bikira Maria: "Maria Msaada wa Wakristo, utuombee". Kwa ma-
kuhani inatosha katika misa kuwa na nia ya wafuasi wote wa ushirika.
Sala hizi zitatumika kama dhamana ya kuunganisha wanachama wote ili
wawe na roho moja na wazo moja kwa ajili ya kumwabudu Yesu aliyeko
katika Ekaristi Takatifu na Mama yake, na kushiriki katika mema yote
yanayotendwa na chama.
[From "Letture Cattoliche", Year XVII, May, Vol. V, pp. 48-50]
Kupokelea wanachama wa Maria Msaada wa Wakristu Jumapili tarehe
24 Januari 2021– St. Thomas Catholic Church Kathiani
IBAADA YA KUWAPOKEA WANACHAMA WAPYA
Baada ya homilia utaratibu huu ufuate:
Kiongozi:
Leo ni siku ya furaha kwenu ninyi mnao tazamia kujiunga na ushirika wa
Maria Msaada wa Wakristo. Mmeomba kuwa wanachama wa ushirika
huu ili kuwa mashahidi wa upendo kwa Bikira Maria Mtakatifu na wajibu
wenu kumfanya atambulike na apendwe. Tuanze sherehe yetu kwa namna
ya tendo la kawaida kwa kuwaita kila mmoja jina. Mwito huu una maana
kwamba Maria Mtakatifu anawaalika kujiunga na ushirika ambao una jina
lake.
Kuwatambulisha Wakandidati
Wakandidati wanaitwa na kiongozi wa Maria Msaada wa Wakristu,
atawaita kwa majina yao yote. Na kila aliyehudhuria ataitika, Nipona
kujongea altare.
Mahojiano
Padre au askofu: Vile unavyojongea altare, unaomba nini?
Wakandidati: Tunaomba kuwa wafuasi wa Ushirika wa Maria Msaada wa
Wakristo.
Padre au askofu: Je mnaelewa majukumu mnayochukua wenyewe kwa
15

7 Page 7

▲back to top


Hali zingine tatu lazima pia ihifadhiwe katika akili; ni msamaha am-
bao unatolewa kwa waamini wote:
1. Fadhila ya waamini ambayo, katika kutekeleza majukumu yao na kuka-
biliana na shida za maisha hujiaminisha kwa unyenyekevu kwa Mungu,
na kuongeza wakati huo huo - hata kiakili - kuomba moyoni.
2. Kutoa fadhila kwa waamini ambao, kwa roho ya imani na huruma, hu-
jiweka wenyewe na mali zao katika huduma ya ndugu au dada aliye na
mahitaji.
3. Fadhila ya mwamini ambaye, kwa roho ya toba, kwa hiari hufanya
malipizi kwa kitu halali.
NYONGEZA III
KANUNI YA WAFUASI WA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Imeandikwa na Don Bosko
1. Katika Kanisa la Torino ambalo limewekwa kwa heshima ya Maria
Msaada wa Wakristo, limewekwa rasmi na kisheria kwa idhini ya Askofu
Mkuu wa Torino mfuasi wa Maria; Wajumbe wa Shirika hilo wanalenga
kukuza heshima kwa Mama wa Mwokozi ili kustahili katika maisha na
hasa wakati wa kufa.
2. Wao wana malengo mawili maalum: kueneza ibada kwa Bikira Maria
na kumheshimiwa Yesu katika Ekaristi Takatifu.
3. Kwa hivyo watatumia maneno, ushauri, kazi njema na ushawishi wa
kukuza utukufu na kujitolea katika karamu, sikukuu na maadhimisho ya-
nayotokea wakati wa mwaka ili kumheshimu Bikira Mtakatifu na
Sakramenti Takatifu zaidi.
4. Kuenea kwa vitabu vyenye mafunyo mazuri, picha, medali na vi-
peperushi, kushiriki katika maandamano kwa heshima ya Maria mtakatifu
sana na Ekaristi Takatifu kwa kuhimiza wengine kufanya hivyo, mara
kwa mara kushirika na kuwepo kwa Misa takatifu, kuambatana na Viati-
cum kwa wanaokufa , ni mambo wanachama wanajaribu kukuza kwa njia
zote zinazowezekana kwa hali yao katika maisha.
5. Wajumbe watajitahidi kamwe kutotumia lugha ya kashfa au kushiriki
katika majadiliano kinyume na dini, na watajitahidi kabisa kuzuia wale
walio chini ya malezi yao kufanya hivyo; wote wataondoa vikwazo katika
njia ya utakaso wa siku za Jumapili na Siku ya Sikukuu.
6. Kila mwanachama, kulingana na ushauri wa Katekismui na waku-
rugenzi wa kiroho, amehimizwa vyema kupokea Sakramenti ya kitubio
na Komunio mara moja kwa mara mbili au mara moja kwa mwezi, na ku-
shiriki Misa ya kila siku ikiwa kazi yake inaruhusu.
7. Kila siku baada ya maombi yao ya asubuhi na usiku, wajumbe wa-
14
hayaendani na nia ya Kanisa)
Zaidi, faidi ya maisha ya sala na ibada inayotolewa katika Basili-
ka la Maria Msaada wa Wakristo huko Torino na katika makanisa mahali
ushirika huu umeanzishwa. Mfuasi akifa, wafuasi wengine katika kikundi
wanaalikwa kushiriki katika Ekaristi ya walio katika mateso na huzuni.
SEHEMU YA PILI
II.MUUNDO WA USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO
Kanuni 6
Ushirika
Katika mtindo wa Don Bosko, muundo upo kwa ajili ya huduma kwa kila
mmoja na ni rahisi sana na yenye kuwezekana, na inaweza kutumika
katika namna mbalimbali na kwa nchi mbalimbali.
Ni ukweli kuwa: ni jambo la muhimu kazi ya Don Bosko iliingi-
ana na maisha ya kawaida hata katika mipangilio yake, ambayo yajieleza.
Aliweza kuonyesha wazi majukumu ya kuendesha, kuimarisha na ku-
kua”(Viganò, Letter to the Rector of the Sanctuary of Mary Help of Chris-
tians in Turin, 24 July 1989).
Kanuni 7
Usimikaji wa ushirika mashinani
Kwa njia ya [Kan. 312-317] na nafasi ya Shirika la Waselesiani, ni waji-
bu wa mkuu wa Waselisiani katika kanda kusimika Ushirika wa Maria
Msaada wa Wakristo katika vyuo vya Waselesiani na Mabinti wa Maria
Msaada wa Wakristo katika sehemu anayotawala. Kwa hali zingine barua
ya Askofu wa mahalia inayoidhinisha huhitajika.
Kanuni 8
Mkusanyiko
Baada ya kusimikwa rasmi, maombi yatakiwa kutumwa haraka kwa ajili
ya mkusanyiko. Yatumwe huko sehemu takatifu ya Maria Msaada wa
Wakristo Torino- Valdocco, ili kumaliza uidhinishaji wa mkusanyiko kwa
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo. Hati kamili, ambayo imetiwa
sahihi na Mkurugenzi wa mahali patakatifu, ndiyo itakuwa hati rasmi ya
uanachama. Inashauriwa kuitunza katika hifadhi maalum na kivuli chake
kubandikwa sehemu ambayo inaweza kuonekana kwa kila mtu.
Kanuni 9
Ushirika na mahali patakatifu pa Maria Msaada wa Wakristo huko Torino
"Ushirika wa Maria Msaada wa wakristo kwa namna ya pekee imeungan-
ishwa na mahali patakatifu kule Torino – Valdocco. Inaweza kusemwa
pia kwamba Maria hakuonekana wa7zi katika ujenzi wa wa mahali pata-

8 Page 8

▲back to top


Kanuni 14.
Mkuu wa Shirika na baraza la kitaifa.
Ikiwezekana, katika ngazi ya juu ya shirika kwaweza kuwa mjumbe
mmoja ambaye anaratibisha na kuongoza mabaraza ya wajumbe mash-
inani na Familia ya Waselisiani.
Baraza katika ngazi ya juu ya kanda huchaguliwa na marais wa
mashinani. Muundo wake ni kama ifuatavyo: Rais, Makamo wa rais, Kat-
ibu, Mweka hazina, na baadhi ya wajumbe kadhaa. Wajumbe wa baraza
wanachaguliwa kwa miaka 4 na wanaweza kuchaguliwa tena kwa awamu
ya pili miaka 4. Mratibu wa kiroho, mke au mume, ni mjumbe wa baraza
hilo. Mahali inapowezekana, muundo wa waratibu wanaweza kuanzish-
wa.
Kanuni 15
Wajibu wa Makao Makuu ya Chama
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo umehusishwa na mahali pata-
katifu pa Maria Msaada wa Wakristo Torino – Valdocco, ambaye ndiye
mrithi na mwendelezaji wa ushirika huu ulioanzishwa na Don Bosko
mwenyewe, na ndivyo unaitwa msingi”.
Kwa sababu ya asili yake na kushirikishwa na mahali patakatifu,
ushirika huu una wajibu wa kupyayusha, kuunganisha na kutoa habari
kuhusu ushirika huu ulimwenguni. Ndio maana inakua kiungo maalum
cha Maria Msaada wa Wakristo, ambayo inachapishwa na jarida la
Maria Ausiliatrice", huko Torino.
Kanuni 16
Baraza la Ulimwengu la Ushirika
Ni wajibu wa rais wa makao makuu ya ushirika kuitisha kikao cha Bara-
za la Ulimwengu la Ushirika. Baraza hili linahusu wafuatao: Makamu wa
Mkuu wa Shirika la Waselisiani, mjumbe wa Shirika la Mabinti wa Ma-
ria Msaada wa Wakristo kutoka ngazi ya juu ambaye ndiye kiungo na
Familia ya Waselisiani, Rais na mratibu wa maisha ya kiroho na mjumbe
kutoka makao makuu ya ushirika, pamoja na wawakilishi wa nafasi zin-
gine.
Kwa hiyo walei watakiwa kuwa wengi mno kuliko mapadre na watawa.
Baraza hili hukutana kila baada ya miaka 6: Katika nyakati maalum ya
kongamano la Maria Msaada wa Wakristo, ambayo inapangwa na baraza
la wajumbe wa makao makuu ya Ushirika.
8
za pia kutumiwa kwa wafu kwa njia ya kutosha.
MSAMAHA WA MUDA MREFU
Hati ya utume wa sheria ya tarehe tarehe 31 Januari 1968 ilitoa msamaha
uliotolewa katika orodha zifuatazo katika nambari 1, na 4 hadi 10, na
tarehe 6 Februari 2002 wale waliopewa 2 na 3, msamaha ulitolewa kwa
muda mrefu.
1. Siku ya kujiunga na chama;
2. Mt. Fransisko wa Sale, 24 Januari;
3. Mt. Yohani Bosko, Januari 31;
4. Kupashwa habari Maria, Machi 25;
5. Maria Msaada wa Wakristo, Mei 24;
6. Hija, Mei 31;
7. Bikira Maria kupalizwa Mbinguni, Agosti 15;
8. Siku ya kuzaliwa kwa Mama yetu, Septemba 8;
9. Bikira Maria Imakulata, Desemba 8;
10. Siku ya Krismasi, Desemba 25.
MASHARTI
1. Kujitolea kupigana dhidi ya dhambi;
2. Kukiri kwa Sakramenti ya Kitubio;
3. Ushirika wa Ekaristi;
4. Sala kwa madhumuni ya Papa;
5. Upyaji, angalau lakini waziwazi, ya ahadi ya kuzingatia kwa uaminifu
Kanuni za Chama.
N.B.
a) Wajumbe wanaweza kupata kibali na msamaha wa muda mrefu kwa
jumla kadiri ya siku zilizoorodheshwa, au siku ambayo sikukuu inaham-
ishwa.
b) Wajumbe wanaweza kupata msamaha wa jumla kwa waamini wote
katika kipindi cha mwaka wa Liturujia, lakini katika hali, ahadi ya kufu-
ata kanuni haitajiki.
MSAMAHA WA MUDA
Kuna sala nyingi sana na matendo mema ambayo kwa kupata msamaha ni
sehemu ya masharti.
Miongoni mwao ni mbili zilizopendekezwa na Don Bosco mwenyewe
katika Kanuni za ADMA:
1. “Isifiwe na itukuzwe sasa na siku zote Sakramenti Takatifu sana ya
Kimungu”.
2. Maria Msaada wa Wakristo, tuombee.
13

9 Page 9

▲back to top


ushirika wa Kanisa unahitaji wote kutambua aina nyingi za halali kati-
ka vyama vya waamini katika Kanisa na wakati huo huo, nia ya ku-
shirikiana katika kufanya kazi pamoja.
- Kukubaliana na kushiriki katika malengo ya kitume ya Kanisa,
yaani, "uinjilisti na utakaso wa ubinadamu na
Kuundwa kwa Kikristo kwa dhamiri ya watu, ili kuwawezesha kui-
fanya roho ya injili katika jamii mbalimbali na nyanja za maisha "[AA
20]. Kwa mtazamo huu, kila aina ya kuweka waamini unaulizwa ku-
wa na bidii ya umisionari ambayo itaongeza ufanisi kwa washiriki
katika uinjilisti tena.
- Kujitolea kwa uwepo katika jamii ya wanadamu, ambayo inaelekea
Mafundisho ya Kanisa ya kijamii, huiweka katika huduma ya jumla
heshima ya mtu. Kwa hivyo, vyama vya waamini vyapaswa kuwa na
matunda ya ushirikiano katika kuleta hali kwamba ni haki zaidi na
upendo ndani ya jamii. Vigezo vya msingi vilivyotajwa wakati huu
kupata ukaguzi wao katika matunda halisi ambayo fomu mbalimbali
za kikundi zinaonyesha ndani ya maisha ya shirika na kazi
wanazofanya, kama vile: rejea upya kwa maombi, kutafakari, liturujia
na maisha ya sakramenti, ufufuo wa wito kwa Wakristo wa ndoa,
ukuhani wa utumishi na maisha ya kujitolea; utayari wa kushiriki kati-
ka mipango na shughuli za Kanisa katika ngazi za mitaa, kitaifa na
kimataifa; kujitolea kwa nguvu na uwezo wa kufundisha na kuunda
Wakristo; tamaa ya kuwa kuwasilisha kama Wakristo katika mazingi-
ra mbalimbali ya maisha ya kijamii na uumbaji na kuamka kwa kazi
za usaidizi, utamaduni na kiroho; roho ya kikosi na umaskini wa ki-
injili inayoongoza zaidi na ukarimu katika upendo kwa wote; uongofu
kwenye maisha ya Kikristo au kurudi kwa ushirika wa Kanisa kwa
wanachama waliobatizwa ambao wameanguka mbali na imani.
(Apostolic Exhortation, 30/12/1988 of John Paul II, n.30)
NYONGEZA II
MSAMAHA
Mungu hutoa msamaha kwa kiburi cha dhambi iliyotendwa ambayo hatia
tayari imesamehewa, waamini ambao wamewekwa vizuri na kwa hali
fulani wanaweza kupata kupitia kuingilia kwa Kanisa ambalo, kama
chombo cha ukombozi, lina mamlaka na kutumia hazina ya kuridhika ili-
yofanywa na Kristo na watakatifu.
Kiburi ni sehemu ya kawaida ya dhambi kwa vile inaelekeza mtu katika
adhabu ya dhambi. Hakuna mtu anayeweza kuomba huruma kwa watu
wengine ambao bado wanaishi. Huruma na msamaha wa kawaida inawe-
12
Kanuni 17
Mali za Ushirika
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo, kwa sababu ni chama cha Kanisa
kinachotawaliwa na sheria, kinaweza kuwa na mali, kutunza na pia ku-
tumia kadiri ya sheria za Kanisa na sheria za nchi husika.
Kanuni 18
Utafisiri wa Sheria
Utafsiri wa sheria kwa lugha zingine ni lazima ufuate maandishi haya ya
kisasa na tena utume Makao makuu kwa kuhakikisha.
NYONGEZA 1
KIGEZO CHA MKUSANYIKO WA WALEI KANISANI
(Christifideles Laici n. 30)
Daima ni kutoka kwa mtazamo wa ushirika wa Kanisa na utume, na si
kinyume na uhuru wa kujiunga, hivyo mtu anaelewa umuhimu wa kuwa
na vigezo wazi na wazi kwa kutambua makundi hayo yaliyowekwa, pia
huitwa "Vigezo wa Ufalme ". Vigezo vya msingi vinavyofuata vinaweza
kusaidia katika kutathmini chama cha waaminifu katika Kanisa:
- Uwezo unaotolewa kwa wito wa kila Mkristo kwa utakatifu, kama
ilivyo imeonyeshwa "katika matunda ya neema ambayo roho hutoa
kwa kila mwaamini "[LG 39] na katika ukuaji kuelekea ukamilifu wa
maisha ya Kikristo na ukamilifu wa upendo [LG 40]. Katika maana
hii chama chochote cha waamini; daima huitwa kuwa chombo zaidi
kinachoongoza kwenye utakatifu Kanisa, kwa kuimarisha na kukuza
"umoja zaidi wa karibu kati ya maisha ya kila siku ya wanachama
wake na imani yao "[AA 19].
- Wajibu wa kudai imani ya Kikatoliki, kukubaliana na kutangaza
ukweli kuhusu Kristo, Kanisa na ubinadamu, katika kutii Magisterium
ya Kanisa, kama Kanisa linalitafsiri. Kwa sababu hii kila ushirika wa
waamini wafuasi lazima uwe jukwaa ambapo imani inatangazwa
pamoja na kufundishwa katika maudhui yake yote.
- Shahidi wa ushirika wa nguvu na wa kweli katika uhusiano na Papa,
kwa kuzingatia kabisa imani kwamba yeye ni kituo cha daima na
kinachoonekana cha umoja wa ulimwengu wote Kanisa [LG 23], na
kwa Askofu wa ndani, "kanuni inayoonekana na msingi wa umoja
"[LG 23] katika Kanisa fulani, na" kwa pamoja heshima kwa aina zote
za utume wa Kanisa "[AA 23]. Ushirika na Papa na Askofu lazima
waonyeshe kwa uwaaminifu utayari wa kukubali mafundisho ya ma-
fundisho na mipango ya wachungaji wa Papa na Askofu. Aidha,
9

10 Page 10

▲back to top


katifu, kwa maneno ya Don Bosko, lakini kuanzia pale alianza kuweka
ulinzi na usimamizi kwa ulimwengu wote. Ndiyo sababu ushirika huu
unapaswa kubaki umeungana na mahali patakatifu” [E. Viganò, Letter to
the Rector of the Sanctuary of Mary Help of Christians in Turin, 24 July
1989].
Kila ushirika wa mashinani, kwa hivyo, unapaswa kutengeneza
ushirika wa maelewano na umoja kwa mahali patakatifu pa Maria
Msaada wa Wakristo kule Torino – Valdocco na hasa na ushirika wa
kwanza ulioanzishwa kule; ushirika ulio makao makuu utatekeleza waji-
bu wake kwa ajili ya muungano.
Kanuni 10
Ushirika wa pekee katika maisha ya Chama
Wakatoliki wote waliobatizwa hasa kuanzia miaka 18 wanaweza
kujisajili kwa uwanachama katika ushirika huu.
Uanachama unadai jukumu la kuishi yote yaliyotajwa katika
Kanuni 4 ya sheria za sasa na pia kushiriki mara kwa mara katika vikao
vya ushirika kwa roho ya umoja na pia uanachama.
Usajili wa mkandidati katika ushirika ni lazima iidhinishwe na
rais pamoja na baraza lake. Hiyo hufanyika baada ya maandalizi ya
kutosha ambayo si chini ya mwaka mmoja, na vikao vya kila mwezi.
Mkandidati aonyeshe uaminifu kwa ushirika wakati wa sherehe
ya Maria Msaada wa Wakristo, na atapata cheti, sheria na beji ya
uanachama.
Ushirika wa mashinani, ni lazima uangalie malezi endelevu ya wanacha-
ma, wapange shughuli zao kadiri ya mazingira yao wakifuata sheria.
Katika roho ya umoja na uanachama, kila mmoja anachangia matoleo
kwa uhuru wake ili kukidhi mahitaji ya ushirika mahali alipo na pia
kupitia mpango wa kanda, ambayo inachangia pia mahitaji ya ushirika
katika makao makuu.
Kanuni 11
Nafasi ya uanachama
Kwa ajili ya ushirika, na kuendeleza malezi, kwa kubadilishana hali ya
maisha, ushirika wa mashinani unapanga yafuatayo:
- Vikao vya kila mwezi (pia wafuasi wengine wa familia ya
Waselesiani wanaweza kushiriki bila pingamizi lolote) kwa ajili
ya malezi ya kanuni, sala na sherehe au kuabudu Ekaristi Ta-
katifu ikiwezekana tarehe 24 kila mwezi, siku ambayo Bikira
Maria anakumbukwa kwe heshima.
-Siku ya Maria ya kila mwaka;
10
- Kushiriki katika sherehe au vikao vya familia ya Waselesiani.
- Mazoezi ya kiroho kwa ajili ya wafuasi;
- Maandamano, hija, siku za ritriti au mfungo;
- Vikao vingine ambavyo vimepangwa na ushirika mahalia.
Taz. Kanuni 4.
Kanuni 12
Baraza la utawala wa kituo katika ushirika
Kila baraza la utawala wa kituo unaratibishwa na baraza, lililochaguliwa
na wanachama wote kutoka orodha ya wanachama ambao wamejitangaza
kuwa watakuwa tayari kuhudumia kwa udugu.
Baraza la utawala mahali, linahusu, raisi, makamu wa rais, mweka
hazina, katibu, na baraza la wajumbe, kadiri ya mahitaji ya ushirika.
Mlezi wa kiroho, mwanamume au mwanamke, pia ni mfuasi wa baraza
hilo.Kwa mkandidati kusajiliwa, anahitaji kura za wachache. Wajumbe
wa bara
za wanabakia ofisini kwa kipindi cha miaka minne na wanaweza
kuchaguliwa kwa miaka mingine minne. Wakati baraza limekamilika,
kazi za pekee ndani yake huamuriwa na baraza.
Rais ndiye huitisha vikao vya baraza na ndiye anaendesha; ana-
tayarisha agenda na kuwasilisha kwa wajumbe wa baraza kupitia katibu.
Rais anawakilisha ushirika katika vikao vya nje na hasa vikao vinaovyo
husu vikundi vingine.
Makamo wa raisi, anachukua nafasi ya raisi wakati labda hana
nafasi ya kuhudhuria vikao kwa sababu ambazo haziwezi kuepukika, hii
hufanyika tu baada ya maelewano na raisi. Mweka hazina anatunza mali
ya chama kulingana na sheria za nchi husika na pia kwa maamuzi ya ba-
raza. Kila mwaka huwakilisha matumizi ya fedha na bajeti.
Katibu, kwa maongozi ya rais, anawatumia wajumbe tarehe na
agenda za mikutano, anaandika , na anatunza hifadhi ya ushirika. Kwa
kila mjumbe wa baraza, anapewa jukumu fulani mahali alipo kwa ajili ya
ushirika. Kwa kawaida baraza hukutana mara moja kwa mwezi.
Kanuni 13
Wanaoongoza katika maswala ya kiroho
Walezi wa kiroho wa ushirika wanachaguliwa na Mkuu wa Waselisiani
katika kanda au na Mkuu wa Mabinti wa Maria Msaada Wa Wakristo.
Hao wanaendesha, kipekee malezi ya kiroho ya Waselesiani na ushirika
katika maisha na miradi ya kanisa mahalia. Wale amabo wanaweza
kuchaguliwa kwa malezi ya kiroho ya wanachama, waweza kuwa kati ya
wanachama wenyewe ikiwa wameandaliwa.
11