DBPP-Prayer Swahili Ahadi na sala


DBPP-Prayer Swahili Ahadi na sala



1 Page 1

▲back to top


SALA NA AHADI
YA WA WANAFUNZI WALIOSOMA DON BOSCO
Mungu Baba Mwenyezi kwa njia ya Mwanao Bwana wetu Yesu Kristu, na maombezi ya
Mtakatifu Yohane Bosco usikilize sala za vijana waliopitia malezi ya Don Bosco popote
ulimwenguni;
Tunakushukuru kwa tunu isiyofutika ya elimu ambayo tumeipokea chini ya malezi ya
Wasalesiani na kuwa chachu katika maisha yetu.
TUNAKUOMBA KWA UAMINIFU WA KIFAMILIA
Utupe nguvu na ujasiri kuuishi ujumbe wa utu na wa kisalesiani kila siku katika jamii
tunayoishi,
Utusaidie tuwe Wachamungu na Raia waaminifu,
Tusaidie kuishi pamoja na kukuza mshikamano ndani na nje ya Umoja wetu,
Utuimarishe katika Imani, Matumaini na Mapendo.
TUNAAHIDI
Kupigana na dhurma, usaliti, unafiki,uzembe na tabia ya kutokujali,
kutetea kwa gharama yoyote ile, maadili yaliyotokana na mafundisho ya Don Bosco, hasa
uhuru na ukweli kwa moyo wa kujitolea kijamii, kisiasa na kiuchumi,
na kuwa, “chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu” yenye ushawishi mkubwa duniani na
katika utume wa Wasalesiani.
TUNAOMBA
Uilinde familia ya Wasalesiani, Wapendwa wetu na kila mmoja wetu. Amina