ADMA-swahili2


ADMA-swahili2



1 Pages 1-10

▲back to top


1.1 Page 1

▲back to top


HISTORIA FUPI
FAMILIA YA MT. YOHANE BOSKO
Kuzaliwa Yohane Bosko
Mtakatifu Yohane Bosko alizaliwa 16 th Agosti 1815 huko Italia,
karibu na mji wa Castelnuovo. Anafahamika kwa jina la kipadre
Don Bosko maana yake Padre Bosko. Padre Bosko alifariki dunia
mnamo 31st Januri 1888. Ni katika siku hiyo aliyokufa
tunaadhimisha sikukuu yake. Alizaliwa katika familia maskini.
Wazazi wake waliitwa Fransisko Bosko na Margaret Occhiena.
Yohane Bosko alikuwa na umri wa miaka miwili wakati Baba
yake alipo aga dunia.
Bada ya Fransisko kufa, mama Margaret ndiye alichukuwa
majukumu yote ya familia. Kwa kweli mama huyo alikuwa mtu
mwema katika roho. Alimwamini Mungu zaidi sana hata katika
mahangaiko na shida za kifamilia. Ni mama ambaye
aliwafundisha watoto wake imani. Msingi wa imani kwa Mungu,
ndio uliwawezesha kupata mahitaji ya familia.
Margareti Occhiena na Fransisko Bosko
Margareti Occhiena Alizaliwa 1 Aprili, 7788 huko Capriglio.
Kwake dini ya karne nyingi, na ibada zake ilikuwa sehemu ya
maisha yake. Alikuwa na imani dhabiti katika sakramenti za
Kanisa na pia alielewa mambo makuu ya mwisho ambayo
yanaunda maisha. Alichukuliwa kwa umuhimu sana mafundisho
ya Katekismu yaliyoendelezwa kufundishwa katika mahubiri na
kudhihirishwa katika maisha ya kila siku na neema na ya Mungu.
Mambo hayo yalikuwa: Mbingu, kifo, toharani na moto wa
milele. Familia yake ilikuwa ya wakulima wa zabibu. Familia yao
yote ilifanya kazi kwa bidii. Walikuwa makini sana nyakati za
sala hasa ile sala ya saa sita ya Malaika. Familia yao ilikuwa na
msingi dhabiti wa imani na sala. Familia ya Margareti Occhiena,
kila siku walihudhuria misa bila kuchelewa.
Katika shuguli zao za kila siku waliweze kukutana na familia ya
Bosko. Fransisko alizaliwa 4 Februari 1784, katika ya watoto 12
sita walikuwa wamekufa wakati alifikia umri wa miaka sita.
Wakati Baba yake alikuwa na umri wa miaka 18. Ilimbidi
1

1.2 Page 2

▲back to top


achukue majukumu ya kuitunza familia yake. Mwaka 1801,
alimuoa Margaret Cagliero ambaye alimzalia watoto wawili,
Anthony aliyezaliwa 1 Machi, 1808 na Theresa aliyezaliwa 16
Februari 1810 na akafa siku mbili baada ya kuzaliwa.
Ukoo wa Bosko tangu mwaka 1624, ulikuwa maarufu sana.
Walikuwa walinzi wa mfalme na pia kazi ambazo zilihitaji ujuzi
wa hali ya juu. Ukoo huu ulijua sana matatizo na mahangaiko ya
nyakati zile hasa wakati wa vita. Mama Margareti alikuwa
mwanamke mwenye sifa ya sala na bidii katika kuitunza familia
yake na hasa aliwachukua watoto wa Fransiko kama wake. Mtu
hangefahamu tofauti yoyote kati ya watoto wa Margaret
Occhiena na wale wa yule mwanamke marehemu aliyekuwa mke
wa kwanza wa Fransisko. Aliwapenda wote na kuwatunza kwa
moyo. Aliilea familia yake katika imani. Kila asubuhi walisali,
walienda misa na pia aliwaanda vema kwa Sakramenti zote.
Alikuwa makini sana kuwaandaa kwa Sakramenti ya kitubio.
Alifahamu vema matunda na baraka ya hizo Sakramenti na hivyo
basi hakutaka familia yake ikose baraka za Mungu.
Alihakikisha walijua sala zote za nyakati mbalimbali,
alimtayarisha vema Yohane Bosko kwa sakramenti za Kanisa.
Alimlea katika imani na maadili hadi kufikia wito wa upadre.
Tuchukulie Yohane Bosko kipekee: alimfundisha kumsalimu
Bikira Maria kila siku kwa sala ya ‘Salamu Maria’. Mama
Margaret aliwafundisha watoto wake kuchukua majukumu ya
familia hasa ya kazi za shambani. Katika hii familia watoto
wengine walikuwa:- Joseph, Anthony na Teresa ambaye alifariki
katika umri mdogo. Hivyo basi, ni wazi kuwa Mama Margaret
alikuwa mama wa kipekee sana;- mama mwenye sala na imani
thabiti moyoni, na pia mama mwenye huruma na uvumilivu
moyoni. Alimtambua Mungu kuwa ndiye mlinzi na mfadhili
wake. Familia ilipata pigo kuu wakati Fransisko Bosko alikufa.
Ni wakati huu ambapo Yohane Bosko alikuwa tu na umri wa
miaka miwili.
Majukumu yote ya familia yalimwangukia Mama Margaret
Occhiena. Mama huyu alionja taabu ya kuwalea watoto bila baba,
2

1.3 Page 3

▲back to top


alipiga moyo konde na kumwamini Mungu. Uwezo wake mkuu
ulitokana katika imani thabiti ambayo alipokea kutoka kwa
wazazi wake. Alitimiza wajibu wake na kumtumainia Mungu
pekee. Yeye ni mfano bora wa mama ambaye anaelewa
majukumu yake ya familia na pia majukumu ya imani yake.
3

1.4 Page 4

▲back to top


MAISHA YA MTAKATIFU YOHANE BOSKO
Yohane Melchior Bosko alizaliwa tarehe 16 Agosti 1815.
Alizaliwa na kukulia katika jami na parokia ya Castelnuovo
d’Asti nyakati hizi inaitwa Castelnuovo Don Bosco, katika kijiji
cha Becchi. Baba yake aliitwa Francis Louis ambaye alikuwa
hapo awali alioa na mkewe wa kwanza akafa, alikuwa na watoto
wawili: Antoni na Teresa ambaye alifariki katika umri mdogo.
Katika ndoa yake ya pili alimwoa Margaret Occhiena wa Serra
Capriglio[ 1788-1856] na walikuwa na watoto wavulana Joseph[
1813-1862] na Yohane[1815-1888]. Yohane alizaliwa 16 Agosti
1815 na akabatizwa siku iliyofuata katika Kanisa la Mt. Andrea
na Padre Joseph Festa. Wasimamizi wake walikuwa Occhiena
Melchior wa Capriglio na Magdalene Bosco wa Castelnuovo.
Familia yake Yohana Bosko ilikuwa maskini sana, walikuwa na
shamba dogo, nyumba kiasi na bustani la mizabibu. Kwa
kuiwezesha familia; baba Fransisko alimfanyia kazi mtu mmoja
tajiri, shambani la mizabibu. Siku moja alirudi akiwa afya yake
imezoroteka kwa kuugua. Bahati mbaya Fransisko alikufa 11
Mei, 1817 wakati Yohane alikuwa na umri wa miezi 21 karibia
miaka miwili hivi. Yohana hakuelewa kuwa baba yake alikuwa
amekufa, alidhani amelala tu na kwa nini haamki. Mama yake
alimfahamisha kuwa hana baba tena na hatamwona katika
ulimwengu huu.
Kifo cha Fransis kilikuwa pigo kubwa sana kwa familia; ilibidi
mama yake Yohana Bosko, yaani Mama Margaret Occhiena,
achukue majukumu yote ya familia. Mama huyu alikuwa mama
wa sala, mnyenyekevu, mvumilivu na aliyewakaribisha maskini,
japo walikuwa familia maskini iliyohangaika sana. Hakuweza
kusoma na kuandika lakini alikariri mafundisho ya Kanisa na
Katekismu moyoni mwake. Antoni yule mwana wa mke wa
kwanza aliwahangaisha sana, hakua mtii. Mama Margaret
alihuzunika sana kwa sababu Antoni alikuwa mtu mnyanyasaji,
mwenye kiburi ambaye alimhangaisha Yohane Bosko katika umri
mdogo alimtaka awe anafanya kazi zote za nyumbani na
shambani. Antoni aliona kwenda shule ilikuwa kupoteza nafasi ya
maendeleo katika familia.
4

1.5 Page 5

▲back to top


Ndoto katika umri wa miaka Tisa
Wito wa Yohane Bosko waanza kujidhihirisha rasmi katika
ndoto, ambayo inakuwa dira ya maisha yake yote. Yohane Bosko
akiwa na umri wa miaka tisa, aliota ndoto ambayo ilimwongoza
katika maisha yake yote. Katika ndoto alijipata akiwa katika
uwanja. Na hapo kulikuwa na watoto waliocheza ambao
walitumia lugha ya matusi. Yohane Bosko alijaribu kuwakanya
kwa kupigana, waache kutumia lugha hiyo iliyowaelekeza katika
dhambi bali hawakumsikiliza.
Mara mwanamume mmoja wa ajabu alijitokeza akamweleza
Yohane Bosko, kuwa hataweza kuwaongoa hao vijana kwa vita
au kupigana nao, bali katika upole na upendo watatambua uovu
wa dhambi na kupenda wema na uadilifu. Hatimaye mwanamke
wa ajabu na mzuri alitokea pia. Alimshika Yohane Bosko mkono
kwa upole akamwonyesha kundi la wanyama wa mwituni
waliogeuka na kuwa wanakondoo. Mama huyo alimwambia,
Uwe mnyenyekevu, mvumilivu na mwenye nguvu”. “Yale
unayoona yakiwatendekea wanyama hawa; nawe utawafanyia
wanangu”. Yohane Bosko alihisi kuwa Yesu na Bikira Maria
wakimpa utume wa kutunza watoto na vijana walio katika shida.
Yohane Bosko, alikuwa bado na hofu, hatimaye aliambiwa na
yule mama, “katika muda mwafaka utaelewa”. Baada ya
Upadrisho alisali misa katika altare ya Bikira Maria Kanisa la
Moyo Mtakatifu wa Yesu, huko Roma. Don Bosko alipatwa na
furaha ambayo iliambatana na machozi kwa sababu aliielewa
hiyo ndoto ya miaka tisa. Na alisema kuwa ni Bikira Maria
aliyemfumbulia hayo.
Maisha ya shule magumu
Antoni hakupenda Yohane Bosko aende shule, alimtaka afanye
kazi ya shamba pamoja na wao kwa sababu hakuelewa umuhimu
wa kwenda shule. Hakuelewa nia ya Yohane Bosko ya kutaka
kuwa padre. Katika umri mdogo Yohane Bosko aliwakusanya
watoto wa umri wake, aliwasomea hadithi za kusisimua,
aliwafanyia michezo ya sarakasi, kutembea juu ya kamba,
mwishowe alisali sala ambayo mama yake alimfundisha - sala ya
5

1.6 Page 6

▲back to top


salamu Maria’. Nia ya michezo yake ilikuwa ni kuwakusanya
watoto na vijana ili kuwafundisha sala na maisha ya Mungu.
Mama yake Margaret alimwandaa kwa Komunyo ya kwanza na
tarehe 26 Mach 1826.
Shamba la Moglia
Kwa vile Antoni aliendelea kumsumbua sana Yohana Bosko,
Mama Margaret alimhamisha Yohane Bosko hadi shamba la
Moglia apate kazi huko na atoke katika usumbufu. Kila Jumapili
aliweza kutembea kwa nusu saa kwenda Sakramenti ya kitubio
huko Moncucco. Muungamishi wake alikuwa Padre Cottino
alisikiliza kitubio chake. Kazi yake ilikuwa kuchunga ngombe au
kazi zingine za shambani.
Katika umri mdogo aliweza kuwafundisha watoto wengine
kumhusu Yesu. Akienda kuchunga ngombe alienda na kitabu cha
Kilatini kujisomea kwa sababu, alisema kuwa anajiandaa kuwa
padre. Kwa sababu ya kukosa baba katika umri mdogo, aliweza
kupatwa na usumbufu wa namna mbalimbali na kukosa mtetezi.
Kufuatana na maisha yake alianza kuelewa pia taabu na magumu
ambazo ziliwapata vijana wengine.
Maisha ya Seminari
Cheri ndiyo Seminari, Yohane Bosko alipata nafasi ya kupata
malezi na elimu ya kuwa padre. Mnamo tarehe 4 Novemba 1831,
Yohane Bosko alingia Seminari iliyokuwa umbali wa kilomita 12
hadi Castelnuovo. Cheri ulikuwa mji wa wamonaki. Yohane
Bosko aliweza kubaki huko miaka 10. Shuleni walisisitiza maisha
ya Kikristo, misa kila siku, Sakramenti ya Kitubio, cheti cha tabia
njema na kitabu cha sala. Yohane Bosko alisoma vizuri na
alikuwa na kumbukumbu ya hali ya juu kimasomo.
Malezi ya Upadre na Daraja ya Upadre
Yohane Bosko alitafuta ushauri wa Padre Cafasso ambaye
alikuwa baba wake wa kiroho. Padre Cafasso na Padre Cincano
walimsaidia akaingia seminari ya jimbo mnamo tarehe 30 Oktoba
1835. Katika seminari aliweza kuacha kiamsha kinywa na
6

1.7 Page 7

▲back to top


kukimbilia Kanisa la Mt. Philipo ili kupokea Ekaristi Takatifu.
Mwaka 1841 alipata ushemasi. Alipadrishwa jumapili ya Utatu
Mtakatifu Jumapili tarehe 5 Juni 1841 na Askofu Mkuu Fransoni.
Baada ya kupata daraja la upadre Don Bosko alijiwekea malengo
yafuatayo siku hiyo:
Kutumia muda wake vizuri;
Kuwa na ukarimu kama wa Mt. Fransisko wa Sale;
Masaa tano au sita kulala usiku na wakati wa mchana
hamna kulala.
Alisali misa yake ya kwanza katika sikukuu ya Utatu Mtakatifu,
katika Kanisa la Mt. Fransisko wa Assisi, Torino katika altare ya
malaika mlinzi. Siku hii ilikuwa kweli yenye furaha na ilikuwa
sikukuu kabisa ambayo aliikumbuka miaka mingi.
Utume kwa vijana
Alitembelea katika njia za miji na akaona vijana wenye umri
mbalimbali wakiwa wanajiingiza katika mambo ya utundu na
maasi. Walikuwa wametoka sehemu mbalimbali za vijiji. Mwaka
1844, alishuhudia vijana 7148, wenye umri wa miaka 10 wakiwa
wameajiriwa kwa kazi mbalimbali kama, ushonaji, wajenzi,
wapaka rangi. Alitembelea magereza na akahuzunishwa sana
kuwaona vijana wenye nguvu na akili umri kati ya miaka 12-18,
wakiwa gerezani. Hali hii ilianza kumpa mawazo ya kutenda
jambo la kuwasaidia hawa vijana.
Mwanzo wa kazi kuu
Tarehe 8 Desemba 1841, Sikukuu ya Maria Mkingiwa dhambi ya
asili, katika Kanisa la Mt. Fransisko wa Assisi, akijiandaa kwa
misa alimwona Comotti msakristia akimfukuza kijana mwenye
umri wa miaka 16. Kijana huyu aliitwa Bartholomayo Garelli.
Alifukuzwa kwa sababu hakujua kutumikia altareni. Baada ya
Padre Yohane Bosko kumhoji, alipata kutambua kijana hakuwa
amepokea Komunyo ya kwanza. Alianza kumfundisha
Katekismu. Kwa kuona upole na upendo wa Padre Yohane
Bosko; Bartholomayo alirudi Jumapili iliyofuata na vijana
7

1.8 Page 8

▲back to top


wengine 6. Idadi ya vijana iliendelea kuongezeka na nafasi
ilianza kuwa ndogo.
Ukarimu na upendo wa Padre Yohane Bosko, uliwavutia vijana
wengi kwake. Na hasa sana ule uwepo wake kati yao. Alitumia
muda mwingi mno kuwa kati ya hawa vijana. Vijana walimwona
padre mwema, aliyewajalia kiroho na kimwili. Padre kuwa kati
yao, ilileta usawa, hamna kijana alimdhulumu mwingine hata
kidogo. Vijana walianza kukua kiroho na kimwili. Walifurahi
kuwa miongoni mwa kundi kubwa lilokuwa karibu na padre.
Nyumba ya Pinardi
Baada ya kuhangaika sana, Padre Yohane Bosko alibahatika
kupata sehemu ya shamba ambapo alianzisha oratori. Mnamo 22
Aprili 1846, Pasaka Jumapili; Askofu Mkuu alibariki hiki
kiwanja. Vijana walipata nafasi ya misa, mafundisho ya dini,
michezo, muziki na mengine mengi yaliwavutia vijana wengi.
Wasaidizi mbalimbali walianza kujitokeza. Tarehe 3 November
1846, Mama Margareti alifika kuwasaidia vijana. Padre Yohane
Bosko alijenga Kanisa dogo ambalo alisali misa pamoja na
vijana. Hadi wa sasa kuna kikanisa kilijengwa ili kuweka huo
ukumbusho. Kauli yake Mtakatifu Yohane Bosko ilikuwa
kuwalea vijana ili wawe Wakristo wema na raia wema.
Vyuo vya ufundi
Bidii na sifa za Don Bosko zilienea Italia nzima. Alitenda miujiza
mingi, alijenga makanisa, shule na vyuo vikuu, shule za ufundi
kama useremala, uhunzi na kadhalika. Lakini kadiri sifa zake
zilivyoenea vivyo hivyo ndivyo alivyopata maadui wengi.
Wafitini na maadui wa dini Katoliki walimsumbua sana Don
Bosko. Mara nyingi walimjaribu na kushindana naye juu ya dini,
lakini hawakufua dafu mbele yake; walishindwa vibaya sana.
Baadaye walikusudia kumua. Walimvizia mara kwa mara, lakini
Mungu alimtuma mbwa mkubwa aliyeitwa Grijo ili amkinge
mtakatifu wake na kuwafukuza maadui. Hata hiyvo Don Bosko
hakujua mbwa huyo alitoka wapi. Maana alimfikia na kumwokoa
wakati alipokuwa katika hatari.
8

1.9 Page 9

▲back to top


Kazi zake zote Don Bosko, mfadhili wake alikuwa Mama wa
Kristo. Alimletea msaada kwa namna mbalimbali. Watu wenye
nia njema na wafadhili walifika kumsaidia katika kazi zake. Kazi
zote zilifikia utimilifu. Na ulinzi na ufadhili huo bado aliukabidhi
kwa kazi zake zote ulimwenguni. Mahali popote ambapo kuna
jumuiya ya Mt. Yohane Bosko; pana ulinzi wa Bikira Maria na
nguvu za Mungu. Ni imani iliyo kuu sana kujua na kuamini hayo
yote.
Shirika la Waselisiani wa Don Bosko
Mwaka 1854 Don Bosko aliwaunganisha wasaidizi wake katika
Shirika, ili kazi yake ya kuwaongoza na kuwalea vijana
iendelezwe nao kwa kuwa alimthamini sana Mt. Fransisko wa
Sale, wasaidizi hao wakaitwa Wasalesiani wa Don Bosko. Baadhi
yao aliwatuma kama wamisionari kuhubiri injili katika nchi za
Amerika ya Kusini, Afrika, China, Ujapani na visiwa vya Uhindi.
Shirika la Waselisiani wa Don Bosko ni la kimataifa na ni la
kimisionari.
Shirika la Masista wa Maria, Msaada wa Wakristo
Zaidi ya kuwaongoza wavulana, Don Bosko alielewa mahitaji ya
wasichana. Hivyo mnamo mwaka 1872 akisaidiana na mama
Maria Mazarello, alianzisha Shirika la mabinti, nalo huitwa
Shirika la Mabinti wa Maria, Msaada wa Wakristo. Shirika hili ni
kwa ajili ya kuwalea wasichana. Maria Mazarello alitangazwa
kuwa Mtakatifu mwaka 1951. Don Bosko alifariki mwaka 31
Januari 1888 akiwa mzee mwenye miaka sabini na mitatu.
Mwaka 1934 alitangazwa rasmi kuwa mtakatifu na msimamizi
wa vijana. Kila mwaka Waselisiani hufanya Sikukuu ya huyo
Mtakatifu kila tarehe 31 Januari.
Vikundi vingine
Katika familia ya Waselisiani wa Don Bosko kuna vikundi hivi
pia: Waselisiani washiriki :- hawa ni wale waamini na watu
mbalimbali ambao wanavutiwa na maisha ya Don Bosko,
wanajiunga ili kuendesha karama ile ya Don Bosko kama walei
9

1.10 Page 10

▲back to top


kwa namna mbalimbali, aidha kuwa wafadhili wa kazi na utume
wa waselesiani au kufundisha na kushiriki kazi zote. Wale wote
waliosoma shule za Don Bosko na wale pia wamelelewa katika
parokia za Don Bosko hao pia wana nafasi maalum katika shirika
na wanashika nafasi ya kusaidia utume wa Don Bosko kwa hali
na mali. Kikundi cha Maria Msaada wa Wakristo nacho,
kinaeneza ibada kwa Ekaristi Takatifu na heshima kwa Mama
Bikira Maria.
Utakatifu wa Yohane Bosko
Yohana Bosko alikuwa mtu aliyesali sana. Alikuwa na imani kuu
kwa Mungu. Msingi wa wake wa utakatifu ulikuwa: - upendo
kwa Bikira Maria, Ibada kwa Yesu katika Ekaristi Takatifu,
Elimu ya malezi kinga ambayo imejikita katika furaha na
matumaini na Ibaada kwa Kanisa na heshima kwa Baba
Mtakatifu. Kwa ukarimu wake, Mungu alimpa yote katika wito
wake. Mungu alimpa miujiza mingi na matendo makuu kwa ajili
ya kudhihirisha utukufu wake. Aliweza kuwaponya watu wengi
wakiwemo viziwi, viwete na wakati mmoja alimfufua kijana
mmoja.
Alikuwa na uwezo wa kutabiri. Aliweza kutumia sala na imani
kuu kwa Mungu kuwasaidia wahitaji. Aliwaeleza vijana wake
kuwa mtakatifu mtu hauhiitaji mambo mengi ya ajabu, ni
kutimiza wajibu wa kila siku hali umeungana na Mungu katika
moyo wako. Aliwaeleza vijana wake wasifanye malipizi ya ajabu.
Aliwaambia Waselesiani na vijana kuwa:- Mungu ataka sisi
tuwe na furaha na kufurahia upendo wa Yesu”.
Don Bosko aliwaeleza kuwa, watimize wajibu wao, nyumbani,
shuleni na majukumu mengine. Aliwaeleza wamtolee Mungu
maisha yao hata nyakati za furaha na huzuni. Aliwafahamisha
kuwa maisha yanatuletea nafasi nyingi kushiriki mateso ya
Kristo: Kama hali ya hewa, kushindwa kufaulu jambo fulani,
ugonjwa wa mwili, huzuni mambo haya yatakufanya mtakatifu.
Katika shule ya Don Bosko kulitokea kijana mtakatifu aliyeitwa
Dominiko Savio. Mt. Dominiko Savio kijana wa Don Bosko
10

2 Pages 11-20

▲back to top


2.1 Page 11

▲back to top


aliaga akiwa na miaka 14, baadaye alitangazwa Mtakatifu. Huyu
anatuonyesha utakatifu upo kwa ajili ya kila mmoja.
Mafundisho kumhusu Mtakatifu Yohane Bosko
Mtakatifu Yohane Bosko alikuwa mtu wa Mungu, rafiki wa
Mungu maana mara zote alikuwa ameunganika na Mungu katika
sala. Aliwaongoza wafuasi na vijana wake katika upendo wa
Mungu. Alielewa kuwa wito wake ulikuwa zawadi kwa watoto na
vijana na ndiposa, akaishi nadhiri ya utii, Useja na ufukara
(Obedience, Chastity and Poverty).
Yaani maisha yake ilikuwa kumpa Mungu utukufu wake kwa
kuwalea vijana katika imani, kazi na furaha. Mtakatifu Yohane
Bosko ni mwalimu kwa sababu yeye alielewa kumkomboa
mwanadamu ni kumpa elimu kuanzia umri mdogo. Kumpa kijana
uhai ni kumfundisha kumjua Mungu, kumtii na kumtumikia
katika talanta na ujuzi wa maisha. Mtakatifu Yohane Bosko ni
baba wa vijana kwa sababu aliwalea vijana wake kwa maadili,
aliwatakia mema na walimwona nyakati nyingi akiwa pamoja
nao; katika michezo, masomo, sala na kazi. Mtakatifu Yohane
Bosko alikuwa rafiki wa Mungu kwa sababu ya mambo muhimu
aliyoweka mkazo:
Upendo kwa Maria Msaada wa Wakristo;
Ibada kwa Yesu katika Ekaristi Takatifu;
Mtindo wa elimu, furaha na matumaini;
Utii na upendo kwa Kanisa la Yesu Kristo.
Kazi na utume wa Don Bosko bado unadhihirika hapa
ulimwenguni na hasa katika Afrika mashariki kuna shughuli
nyingi za utume wa Don Bosko.
Oratori
Mwaka 1840 kando mwa mji wa Torino kulikuwa watu maskini
sana, vijana na watoto waliokuwa wakichukuliwa kufanya kazi
viwandani. Yohane Bosko alitambua utume wake ulikuwa hapo.
Alitembelea magereza na Padre Cafasso ambaye alikuwa baba
wake wa kiroho. Kwa kuwasaidia hawa vijana bila senti lakini
11

2.2 Page 12

▲back to top


kwa imani kwa Bikira Maria alianzaisha Oratori. Oratori ilikuwa
sehemu ya sala na pia ya burudani, ambapo vijana walikusanyika
kila Jumapili. Sehemu hii ilikuwa aidha parokiani, shuleni au
uwanja ulio wazi. Don Bosko aliwafundisha vijana na watoto:
Katekismu, sala, Neno la Mungu na aliwapa pia nafasi ya
kucheza michezo mbalimbali na hatimaye kuwapa wazo njema
kabla hawajatawanyika. Mwanzoni Don Bosko alipata sana shida
kuendeleza utume wake wa Oratori, hakuwa na sehemu maalum
bali alikuwa akihamahama. Alikuwa anakutana na hawa vijana
kila juma.
Oratori ya Mt. Yohane Bosko ilikuwa na madhumuni manne
muhimu. Alitaka Oratori yake kuwa shule, sehemu ya michezo,
sala na nyumbani kwa vijana na watoto. Hizo sehemu zote
zilikuwa muhimu kwa makuzi ya watoto na vijana. Ilikuwa ni
nafasi ya kumsaidia kijana kukua mkamilifu. Kama alimwona
kijana Kanisani tu pekee na katika michezo haonekani alijua kuna
hali yake haikuwa nzuri. Kama kijana alionekana hana ushirika
na wenzake alitafuta kujua ni kwa nini. Kama kijana alipendelea
tu kujisomea na hana ushirika na wengine, angelijitahidi
kumsaidia kujifunza kuishi vema na wengine. Zile sehemu nne za
vijana muhimu kwa makuzi yao ni kama ifuatavyo:
Nyumbani Sehemu ambayo kijana anajisikia nyumbani,
huru sana na salama.
Shule Sehemu ya kuelimika ambayo inamletea kijana
maarifa, mambo mapya ya kumpa matumaini
Kanisa Sehemu ya kuelewa maisha na kukua kiroho,
kumfahamu na kumjua Mungu.
Uwanja wa michezo sehemu ya burudani, kukuza vipaji,
kufurahi na pia kujifunza kushirikiana na wengine.
Kama wazazi, vijana, marafiki na walimu wakielewa maneno
hayo manne hapo juu, basi ni rahisi sana kuelewa kwa kiundani
karama ya Mt. Yohane Bosko. Huyo Yohane Bosko alielewa
kuwa vijana walitaka kujisikia nyumbani, sehemu ambayo
12

2.3 Page 13

▲back to top


wanakaribishwa na kukubalika. Wakati vijana wanajisikia salama
na furaha, ni rahisi kwao kujenga imani na pia makuzi mazuri.
Watakuwa na uhuru wa kueleza mawazo yao na hisia zao. Vijana
wakikosa ile hali ya kuwa wazi na kujisikia salama, basi
watafunga mioyo yao kwa sababu watatawaliwa na woga.
Kama mazingira ya Mt. Yohane Bosko yalikuwa sehemu ya shule
na elimu, basi tukumbuke kwamba ilikuwa ni njia mojawapo ya
kuwaondoa vijana toka umaskini. Shule na elimu kwa Mt.
Yohane Bosko ilikuwa ule upendo moyoni wa kumwona akiwa
na furaha na matumaini. Kama vijana wanaushirikiano mwema
basi wataweza kujifunza mambo ya msingi ya maisha, kama
kujitambua wao ni nani, wana talanta zipi, mapungufu yao. Hivyo
Basi Mt. Yohane Bosko aliweza kufanya kila hali ya kujielimisha
kwa kijana: michezo, kazi, ushauri, mahangaiko na shida
mbalimbali. Alitamani sana katika kila oratori wakati vijana
wamekusanyika kuwepo na Msalesiani au mlezi au mwalimu au
mzazi ambaye atawasaidia kwa kirafiki vijana wajitambue.
Katika michezo vijana na watoto wapaswa kuweka bidii na nguvu
zao katika michezo, mazoezi. Mt. Yohane Bosko alitambua kuwa
waelimishi wengine walifikiri kuwa ilikuwa kupoteza wakati
kuwa kati ya vijana. Mt. Yohane Bosko alielewa michezo kuwa
sehemu maalum kwa kijana, kwa sababu ilikuwa aina moja ya
kusherehekea maisha. Umuhimu wa michezo na shughuli za
kawaida huonekana kuwa si jukumu ngumu. Hivyo basi
inafanyika kwa njia ya upendo na furaha na inatuwezesha
kutumia muda vizuri.
Mt. Yohane Bosko alithamini sana michezo na shughuli za
kawaida zilizompa kijana nafasi ya kucheza na kufurahi hivyo,
kumpa nafasi ya kukua kimwili na kiroho. Nia ya Mt. Yohane
Bosko kuweka Oratori zake karibu na eneo la Kanisa ilikuwa
kushirikisha imani na furaha kama sehemu ya makuzi. Mt.
Yohane Bosko alitaka kila hali itambulike uwepo wa Mungu.
Aliweka kanisa wazi kila siku mpaka jioni. Aliwashauri wote
kwenda ndani ya Kanisa mara kwa mara hata wakati wa michezo
au wakati wa mapumziko. Ndivyo ilivyo desturi katika vyuo na
13

2.4 Page 14

▲back to top


shule zote za Mtakatifu Yohane Bosko, wote wanashauriwa
kutembelea kanisa na kusali kwa muda mfupi hata ingebidii mara
nyingi, kuwakumbusha uwepo wa Mungu.
Oratori ndio maisha ya Waselesiani wa Don Bosko mahali popote
walipo. Hapa Afrika Mashariki na sehemu zingine Afrika na
ulimwenguni kote, utakuta watoto na vijana wakiwa wengi katika
vituo vya Don Bosko. Utapata maisha ya oratori kadiri
ilivyoelezwa hapo juu. Hapa Afrika Mashariki oratori huwa
sehemu kijana wowote hapendi kukosa, maana ndipo mahali
hupata furaha. Wengi waliopata nafasi ya maisha hayo ya Oratori
huwa na kumbukumbu njeam zaidi. Hasa hapa Kenya oratori
zinawapa watoto nafasi ya kukutana na Waselesiani na marafiki
wa Don Bosko kutoka mataifa mbalimbali. Moyo wa Oratori ni
kuwa, wote hujisikia nyumbani na pia katika familia moja. Japo
wengi huvutiwa na michezo pamoja na burudani lakini, hukua
katika hali zote za kiroho na kimwili.
Katika oratori, vijana na watoto huonja upendo wa mchungaji
mwema. Huwa kuna mapadre au masista au mwalimu au
Waselesiani washiriki, ambao kwa uwepo wao huwa alama ya
usalama. Ni watu ambao watawapa mawaidha na pia kuwapa
ulinzi endapo watajisikia wanahitaji lolote. Kwa hivyo watoto na
vijana huwa na furaha na uhuru kwa sababu wanajisikia furaha
kuwa kuna watu ambao watawakimbilia kwa hitaji lolote. Hii
ndiyo alama ya mchungaji mwema kati ya watoto na vijana.
Ukitaka kujua hali ya oratori tembelea vituo vya Waselesiani
hapa Kenya na sehemu zingine za Afrika.
Katika oratori, tulitambua maisha ya Waselesiani wa Don Bosko:
mapadre, mabruda, masista na wasaidizi wengine. Watoto na
vijana wanapofika katika sehemu hizo wanakutana na
makaribisho ya furaha. Ni wao wa kwanza kukufikia na
kukusalimia na pia kukuuliza hali yako na kukupa neno la kukupa
matumaini. Unajisikia upo nyumbani na pia waweza kujifunua
hali yako ya roho na kusema shida ambayo ina kukera, iwe ya
familia yenu au kawaida. Katika oratori, katika umri mdogo
watoto na vijana hukuza vipaji mbalimbali, kama vya michezo,
14

2.5 Page 15

▲back to top


muziki na sana sana, utakuja kukuza paji la sala. Ni hapo
utaelewa maana ya Ekaristi Takatifu, utasikia habari ya Mungu,
utawajua maisha ya watakatifu wengi na zaidi utajifunza kuwa
mkristo mwema na raia mwema, kwa sababu unajifunza kuishi na
wengine katika michezo mbalimbali. Na hapo ndipo unajenga
utu, urafiki na hali ya moyo mwema.
Wazazi na walimu, wakielewa maana ya oratori na kuwapa
watoto wao, mafanikio huwa makubwa sana hasa katika masomo.
Kwa sababu oratori huleta nidhamu ndani ya kijana na watoto
pasipo kutumia ukali na adhabu bali upole na maelekezo mema.
Hali hiyo umfanya mtoto kupenda elimu na imani, mambo
ambayo yanampa makuzi mazuri. Watoto na vijana hujisikia watu
maalum, na hivyo hujenga mawazo mazuri na tabia njema.
Waselesiani wa Don Bosko wapaswa kusambaa Kenya yote ili
watoto na vijana wapate nafasi katika karama hii ya Mtakatifu
Don Bosko. Kilele cha mambo yote, ni kukuza miito. Vijana na
watoto wengi huvutiwa na miito mitakatifu kwa hali ya
wanayoona katika oratori.
Mtindo wa Malezi Kinga wa Mtakatifu Yohane Bosko
Mtakatifu Yohane Bosco ambaye hujulikana kama Don
Bosco, Kanisa lamtambua kuwa Baba na mwalimu wa vijana.
Ajabu ni kwamba katika historia ya maisha yake, Yohane Bosco
alifiwa na baba yake akiwa mdogo sana wa miaka miwili tu ,
mama yake hakuwa na uwezo wa kumpeleka shuleni . Misaada
ya wenye huruma na juhudi zake mwenyewe ndizo zilimwezesha
kumaliza masomo yake. Alijenga maisha yake katika ukarimu wa
watu wengine.
Akiwa Padre kijana, alikabiliana na vijana waliokuwa
wakimiminika katika mji wa Torino, Italia kaskazini, kutafuta
masilahi yao. Hali ilvyokuwa enzi hizo si tofauti sana na sasa
huku kwetu, vijana hawakupewa fursa ya kufanya lolote halali.
Hivyo Don Bosko alisikitishwa sana na hali ya vijana wengi
kuingia gerezani kwa sababu ya makosa mbalimbali. Upotovu
wa vijana ulizidi , na kwa kuwa walikuwa wengi waliomiminika
mjini, mabepari na wowote wanaotaka kujinufaisha kutokana na
15

2.6 Page 16

▲back to top


hali hiyo, waliwanyanyasa vijana. Don Bosko alizoea kuzuru
katika magereza mbalimbali pamoja na Padre mwenzake
aliyeitwa Joseph Cafasso. Kuona hali jinsi ilivyo kuwa Don
Bosco alijiuliza swali, ni tendo lipi laweza kufanyika ili vijana
wasiingie gerezani?
Swali hilo lilimfanya Don Bosko kubuni mbinu za kuwasaidia
vijana wasiingie gerezani. Hayo ndiyo yaliyokuwa mapendo ya
Don Bosko kwa vijana hawa wa mitaani ili wasiingie gerezani
tena. Alianzisha mtindo wa elimu wa kulea vijana ambao
unahusu: kuzuia kuliko kuponya, akauita elimu malezi kinga
(Preventive system of Education)
Mambo Muhimu ya Mtindo huu na kwa nini yafaa yatumiwe
Kwa kawaida kuna mitindo miwili ya malezi ambayo imekuwa
ikitumika kote mpaka sasa. Kuna mtindo wa kuzuia maovu
yasimpate kijana (Preventive) na ule wa kukandamiza kijana au
kumfunga asitende maovu (repressive system). Mitindo hii
huwafanya vijana wasitende maovu au wasipotoke,
kinachofanywa kwanza ni kutunga sheria zinazokataza mambo
fulani. Mtindo wa (repressive) hutawaliwa na yafuatayo:
1. Kuzifanya sheria zijulikane kwa wote.
2. Kuchunguza anayezivunja sheria hizo.
3. Na mwisho kuwaadhibu wavunjao sheria ili mambo hayo
yasirudiwe tena.
Mtindo huo hapa juu ni kinyume kabisa katika malezi ya mtoto
au kijana. Elimu ya malezi kinga (preventive) yahitaji sheria
zitungwe pia na zijulikane kwa wote wanaohusika. Katika mtindo
huu, mkuu au Gombera na wasaidizi wake ni lazima wawe
miongoni mwa vijana na wanafunzi ili vijana wakumbushwe
yawafaayo kufanya na vijana wasipate nafasi ya kutenda jambo
mbaya, mfano kutusiana, kugombana au kupigana.
Walezi wapaswa kuwa miongoni mwa watoto na vijana si kama
polisi au watu wenye kutiisha amri kwa uwezo wao, bali wawe
kama wazazi, ndugu, rafiki, wenye kutoa msaada ukihitajika .
16

2.7 Page 17

▲back to top


Watazungumza na watacheza nao, kuimba nao na hata kutembea
nao, mradi wawe tayari kila mara kuwaonyesha watoto na vijana
yanayoweza kuwapata ili vijana yasiwashawishi kutenda kosa au
dhambi. Sehemu hizo ni Kanisa, bwaloni, michezoni, kazini na
darasani na wakati wa mapumziko.
Msingi wa mtindo wa kuzuia maovu (preventive system) ni :
1. uwezo wa kutoa na kutambua sababu.
2. Imani thabiti katika misingi ya dini - Katoliki
3. Moyo na vitendo vya mapendo.
Mtindo huu wa malezi unafaa kwa sababu zifuatazo:
Kwa kijana aliye na habari ya namna ya mtindo huo unavyo
fanya kazi, hakati tamaa upesi kama akianguka katika makosa au
dhambi.
1. Watoto Ni watukutu tena hawaoni mbali katika mawazo yao,
kidogo tu wamesahau umuhimu wa sheria hii na adhabu au
maonyo yawezayo kufuatia.
2. Ule mtindo wa (repressive) wa malezi , amri kali ya kuzuia
vijana wasifanye makosa unaweza kufanya nidhamu ya
mahali , lakini hauwasaidii wahusika kuwa watoto na vijana
bora zaidi .
3. Kwa mtindo wa kinga maovu ,vijana wanaelewa zaidi
sababu hii au ile ,anenalo kwa lugha ya moyo wakati
wakiwa shuleni au hata katika maisha yao ya baadaye.
Kauli yake Mtakatifu Yohane Bosko ilikuwa kuwalea vijana ili
wawe Wakristo wema na raia wema. Na katika hali ya malezi huo
ndio mtindo bora ambao huyo mtakatifu alitumia kwa miaka
mingi kwa ajili ya kuwaokoa vijana. Alitembelea hata magereza
na kuwaongoa vijana.
17

2.8 Page 18

▲back to top


FAMILIA YA BIKIRA MARIA
Familia ya Bikira Maria
Kumfahamu Bikira Maria ni vema kuanza na familia yake.
Kutokana na mapokeo ya zamani karibu karne ya pili
tunafahamu kuwa Yoakimu na Anna ndio wazazi wa Bikira
Maria. Yoakimu alitokea katika kabila la Yuda na ukoo wa
Daudi. Naye Anna mkewe alizaliwa katika ukoo wa Haruni,
kuhani Mkuu. Katika maandiko ya Mt. Yeronimo anatueleza ya
kuwa; hawa wazazi wawili waligawa mali yao mafungu matatu:
fungu moja lilitumiwa kwa kupamba hekalu la Yerusalemu; fungu
jingine waliwagawia maskini; na fungu la tatu walilihifadhi kwa
chakula chao wenyewe. Ukarimu huo wao ni ishara ya utakatifu
uliokuwa mioyoni mwao. Mazingira yao yalikuwa matakatifu
sana, ndipo Mungu aliwateua wawe wazazi wa Bikira Maria. Hivi
ndivyo familia zapaswa kuwa chemichemi za wito.
Tangu zamani karne ya sita Wakristu walizoee kuwaheshimu
wazazi hao. Mt. Yohani wa Damasko aliwasifu akisema:
Tunawatambua ninyi wawili kutokana na mtoto mliyemzaa”.
Bikira Maria asiye na doa aliweza kuzaliwa tu na wazazi wenye
moyo safi, na mama wa Mungu sharti azaliwe na wazazi
waliokuwa marafiki wa Mungu. Kama katika familia watu
watasali kwa bidii basi hayo yanakuwa makao ya Mungu. Na ni
dhihirisho kuwa familia zote zimo katika mpango wa Mungu.
Kuzaliwa Bikira Maria
Tarehe 8 Desemba tunasherehekea sikuu ya Bikira Maria
mkingiwa dhambi ya asili. Sherehe hii ni ya Maria imakulata
maana yake “asiye na doa”. Tangu zamani za kale Wakristu
wengi wamesadiki kwamba Maria alikingiwa dhambi ya asili.
Mungu alimwuumba Bikira Maria, na tangu milele alikuwa
amemchagua awe Mama yake. Ukweli unaokumbukwa ni
kwamba, Maria tofauti na watu wengine wote, hakurithii dhambi
ya asili wala hakutenda dhambi yo yote kwa hiari yake alipoweza
kuchagua kati ya jema na baya.
18

2.9 Page 19

▲back to top


Hivyo tangu mwanzo wake, alipokuwamo bado tumboni mwa
Mamae Anna, Maria alikuwa Mtakatifu sana akimwelekea
Mungu tu. Mara Maria alipotungwa tumboni mwa Mamae,
Mungu aliijaza roho yake neema ya utakaso, na hivyo Maria
hakujua kabisa tamaa mbaya inayomvuta mtu atende dhambi.
Hali hiyo nzuri iliwezekana kwa ajili ya mastahili ya kifo chake
Yesu Kristo ambaye Maria aliwahi kushirikishwa hata kabla ya
Yesu hajazaliwa bado. Hivyo ni wazi, kwamba kama vile
wanadamu wote, Maria naye aliokolewa na Mwanae Yesu aliye
Mwokozi wa watu wote kabisa.
Fundisho hilo lilitangazwa kuwa nguzo ya imani yetu ya
Kikatoliki mnamo tarehe 8 Desemba 1854 na Papa Pius IX
katika barua yake ineffabilis Deus. Miaka minne baada ya mwaka
1858, Bikira Maria alimtokea Bernadetta wa Lurdi, naye
alimuuliza mwanamke mzuri aliyemwona kwenye pango
kilimani, “unaitwaje”? Maria alikunjua mikono yake akaiinua juu
akaifunga tena, akasema: “Mimi ndimi mkingiwa Dhambi ya
Asili”.
Bikira Maria alikuwa binti wa Israeli, msichana wa Kiyahudi wa
Nazareti na Galilaya. Kumchagua Bikira Maria tangu milele; ni
upendo wa Mungu kwa wanadamu wote. Katika Injili ya [Yohane
3:16], tunasoma, “ kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu
amwaminiye awe na uzima wa milele”. Mungu alimtayarishia
mwili, alitaka ushirikiano huru wa kiumbe. Mungu alipata
ushirikiano huo kutoka kwa Bikira Maria katika uhuru wa imani.
Maana yake kumchagua Mungu pekee na kufuata mwito wake.
Basi Mungu wa milele alimchagua Bikira Maria awe Mama wa
Mwanawe. Mungu alimtuma Mwanawe, lakini kwa ajili ya
kumtayarishia mwili, alitaka ushirikiano huru wa kiumbe. Kwa
ajili hiyo, Mungu wa milele yote alimchagua Bikira Maria awe
mama wa Mwanawe binti wa Israeli, msichana wa Kiyahudi wa
Nazareti ya Galilaya.
19

2.10 Page 20

▲back to top


Kukingiwa dhambi ya Asili
Kwa ajili ya kuwa Mama wa Mkombozi, Bikira Maria
alitajirishwa na Mungu kwa karama nyingi zenye kulingana na
kazi iliyo kubwa hivi. Malaika Gabrieli wakati wa kupasha habari
alimsalimu kama “aliye jaa neema”. Kwa kweli, aweza kutoa
kibali huru cha imani kwa habari ya wito wake, ilikuwa lazima
maisha yote awe amejaa neema ya Mungu. Zaidi ya mtu ye yote
yule aliyeumbwa, Baba “alimbariki kwa baraka zote za
rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo” na
akamchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya
ulimwengu, ili awe mtakatifu na bila hatia mbele zake katika
pendo.
Wakati wa kupashwa habari kwamba angemzaa “Mwana wa
aliye juu” bila kumjua mwanamume, kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu, Maria alijibu kwa utii wa imani: akiwa na hakika
kwamba “hakuna lisilowezekana kwa Mungu”. “Mimi ni
mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema”. Kwa
kukubali Neno la Mungu, Maria amekuwa Mama wa Yesu,
akikumbatia kwa roho yake yote, bila kushikwa na dhambi
yoyote, mapenzi ya Mungu ya Wokovu, na alijitoa kabisa kwa
nafsi yake kwa kazi ya Mwanawe ili kuhudumia fumbo la
ukombozi chini yake na pamoja naye na kwa msaada wa neema
ya Mungu.
Umama wa Bikira Maria
Wanadamu wote huingia hapa duniani kwa njia ya Mama,
ambaye amepewa nafasi ya pekee na Mungu, kupokea mbegu ya
kiume na kuirutubisha katika tumboni mwake. Kwa baraka zake
Mungu mama anashiriki uumbaji wake. Na mtoto hutunzwa na
mama sana hadi mtu mzima. Bikira Maria naye ni Mama wa
Mwokozi si kwa njia kama vile ya kibinadamu bali ya Mungu,
kama vile tunavyoelezwa hapa chini:
Umama wa Bikira Maria umo ndani ya mpango wa Mungu.
Ubikira wa Maria wadhihirisha hatua ya kwanza kabisa ya
Mungu katika Umwilisho. Yesu ni Mungu tu kama Baba. Asilii ya
kibinadamu ambayo ameitwaa haikumtenga kamwe na Baba;
20

3 Pages 21-30

▲back to top


3.1 Page 21

▲back to top


kwa asili ni Mwana wa Baba kadiri ya uungu ; kwa asili ni
Mwana wa mama kadiri ya ubinadamu, lakini Mwana halisi wa
Mungu katika hali hizo mbili.
Maria ni bikira kwa sababu ubikira wake ni alama ya imani yake,
ambayo haikubadilishwa na shaka lolote, na ni alama ya kujitoa
kwake kabisa kwa utashi wa Mungu. Kwa imani ni mama wa
Mwokozi: “Maria ana heri zaidi kupokea imani ya Kristo kuliko
kutungwa mwili wa Kristo. Maria ni bikira na mama wa pamoja
kwa sababu yeye ni ishara na utimilifu wa Kanisa: “ Hakika
Kanisa…kwa kupokea Neno la Mungu kiaminifu, linakuwa pia
mama, kwani kwa mahubiri na ubatizo linazaa watoto
waliotungwa na Roho Mtakatifu na kuzaliwa na Mungu kwa
uzima mpya usiokufa. Ni bikira pia anayetunza imani yote na
safi, aliyompa mchumba wake.
Bikira Maria amejaa Neema
Maria, Mtakatifu kabisa, Mama wa Mungu, Bikira daima ni kilele
cha utume wa Mwana na wa Roho Mtakatifu katika utimilifu wa
nyakati. Kwa mara ya kwanza katika mpango wa wokovu na kwa
sababu ya Roho wake amemtayarisha, Baba apata “makao
ambamo Mwana wake na Roho wake wanaweza kukaa kati ya
watu. Kwa maana hii mapokeo ya Kanisa yamesoma mara nyingi,
kuhusiana na Maria, matini, yaliyo bora sana juu ya hekima.
Maria anaimbwa na kuwakilishwa katika liturjia kama “kiti cha
Hekima”. Ndani yake, “maajabu ya Mungu” ambayo Roho
atayatimiza katika Kristo na katika Kanisa yanaanza kujionyesha.
Roho Mtakatifu, alimtayarisha Maria kwa neema yake: Ilifaa
Mama wa yule ambamo “unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa
jinsi ya Kimwili,” awe “amejaa neema.” Kwa neema tu alichukua
mimba bila dhambi kama kiumbe aliye mnyenyekevu, na
aliyeweza sana kupokea zawadi ya Mwenyezi isiyoelezeka. Kwa
heshima ya haki Malaika Gabrieli amsalimu kama Sayuni:
ufurahi’. Ni shukrani za taifa lote la Mungu, na kwa wimbo
wake, akiwa amechukua ndani yake Mwana wa milele. Ndani ya
Maria, Roho Mtakatifu anatekeleza mpango wa Baba uliojaa
upendo. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Bikira alipata mimba na
21

3.2 Page 22

▲back to top


kumzaaa Mwana wa Mungu. Ubikira wake unakuwa uzazi wa
pekee kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kwa imani.
Katika Maria, Roho Mtakatifu anamdhihirisha Mwana wa Baba
aliyefanyika Mwana wa Bikira. Yeye ni kichaka kiwakacho cha
tokeo halisi la unyenyekevu wa mwili wake na anamfanya
ajulikane kwa maskini na kwa matunda ya kwanza ya mataifa.
Kwa njia ya Maria, Roho Mtakatifu anaanza kuwaweka watu
katika ushirika pamoja na Kristo ambao ndio lengo la pendo la
huruma ya Mungu. Wanyenyekevu ndio wa kwanza kumpokea:
wachungaji, Mamajusi, Simeoni na Anna, wana-arusi wa Kana na
wafuasi wa kwanza.
Katika kilele cha utume wa Roho Mtakatifu, Maria anakuwa
ndiye “Mwanamke,” Eva Mpya (Mama wa walio hai”), Mama
wa “Kristo mzima”. Na kwa namna hiyo yuko pamoja na wale
Thenashara, “wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali,” alfajiri
ya nyakati za mwisho” ambapo Roho ataanzisha asubuhi ya
Pentekoste kwa udhihirisho wa Kanisa.
Maria Mama wa Yesu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu
Malaika aliwatangazia watu wachungaji kwamba Yesu atazaliwa,
kama masiha waliyeahidiwa Waisraeli.
Leo Katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi,
ndiye Kristo Bwana”[ Lk 2:11]. Tangu Mwanzo Yeye ni “Yule
ambaye Bwana alimtakasa na kumtuma ulimwenguni
aliyetungwa mimba kama “Mtakatifu” katika tumbo la Bikira
Maria [Yoh 10:36; Lk 1:35]. Yosefu aliitwa na Mungu “
Umchukue Maria mkeo, maana mimba yake ni kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu, “ ili Yesu aiitwaye “Kristo” azaliwe na
mchumba wa Yosefu katika ukoo wa kimasiha wa Daudi[ Mt
1:20; Mt 1:16; Rom 1:1; 2 Tim 2:8; Ufu 22:16]
Mwana wa Mungu amefanyika Mtu
Katika imani ya Nikea – Konstantinopoli, tunaungama” Kwa ajili
yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu” alishuka toka
mbinguni; akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwake
Yeye Bikira Maria akawa Mwanadamu.
22

3.3 Page 23

▲back to top


Neno alifanyika mwili:
Kwa ajili ya kutuokoa na kutupatanisha na Mungu: “ ni Mungu
aliyetupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa
dhambi zetu, “ Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa
ulimwengu “ Yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi”[ Yoh
4:10k 4:14; 3:5].
Ili tujue pendo la Mungu. Pendo la Mungu lilionekana kwetu,
kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni ili
tupate uzima kwa yeye [1 Yoh 4:9]. “ Kwa maana jinsi hii
Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee,
ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
Milele”[ Yoh 3:16]
Ili tuwe washiriki wa tabia ya uungu. Ndiyo sababu ya Neno
kufanyika Mtu, Na Mwana wa Mungu, amekuwa Mwana wa
mtu Ili mwanadamu, kwa kuingia ushirika na Neno, na kwa
kupata uana wa Mungu, awe mwana wa Mungu.
BIKIRA MARIA KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU
Agano la Kale
Bikira Maria Mtakatifu sana, ni yeye aliyeandikwa katika
Maandiko Matakatifu kuanzia Agano la Kale hadi Agano Jipya.
Maandiko Matakatifu yanatuthibitishia halali ya kuwa Mungu
kamjalia neema kuliko kiumbe chochote kuwa Mama wa
Mwanaye. Ni mpango wa Mungu ambao unaonekana wazi kabisa
kuwa huyu Bikira awe njia ya chemichemi ya baraka za
ulimwengu kwa wanadamu wote.
Tunaelezwa katika Agano la Kale kuwa Maria anaonekana tayari
katika utabiri wa kinabi katika ahadi ya kushinda joko
aliyewashawishi Adamu na Eva kuingia katika dhambi [Mwa
3:15]. Maria pia anaonyeshwa kuwa bikira ambaye atamzaa
mtoto, ambaye jina lake ataitwa Emmanuel [Is 8:14; Mika 5:2-3].
Katika injili pacha na matendo ya mitume ndimo jina Maria
linapatikana.
23

3.4 Page 24

▲back to top


Agano Jipya
Katika Injili ya Yohane, Bikira Maria anaitwa “Mama wa Yesu
au “Mama yake” [Yoh 2:1, 3, 5, 12; 19:25-26]. Maria ametajwa
pia katika katika nyaraka za Mtume Paulo tunapata kutoka [Gal
4:4]”Mungu alimtuma mwanawe azaliwe na mwanamke…”.
Katika injili ya Luka Maria anasalimiwa na Malaika Gabriel
kama yule ambaye amependelewa na Mungu [Lk 1:28, 30]. Yeye
ni mjakazi wa Bwana [Lk 1:38]. Elizabeti anamwita “Mama wa
Bwana”[Lk 1:43]. Yeye ni mwaminifu katika kusikia na kutenda
Neno la Mungu. Maria anakuwepo wakati Yesu anaposulubiwa
[Yoh 19.25-27]. Ni katika msalaba Yesu alimtolea mfuasi wake
ambaye alimpenda sana kwa mama kama mwanawe na Maria
kwa mfuasi kama mama. Hii ni ishara ya mwanzo wa Jumuiya ya
wafuasi wanaoamini. Nyakati hizi , hiyo jumuiya ni Kanisa la
Kikristo na wale wote wanao mwamini Yesu Kristo.
Kuwa Mama wa Mungu ni jambo kubwa sana, lisilo kifani. Kwa
hiyo ilimpasa Maria aandaliwe kwa namna ya pekee kabisa. Kwa
ajili hiyo, Mungu alimjaza Maria neema nyingi [Lk 1:28], na
akamkingia dhambi ya asili tangu nukta alipotungwa mimba
tumboni mwa mama yake Anna. Yeye ambaye angemzaa Bwana
na Mkombozi wa ulimwengu, kwa mastahili ya Kristu,
hakupaswa kuwa na doa lolote la dhambi. Kwa sababu ya
Umwilisho wake, Yesu ni Mungu-Mtu.
Katika Nafsi Moja ya Yesu Kristu kuna hali zote mbili-hali ya
kimungu na hali ya kibinadamu pasipo kutengana. Kwa kuwa
Maria alipata Mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, anastahili
kuitwa “Bikira” au “Bikira daima”. Hii ni imani ya Kanisa,
ambayo limeungama nyakati zote. Tendo hilo la Mungu ni la
ajabu sana, ambalo hekima ya mwanadamu haiwezi kung’amua
bila hekima ya Mungu.
Maria alibaki kuwa Bikira kabla ya wakati na baada ya kumza
Yesu. Alikuwa Bikira kabla ya kumzaa Yesu kwa sababu alipata
mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Alikuwa Bikira wakati
wa kumzaa kwa sababu alijifungua bila kuharibu ubikira wake.
Maria alibaki kuwa Bikira baada ya kumzaa Yesu kwa sababu
aliendelea kuishi na Yosefu kama kaka na dada na hakuwa na
24

3.5 Page 25

▲back to top


watoto wengine. Bikira Maria, kujawa neema za Mungu ndivyo
alikuwa chombo safi kwa ajili ya umama wa kiroho kwa wote
wanaomwamini Mungu. Mungu alipenda tujisikie ulinzi wake na
upendo kwa hali ya kibinadamu ambayo aliifanya ya kimungu.
Na ndipo sasa wanadamu wote wamejenga tumaini kubwa kwa
Mungu, Mungu anayewajali na kuwatunza katika hali
wanayoiona, hisi na pia kuigusa.
Ndugu zake Yesu wanaotajwa katika Injili [Mk 3:31; 6:3], ni
jamaa tu wa karibu, na siyo wa tumbo moja. Katika lugha ya
Kiebrania na Kiaramayo, jamaa wote wanaitwa ndugu, iwe wa
tumbo moja au sivyo. Hakuna hata sehemu moja katika
Maandiko Matakatifu inaposemwa kwamba Maria alikuwa na
watoto wengine zaidi ya Yesu. Kuna vidokeza kadhaa
vinavyoonyesha kuwa Yesu alikuwa Mwana pekee wa Maria [Lk
2; 46-52; Yoh 19:26-27]. Msalabani Yesu alimkabidhi Mama
yake kwa Yohane. Kama Maria angekuwa na watoto wengine,
lisingekuwa jambo la busara kwa Yesu kumkabidhi mamaye kwa
mtu wa pembeni na kuwaacha ndugu zake wa tumbo moja.
Ubikira wa Maria kitheolojia unaonyesha kwanza fumbo la
harusi ambapo Mungu ni bwana arusi. Ubikira ni kuishi na moyo
wa ibada makini kwa Mungu na Mwanaye. Na huu ndio mwito
wa Mungu kwetu sisi wanadamu. Tumepewa Bikira Maria ishara
ya kweli ya utii kwa Mungu. Mungu anayewapenda wanadamu
upeo, na kila mara ataka kuwafanyia jambo nzuri. Ili neema za
Mungu ziwafaidi wanadamu, wapata kuwa na mioyo wazi na utii
kwa Mungu, kama vile Bikira Maria alivyokuwa. Na ni njia rahisi
sana, kuishi na wazo la kumwamini Mungu katika roho yako.
MAFUNDISHO YA KANISA KUMHUSU BIKIRA MARIA
Kanisa Katoliki linatafakari kuhusu mafumbo ya Umwilisho na
Ukombozi wa Bikira Maria. Kanisa limetambua uwepo wa Maria
na kushiriki kwake katika uwmwilisho na Ukombozi. Kanisa
linamwelewa Bikira Maria kuwa, “Mama wa Mungu
(Theotokos), kama kweli Bikira, “Mkingiwa dhambi ya Asili
na “mpalizwa mbinguni-roho na mwili”.
25

3.6 Page 26

▲back to top


Mama wa Mungu [Theotokos]
Katika mapokea na imani ambayo Kanisa linaungama,
Bikira Maria ni kuwa kweli ni Mama wa Mungu. Maria ni mama
wa Yesu Kristu ambaye ni Mungu kweli na Mwanadamu kweli.
Kwa hiyo ni Mama wa Mungu. Hili ni fundisho la imani
lililokubaliwa tangu zamani katika Mtaguso wa Epheso 431.
Mababa Watakatifu walimwita Bikira Mtakatifu “Mama
wa Mungu”(Theotokos). Hii haimanishi kuwa asili ya Neno au
umungu wake ulianzia kwake Bikira Maria, lakini mwili
mtakatifu ambao ulitiwa uzima na roho, ambayo ni “Muungano
wa asili mbili, ya kimungu na ya kibinadamu, katika nafsi
moja=Kristo Mungu-Mtu (Hypostasis), alizaliwa naye.
Fundisho hili lina msingi katika maandiko matakatifu
[Gal 4:4; Lk 1:32, 35,Lk 1:43,45,46; 20:31]. Ni ukweli kuwa
Maria ni Mama wa Yesu, Mwana wa Mungu. Hivyo yeye ni
Theotokos”. Katika kila tarehe ya kwanza ya mwaka,
tunamkumbuka Maria Mama wa Mungu.
Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili
Katika barua ya Papa (Inffabilis Deus tarehe 8 Desemba
1854), Pius IX alitangaza kuwa Kuzaliwa Bikira Maria bila
dhambi ni mafundisho ambayo ni nguzo ya imani. Dogma
yenyewe ilisema hivi: “Bikira Maria Mtakatifu sana, mwanzo
wa kutungwa kwake, alipendelewa na neema ya Mwenyezi
Mungu, Kuwa Mama wa Yesu Kristu, mwokozi wa wanadamu
wote,alikingiwa doa la dhambi ya asili”.
Heshima ya Maria ndiyo ilikuwa sababu ya kukingiwa
dhambi ya asili. Japo katika maandiko Matakatifu hamna
uwazi wa Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili lakini kuna
tafakari ya kina kutoka [Mwa 3:15 “Mwanamke”, Lk 1:28]
umejaa neema”, [LK 1:28] Umebarikiwa kuliko wanawake
wote”. Huu ni udhihirsho kuwa Maria ni Mtakatifu, pia huru
kutoka dhambi ya asili.
Malaika alimsalimia, “umejaa neema” na tena, “usiogope,
Maria kwa kuwa umepata neema za Mungu”, [Lk 1:28-30],
hii pia linatupa mwelekeo wa kuelewa Maria alikingiwa
26

3.7 Page 27

▲back to top


dhambi ya asili. Kadiri ya Agano jipya, neema ni zawadi ya
Mungu, kumtoa Mwanawe [Rum 8:32] ambayo ina zawadi
zingine nyingi. Na si zawadi iliyojificha, bali inamuathiri yule
anayepokea na upendo pamoja na ukarimu wa mtoaji. Na
ndivyo tunafahamu kuwa Mwanamke, “aliyejaa neema”,
tunaongea juu yake kama yule ambaye Mungu yumo ndani
yake.
Maria anaeleweka kama mwanamke ambaye Mungu yumo
ndani yake kwa nafasi ya kipekee na amejawa na uwepo wa
Mungu. Hii inamfanya awe huru kutokana na dhambi na
amejawa sifa ya mng’aro wa Mungu. Huduma ya Maria kwa
Elizabeti na wimbo wake wa shukrani ni ishara ya hali ya
ndani ya moyo wake.
Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria
Sherehe hii husherehekewa tarehe 15 Agosti.
Konstitusio ya Kitume (Munificentissimus Deus) ya Pius XII
tarehe 1 Novemba 1950, ilitangaza kupalizwa Mbinguni
Bikira Maria kuwa ni fundisho la Imani (dogma). Ilitangazwa
hivi, “tunatamka, na tunatangaza kuwa imefunuliwa kwetu,
kuwa Mama wa Mungu, kweli Bikira Maria baada ya
kumaliza maisha yake hapa ulimwenguni alipalizwa
mbinguni mwili na roho”. Maria ameingia utukufu wa
mbinguni, ameshirikishwa utukufu wa Mwanawe.
Theolojia ya kupalizwa Maria Mbinguni: Kupalizwa kwa
mwili na roho ya Maria mbinguni ilikuwa ni zawadi kamili
kutoka kwa Baba na si kitu alichofanikiwa mwenyewe.
Utakatifu wa Kikristu, ukamilifu na Utakatifu wa Kanisa ni
zawadi kamili kutoka kwa Mungu, na si matokeo ya kazi
yetu. Hata hivyo mwelekeo wa mwanadamu ni kuingizwa
katika maisha ya Utatu Mtakatifu. Jinsi ya Maria, kile
kinachofanya Kanisa na kila Mkristu, ni neema: “ kwa neema
umeokolewa katika imani; na hili si tendo lako, ni zawadi ya
Mungu”[Eph 2:8]. Neema ni swala la kwanza la Ukristo na
sababu ya msingi wa Utakatifu.
27

3.8 Page 28

▲back to top


Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria, ni ishara ya kuonyesha
mwelekeo wa wanadamu wote. Mungu aliye Mtakatifu sana
ataka tuishi naye milele. Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria ni
tumaini kwa wanadamu wote, kuwa huko ndiko tunaelekea.
Hivyo basi mioyo yetu, mawazo na matendo ni lazima yawe
na msingi wa uzima wa milele.
Ubikiria wa Maria
Ni fundisho la Imani kuwa Yesu Kristu alizaliwa na
Bikira Maria. Hivi ni kusema kuwa Maria ndiye alikuwa mzazi
wa kibayologia pekee yake. Mwana wa Mtu hakuwa na baba wa
kibayolojia; alitungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Katika
Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli 381 uliongeza kwenye
Kanuni ya Imani ya Nikea maneno haya: “Kwa Roho Mtakatifu
na Bikira Maria” kurejea umwilisho wa Kristu.
MAJINA YA MARIA
Bikira Maria amepewa majina kulingani na nyakati, mazingiria
na matukio mbalimbali ambayo anawafikia watu kuwaletea
ujumbe wa Mungu. Tutatakafakri juu ya baadhi ya majina Bikira
Maria anapewa. Japo kuna majina hayo, Bikira Maria ni Yule
Yule Mama wa Mkombozi. Katekisimu yatufundisha kuwa
Mungu humwita kila mtu kwa jina. Jina la kila mtu ni takatifu.
Na jina ni sanamu ya mtu. Linadai heshima kama ishara ya hadhi
ya yule anayelichukua. Hivyo basi majina hayo yote Bikira Maria
amepewa ni matakatifu na yanatuletea baraka za Mungu.
Aliyejaa neema
Sala ya Salamu Maria, yatuonyesha wazi kuwa Mungu amemjalia
Maria neema. Maria amejaa neema kwa sababu Bwana yu
pamoja naye. Na neema hii ni kuwa amejazwa uwepo wa Yule
aliye chemichemi ya kila neema:
Maria ambaye ndani yake Bwana Mwenyewe anakuja kukaa,
anakuwa sanduku la agano, mahali ambapo utukufu wa
28

3.9 Page 29

▲back to top


Bwana unakaa, yeye ni “maskani ya Mungu pamoja na
wanadamu”.
Katika neema, Maria ametolewa wote kabisa kwa Yule
anayekuja kukaa ndani yake na ambaye yeye atamtoa kwa
ulimwengu.
Salamu ya Malaika Gabrieli inadhihirisha kuwa Maria
amebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo
lake amebarikiwa. Maria amebarikiwa kuliko vizazi vyote
kwa sababu alisadiki katika utimilifu wa Neno la Bwana.
Maria kwa imani yake ni Mama wa waamini, kwa njia yake
mataifa yote ya dunia yanampokea Yule ambaye ni baraka
yenyewe ya Mungu:-Yesu, mzao wa tumbo lako
amebarikiwa”. Maria ametupatia Yesu Mwanawe.
Maria ni Mama wa Mungu na Mama yetu. Tumkabidhi
mahangaiko yetu na maombi yetu: anasali kwa ajili yetu
kama alivyosali kwa ajili yake mwenyewe,“na iwe kwangu
kama ulivyosema.” Tunapojiaminisha kwa sala zake,
tunajiachilia sisi wenyewe kwa mapenzi ya Mungu pamoja
naye: “mapenzi yako yafanyike”.
Utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu”:
Tunapomwita Maria atuombee tunakiri kwamba: tu
wakosefu, maskini na tunajielekeza kwa “Mama wa
Hurumaambaye ni Mtakatifu sana. Tunajitoa kwake sasa
katika “leo” ya maisha yetu. Na tumaini letu linapanuka
kumkabidhi yeye tangu ‘saa ya kufa kwetu’. Awepo pale
kama alivyokuwa katika kifo cha Mwana wake Msalabani.
Saa ya kufa kwetu atupokee kama Mama yetu, ili atuingize
paradiso kwa Mwanae, Yesu.
Maria ndiye mkamilifu anayesali- sura ya Kanisa.
Tunamwomba, tunaungana naye katika mpango wa Baba
anayempeleka Mwanae kuwaokoa watu wote. Kama
mwanafunzi aliyependwa, nasi tunampokea kwetu, Mama wa
Yesu ambaye amekuwa Mama wa wote walio hai. Tunaweza
kusali pamoja naye na kumwomba. Sala ya Kanisa
29

3.10 Page 30

▲back to top


yategemezwa na sala ya Maria nayo imeunganika na Maria
katika tumaini.
Aliyekingiwa dhambi ya asili
Bikira Maria ana neema ya Mungu kwa ajili ya kumpokea
Mwana wa Mungu hivyo basi:
Malaika Gabrieli wakati wa kupasha habari alimsalimu kama
uliyejaa neema”. Karne kwa karne Kanisa limetambua
kwamba Maria alijazwa neema na Mungu. Alikombolewa
tangu mwanzo wa kuchukuliwa kwake mimba. Ndicho
kinatufundisha mafundisho ya imani juu ya kukingiwa
dhambi ya asili yaliyotangazwa na papa Pio IX, mwaka 1854:
Mwenye heri kabisa Bikira Maria, tangu nukta ya kutungwa
kwake mimba, kwa neema na upendeleo wa pekee wa Mungu
Mwenyezi, kwa kutazamia mastahili ya Yesu Kristo,
Mwokozi wa wanadamu wote, alikingiwa na kila doa la
dhambi asili. Kwa neema ya Mungu Maria amebaki safi
kabisa na hakutenda dhambi yoyote maisha yake yote.
Daima Bikira
Matendo makuu ya Mungu ni ya daima.
Kuingia ndani ya imani juu ya umama na ubikira wa Maria,
umeliongoza Kanisa kuungama ubikira wa kweli na wa daima
wa Maria, hata katika kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu
aliyefanyika mtu. Kuzaliwa kwa Kristo, kwa uhakika
hakukupunguza ukamilifu wa ubikira wake, bali
kumeutakatifuza”.
Liturjia ya Kanisa inamtukuza Maria kama = “Bikira Daima”.
Yesu ni Mwana wa pekee wa Maria. Lakini umama wa kiroho
wa Maria unaenea kwa watu wote ambao Yesu amekuja
kuwaokoa: “Alimzaa Mwana ambaye Mungu alimweka,
mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi” yaani waamini.
Maria anashiriki kwa mapendo ya kimama wakati wa kuzaliwa
kwao na kuelewa kwao.
30

4 Pages 31-40

▲back to top


4.1 Page 31

▲back to top


Eva Mpya
Katika Injili Maria anatambulika kama mwanamke
aliyetangazwa, “Maria mama wa Kristo”, kama “Eva Mpya” .
Maria alikuwa wa kwanza kati ya wote na kwa namna ya pekee
kufaidi ushindi ulioletwa na Kristo juu ya dhambi: alikingiwa na
kila doa la dhambi ya asili, na katika maisha yake yote ya hapa
duniani, kwa neema ya pekee ya Mungu, hakutenda dhambi
yoyote.
Kiti cha Hekima
Maria, Mtakatifu kabisa, Mama wa Mungu, Bikira daima ni
kilele cha utume wa Mwana na Roho Mtakatifu katika
utimilifu wa nyakati. Kwa mara ya kwanza katika mpango wa
wokovu na kwa sababu Roho wake amemtayarisha, Baba
anapata “makao” ambamo Mwana wake na Roho wake
wanaweza kukaa kati ya watu.
Mapokeo ya Kanisa yamesoma mara nyingi, kuhusiana na
Maria, mambo yaliyo bora sana juu ya hekima. Maria
anaimbwa na kuwasilishwa katika Litrujia kama “kiti cha
Hekima”. Ndani yake, maajabu ya Mungu ambayo Roho
atayatimiza katika Kristo na katika Kanisa yanaanza
kujionyesha.
Mama wa Kanisa
Bikira Maria anatambuliwa na kuheshimiwa kama “Mama
kweli wa Mungu, na wa Mkombozi Yeye ni pia “ Mama kweli
wa viungo vya Kristo, kwa sababu alishiriki kwa mapendo
yake kuzaliwa kwa waamini ndani ya Kanisa, ambao ni
viungo vya kichwa hicho.
Katika Kanisa kazi ya Bikira Maria haitengani na umoja wake
na Kristo, bali inatoka moja kwa moja humo. Umoja huo
unaonekana tangu kutunga mimba Kristo mpaka kifo chake.
Baada ya Mwanawe kupaa mbinguni.
31

4.2 Page 32

▲back to top


Maria “kwa sala zake alisaidia kuzaliwa kwa Kanisa.”
Akiunganika na mitume na wanawake kadhaa, hata Maria
aliomba kwa sala zake paji la Roho, ambaye wakati wa
kutangazwa kuzaliwa kwa Bwana, yeye mwenyewe
alishampata chini ya kivuli chake.
Bikira Maria alitukuzwa na Bwana kama Malkia wa
ulimwengu, kwa sababu alikuwa amefana sana na Mwanawe,
Bwana wa mabwana, na mshindi wa dhambi na mauti.
Kupalizwa kwa Bikira Mtakatifu ni ushirika kwa namna ya
pekee ufufuko wa Mwanawe na ni utangulizi wa ufufuko wa
Wakristo wengine. Kwa kuambatana kwake kabisa na
mapenzi ya Baba , na kazi ya ukombozi ya Mwanawe, na
Msukumo wote wa Roho Mtakatifu Bikira Maria ni mfano wa
imani na wa mapendo kwa ajili ya Kanisa. Kwa sababu hiyo
yeye, “kwa hakika ni Mwanakanisa kabisa, “yeye ni, “mfano
Mtimilifu” wa Kanisa.
Mama wa Mungu
Maria ni kweli Mama wa Mungu kwa kuchukua mimba ya
kibinadamu ya Mwana wa Mungu katika tumbo lake: “ Ni
Mama wa Mungu siyo kwa sababu Neno wa Mungu ametwaa
kwake asili yake kimungu, lakini kwa sababu ametwa kwake
mwili mtakatifu wenye roho yenye akili, akafanana nao
katika nafsi yake, na ndivyo tunakiri kuwa Neno amezaliwa
kadiri ya mwili.
Maria ni kweli , “ Mama wa Mungu”, kwa sababu ni Mama
wa Mwana wa milele wa Mungu aliyefanyika Mtu, ambaye
Yeye mwenyewe ni Mungu.
Mama wa walio hai
Bikira Maria “alishiriki wokovu wa binadamu kwa imani yake
na utii wake wa hiari. Alitamka ndiyo yake “kwa niaba ya
binadamu wote”. Kwa utii wake amekuwa Eva mpya, mama
wa Walio hai.
32

4.3 Page 33

▲back to top


Mama wa Yesu
Mjakazi wa Bwana Maria amebaki ‘bikira’ katika kutunga
mimba ya Mwanawe, bikira katika kumzaa; bikira
alipomchukua, bikira alipomlisha kifuani pake, bikira daima.
Kwa uwepo wake wote alikuwa ni mjakazi wa Bwana [Lk
1:38]. Baadhi ya majina mengine ni haya:-Mpalizwa
Mbinguni, Mtetezi, Msaidizi, Mfadhili.
IBAADA KWA BIKIRA MARIA
Bikira Maria mwenyewe aliimba kuwa “vizazi vyote wataniita
mbarikiwa” , baada ya kumtembelea Elizabeti aliyetambua kuwa
ni mama wa Mwokozi. Uchaji wa Kanisa kwa Bikira Maria ni wa
ndani kabisa katika ibada ya Kikristo. Bikira Mtakatifu,
“anaheshimiwa kwa haki na Kanisa kwa ibaada ya pekee. Kwa
kweli tangu nyakati za kale zaidi, Bikira Mwenye heri
ameheshimiwa kwa cheo cha “Mama wa Mungu”, waamini
wanamkimbilia ulinzi wake, wanamwita katika hatari zao zote na
mahitaji yao.
Ibada hiyo, ingawa ni ya pekee kabisa ni tofauti kimsingi na
ibada ya kuabudu inayotolewa kwa Neno aliyemwilishwa, pia
kwa Baba na kwa Roho Mtakatifu; ile ya kwanza inakuza ya pili.
Ibada kwa Bikira Maria huonekana katika sikukuu za Kiliturjia
alizowekewa Mama wa Mungu: na katika sala za Maria, kama
Rosari takatifu, “Muhtasari wa Injili yote”.
Katika kuadhimisha kila mwaka mafumbo haya ya Kristo, Kanisa
humheshimu kwa upendo wa pekee Maria mwenye heri, Mama
wa Mungu, ambaye ameunganika na Mwana wake kwa namna
isiyoweza kutengwa katika kazi ya ukombozi. Tena ndani ya
Maria, Kanisa huheshimu na kutukuza tunda bora kuliko yote ya
ukombozi, na hutafakari kwa furaha, kama katika mfano usio na
doa wa yale yote linayoyatamani na kuyatumaini kwa ajili yake.
Sala ya Rozari
Rozari takatifu ni sala ambayo inapendwa sana na inachukua
nafasi muhimu sana kiundani kwa ajili ya sala ya Kikristo.
33

4.4 Page 34

▲back to top


Mamlaka fundishi ya Kanisa na pia imedhibitishwa na watakatifu
kuwa; sala hii ya rozari inaendana na mafundisho ya mtaguso wa
pili wa Vatikano. Inaelezea nafasi ya Bikira Maria, ili waamini
wote waweze kumjongea mwombezi na mwokozi. Bikira Maria
anawaunganisha waamini na Kristo.
Ni kweli kuwa katika sala ya rozari, Bikira Maria awafundisha
watoto wake jinsi ya kuungana na fumbo la Kristo. Hata hivyo
Kanisa linatilia uzito kwa ibaada za Bikira Maria kwa wote
waliopokea wito wa kumfuata Kristo. Mtakatifu Yohane Bosko
alipendekeza kwa wafuasi wake, hadi kuwaeleza kuwa shirika
lake msingi wake umetokana na Bikira Maria.
Papa Paulo VI katika barua yake Marialis cultus”, alitoa
fundisho kuu kuhusu sala ya rozari, akichukulia ule umuhimu wa
ndani na kupendekeza kwa waamini kufanya ibaada. Alisema
rozari ni:
Ni asili ya kuinjilisha: Mafungo yote ya rozari yanatokana na
Injili, tunaweza kusema ni mkusanyiko wa Injili yote.
Inabeba mafundisho ya Kristo: - Rozari inaonyesha mafumbo
yote ya ukombozi.
Inahusika katika liturjia: Rozari inachukua asili yake kutoka
liturjia na kuelekeza waamini kwenye liturjia. rozari na liturjia
ina mwelekeo mmoja tu, mwelekeo wa ukombozi wa Kristo.
Katika kusali rozari, jambo la muhimu ni kutafakari juu ya yale
mafungo ambayo yanamwelekeza mtu katika wazo la kiroho.
Kusali kwa rozari kwa hitaji utulivu, umakini ambao
unamwelekeza anayesali katika kutafakari mafumbo ya maisha ya
Bwana ambayo yako wazi katika macho ya Bikira Maria
aliyempokea kwanza.
Rozari hufananishwa na shule ya ibada ya ndani sana. Rozari
hulinda na hufundisha waamini kwa malezi bora ya kiroho.
34

4.5 Page 35

▲back to top


MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Kanisa la Maria Msaada wa Wakristo huko Torino
Maria Msaada wa Wakristo
Maria Msaada wa Wakristo ni jina la heshima kwa Mama Bikira
Maria. Ibaada ya Bikira Maria ni tendo kamili katika Kanisa
Katoliki ambapo Sikukuu yake husherehekewa tarehe 24 Mei kila
Mwaka. Mtakatifu Yohane Chrsysostom ndiye wa kwanza
kutumia sifa –“Maria Msaada wa Wakristo” mwaka 345. Mt.
Yohane Bosco aliendeleza ibada ya Maria katika kazi zake. Sifa
Maria Msaada wa Wakristo”, huhusishwa na Msaada wa Mungu
ambao Wakristo walipata katika Europa [ Latin na Greek], Afrika
Kaskazini, na nchi kama Syria, uturuki na Uarabuni.
Wakristo walipewa Msaada na Mama Bikira Maria dhidi ya
makundi ya Kiislamu ambayo yaliwashambulia Wakristo na
kuwalazimu kuwacha dini yao na kufuata Uislamu. Baba
Mtakaktifu Pius V aliita majeshi ya Wakristo kuilinda Europa na
35

4.6 Page 36

▲back to top


aliwauliza waamini kusali rozari kwa Mama Bikira Maria. Kwa
sala ya rozari waislamu walishindwa katika vita vyote. Ushindi
huo wa Kanisa unaaminiwa kuletwa na Mama Bikira Maria. Na
ndivyo jina “Maria Msaada wa Wakristo” lilienea; kwa sababu
waliamini kuwa ushindi wao ulitokana na mama wa Mwokozi.
Sikukuu ya Maria Msaada wa Wakristo
Zamani Bikira Maria alipewa sifa zifuatazo: Mama wa Mungu,
Maria Msaada wa Wakristo. Baba Mtakatifu Pius V aliweka sifa
hii katika Litania ya Loreto baada ya vita vya Lepanto. Sikukuu
ya Maria Msaada wa Wakristo ilitangazwa rasmi na Papa Pius
VII. Mfalme Napoleon I alimweka mateka Papa huyo mnamo
tarehe 5 Juni, 1808. Aliwekwa huru tarehe 17 Machi 1814 Jioni
ya sikukuu ya Maria Mama wa huruma.
Papa Pius VII aliona kuwa ushindi uliopatikana kwa Wakristo
ulitokana na Msaada ulioletwa na Mama Bikira Mari; nyakati za
vita dhidi ya Wakristo; Papa aliwahimiza Wakristo wasali rozari
na majitoleo mengine. Wale walioenda vita walipata nguvu za
kushinda. Kwa namna hiyo Mama Bikira Maria alionekana wazi
kuwa msaada wa Wakristo. Baada ya Papa kutoka uhamishoni,
alienda kusali kwenye makanisa ya Bikira Maria akitoa shukrani.
Huyu Baba Mtakatifu alirudi Roma 24 Mei 1814. Kuonyesha
moyo wa shukrani kwa Bikira Maria Mtakatifu; Baba Mtakatifu
Pius VII, tarehe 15 Septemba 1815, aliweka sikukuu ya Maria
Msaada wa Wakristo iwe kila mwaka tarehe 24 Mei. Sikukuu hii
ilianza kusherehekewa tarehe 24 Mei 1913.
Walioeneza ibada ya Maria Msaada wa Wakristo
Mtakatifu Yohane Bosko na Mt. Vincent Pallotti walieneza ibada
kwa kwa Maria Msaada wa Wakristo huko Italia na mahali
kwingi. Mwaka 1868 Yohane Bosko alijenga Kanisa kuu la
Maria Msaada wa Wakristo kule Torino -Italia na akaanzisha
shirika la, “Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo” (The
Daughters of Mary Help of Christians). Kulingana na sifa hii
aliyopewa Bikira Maria; Kanisa katika utamaduni wake
limesisitiza mambo mawili:
36

4.7 Page 37

▲back to top


Katika sikukuu ya Maria Msaada wa Wakristo; Kanisa
linatilia mkazo wa wito wa Bikira Maria kuwa mwombezi na
msaidizi katika kuvipiga vita dhidi ya dhambi katika maisha ya
mwaamini (Mkristo).
Kanisa linamwangalia Bikira Maria kuwa yule ambaye
anawasaidia Jumuiya ya Wakristo kwa maombezi yake, kulilinda
Kanisa dhidi ya wale wapinga Kristo na vikwazo mbalimbali.
Baada ya Mtaguso wa Vatikano II; Sikukuu hii ilifikiriwa
kuadhimishwa Jumapili kabla ya tarehe 24 Mei au Jumapili
inayofuata. Sikukuu hii ya Maria Msaada wa Wakristo ni
muhimu sana, Mtakatifu Yohane Bosko mwanzilishi wa shirika la
Waselesiani wa Don Bosko( Salesians of Don Bosco), kazi zake
zote aliziweka chini ya ulinzi wa Maria Msaada wa Wakristo,
kuanzia Kanisa Mama la huko Torino 9 Juni 1868. Waselesiani
wameeneza ibaada hii mahali popote walipoenda ambapo
wanaendesha Utume.
Ekaristi Takatifu na Upendo kwa Bikira Maria
Nyakati nyingi Wakristo ulimwenguni wamepata miujiza ya
Maria Msaada wa Wakristo. Mojawapo ni ule ushindi wa
Lepanto, wakati kundi la Waislamu, wazushi na watu wasio dini
walianza kushambulia Ulaya. Baba Mtakatifu Pius V aliwasihi
Wakristu waanzishe vita vya kiroho kwa kusali rozali na
maandamano ya Ekaristi Takatifu kila mahali. Ni kwa nguvu za
Ekaristi Takatifu na sala ya rozari vita hivyo vilishindwa.
Wakristo katika makundi makubwa walisali rozari hadharani
katika maandano mbalimbali. Mwanzoni mwa vita Wakristo
walishindwa sana, lakini baadaye walianza kupata ushindi.
Ushindi wa vita hivyo uliletwa wazi na ibada kwa Ekaristi
Takatifu na sala ya rozari. Kwa heshima ya utukufu wa Mungu na
ushindi kwa njia ya ya Ekaristi Takatifu na sala ya rozari; Baba
Mtakatifu Pius V aliamuru sikukuu ya rozari Takatifu na
akaaongeza sala, “Maria Msaada wa Wakristo, Utuombee”.
Mwaka 1809, sala na maombezi pia zilimfikia Maria Msaada wa
Wakristo. Mfalme Napoleon wakati alitengwa na Kanisa aliamua
37

4.8 Page 38

▲back to top


kumteua Baba Mtakatifu Pius, VII. Alimkandamiza aweke
mkataba kuwa mfalme ndiye atakuwa na uamuzi wa mwisho
katika maswala ya Kanisa na jamii huko Ufaransa. Ni kwa
mujibu wa ibada kwa Ekaristi Takatifu na sala ya rozari Baba
Mtakatifu Pius VII aliwekwa huru. Tarehe 24 Mei 1815, Baba
Mtakatifu aliweka wakfu siku hiyo kwa heshima ya Bikira Maria
na akaanzisha siku kuu ya Maria Msaada wa Wakaristo.
Maria Msaada wa Wakristo na Yohane Bosko
Roho wa Mungu aliamsha ndani ya Mtakatifu Yohane Bosko,
ibada kwa Maria Msaada wa Wakristo (1815-1888) kwa ajili ya
wokovu wa vijana. Katika miaka yake ya upadre Yohane Bosko
alieneza ibaada ya Moyo Mtakatifu wa Maria na Mama wa
Huruma katika jina la Maria Msaada wa Wakristo. Mwaka 1863,
Yohane Bosko alianza kumheshimu Bikira Maria katika sifa ya
Maria Msaada wa Wakristo”.
Wapinzani wa Kanisa walikuwa wameanza kumshambulia Baba
Mtakatifu na Kanisa. Mwaka 1862, picha ya Bikira Maria
iliyochorwa ikampendeza Askofu mkuu wa Spoletto ambaye
aliiheshimu kwa sifa "Maria Msaada wa Wakristo". Yohane
Bosko aliongozwa na Roho wa Mungu ajenge Kanisa ambalo
litakuwa chini ya ulinzi wa Maria Msaada wa Wakristo huko
Torino - Italia.
Hata hivyo Yohane Bosko alipata vikwazo vingi sana kutoka kwa
viongozi wa serikali, wapinga Kanisa na pia alikosa uwezo wa
kifedha. Basilika ya Maria Msaada wa Wakristo ilimalizika
kimujiza mwaka 1868. Kwa Yohane Bosko, msaada wa Maria
ulikuwa muhimu sana sababu kulikuwa na Wakristo ambao
hawakuwa wenye bidii katika imani, wadhambi na watu wema.
Kanisa Katoliki pia lilikuwa katika mashambulizi. Kwa kumwita
Maria Msaada wa Wakristo, alimwezesha kufanya miujiza na
kufanya bidii kuwaongoa vijana walio kuwa wengi. Alifanya
bidii sana kueneza ibada kwa Maria Msaada wa Wakristo,
aliwasihi watu kuwa na imani kwa maombezi ya Bikira Maria.
Mara nyingi alisema, “uwe na ibada kwa Bikira Maria, utaona
miujiza
38

4.9 Page 39

▲back to top


KANISA LA MARIA MSAADA WA WAKRISTO HAPA
KENYA
Waselesiani wa Don Bosko kutoka India walifika hapa Kenya
mwaka wa 1982, walifikia Korr kwanza hapa Kenya na Tanzani
baadaye Uganda na Sudan. Pia Waselesiani wa Don Bosko
wamekuwepo katika nchi zingine za Afrika tangu hapo zamani.
Waselesiani hao waliotoka India, walianzisha ibada ya Maria
Msaada wa Wakristo na karama ya Mtakatifu Yohane Bosko
mahali popote walipoenda. Mwaka 1992 Kanisa la Maria Msaada
wa Wakristo lilifunguliwa hapa mji mkuu wa Kenya - Nairobi
sehemu ya Upperhill. Hapo ndipo palipo makao makuu ya
Waselesiani wa Don Bosko hapa Afrika Mashariki. Kanisa hilo
lilifunguliwa rasmi na Mkuu wa Shirika la Waselesiani Egidio
vigano mwaka 1993. Ni sehemu takatifu kwa Waselesiani wa
Don Bosko. Mnamo mwaka 2011, masalia ya Mt. Yohane Bosko
yalipitishwa katika vituo vyote vya Mtakatifu Yohane Bosko
ulimwenguni mwote, ilikuwa namna ya kujiandaa kwa Yubilee
ya miaka mia mbili tangu kuzaliwa Mt. Yohane Bosko. Safari hii
39

4.10 Page 40

▲back to top


ilileta baraka hapa Afrika mashariki, miujiza mingi ilitendeka.
Zilikuwa siku za sala maalum kwa ajili ya kumshukuru Mungu.
Hapa Kenya tuna baraka za pekee na neema za Mungu. Mkuu wa
Shirika la Waselesiani na Kamati yake walitoa masalai ya Mt.
Yohane Bosko kwa hapa Kenya kwa ajili ya Afrika nzima.
Tarehe 28 Januari 2017, Masalia ya Mtakatifu Yohane Bosko,
yalihamishwa kutoka seminari kuu ya Don Bosco Utume hadi
katika Kanisa la Maria Msaada wa Wa Wakristo Nairobi
Upperhill. Ilikuwa ni siku kubwa mno, iliyo ambatana na sala ya
Misa Takatifu. Vijana kwa watoto, watu wazima wote walifika
kwa wingi toka pande zote za vituo vya Mt. Yohane Bosko.
Masalia hayo yaliwekwa chumba maalum ndani ya Kanisa kuu.
Don Bosko Upperhill kwetu Waselesiani ni sehemu takatifu ya
hija. Kanisa la Maria Msaada wa Wakristo ni ishara ya upendo
kwa Bikira Maria. Masalia ya Mt. Yohane Bosko ni ishara ya
uwepo wake kati yetu. Na anaendelea kuziongoza kazi alizopewa
na Mungu ndani ya Waselesiani wa Don Bosko. Don Bosco
Upperhill ni sehemu takatifu ya hija kwa Waselesiani na pia kwa
watu wote. Masalia haya ya Mt. Yohane Bosko yamepeanwa kwa
ajili ya Afrika yote. Ni bahati ilioje na neema za Mwenyezi
Mungu.
Kanisa hili la Maria Msaada wa Wakristo katika atare kuu nyuma
yake, utapata picha iliyounganishwa vizuri ya njozi ya Don
Bosko akiwa miaka tisa. Ni picha inayovutia sana, na pia
kutukumbusha wito wa Mungu kwa mwanzo wa Shirika la
Waselesiani wa Don Bosko. Katika hiyo picha, kuna Yesu, Maria
mama yake, vijana, wanyama na Yohane Bosko. Kwa picha
maelezo yote ya njozi yake yanaonekana wazi. Katika kikanisa
kilicho chini kabisa, pia kuna picha nyingi za Don Bosko
zilizochworwa na msani D’sasi. Kuna picha ya mji wa Nairobi,
vijana, Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo, Mtakatifu
Yohane Bosko. Kila siku kuna misa katika Kanisa hili ndogo.
Waamini wanapata nafasi ya misa asubuhi, saa saba mchana na
jioni. Kweli ni mahali patakatifu pa kumsifu Mungu. Hapa chini
ni picha za Kanisa Kuu la Maria Msaada wa Wakristo.
40

5 Pages 41-50

▲back to top


5.1 Page 41

▲back to top


KANUNI ZA USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
UTANGULIZI NA KIAMBATANISHO CHA KANUNI
Mafundisho Mafupi ya Maria
Picha hii ilikuwa ni wazo fupi la Don Bosko; alimwomba msani
Tommaso Lorenzone kuichora mnamo1865, na baada ya miaka
mitatu ya kazi, picha hiyo kubwa iliwekwa mahali ilipo katika
Basilika. Don Bosko alieleza kwa maneno haya:
41

5.2 Page 42

▲back to top


“Bikira Mtakatifu anaelea katika bahari ya mwanga na ukuu
amezungukwa na jeshi la malaika, ambao wanamweshimu kama
Malkia wao. Kulia ameshika fimbo, alama ya nguvu; na kushoto
anamshikilia Mtoto, ambaye amefumbua mikono, anatolea kwa
namna hii neema na huruma kwa wote ambao wanamkimbilia
Mama yake mpendwa. Kila pande na chini ni Watakatifu Mitume
na Wainjilisti. Wamejawa na furaha, kama kusema “Malkia wa
Mitume, Utuombee”, wanamwangalia Bikira Mtakatifu kwa
mshangao.
Katika msingi wa picha ni mji wa Torino, na Madhabahu ya
Valdocco inayoonekana na Supergo kwa umbali.
Maelezo ya Don Bosko, yanamaanisha kuwa picha hiyo ni halisi
inayoonyesha heshima,
Maria, Mama wa Kanisa”.
Maria , kwa sababu, ni Mama wa Mwana wa Mungu, Yeye ni
Malkia wa mbingu na nchi; Kanisa lote, likiwakilishwa na
Mitume na Wataakatifu, linamtangaza kama Mama na Msaidizi
mwenye
Nguvu.
KANUNI MPYA ZA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Julai 2003
DIREZIONE GENERALE OPERE DON BOSCO
Via della Pisana, 1111 00163
Roma Gombera Mkuu
Utambulisho wa Kanuni mpya kwa wanachama wa ushirika.
Kwa Wanachama,
Katika Sikukuu ya Mt. Yohane Bosko, baba na mwansilishi wetu,
ninafuraha kutambulisha kanuni hii mpya kwenu. Haya ni
matokeo ya kazi ya ziada kwa sehemu ya kila mmoja na vikundi
na sana kwa namna ya pekee kwa kikundi cha Kwanza huko
Torino kwa nyote nawashukuru. Kanuni hizi zimeidhinishwa na
42

5.3 Page 43

▲back to top


kitengo cha mashirika ya maisha ya wakfu na jumuiya za maisha
ya utume, tarehe 7 Oktoba 2003.
Kwa kuwa Kanuni hizo zimesharudiwa na kurekebisha, ni ishara
kuwa ushirika huu upo hai, ambao una nia ya kuendelea katika
kazi ya utume na kiroho katika uhusiano mwema na Kanisa
pamoja na Familia ya Waselesiani. Ni pia ishara kweli ya kilelezo
cha uwajibikaji wa nguvu na uaminifu kwa Don Bosko, ambaye
alitaka ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo kuwa alama ya
shukrani kwa uwepo wa kimama wa Bikira Maria katika maisha
yake na kazi zake, na mfano wa maisha ya Kikristo ambao kiini
chake ni elimu, upendo na kumuenzi Bikira Maria.
Nimetumaini yangu ya dhati kuwa wanachama wote wa ushirika
huu, wataweza kusoma kwa undani maandishi haya mapya na
kupata roho ya Waselesiani iliyoelezwa ndani yake.
Ninawakabidhi nyote kwa Mama yetu, Msaada wa Wakristo.
Roma, 31 Januari 2004
Sikukuu ya Mt. Yohane Bosko
Fr Pascual Chávez V.
Mkuu wa Shirika
43

5.4 Page 44

▲back to top


AMRI
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo, ulianzishwa na Mt.
Yohane Bosko, “kuendeleza heshima kwa Sakramenti Takatifu
na upendo kwa Maria Msaada wa Wakristo”, kisheria ilisimikwa
katika madhabahu ya Maria Msaada wa Wakristo huko Torino
tarehe 18 Aprili 1869, na kuinuliwa na Mwenyeheri Pius IX
tarehe 5 Aprili 1870 katika daraja la jumuya kubwa, ambayo ni
mali ya Familia ya Waselesiani.
Msaidizi wa Mkuu wa Shirika (The Vicar of the Rector Major)
ametambulisha kanuni hizi kwa ofisi kuu ya Utume kwa ajili ya
kibali.
Kitengo cha mashirika ya maisha ya wakfu na jumuiya ya maisha
ya Utume, baada ya kutathimini kwa uangalifu, Kanuni
zilizotajwa, liliidhinisha katika lugha ya Kitaliano iliyowekwa
katika hifadhi, masharti yote ya sheria yalifuatwa.
Kitu chochote kinyume hakikubaliki.
Ilitolewa Vatikani, 7 Oktoba 2003,
Sikukuu ya Bikira wa Rozari.
Eduardo Card. Martinez Somal
Mkaguzi
Piergiorgio Silvano Nesti,
C.P. Katibu
44

5.5 Page 45

▲back to top


KANUNI ZA JAMII YA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Masahisho ya Julai 2003
DIBAJI
Akisukumwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya mahitaji ya dharura
na ishara za nyakati, Don Bosko, alianzisha katika utume wake
chama kikubwa cha watu ambao wangefanya kazi kwa namna
mbalimbali kwa ajili ya faida ya vijana na kundi la wale
wafanyikazi.Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo ulianzishwa
na Don Bosko kama chombo maalum cha “Kutangaza heshima
kwa Sakramenti Takatifu na upendo kwa Maria Msaada wa
Wakristo”.
Ilizinduliwa kisheria katika madhabahu ya Maria Msaada wa
Wakristo huko Torino 18 Aprili 1868, na “aliitazamia kuwa
sehemu maalum katika jumuiya ya Waselesiani(Fr Pietro
Ricaldone, Maria Ausiliatrice, Colle Don Bosco 1951, p. 83).
Katika mhutasari mfupi 5 Aprili 1870, Pius IX aliuinua katika
darala la Jumuiya kubwa, na ibada ya pamoja ya vyama ambavyo
vinaibuka katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa kijana
hilo na nia hiyo.
5 Julai 1989, Mkuu wa Waselesiani, Pd. Egidio Viganò pamoja
na halmashauri yake, rasmi walitambua ushirika wa Maria
Msaada wa Wakristo kama mwanachama wa familia ya
Waselesiani.
TESTUS APPROBATUS
Romae, die 7-10-2003
45

5.6 Page 46

▲back to top


KANUNI YA USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO
ASILI NA SABABU YA USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO [ADMA]
Kipengee1
Tendo la Msingi
Baada ya Don Bosko kujenga madhabahu ya heshima ya Bikira
Maria ambayo yaliwekwa wakfu kwa ajili ya Msaada wa
Wakristo [Torino 1868], kwa kufuatia ishara zake alizopata
kutoka njozi, alielewa baada ya mwaka ilikuwa hamu ya kujenga
Basilika. Ushirika wa wafuasi wa Maria Msaada wa Wakristo(18
April 1869) una wajibu wa kueneza ulimwenguni mwoto ibada
kwa Maria Maria kwa jina hilo.
Kanisa la Maria Msaada wa Wakristo, ndilo kiini cha kusambaza
utume huu, ulimwenguni pote, mahali hapa kwa Don Bosko
ilikuwa ukamilifu wa kazi zake zote, kisima cha neema na
madhabahu ya ulimwengu.
Upendo wa Don Bosko kwa Maria Msaada wa Wakristo
unapatikana katika ushirika huu kwa namna ya maelezo ya
kulinda na kutetea imani.
“Sisi Wakristo ni lazima tuunganike katika nyakati ngumu. Kuwa
miongoni mwa wale wanaotenda wema, ni chemichemi
inayochangamsha na kuchochea wema kwetu, bila kuelewa
zaidi”[MB 7, 602)
Uzoefu, “unatuoenyesha kuwa utume wa Maria kama
mama wa Kanisa na Msaada wa Wakristo, alioanza duniani,
unaendelea kutoka mbinguni kwa namna ya ajabu kwa
ulimwengu wote”.
(G.BOSCO, Meraviglie della Madre di Dio invocata sotto
il titolo di Maria Ausiliatrice, Torino, 1868, p. 45).
Uwepo huu wa Kimama wa Bikira Maria ndio msingi wa
Ushirika na msukumo wa majukumu ya wafuasi kwa ajili ya
huduma ya Ufalme wa Mungu.
46

5.7 Page 47

▲back to top


Kipengee 2
Asili na Sababu
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo unatoa nafasi ya
kukutana kwa waamini ambao hushiriki kazi maalumu ya Bikira
Maria.
Katika Kanisa, Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo ni
ushirika wa hadharahi wa waamini tukirejelea Sheira za Kanisa
[Kan. 298-320]. Tena ushirika huu una sifa ya sheria za Kanisa.
Katika nchi zote ushirika huu waweza fuata usajili wa kisheria,
hata hivyo ushirika huu si wa kisiasa, au wakutengeneza faida.
Ushiriki huu wa Maria Msaada wa wakristo unatoa mwongozo
wa utakatifu kwa ajili ya utume wa Waselesiani[ ni mapenzi yake
Bikira Maria tumheshimu kwa jina la Maria Msaada wa
Wakristo. Nyakati zetu ni ngumu, twahitaji huyu Bikira
Mtakatifu kutusaidia kutunza na kulinda imani ya Kikristo” MB
7,334]. Kwa njia ya pekee Don Bosko alianzisha ushirika huu ili
kuwashirikisha wafanya kazi katika maisha ya kiroho na utume
wa Shirika la Waselisiani, kama kikundi cha pili maalum katika
kazi zake [GC 24, 80]
Ushirika huu, unatoa nafasi ya pekee kabisa kwa ajili ya Ibada
kwa Ekaristi Takatifu na upendo kwa Maria Msaada wa Wakristo
katika kila namna, kwa matumizi ya binafsi au kwa ibada
hadharani ambayo imeidhinishwa na Kanisa.
Inatimiza wajibu wake kwa ushirika na utii kwa maaskofu wa
Kanisa na ushirikiano na vyama vingine vya Kanisa, hasa Familia
ya Waselesiani.
Jina lake rasmi ni Ushirika wa Maria Msaada wa
Wakristo au ASSOCIATION OF MARY HELP OF
CHRISTIANS (AMHC), na makao yake makuu yapo Torino,
via Maria Ausiliatrice 32, karibu na madhabahu ya Maria Msaada
wa Wakristo.
47

5.8 Page 48

▲back to top


Kipengee 3
Ushirika huu katika familia ya Waselesiani
Wafuasi wanaunda sehemu ya Familia ya Waselesiani, “kwa njia
ya heshima kwa Msaada wa Wakristo kadiri Don Bosko alivyo
weka msingi. Kuwa mfuasi ni kujitolea kumheshimu Maria,
msaada na Mama wa Kanisa, kwa kushiriki utume wa Don Bosko
kwa watu, hasa, vijana na zaidi katika kulinda na kuiteta imani ya
Kikristo”.(Egidio Viganò, Lettera Al Rettore del Santuario di
Maria Ausiliatrice a Torino del 24/07/1989).
Katika Familia ya Waselesiani, ushirika huu unahamasisha na
kueneza ibada kwa Maria kama namna ya kuinjilisha na
kuwasaidia watu, hasa vijana na wale maskini.
Ushirika huu unatambua [Rector Major] , mwandamizi wa Don
Bosko, kama baba na umoja wa Familia ya Waselisiani wote.
Kipengee 4
Wajibu wa kila mwanachama
Ufuasi kamili kwa ushirika huu, yadhihirisha kufuata kuwajibika,
hasa katika familia na mahali unaishi, na sehemu za kazi na wale
wote unashirikiana nao.
Bidii na heshima ya kushiriki maisha ya Liturjia, kwa kuungana
na Kanisa ambalo Maria ni sura na mfano ; na hasa kwa namna
ya kipekee kwa Sakramenti ya Ekaristi na Sakramenti ya Kitubio,
na jinsi ya kuishi binafsi maisha ya Ukristo:
-
Kuishi na kueneza ibada kwa Maria Msaada wa
Wakristo kadiri ya roho ya Don Bosko, hasa katika Famila ya
Waselisiani(Egidio VIGANÒ, Circular Letter: Mary renews Don
Bosco’s Salesian Family in ASC 289 January-June 1978);
- Kufanya upya, kuimarisha na kuishi ibada na maisha ya
kiroho kwa pamoja:
- Kumbukumbu ya Maria Msaada wa Wakristo kila Mwezi tarehe
24;
- Kusali rozari;
48

5.9 Page 49

▲back to top


- Novena kwa maandalizi ya Sikukuku ya Maria Msaada wa
Wakristo;
- Baraka ya Maria Msaada wa Wakristo;
-Hija kwa mahali patakatifu pa Maria;
- Maandamano ya sala;
- Kushiriki maisha ya parokia: Liturjia, Katekesi, kuwatembelea
wagonjwa na wazee, na mahitaji na huduma zingine katika
Kanisa.
-Kumuenzi Maria kwa namna ya kuishi maisha ya Ukristo katika
familia yako na pia kuwa mkarimu na yule ambaye anakaribisha;
- Kujihusisha na sala pamoja na matendo mema dhidi ya vijana
masikini na watu wengine wanaohitaji;
- Kusali na kuwaimarisha walei, watawa na wale amabo wana
vyeo ndani ya Kanisa na kwa namna ya pekee Familia ya
Waselisiani;
- Kila siku kuishi maisha ya kiroho yenye mwelekeo wa fadhila za
Injili, hasa kumshukuru Mungu kwa maajabu yanaoyoonekana
katika kazi zake, na kuwa mwaminifu kwake hata katika nyakati
za mateso na msalaba, kwa kufuata mfano wa Maria.
Kipengee 5
Kuwa mkarimu kwa zawadi za kiroho
Wafuasi hushirikishana faida ya neema na maisha ya kiroho
ambayo kwayo ni rasmi kwa ushirika na kwa yale katika familia
ya Waselesiani(Wafuasi hushiriki katika msamaha na faida ya
kiroho ambayo ni ya kipekee kwa chama na familia ya
Waselesiani. Tumepewa katika Nyongeza II maelezo muhimu kwa
ajili ya kutusaidia kuepuka matendo amabyo hayaendani na nia
ya Kanisa)
Zaidi, faidi ya maisha ya sala na ibada inayotolewa katika
Basilika la Maria Msaada wa Wakristo huko Torino na katika
makanisa mahali ushirika huu umeanzishwa.
Mfuasi akifa, wafuasi wengine katika kikundi wanaalikwa
kushiriki katika Ekaristi ya walio katika mateso na huzuni.
49

5.10 Page 50

▲back to top


II. MUUNDO WA USHIRIKA WA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO
Kipengee 6.
Ushirika
Katika mtindo wa Don Bosko, muundo upo kwa ajili ya huduma
kwa kila mmoja na ni rahisi sana na yenye kuwezekana, na
inaweza kutumika katika namna mbalimbali na kwa nchi
mbalimbali.
Ni ukweli kuwa: ni jambo la muhimu kuwa kazi ya Don Bosko
iliingiana na maisha ya kawaida hata katika mipangilio yake,
ambayo yajieleza. Aliweza kuonyesha wazi majukumu ya
kuendesha, kuimarisha na kukua”(Viganò, Letter to the Rector of
the Sanctuary of Mary Help of Christians in Turin, 24 July 1989).
Kipengee 7.
Usimikaji wa ushirika mashinani
Kwa njia ya [Kan. 312-317] na nafasi ya Shirika la Waselesiani,
ni wajibu wa mkuu wa Waselisiani katika kanda kusimika
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo katika vyuo vya
Waselesiani na Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo katika
sehemu anayotawala. Kwa hali zingine barua ya Askofu wa
mahalia inayoidhinisha huhitajika.
Kipengee 8.
Mkusanyiko
Baada ya kusimikwa rasmi, maombi yatakiwa kutumwa haraka
kwa ajili ya mkusanyiko. Yatumwe huko sehemu takatifu ya
Maria Msaada wa Wakristo Torino- Valdocco, ili kumaliza
uidhinishaji wa mkusanyiko kwa Ushirika wa Maria Msaada wa
Wakristo.
Hati kamili, ambayo imetiwa sahihi na Mkurugenzi wa mahali
patakatifu, ndiyo itakuwa hati rasmi ya uanachama. Inashauriwa
50

6 Pages 51-60

▲back to top


6.1 Page 51

▲back to top


kuitunza katika hifadhi maalum na kivuli chake kubandikwa
sehemu ambayo inaweza kuonekana kwa kila mtu.
Kipengee 9
Ushirika na mahali patakatifu pa Maria Msaada WA Wakristo huko Torino
"Ushirika wa Maria Msaada wa wakristo kwa namna ya pekee
imeunganishwa na mahali patakatifu kule Torino Valdocco.
Inaweza kusemwa pia kwamba Maria hakuonekana wazi katika
ujenzi wa wa mahali patakatifu, kwa maneno ya Don Bosko,
lakini kuanzia pale alianza kuweka ulinzi na usimamizi kwa
ulimwengu wote. Ndiyo sababu ushirika huu unapaswa kubaki
umeungana na na mahali patakatifu” [E. Viganò, Letter to the
Rector of the Sanctuary of Mary Help of Christians in Turin, 24
July 1989].
Kila ushirika wa mashinani, kwa hivyo, unapaswa kutengeneza
ushirika wa maelewano na umoja kwa mahali patakatifu pa Maria
Msaada wa Msaada wa Wakristo kule Torino Valdocco na hasa
na ushirika wa kwanza ulioanzishwa kule; Ushirika ulio makao
makuu utatekeleza wajibu wake kwa ajili ya muungano.
Kipengee 10
Ushirika wa pekee katika maisha ya Chama
Wakatoliki wote waliobatizwa hasa kuanzia miaka 18 wanaweza
kujisajili kwa uwanachama katika ushirika huu.
Uanachama unadai jukumu la kuishi yote yaliyotajwa katika
kipengee 4 cha sheria za sasa na pia kushiriki mara kwa mara
katika vikao vya ushirika kwa roho ya umoja na pia uanachama.
Usajili wa mkandidati katika ushirika ni lazima iidhinishwe na
rais pamoja na baraza lake. Hiyo hufanyika baada ya maandalizi
ya kutosha ambayo si chini ya mwaka mmoja, na vikao vya kila
mwezi.
Mkandidati aonyeshe uaminifu kwa ushirika wakati wa sherehe
saa ya Maria Msaada wa Wakristo, na atapata cheti, sheria na beji
ya uanachama.
51

6.2 Page 52

▲back to top


Ushirika wa mashinani, ni lazima uangalie malezi endelevu ya
wanachama, wapange shughuli zao kadiri ya mazingira yao
wakifuata sheria.
Katika roho ya umoja na uanachama, kila mmoja anachangia
matoleo kwa uhuru wake ili kukidhi mahitaji ya ushirika mahali
alipo na pia kupitia mpango wa kanda, ambayo inachangia pia
mahitaji ya ushirika katika makao makuu.
Kipengee 11
Nafasi ya uanachama
Kwa ajili ya ushirika, na kuendeleza malezi, kwa kubadilishana
hali ya maisha, ushirika wa mashinani unapanga yafuatayo:
- Vikao vya kila mwezi (pia wafuasi wengine wa Familia ya
Waselesiani wanaweza kushiriki bila pingamizi lolote) kwa ajili
ya malezi ya kanuni, sala na sherehe au kuabudu Ekaristi
Takatifu ikiwezekana tarehe 24 kila mwezi, siku ambayo Bikira
Maria anakumbukwa kwe heshima.
-Siku ya Maria ya kila mwaka;
- Kushiriki katika sherehe au vikao vya Familia ya Waselesiani.
- Mazoezi ya kiroho kwa ajili ya wafuasi;
- Maandamano, hija, siku za ritriti au mfungo;
- Vikao vingine ambavyo vimepangwa na ushirika mahalia.
- Taz. Kipengee 4
Kipengee 12
Baraza la utawala wa kituo katika ushirika
Kila baraza la utawala wa kituo unaratibishwa na baraza,
lililochaguliwa na wanachama wote kutoka orodha ya
wanachama ambao wamejitangaza kuwa watakuwa tayari
kuhudumia kwa udungu.
Baraza la utawala mahali, linahusu, raisi, makamu wa rais,
mweka hazina, katibu, na baraza la wajumbe, kadiri ya mahitaji
ya ushirika. Mlezi wa kiroho, mwanamume au mwanamke, pia ni
mfuasi wa baraza hilo.
52

6.3 Page 53

▲back to top


Kwa mkandidati kusajiliwa, anahitaji kura za wachache.
Wajumbe wa baraza wanabakia ofisini kwa kipindi cha miaka
minne na wanaweza kuchaguliwa kwa miaka mingine minne.
Wakati baraza limekamilika, kazi za pekee ndani yake
huamuriwa na baraza.
Rais ndiye huitisha vikao vya baraza na ndiye
anaendesha; anatayarisha agenda na kuwasilisha kwa wajumbe
wa baraza kupitia katibu. Rais anawakilisha ushirika katika vikao
vya nje na hasa vikao vinaovyo husu vikundi vingine.
Makamo wa raisi, anachukua nafasi ya raisi wakati labda
hana nafasi ya kuhudhuria vikao kwa sababu ambazo haziwezi
kuepukika, hii hufanyika tu baada ya maelewano na raisi.
Mweka hazina anatunza mali ya chama kulingana na sheria za
nchi husika na pia kwa maamuzi ya baraza. Kila mwaka
huwakilisha matumizi ya fedha na bajeti.
Katibu, kwa maongozi ya rais, anawatumia wajumbe tarehe na
agenda za mikutano, anaandika , na anatunza hifadhi ya ushirika.
Kwa kila mjumbe wa baraza, anapewa jukumu fulani mahali
alipo kwa ajili ya ushirika.
Kwa kawaida baraza hukutana mara moja kwa mwezi.
Kipengee. 13
Wanaoongoza katika maswala ya kiroho
Walezi wa kiroho wa ushirika wanachaguliwa na Mkuu wa
Waselisiani katika kanda au na Mkuu wa Mabinti wa Maria
Msaada Wa Wakristo. Hao wanaendesha, kipekee malezi ya
kiroho ya Waselesiani na ushirika katika maisha na miradi ya
kanisa mahalia.
Wale amabo wanaweza kuchaguliwa kwa malezi ya kiroho ya
wanachama, waweza kuwa kati ya wanachama wenyewe ikiwa
wameandaliwa.
Kipengee 14.
Mkuu wa Shirika na baraza la kitaifa.
53

6.4 Page 54

▲back to top


Ikiwezekana, katika ngazi ya juu ya shirika kwaweza kuwa
mjumbe mmoja ambaye anaratibisha na kuongoza mabaraza ya
wajumbe mashinani na Familia ya Waselisiani.
Baraza katika ngazi ya juu ya kanda huchaguliwa na marais wa
mashinani. Muundo wake ni kama ifuatavyo: Rais, Makamo wa
rais, Katibu, Mweka hazina, na baadhi ya wajumbe kadhaa.
Wajumbe wa baraza wanachaguliwa kwa miaka 4 na wanaweza
kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili miaka 4.
Mratibu wa kiroho, mke au mume, ni mjumbe wa baraza hilo.
Mahali inapowezekana, muundo wa waratibu wanaweza
kuanzishwa.
Kipengee 15
Wajibu wa Makao Makuu ya Chama
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo umehusishwa na mahali
patakatifu pa Maria Msaada wa Wakristo Torino Valdocco,
ambaye ndiye mrithi na mwendelezaji wa ushirika huu
ulioanzishwa na Don Bosco mwenyewe, na ndivyo unaitwa
“msingi”.
Kwa sababu ya asili yake na kushirikishwa na mahali patakatifu,
ushirika huu una wajibu wa kupyayusha, kuunganisha na kutoa
habari kuhusu ushirika huu ulimwenguni.
Ndio maana inakua kiungo maalum cha Maria Msaada wa
Wakristo, ambayo inachapishwa na jarida la “Maria
Ausiliatrice", huko Torino.
Kipengee 16
Baraza la Ulimwengu la Ushirika
Ni wajibu wa rais wa makao makuu ya ushirika kuitisha kikao
cha Baraza la Ulimwengu la Ushirika.
Baraza hili linahusu wafuatao: Makamu wa Mkuu wa Shirika la
Waselisiani, mjumbe wa Shirika la Mabinti wa Maria Msaada wa
Wakristo kutoka ngazi ya juu ambaye ndiye kiungo na Familia ya
Waselisiani, Rais na mratibu wa maisha ya kiroho na mjumbe
54

6.5 Page 55

▲back to top


kutoka makao makuu ya ushirika, pamoja na wawakilishi wa
nafasi zingine.
Kwa hiyo walei watakiwa kuwa wengi mno kuliko mapadre na
watawa.
Baraza hili hukutana kila baada ya miaka 6: Katika nyakati
maalum ya kongamano la Maria Msaada wa Wakristo, ambayo
inapangwa na baraza la wajumbe wa makao makuu ya Ushirika.
Kipengee 17.
Mali za Ushirika
Ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo, kwa sababu ni chama cha
Kanisa kinachotawaliwa na sheria, kinaweza kuwa na mali,
kutunza na pia kutumia kadiri ya sheria za Kanisa na sheria za
nchi husika.
Kipengee cha 18
Utafisiri wa Sheria
Utafsiri wa sheria kwa lugha zingine ni lazima ufuate maandishi
haya ya kisasa na tena utume Makao makuu kwa kuhakikisha.
NYONGEZA 1
KIGEZO CHA MKUSANYIKO WA WALEI KANISANI
(Christifideles Laici n. 30)
Daima ni kutoka kwa mtazamo wa ushirika wa Kanisa na utume,
na si kinyume na uhuru wa kujiunga, hivyo mtu anaelewa
umuhimu wa kuwa na vigezo wazi na wazi kwa kutambua
makundi hayo yaliyowekwa, pia huitwa "Vigezo wa Ufalme ".
Vigezo vya msingi vinavyofuata vinaweza kusaidia katika
kutathmini chama cha waaminifu katika Kanisa:
- Uwezo unaotolewa kwa wito wa kila Mkristo kwa utakatifu,
kama ilivyo imeonyeshwa "katika matunda ya neema ambayo
roho hutoa kwa kila mwaamini "[LG 39] na katika ukuaji
kuelekea ukamilifu wa maisha ya Kikristo na ukamilifu wa
upendo [LG 40]. Katika maana hii chama chochote cha waamini;
55

6.6 Page 56

▲back to top


daima huitwa kuwa chombo zaidi kinachoongoza kwenye
utakatifu Kanisa, kwa kuimarisha na kukuza "umoja zaidi wa
karibu kati ya maisha ya kila siku ya wanachama wake na imani
yao "[AA 19].
- Wajibu wa kudai imani ya Kikatoliki, kukubaliana na kutangaza
ukweli kuhusu Kristo, Kanisa na ubinadamu, katika kutii
Magisteriam ya Kanisa, kama Kanisa linalitafsiri. Kwa sababu hii
kila ushirika wa waamini wafuasi lazima uwe jukwaa ambapo
imani inatangazwa pamoja na kufundishwa katika maudhui yake
yote.
- Shahidi wa ushirika wa nguvu na wa kweli katika uhusiano na
Papa, kwa kuzingatia kabisa imani kwamba yeye ni kituo cha
daima na kinachoonekana cha umoja wa ulimwengu wote Kanisa
[LG 23], na kwa Askofu wa ndani, "kanuni inayoonekana na
msingi wa umoja "[LG 23] katika Kanisa fulani, na" kwa pamoja
heshima kwa aina zote za utume wa Kanisa "[AA 23]. Ushirika
na Papa na Askofu lazima waonyeshe kwa uwaaminifu utayari
wa kukubali mafundisho ya mafundisho na mipango ya
wachungaji wa Papa na Askofu. Aidha, ushirika wa Kanisa
unahitaji wote kutambua aina nyingi za halali katika vyama vya
waamini katika Kanisa na wakati huo huo, nia ya kushirikiana
katika kufanya kazi pamoja.
- Kukubaliana na kushiriki katika malengo ya kitume ya Kanisa,
yaani, "uinjilisti na utakaso wa ubinadamu na
Kuundwa kwa Kikristo kwa dhamiri ya watu, ili kuwawezesha
kuifanya roho ya injili katika jamii mbalimbali na
nyanja za maisha "[AA 20]. Kwa mtazamo huu, kila aina ya aina
ya kuweka waamini unaulizwa kuwa na bidii ya umisionari
ambayo itaongeza ufanisi kwa washiriki katika uinjilisti tena.
- Kujitolea kwa uwepo katika jamii ya wanadamu, ambayo
inaelekea Mafundisho ya Kanisa ya kijamii, huiweka katika
huduma ya jumla heshima ya mtu. Kwa hivyo, vyama vya
waamini vyapaswa kuwa na matunda ya ushirikiano katika kuleta
hali kwamba ni haki zaidi na upendo ndani ya jamii. Vigezo vya
56

6.7 Page 57

▲back to top


msingi vilivyotajwa wakati huu kupata ukaguzi wao katika
matunda halisi ambayo fomu mbalimbali za kikundi zinaonyesha
ndani ya maisha ya shirika na kazi wanazofanywa, kama vile:
rejea upya kwa maombi, kutafakari, liturujia na maisha ya
sakramenti, ufufuo wa wito kwa Wakristo wa ndoa, ukuhani wa
utumishi na maisha ya kujitolea; utayari wa kushiriki katika
mipango na shughuli za Kanisa katika ngazi za mitaa, kitaifa na
kimataifa; kujitolea kwa nguvu na uwezo wa kufundisha na
kuunda Wakristo; tamaa ya kuwa kuwasilisha kama Wakristo
katika mazingira mbalimbali ya maisha ya kijamii na uumbaji na
kuamka kwa kazi za usaidizi, utamaduni na kiroho; roho ya
kikosi na umaskini wa kiinjili inayoongoza zaidi na ukarimu
katika upendo kwa wote; uongofu kwenye maisha ya Kikristo au
kurudi kwa ushirika wa Kanisa kwa wanachama waliobatizwa
ambao wameanguka mbali na imani.
(Apostolic Exhortation, 30/12/1988 of John Paul II, n.30)
NYONGEZA II
MSAMAHA
Mungu hutoa msamaha kwa Kiburi cha dhambi iliyotendwa
ambayo hatia tayari imesamehewa, waamini ambao
wamewekwa vizuri na kwa hali fulani wanaweza kupata kupitia
kuingilia kwa Kanisa ambalo, kama chombo cha ukombozi, lina
mamlaka na kutumia hazina ya kuridhika iliyofanywa na Kristo
na watakatifu.
Kiburi ni sehemu ya kawaida ya dhambi kwa vile inaelekeza mtu
katika adhabu ya dhambi. Hakuna mtu anayeweza kuomba
huruma kwa watu wengine ambao bado wanaishi. Huruma na
msamaha wa kawaida inaweza pia kutumiwa kwa wafu kwa njia
ya kutosha.
MSAMAHA WA MUDA MREFU
Hati ya utume wa sheria ya tarehe tarehe 31 Januari 1968 ilitoa
msamaha uliotolewa katika orodha zifuatazo katika nambari 1, na
4 hadi 10, na tarehe 6 Februari 2002 wale waliopewa 2 na 3,
msamaha ulitolewa kwa muda mrefu.
57

6.8 Page 58

▲back to top


1. Siku ya kujiunga na chama;
2. Mt. Fransisko wa Sale, 24 Januari;
3. Mt. Yohani Bosko, Januari 31;
4. Kupashwa habari Maria, Machi 25;
5. Maria Msaada wa Wakristo, Mei 24;
6. Hija, Mei 31;
7. Bikira Maria kupalizwa Mbinguni, Agosti 15;
8. Siku ya kuzaliwa kwa Mama yetu, Septemba 8;
9. Bikira Maria Imakulata, Desemba 8;
10. Siku ya Krismasi, Desemba 25.
MASHARTI
1. Kujitolea kupigana dhidi ya dhambi;
2. Kukiri kwa Sakramenti kwa Sakramenti ya Kitubio;
3. Ushirika wa Ekaristi;
4. Sala kwa madhumuni ya Papa;
5. Upyaji, angalau lakini waziwazi, ya ahadi ya kuzingatia kwa
uaminifu Kanuni za Chama.
N.B.
a) Wajumbe wanaweza kupata kibali na msamaha wa muda
mrefu kwa jumla kadiri ya siku zilizoorodheshwa, au siku
ambayo sikukuu inahamishwa.
b) Wajumbe wanaweza kupata msamaha wa jumla kwa waamini
wote katika kipindi cha mwaka wa Liturujia, lakini katika hali,
ahadi ya kufuata kanuni haitajiki.
MSAMAHA WA MUDA
Kuna sala nyingi sana na matendo mema ambayo kwa kupata
msamaha ni sehemu ya masharti.
Miongoni mwao ni mbili zilizopendekezwa na Don Bosco
mwenyewe katika Kanuni za ADMA:
1. Isifiwe na itukuzwe sasa na siku zote Sakramenti Takatifu
sana ya Kimungu”.
2. Maria Msaada wa Wakristo, tuombee.
58

6.9 Page 59

▲back to top


Hali zingine tatu lazima pia ihifadhiwe katika akili; ni
msamaha ambao unatolewa kwa waamini wote:
1. Fadhila ya waamini ambaye, katika kutekeleza majukumu yao
na kukabiliana na shida za maisha hujiaminisha kwa
unyenyekevu kwa Mungu, na kuongeza wakati huo huo - hata
kiakili - kuomba moyoni.
2. Kutoa fadhila kwa waamini ambao, kwa roho ya imani na
huruma, hujiweka wenyewe na mali zao katika huduma ya ndugu
au dada aliye na mahitaji.
3. Fadhila ya mwamini ambaye, kwa roho ya toba, kwa hiari
hufanya malipizi kwa kitu halali.
NYONGEZA III
KANUNI YA WAFUASI WA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO
Imeandikwa na Don Bosko
1. Katika Kanisa la Torino ambalo limewekwa kwa heshima ya
Maria Msaada wa Wakristo, limewekwa rasmi na kisheria kwa
idhini ya Askofu Mkuu wa Torino mfuasi wa Maria; Wajumbe
wa Shirika hilo wanalenga kukuza heshima kwa Mama wa
Mungu wa Mwokozi ili kustahili katika maisha na hasa wakati
wa kufa.
2. Wao wana malengo mawili maalum: kueneza ibada kwa Bikira
Maria na kumheshimiwa Yesu katika Ekaristi Takatifu.
3. Kwa hivyo watatumia maneno, ushauri, kazi njema na
ushawishi wa kukuza utukufu na kujitolea katika karamu, sikukuu
na maadhimisho yanayotokea wakati wa mwaka ili kumheshimu
Bikira Mtakatifu na Sakramenti Takatifu Zaidi.
4. Kuenea kwa vitabu vyema, picha, medali na vipeperushi,
kushiriki katika maandamano kwa heshima ya Maria mtakatifu
sana na Ekaristi Takatifu kwa kuhimiza wengine kufanya hivyo,
mara kwa mara kushirika na kuwepo kwa Misa takatifu,
kuambatana na Viaticum kwa wanaokufa , ni mambo wanachama
wanajaribu kukuza kwa njia zote zinazowezekana kwa hali yao
katika maisha.
59

6.10 Page 60

▲back to top


5. Wajumbe watajitahidi kamwe kutotumia lugha ya kashfa au
kushiriki katika majadiliano kinyume na dini, na watajitahidi
kabisa kuzuia wale walio chini ya malezi yao kufanya hivyo;
wote wataondoa vikwazo katika njia ya utakaso wa siku za
Jumapili na Siku ya Sikukuu.
6. Kila mwanachama, kulingana na ushauri wa Katekismui na
wakurugenzi wa kiroho, amehimizwa vyema kupokea
Sakramenti ya kitubio na Komunio mara moja kwa mara mbili
au mara moja kwa mwezi, na kushiriki Misa ya kila siku ikiwa
kazi yake inaruhusu.
7. Kila siku baada ya maombi yao ya asubuhi na usiku, wajumbe
watasema kwa heshima ya Sakramenti Takatifu: “Isifiwe na
itukuzwe sasa na siku zote Sakramenti Takatifu sana ya Kimungu
"; na kwa heshima ya Bikira Maria: "Maria Msaada wa Wakristo,
utuombee". Kwa makuhani inatosha katika misa kuwa na nia ya
wafuasi wote wa ushirika. Sala hizi zitatumika kama dhamana ya
kuunganisha wanachama wote ili wawe na roho moja na wazo
moja kwa ajili ya kumwabudu Yesu aliyeko katika Ekaristi
Takatifu na Mama yake, na kushiriki katika mema yote
yanayotendwa na chama.
[From "Letture Cattoliche", Year XVII, May, Vol. V, pp. 48-50]
60

7 Pages 61-70

▲back to top


7.1 Page 61

▲back to top


IBAADA YA KUWAPOKEA WANACHAMA WAPYA
Aya no 10 ya sheria yatueleza kuwa: Mkandidati anaonyesha
uaminifu kwa ushirika, katika sherehe kwa heshima ya Maria
Msaada wa Wakristo. Baada ya homilia utaratibu huu ufuate:
Kiongozi:
Leo ni siku ya furaha kwenu ninyi mnao tazamia kujiunga na
ushirika wa Maria Msaada wa Wakristo. Mmeomba kuwa
wanachama wa ushirika huu ili kuwa mashahidi wa upendo kwa
Bikira Maria Mtakatifu na wajibu wenu kumfanya atambulike na
apendwe. Tuanze sherehe yetu kwa namna ya tendo la kawaida
kwa kuwaita kila mmoja jina. Mwito huu una maana kwamba
Maria Mtakatifu anawaalika kujiunga na ushirika ambao una jina
lake.
Kuwatambulisha Wakandidati
Wakandidati wanaitwa na kiongozi wa ADMA, atawaita kwa
majina yao yote. Na kila aliyehudhuria ataitika, “Nipo” na
kujongea altare.
MAHOJIANO
Kiongozi: Kadiri unavyojongea altare, unaomba nini?
Wakandidati: Tunaomba kuwa wafuasi wa Ushirika wa Maria
Msaada wa Wakristo.
Kiongozi: Je mnaelewa majukumu mnayochukua wenyewe kwa
kujiunga
na
ushirika
huu?
Wakandidati: Kila mmoja binafsi atafanya maisha yake ya
kiroho yawe mfano wa Bikira Maria, kuyafanya maisha yetu
yawe kama yake, kumwamini Mungu pekee, na kufanya hii kuwa
jukumu la maisha yote.
Hivyo, kusikiliza kama bikira alivyosikiliza, tutabaki makini kwa
kusikiliza Neno la Mungu, ambalo tutatangaza kwa neno na
mifano ya maisha yetu.
Kama vile bikira alivyosali, tutahakikisha kuwa maisha yetu
61

7.2 Page 62

▲back to top


yatanurishwa na sala ya rohoni katika mawazo na shukrani
mbele ya Baba. Kama Bikira Mama, tutashirikiana na Papa na
maaskofu kwa ajili ya kukua kwa watu wa Mungu.
Kama vile bikira alivyojitolea mwenyewe, tutafanya maisha yetu
matoleo kwa Mungu, kwa furaha ya kukamilishwa na mapenzi ya
Baba ambayo ndiyo njia ya kutakatifuzwa.
Kiongozi: Ni majukumu yapi ya kipekee unayojiwekea kama
mwanachama
wa
ushirika
huu?
Wakandidati: Kama tabia yetu ya kipekee na wajibu,
tunatazamia kueneza ibada kwa Maria Msaada wa Wakristo na
kumwabudu Yesu katika Ekaristi Takatifu katika jamii yetu.
Hayo yote tutatimiza kwa maneno yetu na matendo ambayo
yanatokana na Injili na maisha ya kiroho na utume wa Mtakatifu
Yohane Bosko.
Baraka juu ya beji na kadi za uanachama:
Kiongozi: Bwana unadhihirisha upendo wako ndani ya Bikira
Maria, Mama yetu na msaada. Tunakuomba picha hizi, ziwe,
ishara ya wokovu wako miongoni mwetu. Amina!
(Kiongozi
ananyunyizia
maji
ya
Baraka)
Kiongozi: Beji hizi zilizo na ishara picha ya Maria Msaada wa
Wakristo zikukumbushe uanachama wako wa Ushirika wa Maria
Msaada wa Wakristo ulionzishwa na Mt. Yohane Bosko. Maria
Msaada wa Wakristo akuwezeshe kukuwa katika Bwana Yesu
Kristo, kwa yule ambaye umechukua majukumu kuwa mfausi
wake mwaminifu. Bikira Maria akupe ulinzi na usaidizi wa
Mama.
Amina!
Kiapo wanachochukua Wakandidati
[Wakandidati wote hupiga magoti na kusema yafuatayo]
Bikira Maria, Msaada wa Wakristo na Mama wa Kanisa, kwa
kuwa mfuasi wa ushirika wako, ninaahidi kuwa shahidi
mwaminifu wa Kristo katika maisha yangu ya kila siku, hasa kwa
familia yangu, sehemu ya kazi, na katika jamii na Kanisa, kwa
nguvu na uwezo unaotokana na sala, na katika kuopkea
62

7.3 Page 63

▲back to top


Sakramenti ya Kitubio na Ekaristi mara kwa mara. Ninaahidi
kuomba kwa ajili ya miito kwa ajili ya Kanisa na familia ya
Kiselesiani, kwa kufuata mafundisho na mifano ya Mt. Yohane
Bosko na kujiaminisha kwa msaada wa kimama utakao nipa.
Wakristo wote hujibu. Amina.
Basi kila mwanachama hupewa katiba, beji na kadi ya
uanachama.
Kiongozi: Sasa wewe ni mwanachama Kamili wa Ushirika wa
Maria Msaada wa Wakristo, na mshiriki wa neema za kiroho za
ushirika huu, na kazi zote njema zinafanywa ndani ya familia ya
Waselesiani iliyoanzishwa na Mt. Yohane Bosko.
Kiongozi:
Maria Msaada wa Wakristo.
Wote wanaitikia: Utuombee.
SALA ZA WAAMINI
Kiongozi:
Ndugu na dada, tumwombe Mungu Mwenyezi katika huruma
yake, asikie sala tunazomtolea kwa maombezi ya Maria msaada
wa Wakristo.
Kiitikio: Bwana Utusikie
1. Tunaliombea Kanisa Takatifu la Mungu, ili “Maria, Bikira
mwenye nguvu, mtetezi wa Kanisa”, alisaidie Kanisa kwa upendo
wa
kimama.
2. Tunaomba kwa ajili ya Baba Mtakatifu: Kama watangulizi
wake Mt. Pio V na Pio VII apate ulinzi kamili wa Maria Msaada
wa Wakristo katika majaribu yote na magumu katika Kanisa.
3. Kwa ajili ya maaskofu, mapadre na watawa, ili katika ushirika
na Baba Mtakatifu, waongozwe katika imani na maisha ya
Kikristo ambayo wamepewa kwa ajili ya kutunza na kulilinda
Kanisa la Mungu.
4. Kwa ajili ya recta meja mkuu wa Waselisiani, na kwa wakuu
na kamati mbalimbali za Familia ya Waselisiani, waweze kupata
63

7.4 Page 64

▲back to top


ulinzi wa Maria Msaada wa Wakristo na Mt. Yohane Bosko
katika shughuli zote za kuwaongoza Waselisiani.
5. Kwa ajili ya wote tulio hapa, wafuasi wa ushirika wa Maria
Msaada wa Wkaristo, ulimwenguni kote na hasa kwa wale ambao
wamekuwa wafuasi leo, kwamba katika kusherehekea na
kuheshimu Maria Msaada wa Wakristo, tujisikie tumeungana
katika sala na kuishi kwa kuendeleza ibada kwa Maria Msaada
wa Wakristo, kwa ajili ya kutafuta miito mitakatifu kwa ajili ya
Kanisa
na
Familia
ya
Waselisiani.
Kiongozi:
Baba, ulimchagua Maria ashiriki katika mpango wako wa
ukombozi wa Mwanadamu, sikiliza sala na maombi yetu
ambayo tunakutolea katika imani, tunamwita yule ambaye
umetupatia awe Mama na Msaada. Kwa njia ya Kristo
Bwana wetu. Amina.
64

7.5 Page 65

▲back to top


NOVENA
MAANA YA SALA YA NOVENA
Neno la Kilatini Novena humaanisha tisa. Novena ni siku tisa za
sala au ibada katika dini ya Kikristo. Inahusu sala za mtu binafsi
au jamii ya watu. Novena imepata maana mpya kuwa alama ya
kumbukumbu ya maisha ya sala kwa ajili ya jambo fulani. Kabla
ya Yesu kupaa mbinguni aliwaagiza Mitume wake wabaki
Yerusalemu hadi atakapokuja tena. Mitume wa Yesu na Bikira
Maria walisali kuanzia kupaa kwake hadi wakati wa Pentekoste.
Inahesabika kuwa tangu kupaa hadi Pentekoste ilikuwa kibindi
cha siku tisa. Hivyo basi novena katika maana yake Kikristo ni
siku tisa za sala maalum kwa ajili ya kumwelekea Mungu kiroho
kila siku [Matendo ya Mitume 1:12-2:5]. Novena huwa na lengo
maalum la kumwomba Mungu. Katika nyakati hizo za novena,
waweza kutoa maombi nia yako, kwa ajili ya jambo fulani. Zaidi
sana mtu yule hushiriki novena yoyote, hupokea neema kwa ajili
ya kumwabudu Yesu akisaidiwa kwa maombezi ya Bikira Maria
na Watakatifu.
FAIDA YA NOVENA
Kusali novena humsaidia mtu kukua kiimani na pia kupata neema
za Mungu kwa ajili mahitaji fulani. Katika Ubatizo tumefanywa
kuwa wana wa Mungu na katika imani tunamfikia. Hivyo basi,
ukiwa na shida, hitaji lolote, magonjwa na mahangaiko yoyote,
novena hukuwezesha kujipa hamu na nidhamu ya kusali kila siku.
Hali hiyo hukupa heri na neema za Mungu kila siku. Maana
mawasiliano yako na Mungu huwa yapo kila siku na ushirika
huu, hukufaidi wewe mwanadamu kwa kuwa katika hali ya
neema. Utajaliwa amani na furaha katika maisha.
Tunasali novena kwa kujiandaa kwa tukio kuu la kiibaada au siku
kuu Mfano: Kristmasi, sherehe au sikukuu ya mtakatifu
msimamizi wetu na pia novena waweza kusali kwa ajili ya
shukrani kwa Mungu kwa ajili ya jambo fulani, au kwa ajili ya
kujiandaa kwa tukio fulani: mfano mitihani, afya, kwa ajili ya
mpango fulani ya familia na mengine mengi. Zaidi ya yote
65

7.6 Page 66

▲back to top


novena hukuimarisha katika imani na maisha ya kiroho. Katika
novena utapata neema nyingi za Mungu kwa ajili ya kukabiliana
na hali zote za maisha bila kupoteza matumaini au kukosa amani.
NAMNA YA KUJIANDAA KWA NOVENA
Fuata hatua zifuatazo:
i) Kuwa na lengo mahsusi la kumrudia Mungu katika imani
yako.
ii) Kuwa na lengo maalum au nia ambayo wataka kusali kwa
ajili yake.
iii) Katika siku hizo za Novena, shiriki sakramenti ya kitubio.
iv) Pokea Ekaristi Takatifu.
v) Unaweza kumshirikisha mtu yeyote awe rafiki wa sala
katika novena yako.
vi) Maliza Novena yako kwa Misa Takatifu.
vii) Baada ya kumaliza novena fanya tendo la huruma kwa
kuwasaidia wengine wamjue Mungu.
viii) Fanya tendo la ukarimu, kulisaidia Kanisa kwa sala,
sadaka, michango na ustawi wa maendeleo ya Kanisa kwa jumla.
WAJIBU WA MTU ANAYESALI NOVENA
Mtu yeyote anayesali novena, aonyesha shukrani kwa neema
ambazo amepata kwa Mungu. Maana siku zote unazosali novena
ni za neema. Baada ya kusali novena siku tisa, onyesha shukrani
kwa Mungu kadiri ya uwezo wako kulisaidia Kanisa kwa namna
ya matoleo na ukarimu na pia kuwa mfano mwema kwa jamii.
Uwe kielelezo cha imani. Novena haichukui nafasi ya majukumu
ambayo wapaswa kutenda, bali inakupa neema ya kujipa
matumaini na kuunganika na Mungu.
Ni chaguo lako kufuata novena yeyote, maana lengo kuu la
novena ni Shukrani kwa Mungu kwa neema ambazo
tunapata na pia kudumu katika urafiki wake.
66

7.7 Page 67

▲back to top


Zifuatazo ni Baadhi ya Novena ambazo waweza kutumia katika
kuimarika kiimani.
1. NOVENA YA DAIMA KWA BIKIRA MARIA MSAADA
WA WAKRISTO
Novena hii ni kama ilivyoshauriwa na Mtakatifu Yohane Bosko
kwa ajili ya kupata neema na misaada ya Mungu.
KWA YESU KATIKA SAKRAMENTI YA EKARISTI
TAKATIFU
Wote: Ee Yesu mpendelevu sana ambaye unapendezwa mno
kukaa kati ya watu na kuwa chakula cha roho zao utusaidie
tunakusihi- kwa njia ya mastahili ya Mt. Yohane Bosko ambaye
alijibidisha sana kuamsha katika vijana na Wakristu tamaa ya
kujiunganisha nawe mara nyingi- katika Sakramenti ya Ekaristi
Takatifu- yaani Sakramenti ya upendo wako tuweze kupata
tunaloomba kwa unyenyekevu na tamaa kubwa ya roho zetu.
Salamu Maria x3……. Baba yetu x3…… Atukuzwe Baba x
3….”Isifiwe na itukuzwe sasa na siku Zote Sakramenti Takatifu
sana ya Kimungu”
KWA BIKIRA MARIA, MSAADA WA WAKRISTO
Wote: Ee Bikira Mtakatifu sana msaada wa Wakristo ambaye,
kwa njia ya Mt. Yohane Bosko- ulitenda, na bado unaendelea
kutenda miujiza mingi utupatie twakusihi kwa wema wako
wakimama-na kwa mastahili yake- sisi maskini wakosefu- tuweze
kupata misaada tunayohitaji-ambayo tunaiomba-kwa tamaa
kubwa ya roho zetu.
Salamu malkia, mama mwenye huruma x3,…Maria Msaada wa
Wakristo utuombee!
KWA MTAKATFIU YOHANE BOSKO
Wote: Nawe, Mt. Yohane Bosko uwatolee Yesu na Maria sala
zetu basi pamoja na neema tunaomba-pia utuwezeshe kwa
maombezi yako kupata na kuongezewa zaidi na zaidi- upendo
67

7.8 Page 68

▲back to top


kwa Yesu katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na kwa Bikira
Maria Msaada wa Wakristo Amina.
Mt. Yohane Bosko Utuombee!
BARAKA YA BIKIRA MARIA MSAADA WA WAKRISTU
Padri: Msaada wetu katika jina la Bwana.
Wote: Aliyeumba mbingu na dunia.
Salamu Maria………………
Wote: Tunakimbilia ulinzi wako Ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu
usitunyime tukiomba katika shida zetu utuopoe daima katika
hatari zote ewe Bikira Mtukufu mwenye baraka.
Padri: Maria Msaada wa Wakristo!
Wote: Utuombee!
Padri: Ee Bwana usikilize sala yangu,
Wote: Mlio wangu ukufikie!
Padri: Bwana awe nanyi!
Wote: Awe pia nawe!
Tuombee
Mungu Mwenyezi wa milele ambaye kwa msaada wa Roho
Mtakatifu ulitayarisha mwili na roho ya Bikira Maria
Mtukufu kuwa kikao kistahilifu cha mwanao utujalie
kwamba kama tunavyosherehekea
kwa furaha
kumbukumbu yake tuweze kwa maombezi yake ya kipendo
kutenganishwa na mabaya ya dunia hii na upotevu wa milele
kwa njia ya Yesu Kristu Bwana wetu. Amina!
Padri: Baraka yake Mungu Mwenyezi ya Baba na Mwana, na
Roho Mtakatifu, iwashukie na kukaa nanyi daima. Amina!
2. NOVENA YA EKARISTI KWA MARIA MSAADA WA
WAKRISTO
Yohane Bosko alikuwa muenezaji mkuu wa ibaada kwa Maria
Msaada wa Wakristo. Kwa wale wote waliomwomba msaada,
aliwashauri wasali novena hii kwa Maria Msaada wa Wakristo.
68

7.9 Page 69

▲back to top


Miujiza mingi ilitendeka kwa wale waliofuata ushauri wa
Mtakatifu Yohane Bosko.
i. Kwa siku 9 sali sala zifuatazo kwa heshima ya Yesu katika
Ekaristi Takatifu, Baba yetu…….. x3, Salamu Maria………. x
3, Atukuzwe Baba………….. x3 pamoja na sala fupi; “ Isifiwe
na itukuzwe sasa na siku zote Sakramenti Takatifu sana ya
Kimungu”. Halafu sala ya Salamu Malkia….x3 …pamoja na
sala fupi: “Maria Maria Msaada wa Wakristo utuombee!
ii.Shiriki Sakramenti ya Kitubio kadiri ya mahitaji yako na Ekaristi
Takatifu katika siku hizi za Novena. Kuwa mkarimu kwa kazi za
Don Bosco kadiri ya uwezo wako kwa namna ya matoleo au
mchango wowote.
3. NOVENA KWA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Novena ifuatayo ni ile ndefu, kwa siku tisa. Utaratibu wake wa
imbada upo baada ya Novena hii.
SIKU YA KWANZA
UTII
KKK 2216-17; 2251; 411, 475, 532, 539, 612, 615, 908, 1009,
1269
Katika maana na hali ya kawaida, utii ni kusikiliza na kutii amri
kutoka kwa yule aliye mkuu na kufuata maagizo yake. Ukifuata
utapata heshima na pia baraka. Ukikosa kusikia na kutekeleza
utapata adhabu. Utii katika Maandiko Matakatifu, ni kusikiliza
Neno la Mungu na kutimiza yale unayoambiwa. Ukiwa mtii kwa
Neno la Mungu, basi una baraka, ukikosa wewe una laana. Utii
katika Ukristo unamaanisha kusikia; kuamini; kujitoa kwa Mungu
na Neno lake.
Bwana wetu Yesu Kristo alitupatia matumaini kuwa amefika
hapa ulimwenguni si kufanya mapenzi yake bali mapenzi ya Baba
yake. Tunasoma jinsi anavyoeleza mwenyewe:
69

7.10 Page 70

▲back to top


Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye
mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi
yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa
nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. Kwa
kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila
amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa
milele; nami nitamfufua siku ya mwisho”[ Yoh 6:38-40]
Maisha yake Yesu yalikuwa utii kwa Baba. Yeye alijulikana
kama Mwana na Mtumishi kuonyesha kwamba alikuwa na umoja
na Baba kwa kumtii. Utii unamfanya kuwa tayari katika kazi ya
utume kuwakomboa watu. Kuwa mfuasi wa Kristo utii ni
muhimu humpa mtu heri kwa kumtayarisha kwa ajili ya utume
ambao ameitwa kutekeleza. Utume huo ni lazima uwe na
majukumu yanayodai ukarimu na moyo wakujitolea.
Roho ya utii yapaswa yafuatayo:
Kuishi imani kikamilifu.
Ni kuweka maanani katika jambo linalompendeza Mungu
Baba na kuwachana na mambo ya tamaa ambayo
yanakupendeza wewe na kukufanya uwe mbinafsi na mnafiki.
Kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya sala, utume,
kutafuta ushauri na kufuata ishara ambazo Mungu
anatujalia.
Kukubali kwa hiari imani tuliyopewa na kutafuta utakatifu
katika maisha ya kila siku. Kukubali mafundisho na
mwongozo wa viongozi wa Kanisa hasa baba mtakatifu,
maaskofu na mapadre. Kufuata amri kumi za Mungu na amri
za Kanisa.
Kutimiza wajibu wako kila siku Kwa ubunifu na ukarimu,
kutumia muda wako kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Kujitolea kwa hali na mali katika kusitawisha Kanisa kwa
kuwa mkarimu.
Kuwa mvumilivu nyakati za shida kwa kumwangalia Yesu
Kristo Msalabani.
70

8 Pages 71-80

▲back to top


8.1 Page 71

▲back to top


Sote tuu washiriki wa Kanisa, mbatizwa hawi wake yeye
mwenyewe bali wa yule aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu.
Toka hapo umeitwa kujiweka chini ya wengine, kuwatumikia
katika umoja wa Kanisa na kuwa “mtii” na “mnyenyekevu” kwa
viongozi wa Kanisa na kuwaheshimu na kuwapenda. Sawa kama
Ubatizo ulivyo asili ya uwajibikaji na majukumu, vivyo hivyo
mbatizwa hufurahia haki katika Kanisa: kupokea Sakramenti,
kulishwa Neno la Mungu na kusaidiwa na misaada mbalimbali ya
kiroho ya Kanisa [KKK 1269].
Uhai, uwezo na vipaji tulivyo navyo Mungu anatuita tuvitumie
kwa ajili ya wengine. Japo huwa jambo gumu, lakini tunao mfano
dhabiti wa kimsingi kutoka Mwana wa Mungu.
SABABU MUHIMU KUMTII MUNGU
1. Yesu atualika kuwa watii
Yesu Kristo ndiye mfano bora wa utii. Kama wafuasi wake ni
lazima kufuata mfano wake na amri zake. Sababu kuu ya kuwa
watii ni kama ifuatavyo:
Mkinipenda mtazishika amri zangu”[Yoh 14:15]
2. Utii ni Ishara na alama ya Ibada
Ukombozi ni zawadi ya Mungu mwenyewe, kwa namna zetu
wenyewe hatuwezi kumiliki. Utii wa kweli wa Mkristo hutokana
na hali yake ya shukrani na neema ambayo imetoka kwa Mungu.
“Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni
miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu,
ndiyo ibada yenu yenye maana” [Rum 12:1].
71

8.2 Page 72

▲back to top


3. Mungu huzawadia Utii
Katika maandiko Matakatifu tunasoma kuwa Mungu hubariki
mtu yeyote ambaye anatii.
“…na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa
sababu umetii sauti yangu”[ Mwa 22:18];Mwa 22:18; Kutoka
19:5; Luka 11:28; Yakobo 1: 22-25
4. Utii kwa Mungu ni ishara ya Upendo wetu kwake
Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu:
tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake”[ 1 Yoh 5:2-3]; 2
Yoh 6
5. Uti kwa Mungu ni alama ya Imani
“Na katika hili twajua yakuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika
amri zake. Yeye asemaye, “Nimemjua,” wala hazishiki amri
zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye
ashikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika
kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye
asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda
mwenyewe vilevile kama yeye alivyoenenda.
6. Utii ni afadhali kuliko Sadaka
[1 Sam 15:22-23]
7. Kutotii humwelekeza mtu katika dhambi na kifo
Kutotii kwa Adam kulileta dhambi na kifo katika ulimwengu.
Utii wa Kristo ulileta ushirika na Mungu kwa wale wanao
mwamini.
72

8.3 Page 73

▲back to top


Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja, watu wengi
walingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii
kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye
haki [Rum 5:19; 1 Kor 15:22]
8. Katika Utii, tunapata baraka takatifu katika maisha
Ni Yesu pekee aliye mkamilifu, ni yeye tu aliyeweza kuwa na utii
kamili. Tukimkubali Roho Mtakatifu kutuongoza na
kutubadirisha kutoka ndani mwetu, tunaanza kukua katika
utakatifu.
Heri walio kamili njia zao; waendao katika sheria ya
Bwana….[Zab 119:1-8], Isaya 48:17-19; 2 Kor 7:1]
Tafakri ya Maandiko Matakatifu
Wafilipi 2:1-11, Zab 40
Tuombe
Bikira Mtakatifu
, Msaada mkubwa wa Wakristo, nakuelekea katika imani. Katika
huruma yako sikiliza sala yangu mimi mdhambi maskini, nina
kuomba msaada wako nishinde dhambi na kuepuka mazingira
yake.
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA PILI
Ufukura
Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape
maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo
unifuate”[Mt 19:21]
Yesu alichagua hali ya ufukara kuwa njia yake ya utume na
ukarimu. Alijitolea sadaka na kutimiza mapenzi ya Baba. Nasi
73

8.4 Page 74

▲back to top


tupate utajiri wetu mkuu kwa ajili ya ukarimu kwa wahitaji.
Ufukara ni hali ya moyo na jambo la kitume. Ni hali ya maisha
ambayo yanamweka mtu huru na tayari katika utumishi. Ufukara
huu, sio ule umaskini; ni hali ya roho ya kumchagua Mungu dhidi
ya vitu vyote vya ulimwengu. Ufukara hutuwezesha kuchagua
mambo adili na wema wa jumuiya, kama haki na usawa wa watu
wote katika jamii.
Mambo yafuatayo yaweza kumsaidia mtu kukua katika
wema:
Kufuata mfano wa Yesu wa ufukara na kupata hazina kuu.
“zaidi ya hayo nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya
uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu;
ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote
nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo”[ Wafilipi 3: 8]
Ufukara Ni kuishi maisha ya kawaida, bidii na furaha katika
utendaji bila kujitakia makuu, kupenda wito wa kutumikia na
siyo kutumikiwa na kufanya majitoleo kwa ajili ya wengine.
Kumwamini Mungu kuwa Yeye ndiye anaongoza maisha yako
na kukupa kila kitu chema. Kutumia uhai ulio nao vema na
kuwa mkarimu kwa vitu vyote Mungu amekujalia kupata katika
maisha.
Katika msingi wa imani uliopokea; ni kupenda kuwa mkarimu
na kuwasaidia wale ambao wana hali duni ya maisha.
Katika ufukara kila mmoja huweka wazi uwezo wake wa vitu,
mali, muda, elimu na ujuzi, na maisha ya kiroho kwa ajili ya
utukufu wa Mungu kwa kuwahudumia wengi na utume wa
Kanisa na kazi zake. Tunatambua ukarimu wa Bwana wetu Yesu
Kristo: Japo alikuwa tajiri alijifanya fukara ili sisi tuwe tajiri [2
Kor 8:9]. Tunaamua kumfuata mkombozi ambaye alizaliwa
katika ufukara, ambaye hakumiliki kitu chochote na akafa
msalabani akiwa nusu uchi.
Bwana wetu Yesu Kristu, anatualika kuwa huru kutokana na
wasiwasi na mahangaiko ya vitu vya ulimwengu. Anataka
74

8.5 Page 75

▲back to top


tumwamini katika ufadhili wake na ufadhili wa Mungu Baba.
Twapaswa kujitolea kutangaza habari njema ya Injili [Mt 6:25].
Wakristo wa Kwanza walituwekea mfano tayari wa ukarimu
katika kushirikishana vitu vya ulimwengu huu. Nasi tumepewa
vipaji vingi na Mungu kwa ajili ya ukarimu huo.
Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Matendo ya Mitume 4:32-37; Zab 103
Tuombe
Ewe Bikira Maria Mtakatifu, Mama mwenye huruma na
neema, kwa msaada wa kweli umewaokoa Wakristo kutoka
mashambulizi ya adui, nakuomba uilinde roho na mwili
wangu dhidi ya mashambulizi ya muovu wa ulimwengu
huu,ili niwe mshindi dhidi ya maadui wa roho yangu. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….
Salamu Malkia
SIKU YA TATU
Usafi wa Moyo
Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba , wala mauti,
wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo,
wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala
yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza
kututenganishwa na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Bwana
wetu”[ Rum 8:38-39]
Usafi wa moyo ni kukamilisha ujinsia ndani ya mtu. Ni pamoja
na majifunzo ya kujitawala nafsi [KKK 2395]
Usafi wa moyo ni zawadi ambayo Mungu hutujalia kwa sababu
ya Ufalme wa Mungu. Katika imani tunakubali kwa shukrani na
tunajiweka katika namna ya kuishi kiaminifu. Tumfuate Yesu
75

8.6 Page 76

▲back to top


Kristo kiaminifu kwa kuchagua njia ya mapendo kumpenda
Mungu na jirani kwa moyo wote.
Tuishi maisha yetu kwa ajili ya upendo wa Mungu na upendo wa
wanadamu usio na mipaka. Twapaswa kuwapenda vijana na
watoto wanaokuwa kwa kuwaonyesha wema wa Mungu na ndio
maana ya malezi. Namna ya kukua katika usafi wa moyo:
Upendo ndio msingi wa maisha ya mwanadamu. Upendo
hauhusu tu kimwili bali pia maisha ya kiroho na kimwili.
Tuelewe kuwa upendo kamili ni kwa ajili ya mwingine. Ni
zawadi ambayo humwezesha mtu kujinyima na kufanya
majitoleo.
Kumpenda Mungu kwa roho na nguvu zako zote katika
kupenda wito wako na kuwatumikia wengine.
Ni vema kuelimika katika ukarimu na upendo kwa ajili yaw
engine. Hii inahusu ukweli, haki, uaminifu, urafiki, kuelewana
na kushinda vikwazo vyote dhidi yake.
Ni vema kuelewa udhaifu wako Ili ujiwekee njia ya kinga, Kwa
kuweza kutawala vionjo, kuwa mwangalifu katika uhusiano na
urafiki na kutumia vema vyombo vya mawasiliano na
mitandao.
Kumwomba Mungu msaada wake na neema, ili kumpenda
sana Kristo. Kushiriki Sakramenti ya Kitubio kama namna ya
kujitakasa na kumpenda Mama Bikira Maria.
Usafi wa moyo ni fadhila ya maadili. Pia ni kipaji kutoka kwa
Mungu, ni neema, ni tunda la juhudi za kiroho. Roho Mtakatifu
humwezesha mtu ambaye maji ya ubatizo yamemzaa mara ya pili
kuiga usafi wa Kristo [KKK 2345].
Wabatizwa wote wanaitwa kuwa na usawi wa moyo. Mkristo
‘amemvaa Kristo”, kielelezo cha usafi wa moyo. Waamini wote
katika Kristo wanaitwa kuishi maisha ya usafi wa moyo
kufuatana na hali zao za pekee katika maisha. Wakati wa Ubatizo
wake Mkristo anajikabidhi kuishi hisi zake katika usafi wa moyo
[KKK 2346]
76

8.7 Page 77

▲back to top


Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Rum 8:35-37 au 2 Kor 10:17-11.2; Zaburi 11
Tuombee
Maria Malkia mwenye nguvu, Ni wewe pekee ulishinda
uzushi ambao ulitaka kuligawanya Kanisa, nisadie,
nakuomba nishike imani yangu na uniokoe na vitisho na
mafundisho potofu. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA NNE
Sakramenti ya Ekaristi
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa
milele, nami nitamfufua siku ya mwisho [Yoh 6:54]
Kanisa latufundisha kuwa, Ekaristi ni “chemichemi na kilele cha
maisha yote ya Kikristo” .Katika Ekaristi takatifu mna kila hazina
ya kiroho ya Kanisa, yaani Kristo mwenyewe, “Pasaka wetu”.
Ekaristi ni kilele cha tendo la Mungu la kuutakatifuza ulimwengu
katika Kristo, na kilele cha tendo la kumwabudu Mungu wampalo
watu Kristo, na kwa njia yake wampalo Baba katika Roho
Mtakatifu.
Ekaristi Ni tendo la shukrani na masifu kwa Baba
Ni sakramenti ya wokovu iliyotekelezwa na Kristo Msalabani,
ni pia sadaka ya sifa katika shukrani kwa ajili ya kazi ya
uumbaji. Katika sadaka hii, kila kiumbe kinachopendwa na
Mungu hutolewa kwa Baba kwa njia ya kifo na ufufuko wa
Kristo.
Kwa njia ya Kristo, Kanisa latoa sadaka ya sifa katika
shukrani kwa ajili ya kila kitu ambacho Mungu amekifanya
chema, kizuri, Na sawa, katika uumbaji na katika binadamu.
Ekaristi Ni sadaka ya shukrani Kwa Baba, Ni Baraka ambayo
kwayo Kanisa huonyesha shukrani yake Kwa Mungu Kwa
77

8.8 Page 78

▲back to top


ajili ya fadhili zake zote, Kwa ajili ya kila kitu ambacho
amekifanya Kwa njia ya uumbaji, ukombozi na utakaso.
Mhali pa kwanza, Ekaristi ni “shukrani”.
Ekaristi ni sadaka ya sifa, kwa hii Kanisa huimba utukufu
kwa Mungu kwa jina la viumbe vyote. Sadaka hii ya sifa
yawezekana tu kwa njia ya Kristo.
Matunda ya Komunyo Takatifu
Komunyo Takatifu huukuza muungano wetu na Kristo:
Tunda la msingi la kupokea Komunyo takatifu ni umoja wa
ndani na Kristo. Yeye mwenyewe husema:
Aulaye mwili wangu ma kuinywa Damu yangu hukaa ndani
yangu, nami hukaa ndani yake”[Yoh 6:56]
Komunyo takatifu yatutenga na dhambi: Mwili wa Kristo
tunaoupokea katika komunyo takatifu, “hutolewa kwa ajili
yetu” na damu tunayokunywa “inamwagika kwa ajili ya wengi
kwa maondoleo ya dhambi.” Kwa sababu hiyo Ekaristi
Takatifu inatuunganisha na Kristo kwa sababu anatukinga na
dhambi.
Umoja wa Mwili wa Fumbo: Ekaristi inaunda Kanisa.
Wanaopokea Ekaristi huunganishwa kwa ndani Sana na Kristo.
Kwa njia yake Kristo huwaunganisha hawa na waamini wote
katika mwili mmoja: Ndilo Kanisa.[ 1 Kor 12:13; 1 Kor 10:16-17]
Ekaristi yatufanya tujitoe mhanga kwa maskini: Ili
kupokea katika kweli Mwili wa Kristo na Damu ya Kristo
iliyotolewa kwa ajili yetu, lazima kumtamani Kristo ndani ya
ndugu zake walio fukara sana.
Kuabudu Ekaristi
Katika Misa twaonyesha imani yetu kwa uwepo wa Kristo chini
ya maumbo ya mkate na divai, kati yam engine, kwa kupiga
magoti au kwa kujiinamisha kifudifudi kama ishara ya
kumwabudu Bwana. “Kanisa Katoliki daima lilitoa na
linaendelea kutoa ibada ya kuabudu inayostahili Sakramenti ya
Ekaristi, sit u wakati wa Misa pia nje ya adhimisho lake: Kwa
78

8.9 Page 79

▲back to top


kuhifadhi kwa uangalifu mkubwa sana hostia zilizogeuzwa, kwa
kuziweka mbele ya waamini ili waziabudu kwa heshima kubwa,
wakizichukua katika maandamano.
Kristo amependa awemo katika Kanisa lake kwa namna ya pekee.
Kwa kuwa Kristo alikuwa anawaacha walio wake wasimwone
tena kimwili, alipenda kutupatia uwepo wake kisakramenti; na
kwa kuwa alikuwa anaend kujitoa msalabani ili kutuokoa, alitaka
sisi tuwe na kumbukumbu ya upendo ambao kwao alitupenda
hadi kutoa uzima wake.
Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Isa 25:6; 55:1-2; Zab 22:26; Mt 22:2-14; Lk 14:15; Ufu 3:20;
19:9; Yoh 19:36; 1 Kor 5:7, Rejea Sakramenti ya Ekaristi
Tuombee
Ewe Bikira Maria, Mama Mwema, Malkia wa Mashahidi,
ujaze moyo wangu na nguvu za kuvumilia, nishinde
ubinadamu wangu, ili niishi imani ya dini yangu, kikamilifu
nyakati zote kama mtoto wako mwaminifu. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA TANO
Sakramenti ya Kitubio
Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni na
kuiamini Injili” [Mk 1:15]
Sakramenti ya Kitubio huleta huruma ya Mungu ambayo ni
ondoleo la kosa lililotendwa dhidi yake, na papo hapo
hupatanishwa na Kanisa ambalo dhambi yao imejeruhi, na
ambalo kwa mapendo, mfano na sala huhangaikia wongofu wao.
79

8.10 Page 80

▲back to top


Kwa njia ya Sakramenti za kuingizwa katika Ukristo, mtu
hupokea uzima mpya wa Kristo. Lakini twauchukua uzima huu
katika “vyombo vya udongo” nao hubaki “umefichika pamoja na
Kristo”. Tumo bado katika “makao ya duniani” tukielemewa na
hali ya mateso, magonjwa na kifo. Uzima huu mpya wa mtoto wa
Mungu waweza kudhoofika na hata kupotezwa kwa dhambi.
Namna mbalimbali za toba:
Sala, Kufunga na sadaka:- Huu ni uongofu kuhusu mtu
mwenyewe kwa kupata msamaha kutoka kwa Mungu. Ni
juhudi zinazofanywa Ili kujipatanisha Na jirani, juhudi kwa
ajili ya wokovu wa jirani.
Maisha ya kila siku: Wongofu hufanyika Kwa matendo ya
upatanishi, msaada Kwa maskini, kutenda Na kutetea haki Na
sheria, kukiri makosa, kuonyana, kupokea mateso, kuvumilia
madhulumu kwa ajili ya haki. Kubeba msalaba kila siku na
kumfuata Yesu diyo njia ya hakika ya toba.
Ekaristi na toba: Ekaristi huifanya iwepo sadaka ya Kristo
iliyotupanisha na Mungu. Ekaristi ni kinga inayotuokoa na
makosa yetu ya kila siku na hutukinga na dhambi za mauti.
Maandiko Matakatifu na sala ya Liturjia: Kusoma
maandiko Matakatifu, kusali sala ya Liturjia ya vipindi na
sala ya Baba yetu, kila tendo nyofu la kumwabudu Mungu au
uchaji huhuisha ndani yetu roho ya wongofu na ya toba na
huchangia katika msamaha wa dhambi zetu.
Nyakati na siku za toba: Katika mwaka wa Liturjia [Kipindi
cha Kwaresima, kila Ijumaa kukumbuka kifo cha Bwana] ni
nyakati nzito za zoezi la toba ya Kanisa. Nyakati hizi za pekee
zimewekwa Kwa ajili ya zoezi ya kiroho, liturjia ya toba,
kuhiji Kama ishara ya toba, kujinyima Kwa hiari Kama
kufunga Na kutoa sadaka, kushiriki kidugu kazi za mapendo
na za kimisionari.
Matunda ya Sakramenti ya Kitubio:
Upatanisho na Mungu: Sakramenti hii hukurudisha katika
neema ya Mungu, na kukuunganisha naye katika urafiki wa
ndani. Inakuletea amani na utulivu wa dhamiri inayosindikizwa
80

9 Pages 81-90

▲back to top


9.1 Page 81

▲back to top


na faraja kubwa ya kiroho. Hurudisha hadhi na mema ya maisha
ya watoto wa Mungu, ambayo lililo na thamani zaidi ni urafiki
wa Mungu.
Upatanisho na Kanisa: Dhambi huharibu na kuvunja
ushirika wa kidugu. Sakramenti ya Kitubio huutengeneza upya
umoja huowa Kanisa.
Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Law 16:1; Ebr 9:6-14; Ayu 42:7-9; Isa 53:12; Rejea Sakramenti
ya Upatanisho
Tuombe
Ewe Mama Bikira Maria, katika ushindi wa Papa Pius VII,
umeonyesha, ulinzi wako mkuu, ulilinde Kanisa lote na
kiongozi wake. Mlinde dhidi ya adui zake walio wengi, ili
aweze kuendesha kazi aliyokabidhiwa Petro ya kulilinda
Kanisa na kutunza imani yake. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA SITA
Sala
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka kaenda zake
mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko” [Mk 1:35]
Sala ni “ukumbusho wa Mungu”, ambayo ni kumbukumbu ya
moyo. Mapokeo ya Kikristo yamehifadhi mitindo mitatu
mikubwa ya maisha ya sala. Na yote ina tabia moja tu: Utulivu
wa moyo.
Sala ya Sauti
Mungu anasema na mtu kwa njia ya Neno lake. Kwa njia ya
maneno, ya akili au ya sauti sala yetu hutwaa mwili.
Mungu huwatafuta wamwabuduo katika roho na kweli, na
kwa hiyo sala ahia inayopanda vilindi vya moyo.
81

9.2 Page 82

▲back to top


Sala ya sauti ni sala ya vikundi kwa namna ya pekee. Sala
huwa ya ndani kadiri tunavyomtambua yule ambaye
“tunasema naye”. Sala ya sauti huwa hatua ya kwanza ya
sala ya tafakari.
Sala ya Fikara
Fikara ni hasa kutafuta. Roho inatafuta kufahamu kwa nini
Na jinsi gani ya maisha ya Kikristo, ili kushikamana na
kujibu kile ambacho Bwana anataka.
Tunasaidiwa katika sala ya fikara: kwa kusoma Maandiko
Matakatifu na kutafakari juu yake. Au hata rozari inatuingiza
katika maswala ya imani.
Sala ya Taamuli
Sala ya taamuli ni sala ya moyo, inayouelekeza moyo wa
mwanadamu kuwa na ushirika wa ndani na Mungu.
Sala ya taamuli ni sala ya mtoto wa Mungu, ya mdhambi
aliyesamehewa anayekubali kuyakaribisha mapendo ambayo
kwayo anapendwa, na anayetaka kuyajibu kwa kupenda hata
zaidi.
Sala ya taamuli ni mtazamao wa imani uanomkazia macho
Yesu. Ni kusikiliza Neno la Mungu. Ni sala ya ukimya ambao
ni alama ya ulimwengu ujao.
Sala ya taamuli ni uonyesho tu wa fumbo la sala. Ni mapendo
ya kimya na inatufanya tushiriki fumbo la Kristo.
Tafakari ya Maandiko Matakatifu:
Mt 14:23; Mk 1: 35; Mt 14:19; 15:36; Lk 23:34; Yn 17:9-24; Ebr
5:7; Zaburi 35; Zaburi 31;
Tuombe
Ewe Bikira Maria, Malkia wa Mitume, walinde Maaskofu,
mapadre na watoto wote wa Kanisa Katoliki,wape roho wa
umoja, uti kamili kwa baba mtakatifu, na bidii kwa ajili ya
wokovu wa wanadamu.Nakuomba uwalinde wamissionari, ili
waweze kuleta kabila zote katika imani ya kweli ya kumfuata
82

9.3 Page 83

▲back to top


Yesu Kristo!, ili kuwe na kundi moja la kondoo na mchungaji
mmoja. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA SABA
Utakatifu
Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie,
mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni
mtakatifu”[Mambo ya Walawi 19:2]
Utakatifu ni sifa na hali ya Mungu anayeumba, ni sifa pia ya
Yesu Kristo Mwana wa pekee wa Mungu anayekomboa, ni sifa
na hali ya Roho Mtakatifu anayetakaza. Mungu Mwenyezi
ametuumba katika utakatifu na ndivyo anaendelea kutoa mwaliko
na mwito kila siku: Bwana akanenana na Musa, akamwambia,
“Nena na mkutano wote wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa
watakatifu, kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni
mtakatifu”..[Mambo ya Walawi 19:1-2]. Yesu pia alirudia haya
maneno ya Baba kwa kusema, “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu,
kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu” [Mat 5:48].
Kuwa mtakatifu ni uhuru kamili ndani ya Mungu.
Katika imani tunamsadiki Kristo ambaye amezaliwa na Mama
Bikira Maria. Huyu Bikira Maria, Baba alimbariki Kwa
Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu WA roho, ndani yake
Kristo, Na akamchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi
ya ulimwengu, ili awe mtakatifu na bila hatia mbele zake
katika upendo.
Katika imani binadamu anafanywa mwana wa Mungu kwa
kupewa uwezo wa kuwa mfano wa Kristo. Hali hii
humwezesha kutenda yaliyo mema. Katika umoja Na Mwokozi
wake mwanafunzi hupata ukamilifu WA mapendo, yaani
utakatifu.
83

9.4 Page 84

▲back to top


Njia ya ukamilifu hupitia kwa njia ya Msalaba. Hakuna
utakatifu bila majikatalio na bila vita vya kiroho. Maendeleo
ya kiroho ni pamoja Na kujinyima, kujitesa kunakopelekea
pole pole kuishi siza za heri kwa amani na furaha.
Wito wa utimilifu wa maisha ya Kikristo na wa wa ukamilifu
wa upendo wanapewa wale wanaomsadiki Kristo wa kila cheo
na hali ya maisha. Wote wanaitwa kuwa watakatifu. Utimilifu
wa Kikristo una mpaka mmoja tu, ule wa kutokuwa na
chochote.
Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Law 11:44-45; 19:2; 20:7, 26; 21:8; 22:32; Kut 19:12; 16;23; 2
Sam 6:7; Kut 30:29; Eze 33:15; Bar 3:9; Ebr 4:12; 1 Pet 1:23;
Yn 3:12; 1 Yoh 5:12. KKK 2015, 1709, 2015,492...2013-14, 2028
Tuombe
Ewe Maria, uliyejaa neema na huruma, kwa msaada wako,
umewaokoa Wakristo kutoka magonjwa na matatizo mengi,
nisaidie na uniweke huru dhidi ya uvivu wa sala na kutolitumikia
Kanisa unaoniandama, nakuomba, walinde watu wema ili wawe
wakarimu na watunze wanyonge wa jumuiya yetu, na pia
uwavute watu wote wapate kufanya majuto ya kweli, ili ukweli
na ufalme wa Yesu Kristo uweze kutawala ulimwengu wote, ili
utukufu wa Mungu uenee na watu wote wawe watakatifu. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA NANE
Dhambi
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na
utukufu wa Mungu” [Warumi 3:23]
84

9.5 Page 85

▲back to top


Dhambi ni kosa dhidi ya akili, ukweli na dhamiri sahihi. Ni
kushindwa kuwa na mapendo kweli kwa Mungu na jirani kwa
sababu ya mapendo potofu ya mambo fulani. Hujeruhi tabia ya
mtu na kuharibu mshikamano wa kibinadamu. Dhambi ni
kumwasi Mungu kwa kutaka kuwa “sawa na miungu”. Hivyo
basi dhambi ni kujienda mwenyewe mpaka kumdharau Mungu.
Bwana ametufundisha kuwa mzizi wa dhambi umo ndani ya
moyo wa mtu, katika utashi wake huru, “moyoni hutoka mawazo
mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uwongo na
matukano; hayo ndio yamtiayo mtu unajisi [Mt 15:19-20].
Moyoni pia hukaa upendo, msingi wa kazi njema na safi, ambao
dhambi hujeruhi.
Dhambi ya Mauti: huaribu yoendo katika moyo wa ntu
kwa uvunjaji mzito wa sheria ya Mungu, inamgeuza mtu mbali na
Mungu ambaye ndiye kikomo chake kwa kupendelea kitu kidogo
kuliko yeye.
Dhambi ya mauti hutendwa kwa ujuzi kamili, na kutaka kwa
makusudi.
Dhambi ndogo [nyepesi]: Inadhoofisha mapendo,
inaonyesha mapendo ya viumbe yasiyo na taratibu; inazuia
maendeleo ya roho katika zoezi la fadhila na kuishi maisha
mema. Dhambi ndogo haimwondolei mkosefu neema ya
utakaso, urafiki wa Mungu, na furaha ya milele.
Ukweli kuhusu dhambi
Mtume Paulo atueleza kuwa sote tumetenda dhambi, na kwa hiyo
hali tumepungukiwa na utukufu wa Mungu [Rum 3:23]. Naye
Mtume Yakobo atueleza kuwa tukisema kuwa hatuna dhambi,
twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata
atuondelee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. [1 Yoh
1:8-9].
85

9.6 Page 86

▲back to top


Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Mwa 3; Rum 7:14-24; Lawi 15:19; 1 Kor 15:21-22; Mt 12:32;
Ebr 6:4-6; 10:26-31; Yn 8:21; 1 Yoh 5:16. Rejea Sakramenti ya
upatanisho.
Tuombe
Ewe Maria, Mnara wa Kanisa na Msaada wa Wakristo,
nakuomba unisaidie niwe na imani dhabiti na nitunze uhuru
wa watoto wa Mungu. Kwa msaada wa neema, ninaapa kuwa
mtii kwa baba mtakatifu na maaskofu walio katika ushirika
naye, nikiwa na hamu ya kuishi na kufa katika imani ya
Kanisa Katoliki, ambapo kuna matumaini ya uzima wa
milele.Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
SIKU YA TISA
Huruma ya Mungu
“Tazama, nimekuchora katika viganja vya mikono yangu, kuta
zako ziko mbele zangu daima” [Is 49:16]
Mungu ni mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa
hasira, mwingi wa rehema na kweli; na hapo Musa
anamwungama Bwana kuwa ni Mungu anayesamehe[ Kut 34:5-6;
34:9]. Jina la Mungu, “Mimi Niko’ au “Aliyeko” laonyesha
uaminifu wa Mungu licha ya dhambi ya uasi wa watu na adhabu
wanayostahili; anawaonea huruma watu elfu elfu. Mungu
anaonyesha huruma yake:
Kwa kumtoa Mwanawe wa pekee. Kwa kutoa uhai wake ili
kutukomboa na dhambi.
Yesu anafunua kwamba hata Yeye anachukua jina la Mungu.
86

9.7 Page 87

▲back to top


Mungu anatujalia mahitaji yetu yote; kwa kutufanya wana
anakotujalia.
Mungu anaonyesha uweza wake mkubwa, hasa kwa
kusamehe dhambi kwa hiari.
Mungu alituumba bila sisi, lakini hakutaka kutuokoa bila sisi;
kupokea huruma yake ni lazima kukikiri makosa yetu.
Kupata huruma ya Mungu twadaiwa kuwasamehe wale wote
wanaotukosea kwa kuungama dhambi zetu, mioyo yetu
inafungukia neema yake. Toba ya kweli ni kuwaombea wote
ambao wametukosea na wale ambao tumekosea huruma kwa
Mungu na msamaha wa dhambi.
Tafakari ya Maandiko Matakatifu
Hosea 1:66; 2;1,23; Yer 31:20; Isa 49:14-16; 1 Yoh 4:10,19;
Rum 11:29; Zab 100:5; 136; 1 Yoh 3:1-2; Kumb 7:37; 7:8:10:15
KKK 210-11,270, 2100, 1847, 2840,
Tuombe
Mama mkarimu Sana, katika kila kizazi, unapenda kiwe
Wakristu, nisaidie na msaada wako katika maisha, hasa
wakati wa kifo changu, ili baada ya kukupenda na
kukuheshimu hapa ulimwenguni, nipate kuja kwako huko
mbingu milele. Amina!
Baba yetu….x3; Salamu Maria…x3; Atukuzwe Baba….x3
Salamu Malkia…..
87

9.8 Page 88

▲back to top


UTARATIBU WA KUENDESHA IBADA YA NOVENA KWA
BIKIRA MARIA MSAADA WA WAKRISTO
Wakristo ambao wanapenda kupata baraka na neema katika
maisha yao ya Ukristo wapaswa kuwa na ushirika wa ndani na
Bikira Maria. Unataka kuwa mtakatifu? Jenga ushirika wa ndani
na Bikira Maria kwa kusali rozari, kusoma mapokeo ya Kanisa ili
umjue Mama wa Mkombozi. Namna ya kusali pamoja na Bikira
Maria; ufuatao ni utaratibu wa ibada ya Bikira Maria.
1. Utangulizi
Wimbo wa Bikira maria
Ishara ya Msalaba… na kama kawaida ya ibada.
2. Sala
Sala ya Mwanzo
Tuombe
Ewe Mungu Mwenyezi wa Milele, tunakushukuru kwa upendo
wako unaotujalia kwa njia ya Mwanao Yesu Kristo. Neno alikaa
kwetu na akatwaa mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Ulimpenda Bikira Maria awe Mama wa Mwokozi na wa
wanadamu wote. Tunakuomba utujalie neema na ulinzi wako siku
zote. Na kwa msaada wa maombezi yake tupate ahadi za uzima
wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
Amina!
3. Mafundisho
Waamini wote hukaa na kusikiliza mafundisho ya Bikira Maria
katika kitabu hiki, au Mt. Yohane Bosko na pia mafundisho
kuhusu Maandiko Matakatifu kadiri imepeanwa kwa siku.Pia
sehemu za injili zifuatazo zaweza kutumika.
Luka 1:26-38; Luka 1:48; Luka:36-39; Luka 2:21, 22, 40; Luka
1:46-49;Luka 2:22-24; Luka 1:48, 2:24; Matendo 1:12-
14;Yohana 19:25-27
Baada ya fundisho kumhusu Bikira Maria na kusoma sehemu ya
Injili, wanachama wanaweza kugawanyika katika makundi na
88

9.9 Page 89

▲back to top


kutafakari juu ya Bikira Maria kadiri walivyofundishwa. Sala ya
siku na tafakari yake inasomwa.
Sala za waamini
Hatua inayofuata ni sala za waamini, halafu zinafuata zile
5. Sala ya Rozari
Sala ya Rozari ya Bikira Maria pamoja na Litania yake
6. Sala ya Mwisho
Sala ya Mwisho
Bikira Maria Msaada wa Wakristo, wewe uliye mtakatifu sana
tunakukimbilia tukiomba msaada wako. Wewe ni Mama ambaye
hauwezi kumsahau Mwanao. Tunakuomba utujalie msaada wa
daima katika maombi yetu, na hasa katika mahangaiko na taabu
na katika majaribu ya kila siku. Uwape msaada wako wa kimama
wale wote wanaoteseka. Wasaidie maskini na wadhaifu, waponye
wagonjwa, waongoe wadhambi. Tunajiweka katika ulinzi wako
pamoja na familia zetu. Utujalie imani dhabiti na miito mingi
ndani ya Kanisa. Tunakuomba Ewe Maria Msaada wa Wakristo,
utujalie moyo wa kukupenda nyakati zote na utuelekeze
mbinguni kwa Mwanao. Amina!
7. Litania ya Bikira Maria
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristu utuhurumie
Kristu utuhurumie
Bwana utusikie
Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni, Mungu
utuhurumie
89

9.10 Page 90

▲back to top


Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu
Roho Mtakatifu, Mungu, Utuhurumie
Utatu Mtakatifu m Mungu Mmoja ,
Maria Mtakatifu….Utuombee
Mzazi Mtaktifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu, mkuu wa mabikira….
Mama wa Kristu,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama Mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama Msaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Mwumba,
Bikira Mwenye utaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kioo cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha hekima,
Chombo bora cha ibaada,
Waridi lenye fumbo, Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhu,
Afya ya wagonjwa,
90
Utuhurumie
utuhurumie.

10 Pages 91-100

▲back to top


10.1 Page 91

▲back to top


Makimbilio ya wakosefu,
Mfariji wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristo,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashahidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili,
Malkia uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari Takatifu,
Malkia wa Amani.
Mwana kondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
utuhurumie x3
K: Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe
Ee Bwana, twakuomba utujalie sisi watumishi wako tuwe siku
zote na afya ya roho na mwili; na kwa maombezi matukufu ya
Maria Mtakatifu, Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya sasa,
tupate na furaha za milele. Kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
Amina!
Kumbuka
Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema, haijasikika
kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako,
akiomba shime kwako, akitaka umwombee. Nami kwa
matumaini hayo, nakukimbilia, ee Mama, mkuu wa
mabikira; nakuja kwako, nasimama mbele yako nikilalamika
91

10.2 Page 92

▲back to top


mimi mkosefu, ewe Mama wa Neno wa Mungu, usiyakatae
maombi yangu, bali uyasikilize kwa wema, na unitimizie.
Amina!
8. Wimbo wa Bikira Maria
92

10.3 Page 93

▲back to top


MISA YA MTAKATIFU YOHANE BOSKO
Tarehe 31 Januari
Antifona: Njoni, enyi wana, mnisikilize, nami nitawafundisha
kumcha Bwana, mtukuzeni Bwana pamoja nami, na
tuliadhimishe jina lake pamoja [Zab 34:11, 31]
Sala ya Mwanzo
Ee Bwana Mungu wetu, katika maongozi yako ya ajabu
umetujalia Mtakatifu Yohani Bosko awe baba na mwalimu wa
vijana. Huyo mtumishi wako mwaminifu, akiongozwa na Bikira
Maria alijituma katika utume wa vijana kwa ajili ya manufaa ya
Kanisa. Utujalie moyo ule ule wa kutafuta roho za watu, hivi
kukutumikia Wewe uliye peke yako Mwema. Tunaomba hayo,
kwa njia ya Kristo Bwana wetu, anayeishi na kutawala nawe
katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima na Milele.
Amina
Kuombea Dhabihu
Ee Bwana pokea dhabihu zetu tunazokutoa kwa uchaji.
Tunakuomba utujalie ibada hii itusaidie tukupende kuliko vyote,
na maisha yetu yageuke kuwa wimbo wa utukufu wako.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina!
Prefasio
P. Bwana Awe nanyi
W. Awe Pia nawe
P. Inueni Mioyo
W. Tumeinua kwa Kwa Bwana
P. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki
Kweli ni vema na haki tukushukuru daima na po pote, ee Bwana,
Baba mwema, Mungu Mwenyezi wa milele,
93

10.4 Page 94

▲back to top


kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Baba mwenye upendo wa milele, umemteua Mtakatifu Yohani
Bosko katika Kanisa lako awe baba na rafiki wa vijana ili
kuwaongoza katika njia ya uzima.
Ulimpa maono ya kinabiii ili kuwaandaa vijana kukabili maisha
kwa matumaini, uaminifu na imani iliyo hai. Akiangazwa na
Roho Mtakatifu, aliunda familia kubwa ili kuendeleza utume
wake po pote duniani kama baba na mwalimu wa vijana.
Kwa hiyo, sisi tuliokusanyika katika adhimisho hili, pamoja na
majeshi ya malaika na watakatifu wote twaimba wimbo wa
utukufu wako tukisema kwa furaha:
Mtakatifu, Mtakatifu………………………….
Sala Baada ya Komunyo
Ee Baba, umetulisha kwa Sakramenti ya wokovu, tunakuomba
utusaidie kuiga mfano wa Mtakatifu Yohane Bosko kuwaelekeza
watu kwa Kristo aliye chemichemi ya uzima na utakatifu.
Tunaomba hayo kwa Njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.
Baraka Kuu
Bwana aliye chanzo cha kila nia njema awalinde daima kwa
neema yake na kudumisha uaminifu wa ahadi zenu za Ubatizo.
Amina
Kristo aliye Mchungaji Mwema awawezeshe kuwatumikia jirani
zenu kwa uchangamfu na upendo wa Mtakatifu Yohani Bosko.
Amina
Bwana awajalie ninyi nyote mlioadhimisha Sikukuu hii kwa
furaha ya kutembea katika imani, matumaini na mapendo. Amina.
Na Baraka yake Mungu Mwenyezi + ya Baba, na ya Mwana,
Na ya Roho Mtakatifu, iwashukie na kukaa nanyi daima nanyi.
Amina!
Nendeni na Amani
W. Tumshukuru Mungu
94

10.5 Page 95

▲back to top


SALA YA MISA
SIKUKUU YA MARIA MSAADA WA WAKRISTO 24 Mei
Sala ya Mwanzo
Ee Bwana Mungu, ulimchagua Bikira Maria awe Mama na
Msaada wa Wakristo, kwa msaada wa sala zake, lijalie Kanisa
nguvu ya Roho Mtakatifu, ili katika uvumilivu na upendo
waamini washinde majaribu yote na kushiriki ushindi wa Kristo
Mwanao. Anayeishi na kutawala, katika umoja wa Roho
Mtaktifu, Mungu, daima na milele. Amina
Sala kwa ajili ya Vipaji
Baba, Tunakuomba upokee , sala na vipaji watu wako
wanakutolea katika sherehe hii ya Bikira Maria Msaada wa
Wakristo, kwa maombezi yake , tujalie imani, matumaini na
upendo, ili tufanana na Kristo Bwana wetu , ambaye alijitolea
Mwenyewe kwa ajili ya uhai wa ulimwengu. Anayeishi na
kutawala daima na Milele. Amina.
Preface
P. Bwana Awe nanyi
W. Awe Pia nawe
P. Inueni Mioyo
W. Tumeinua kwa Kwa Bwana
P. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki
Kweli ni vema na haki tukushukuru daima na po pote, ee Bwana,
mwema , Mungu Mwenyezi wa milele kwa njia ya Kristo Bwana
wetu. Nasi katika Sikukuu hii ya Bikira Maria Msaada wa
Wakristo, tukutukuze kwa shangwe ipasayo. Yeye, mtumishi
wako mnyeyekevu na mfano wa fadhili zote, alishiriki mpango
wako wa upendo, katika utii wa imani na mapenzi katika utume
wa Kristo Bwana wetu. Kushirikiana naye katika Utukufu,
anaendelea utume wa Kanisa: Kwa moyo wa kimama
anawasaidia wanawe katika mahangaiko na hatari, katika safari
ya kuelekea Mbingu ya Yerusalemu. Kwa zawadi ya wema wako,
95

10.6 Page 96

▲back to top


mbingu na dunia huunganika katika shangwe kwa kuimba wimbo
mpya.
Sala Baada ya Kumunio
Baba, umetulisha na mkate wa mbinguni, Yesu Kristo,
aliyezaliwa na Bikira Maria na akafufuka kama tunda la kwanza
la kizazi kipya; tujalie tufanywe upya na tushiriki katika Ufalme
wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
BARAKA KUU
Mungu amependa, Maria awe msaada wa Wakristo, awashushie
baraka zake.
W. Amina
Naye Yesu Kristo, ambaye alishinda mauti msalabani na
kutupatia Maria kuwa Mama yetu, awajalie mshiriki uzima wa
milele.
W. Amina
Roho Mtakatifu aliyewashukia Mitume waliokuwa pamoja na
Bikira Maria, awafanye muwe mashahidi wa ufufuko duniani.
W. Amina.
Na Baraka yake Mungu Mwenyezi, ya Baba na Mwana, + na
Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima. Amina!
Nendeni na Amani
W. Tumshukuru Mungu
96

10.7 Page 97

▲back to top


KALENDA YA WATAKATIFU NA WENYEHERI KATIKA
SHIRIKA LA WASELISIANI WA DON BOSKO
JANUARI
15. Januari: Mwenyeheri Louis Variara, - Padre
(Kumbukumbu)
22. Januari: Mwenyeheri Laura Vicuńa, kijana (Kumbukumbu ya
hiari)
24. Januari: Mtatkatifu Fransisko wa Sale Msimamizi wa
Shirika la Waselisiani (Sikukuu)
30. Januari: Mwenyeheri Bronislas Markiewicz, Padre
(Kumbukumbu ya Hiari)
31. Januari: Mtakatifu Yohane Bosko, Padre Mwanzilishi
wa Shirika la Waselesiani wa Don Bosco na Mabinti wa
Maria Msaada wa Wakristo na pia Ushirika wa Maria
Msaada wa Wakristo (Sherehe)
FEBRUARI
1. Februari: Kumbukumbu ya Wazazi wa Waselesiani (Misa
husomwa katika vituo vyote vya Waselesiani wa Don Bosko)
7. Februari: Mwenyeheri Pius IX, Papa (kumbukumbu ya hiari)
9Februari: Mwenyeheri Eusebia Palomino Yenes, Bikira
(Kumbukumbu kwa Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo)
25 Februari: Wat. Mashahidi Louis Versiglia, Askofu na
Callistus Caravario, Padri (Sikukuu)
MACHI
19 Machi Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu mlinzi na msimamizi
ya Shirika la Waselesiani.
MEI
6 Mei: Mt. Dominiko Savio, kijana (Sikukuu)
13 Mei: Mt. Maria Domeniko Mazarello, Bikira (Sherehe kwa
mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo)
16 Mei: Mt. Louis Orione, Padre (Kumbukumbu ya hiari)
97

10.8 Page 98

▲back to top


18 Mei: Mt. Leonard Murialdo, Padre (Kumbukumbu ya hiari)
24 Mei: Sherehe ya Maria Msaada wa Wakristo- Bikira
Maria ndiye Msimamizi Mkuu wa Shirika la Waselesiani wa
Don Bosco na Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo
(Sherehe)
29 Mei: Mwenyeheri Joseph Kowalski, Padre na Shahidi
(Kumbukumbu)
JUNI
12 Juni: Mwenyeheri Francis Kesy na wenzake, mashahidi
(Kumbukumbu ya hiari)
23 Juni: Mtakatifu Yosefu Cafasso, Padre (Kumbukumbu).
JULAI
7 Julai: Mwenyeheru Maria Romero Meneses, Bikira
(Kumbukumbu ya Hiari)
AGOSTI
2 Agosti: Mwenyeheri Augustus Czartoryski, Padre
(Kumbukumbu ya Hiari).
26 Agosti: Zephrinus Namuncura, kijana (Kumbukumbu ya
Hiari).
SEPTEMBA
22 Septemba: Wenyeheri Joseph Calasanz Marques na Henry
Saiz Aparicio, Padre na wenzake, mashahidi (Kumbukumbu).
OKTOBA
5 Oktoba: Mwenyeheri Albert Marvelli (kumbukumbu ya hiari).
13 Oktoba: Mwenyeheri Alexandrina Maria da Costa, Bikira
(kumbukumbu).
24 Oktoba: Mt. Louis Gaunella, Padre (Kumbukumbu ya hiari).
29 Oktoba: Mwenyeheri Mikaeli Rua, Padre (kumbukumbu).
NOVEMBA
98

10.9 Page 99

▲back to top


13 Novemba: Mwenyeheri
(Kumbukumbu ya Hiari).
15 Novemba: Mwenyeheri
(kumbukumbu ya Hiari).
Artemides Zatti,
Madeleine Morano,
Mtawa
Bikira
DESEMBA
5 Desemba: Mwenyeheri Filipo Rinaldi, Padre na mwanzilishi
wa Volunteers of Don Bosco (Kumbukumbu).
99

10.10 Page 100

▲back to top


Kumbukumbu ya Waselesiani Marehemu
Tumshukuru Mungu kwa Waselesiani walioleta karama ya
Mtakatifu Yohane Bosko hapa Afrika Mashariki. Wengi wa hao
Waselesiani ndio walianzisha vituo vingi vya Don Bosko
ambavyo vinawafaidi vijana na watoto katika Afrika Mashariki.
Walijitolea kwa hali zote. Nyakati walifika walipata shida nyingi
sana, hasa lugha ilibidi wajifunze lugha zetu na tamaduni zetu ili
tupate kukombolewa. Wengi wao ndio waliweka misingi ya vituo
vyote vya Don Bosko tulivyo navyo. Hivyo basi tuwaombea kwa
Mungu siku zote. Ni wao walileta utamaduni wa Waselesiani na
pia kueneza ibada kwa Maria Msaada wa Wakristo.
Mwezi
Januari
Jina
Pd. Thomas
Punchekunnel,SDB
Pd. Lee Tae Seak
John
Br. Umberto Rizzetto
Mahali
alipofanya utume
Marsabit,
Upperhil,
Nzaikoni, Don
Bosco Boys
Town, Iringa Tz
Tonj Sudan
Don Bosco Embu
Tarehe
aliyoaga
4.01.2017
14.01.2010
21.01.2017
Februari
Pd. Thazhoor
Chacko,SDB
Pd. Thomas
Thayil,SDB
Machi
Pd. Edwin
Kaigarurala
Aprili Br. Palathinkal
Dodoma Tz,
Korr, Oysterbay
TZ
Don Bosco
Upperhill, Moshi
Tz, Dodoma Tz
Don Bosco Didia
Tz, Don Bosco
Mafinga seminary
Tz, Makuyu
Kenya
Marsabiti Kenya,
08.02.07
23.02.2010
14.03. 2011
16.04.1994
100

11 Pages 101-110

▲back to top


11.1 Page 101

▲back to top


Cherian,SDB
Don Bosco Boys
Town Kenya
Pd.
Marsabiti Kenya, 19.04.2012
Padinjaraparambil Korr Kenya, Don
George,SDB
Bosco Upperhill,
Don
Bosco
Moshi,
Don
Bosco Didia Tz,
Don
Bosco
Mafinga
Seminary Tz,
Don Bosco Boys
Town
Pd. Puthenveettil
Don Bosco
02.05.2008
Mei
Jacob,SDB
Upperhill, Don
Bosco Boys
Town
Pd. Listelo
Don Bosco
11.06.2000
Benjamini,SDB
Embu, Don
Bosco Makuyu,
Don Bosco Moshi
Pd. Pullenkannapallil Don
Bosco 23.06.2005
Manuel,SDB
Mafinga, Don
Bosco Korr, Don
Bosco Upanga
Juni
Pd. Daoura Charbel El Obeid Sudan 23.06.2015
A., SDB
Pd. Lobo
Don Bosco Iringa 29.06.2015
Joaquim,SDB
Tz, Don Bosco
Dodoma Tz, Don
Boscko Khartoum
Br. Fernandez
Juba Sudan, Don 22.07.2008
Gabriel,SDB
Bosco Iringa ,
Don Bosco
101

11.2 Page 102

▲back to top


Julai
Agosti
Septemba
Br. Pinakatt
Abrahama,SDB
Pd. Popowski
Bernard,SDB
Pd. Cais
Demetrio,SDB
Br. John
Williams,SDB
Pd. Braganza
Thomas,SDB
Pd. Gariglio
Luigi,SDB
Pd. Abate Luigi,SDB
Pd. Soreng
Patrick,SDB
Dodoma, Don
Bosco Khartoum
Don Bosco
Iringa, Don
Bosco Dodoma,
Don Bosco Boys
Town, Don Bosco
Moshi
Don Bosco
Bombo Uganda,
Don Bosco
Siakago
Don
Bosco
Iringa,
Don
Bosco Moshi,
Don Bosco Dar es
Salaam, Don
Bosco Upperhill,
Don
Bosco
Utume Kenya
Don
Bosco
Mafinga Parish,
Don
Bosco
Upanga
Don
Bosco
Makuyu, Don
Bosco Embu
Don
Bosco
Embu,
Don
Bosco Makuyu
Don Bosco Wau,
Don Bosco El
Obeid,
Don
Bosco Khartoum,
Don Bosco Juba
23.07.2011
27.08.1999
31.08.1997
01.09.2010
08.09.1992
09.09.2014
10.09.1993
16.09.2013
102

11.3 Page 103

▲back to top


Oktoba
Pd. Masichio
Luka,SDB
Br. Morcelli
Alphonso,SDB
Don
Bosco
Embu,
Don
Bosco Makuyu
Don Bosco
Embu, Don
Bosco Oysterbay,
Don Bosco
Moshi, Don
Bosco
Dododoma, Don
Bosco Khartoum
19.09.1994
23.10.2010
Pd McFerran
Sean,SDB
Pd. D’Souza
Crispin,SDB
Novemba Pd. Anthony
Lucrasio Pinto,SDB
Don Bosco Boys
Town
Don Bosco
Dodoma, Don
Bosco Iringa
Don Bosco
Upperhill, Don
Bosco Boys
Town, Don Bosco
Boys, Don Bosco
Nzaikoni
12.11.1998
13.11.2010
26.11.2005
Pd. Malieckal
Joseph,SDB
Desemba Pd.Kizhakeyil
Jacob,SDB
Pd. Valayam Philip,
SDB
Don Bosco
Mafinga
Seminary
Don Bosco
Maridi, Don
Bosco Korr
Don Bosco
Moshi, DBYES
02.12.1996
20.12.1994
25.12.2005
103

11.4 Page 104

▲back to top


REJEA
AUBRY J., The renewal of our Salesiani Life, New York 1984.
DESRAMAUT, F., Life of Fr. Michael Rua Don Bosco’s
Successor, 1837-1910), Rome 2010.
HUBERT J.T, - DONALD A., Butler’s Lives of Saints,
Westminster, Mary Land, 1990.
J.PUTHENKALAMA, - A. MAMPRA, Sanctity in the Salesian
Family, Tamil Nadu 2002.
LENTI A.J, Don Bosco: History and Spirit Vol III, Rome 2008.
LENTI A.J, Don Bosco: History and Spirit Vol IV, Rome 2008.
LENTI A.J, Don Bosco: History and Spirit Vol VI, Rome 2009
LENTI A.J, Don Bosco: History and Spirit Vol VII, Rome 2010.
Salesians of Don Bosco Province od Eastern Africa, Province
Directory 2017-2018.
In dialogue with the Lord; Manual of prayer for the Salesian
Communities, New Delhi India, 2004
Salesian Proper Offices Calendar and Liturgical Texts, Rome
2011.
General Chapter XXVI, “Da Mihi Animas Cetera Tolle
“Salesians of Don Bosco, Rome 23 Febraury 2008.
THE NEW ADMA REGULATIONS, Association of Mary Help of
Christians [ADMA] , Pisana Roma July 2003
Katekisimu ya Kanisa Katoliki, Nairobi 2000.
Maisha ya Watakatifu, Tabora Tanzania 1996.
Misale ya Waumini, Tabora Tanzania, 1978.
Biblia Takatifu, Iringa 2004.
Hati za Mtaguso Mkuu wa Vatikano II, Iringa 2001.
104