ADMA-swahili1


ADMA-swahili1

1 Page 1

▲back to top
Niliingia shule ya ufundi ya Don Bosko, -
Don Bosco Boys Town Karen Nairobi
1990. Nilikutana na mapadre Waselesiani
waliokuwa tofauti kabisa na mapadri wen-
gine. Walikuwa wakarimu, marafiki, wali-
mu. Hawa mapadre na Mabruda walishiriki
kazi zetu, tulicheza pamoja nao, tulisali
pamoja, walitufundisha darasani; walitu-
penda sana. Wakati wa mapumziko
walikuwa pamoja nasi, na hata mara nyingi
sana walikula chakula pamoja nasi. Tukiwa
Karakana, walitembea kuona maendeleo
yetu, na pia walitusaidia kuelewa maarifa hapa na pale na kutupatia
matumaini.
Mapadre Waselesiani pamoja na Mabruda walitupatia nafasi za
purudani, michezo na mambo yanayofurahisha vijana. Kukaa Don
Bosko kila mmoja aliweza kuelewa na kukuza talanta yake, katika
michezo, muziki, uchoraji na pia katika utakatifu na elimu. Mara
nyingi tukiwa wanafunzi, mapadre hao walitufundisha hasa kumhusu
Mt. Yohane Bosko, Mt. Dominiko Savio na pia Maria Msaada wa Wa-
kristo.
Mwaka 1992 nilienda Don Bosco Embu, shule ya sekondari na
ufundi ya Waselesiani wa Don Bosko. Hapo kulikuwa na mapadre
Wataliano ambaye waliokuwa wamebobea katika muziki, ufundi, uku-
lima na elimu. Hao pia walinilea katika karama hiyo hiyo ya Mt. Yo-
hane Bosko. Nyakati zote nilijisikia nyumbani. Ndivyo nilivutiwa na
wito wa kuwa mmoja wao hadi sasa mimi ni padre Msalesiani. Natoa
shukrani zangu kwa Mungu kwa njia ya kuandaa kitabu hiki cha Maria
Msaada wa Wakristo kwa ajili ya kueneza ibada hii ya Maria Msaada
wa Wakristo na pia kukuza Karama ya Mt. Yohane Bosko ndani ya
vijana. Baada ya kusomea na kulelewa katika shule na Seminari za Mt.
Yohane Bosko najivunia kuwa Msalesiani wa Don Bosko. Ni wajibu
wangu kupekua yaliyo ndani na kuwasaidia wengine kuelewa zaidi.
Pd. Paul Luseno Khanyonyi, SDB
Pd. Paul Luseno Khanyonyi, SDB